1 Samuel 10 (BOKCV)

1 Ndipo Samweli akachukua chupa ndogo ya mafuta na kuyamimina juu ya kichwa cha Sauli, akambusu, akisema, “Je, BWANA hakukutia mafuta uwe kiongozi juu ya watu wake Israeli? 2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na watu wawili karibu na kaburi la Raheli, huko Selsa kwenye mpaka wa Benyamini. Watakuambia, ‘Punda wale uliotoka kwenda kuwatafuta, wamekwisha kupatikana. Sasa baba yako ameacha kufikiri kuhusu punda na sasa ana hofu kukuhusu wewe. Anauliza, “Nitafanyaje kuhusu mwanangu?” ’ 3 “Kisha utakwenda mbele kutoka hapa mpaka uufikie mwaloni wa Tabori. Watu watatu wanaopanda kwa Mungu huko Betheli watakutana nawe hapo. Mmoja atakuwa amechukua wana-mbuzi watatu, mwingine mikate mitatu, na mwingine kiriba cha divai. 4 Watakusalimu na kukupa mikate miwili, ambayo utaipokea kutoka kwao. 5 “Baada ya hayo utakwenda Gibea ya Mungu, ambapo hapo kuna kambi ya Wafilisti. Unapokaribia mji utakutana na kundi la manabii wakiteremka kutoka mahali pa juu wakiwa na vinubi, matari, filimbi na zeze vikipigwa mbele yao, nao watakuwa wakitoa unabii. 6 Roho wa BWANA atakuja juu yako kwa nguvu, nawe utatoa unabii pamoja nao; nawe utageuzwa kuwa mtu wa tofauti. 7 Mara ishara hizi zitakapotimizwa, fanya lolote mkono wako upasao kufanya, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe. 8 “Tangulia kushuka mbele yangu mpaka Gilgali. Hakika nami nitateremka nikujie ili kutoa dhabihu za sadaka za kuteketezwa na dhabihu za amani, lakini lazima ungoje kwa siku saba hata nitakapokujia na kukuambia likupasalo kufanya.” 9 Ikawa Sauli alipogeuka kumwacha Samweli, Mungu aliubadilisha moyo wa Sauli, na ishara hizi zote zikatimizwa siku ile. 10 Walipofika Gibea, akakutana na kundi la manabii. Roho wa Mungu akaja juu yake kwa nguvu, naye akajiunga nao katika kutoa unabii kwao. 11 Ikawa wale wote waliomfahamu hapo mwanzo walipomwona akitoa unabii pamoja na manabii, wakaulizana, “Ni nini hiki kilichomtokea mwana wa Kishi? Je, Sauli naye pia yumo miongoni mwa manabii?” 12 Mtu mmoja ambaye aliishi huko akajibu, “Je, naye baba yao ni nani?” Basi ikawa mithali, kusema, “Je, Sauli pia yumo miongoni mwa manabii?” 13 Baada ya Sauli kumaliza kutoa unabii, alikwenda mahali pa juu. 14 Basi babaye mdogo akamuuliza Sauli na mtumishi wake, “Je, mlikuwa wapi?”Akajibu, “Tulikuwa tukiwatafuta punda. Lakini tulipoona hawapatikani, tulikwenda kwa Samweli.” 15 Babaye mdogo Sauli akasema, “Niambie Samweli amekuambia nini.” 16 Sauli akajibu, “Alituhakikishia kwamba punda wamepatikana.” Lakini hakumwambia babaye mdogo kila kitu Samweli alichomwambia kuhusu ufalme. 17 Samweli akawaita watu wa Israeli kuja kwa BWANA huko Mispa, 18 naye akawaambia, “Hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, nami niliwaokoa toka nguvu za Misri na falme zote zilizowaonea.’ 19 Lakini sasa mmemkataa Mungu wenu, ambaye anawaokoa toka katika maafa yenu yote na taabu zenu zote. Nanyi mmesema, ‘Hapana, tuteulie mfalme atutawale.’ Sasa basi, jihudhurisheni wenyewe mbele za BWANA kwa kabila zenu na kwa koo zenu.” 20 Samweli alipoyasogeza makabila yote ya Israeli, kabila la Benyamini likachaguliwa. 21 Kisha akalisogeza mbele kabila la Benyamini, ukoo kwa ukoo, nao ukoo wa Matri ukachaguliwa. Mwishoni Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipomtafuta, hakuonekana. 22 Wakazidi kuuliza kwa BWANA, “Je, huyo mtu amekwisha kufika hapa?”Naye BWANA akasema, “Ndiyo, amejificha katikati ya mizigo.” 23 Wakakimbia na kumleta kutoka huko, naye aliposimama katikati ya watu, alikuwa mrefu kuliko watu wengine wote. 24 Samweli akawaambia watu wote, “Je, mnamwona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hayupo aliye kama yeye miongoni mwa watu wote.”Ndipo watu wakapiga kelele, wakasema, “Mfalme na aishi maisha marefu.” 25 Samweli akawaeleza watu madaraka ya ufalme. Akayaandika kwenye kitabu na kuweka mbele za BWANA. Kisha Samweli akawaruhusu watu, kila mmoja aende nyumbani kwake. 26 Sauli pia akaenda nyumbani kwake huko Gibea, akisindikizwa na watu hodari ambao Mungu alikuwa amegusa mioyo yao. 27 Lakini baadhi ya watu wakorofi walisema, “Huyu mtu atawezaje kutuokoa?” Wakamdharau na wala hawakumletea zawadi. Lakini Sauli akanyamaza kimya.

