1 Samuel 26 (BOKCV)

1 Hao Wazifu wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kinachotazamana na Yeshimoni?” 2 Hivyo Sauli akashuka kwenda katika Jangwa la Zifu, akiwa na watu wake 3,000 wa Israeli waliochaguliwa, kumsaka Daudi huko. 3 Sauli akapiga kambi yake kando ya barabara juu ya kilima cha Hakila kinachotazamana na Yeshimoni, lakini Daudi alikuwa anaishi huko jangwani. Alipoona kuwa Sauli amemfuata huko, 4 Daudi akatuma wapelelezi na akapata habari kwa hakika kwamba Sauli alikuwa amewasili. 5 Ndipo Daudi akaondoka, akaenda hadi mahali Sauli alikuwa amepiga kambi. Akaona mahali Sauli na Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi, walipokuwa wamelala. Sauli alikuwa amelala ndani ya kambi, jeshi likiwa limemzunguka. 6 Basi Daudi akamuuliza Ahimeleki Mhiti, na Abishai mwana wa Seruya, nduguye Yoabu, akisema, “Ni nani atakayeshuka pamoja nami kambini kwa Sauli?”Abishai akajibu, “Nitakwenda pamoja nawe.” 7 Hivyo Daudi na Abishai wakaenda kwenye jeshi wakati wa usiku, tazama Sauli, alikuwa amelala ndani ya kambi na mkuki wake umekitwa ardhini karibu na kichwa chake. Abneri na askari walikuwa wamelala kumzunguka Sauli. 8 Abishai akamwambia Daudi, “Leo Mungu amemtia adui yako mikononi mwako. Sasa niruhusu nimchome mpaka ardhini kwa pigo moja la mkuki wangu; sitamchoma mara mbili.” 9 Lakini Daudi akamwambia Abishai, “Usimwangamize! Ni nani awezaye kutia mkono juu ya mpakwa mafuta wa BWANA na asiwe na hatia?” 10 Daudi akasema, “Hakika kama vile BWANA aishivyo, BWANA mwenyewe atampiga; au wakati wake utafika, naye atakufa, au atakwenda vitani na kuangamia. 11 Lakini Mungu na apishie mbali nisije nikainua mkono juu ya mpakwa mafuta wa BWANA. Sasa chukua huo mkuki na hilo gudulia la maji vilivyo karibu na kichwa chake, tuondoke.” 12 Hivyo Daudi akachukua huo mkuki na hilo gudulia la maji vilivyokuwa karibu na kichwa cha Sauli, nao wakaondoka. Hakuna yeyote aliyeona au kufahamu habari hii, wala hakuna hata mmoja aliyeamka usingizini. Wote walikuwa wamelala, kwa sababu BWANA alikuwa amewatia kwenye usingizi mzito. 13 Kisha Daudi akavuka upande mwingine na kusimama juu ya kilima mahali palipokuwa na nafasi pana kati yao. 14 Daudi akalipigia kelele jeshi na Abneri mwana wa Neri, akisema, “Je, Abneri, hutanijibu?”Abneri akajibu, “Nani wewe umwitaye mfalme?” 15 Daudi akasema, “Wewe si ni mtu shujaa? Ni nani aliye kama wewe katika Israeli? Kwa nini basi hukumlinda mfalme bwana wako? Mtu mmoja alikuja kumwangamiza mfalme, bwana wako. 16 Ulichokifanya si kizuri. Kwa hakika kama aishivyo BWANA, wewe na watu wako mnastahili kufa, kwa sababu hamkumlinda bwana wenu, mpakwa mafuta wa BWANA. Tazameni hapo mlipo. Uko wapi mkuki wa mfalme na gudulia la maji ambavyo vilikuwa karibu na kichwa chake?” 17 Sauli akatambua sauti ya Daudi, na kusema, “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?”Daudi akajibu, “Naam, hiyo ndiyo, bwana wangu mfalme.” 18 Pia akaongeza, “Kwa nini bwana wangu anamfuatia mtumishi wake? Nimefanya nini, nalo kosa langu ni lipi nililolifanya niwe na hatia? 19 Sasa mfalme bwana wangu na asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama BWANA amekuchochea dhidi yangu, basi yeye na aipokee sadaka yangu. Lakini hata hivyo, kama ni wanadamu waliofanya hivyo, walaaniwe mbele za BWANA! Wao sasa wamenifukuza kutoka sehemu yangu katika urithi wa BWANA wangu wakisema, ‘Nenda ukatumikie miungu mingine.’ 20 Basi usiache damu yangu imwagike kwenye ardhi mbali na uso wa BWANA. Mfalme wa Israeli ametoka kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware katika milima.” 21 Ndipo Sauli akasema, “Nimetenda dhambi. Rudi, Daudi mwanangu. Kwa kuwa uliyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani leo, sitajaribu kukudhuru tena. Hakika nimetenda kama mpumbavu na nimekosa sana.” 22 Daudi akajibu, “Mkuki wa mfalme uko hapa. Mmoja wa vijana wako na avuke kuuchukua. 23 BWANA humlipa kila mtu kwa ajili ya haki yake na uaminifu wake. BWANA alikutia katika mikono yangu leo, lakini sikuinua mkono wangu juu ya mpakwa mafuta wa BWANA. 24 Kwa hakika kama vile maisha yako yalivyokuwa ya thamani kwangu leo, vivyo hivyo maisha yangu na yawe na thamani kwa