In Other Versions

1 Samuel 10 in the ANGEFD

1 Samuel 10 in the ANTPNG2D

1 Samuel 10 in the AS21

1 Samuel 10 in the BAGH

1 Samuel 10 in the BBPNG

1 Samuel 10 in the BBT1E

1 Samuel 10 in the BDS

1 Samuel 10 in the BEV

1 Samuel 10 in the BHAD

1 Samuel 10 in the BIB

1 Samuel 10 in the BLPT

1 Samuel 10 in the BNT

1 Samuel 10 in the BNTABOOT

1 Samuel 10 in the BNTLV

1 Samuel 10 in the BOATCB

1 Samuel 10 in the BOATCB2

1 Samuel 10 in the BOBCV

1 Samuel 10 in the BOCNT

1 Samuel 10 in the BOECS

1 Samuel 10 in the BOGWICC

1 Samuel 10 in the BOHCB

1 Samuel 10 in the BOHCV

1 Samuel 10 in the BOHLNT

1 Samuel 10 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 10 in the BOICB

1 Samuel 10 in the BOILNTAP

1 Samuel 10 in the BOITCV

1 Samuel 10 in the BOKCV2

1 Samuel 10 in the BOKHWOG

1 Samuel 10 in the BOKSSV

1 Samuel 10 in the BOLCB

1 Samuel 10 in the BOLCB2

1 Samuel 10 in the BOMCV

1 Samuel 10 in the BONAV

1 Samuel 10 in the BONCB

1 Samuel 10 in the BONLT

1 Samuel 10 in the BONUT2

1 Samuel 10 in the BOPLNT

1 Samuel 10 in the BOSCB

1 Samuel 10 in the BOSNC

1 Samuel 10 in the BOTLNT

1 Samuel 10 in the BOVCB

1 Samuel 10 in the BOYCB

1 Samuel 10 in the BPBB

1 Samuel 10 in the BPH

1 Samuel 10 in the BSB

1 Samuel 10 in the CCB

1 Samuel 10 in the CUV

1 Samuel 10 in the CUVS

1 Samuel 10 in the DBT

1 Samuel 10 in the DGDNT

1 Samuel 10 in the DHNT

1 Samuel 10 in the DNT

1 Samuel 10 in the ELBE

1 Samuel 10 in the EMTV

1 Samuel 10 in the ESV

1 Samuel 10 in the FBV

1 Samuel 10 in the FEB

1 Samuel 10 in the GGMNT

1 Samuel 10 in the GNT

1 Samuel 10 in the HARY

1 Samuel 10 in the HNT

1 Samuel 10 in the IRVA

1 Samuel 10 in the IRVB

1 Samuel 10 in the IRVG

1 Samuel 10 in the IRVH

1 Samuel 10 in the IRVK

1 Samuel 10 in the IRVM

1 Samuel 10 in the IRVM2

1 Samuel 10 in the IRVO

1 Samuel 10 in the IRVP

1 Samuel 10 in the IRVT

1 Samuel 10 in the IRVT2

1 Samuel 10 in the IRVU

1 Samuel 10 in the ISVN

1 Samuel 10 in the JSNT

1 Samuel 10 in the KAPI

1 Samuel 10 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 10 in the KBV

1 Samuel 10 in the KJV

1 Samuel 10 in the KNFD

1 Samuel 10 in the LBA

1 Samuel 10 in the LBLA

1 Samuel 10 in the LNT

1 Samuel 10 in the LSV

1 Samuel 10 in the MAAL

1 Samuel 10 in the MBV

1 Samuel 10 in the MBV2

1 Samuel 10 in the MHNT

1 Samuel 10 in the MKNFD

1 Samuel 10 in the MNG

1 Samuel 10 in the MNT

1 Samuel 10 in the MNT2

1 Samuel 10 in the MRS1T

1 Samuel 10 in the NAA

1 Samuel 10 in the NASB

1 Samuel 10 in the NBLA

1 Samuel 10 in the NBS

1 Samuel 10 in the NBVTP

1 Samuel 10 in the NET2

1 Samuel 10 in the NIV11

1 Samuel 10 in the NNT

1 Samuel 10 in the NNT2

1 Samuel 10 in the NNT3

1 Samuel 10 in the PDDPT

1 Samuel 10 in the PFNT

1 Samuel 10 in the RMNT

1 Samuel 10 in the SBIAS

1 Samuel 10 in the SBIBS

1 Samuel 10 in the SBIBS2

1 Samuel 10 in the SBICS

1 Samuel 10 in the SBIDS

1 Samuel 10 in the SBIGS

1 Samuel 10 in the SBIHS

1 Samuel 10 in the SBIIS

1 Samuel 10 in the SBIIS2

1 Samuel 10 in the SBIIS3

1 Samuel 10 in the SBIKS

1 Samuel 10 in the SBIKS2

1 Samuel 10 in the SBIMS

1 Samuel 10 in the SBIOS

1 Samuel 10 in the SBIPS

1 Samuel 10 in the SBISS

1 Samuel 10 in the SBITS

1 Samuel 10 in the SBITS2

1 Samuel 10 in the SBITS3

1 Samuel 10 in the SBITS4

1 Samuel 10 in the SBIUS

1 Samuel 10 in the SBIVS

1 Samuel 10 in the SBT

1 Samuel 10 in the SBT1E

1 Samuel 10 in the SCHL

1 Samuel 10 in the SNT

1 Samuel 10 in the SUSU

1 Samuel 10 in the SUSU2

1 Samuel 10 in the SYNO

1 Samuel 10 in the TBIAOTANT

1 Samuel 10 in the TBT1E

1 Samuel 10 in the TBT1E2

1 Samuel 10 in the TFTIP

1 Samuel 10 in the TFTU

1 Samuel 10 in the TGNTATF3T

1 Samuel 10 in the THAI

1 Samuel 10 in the TNFD

1 Samuel 10 in the TNT

1 Samuel 10 in the TNTIK

1 Samuel 10 in the TNTIL

1 Samuel 10 in the TNTIN

1 Samuel 10 in the TNTIP

1 Samuel 10 in the TNTIZ

1 Samuel 10 in the TOMA

1 Samuel 10 in the TTENT

1 Samuel 10 in the UBG

1 Samuel 10 in the UGV

1 Samuel 10 in the UGV2

1 Samuel 10 in the UGV3

1 Samuel 10 in the VBL

1 Samuel 10 in the VDCC

1 Samuel 10 in the YALU

1 Samuel 10 in the YAPE

1 Samuel 10 in the YBVTP

1 Samuel 10 in the ZBP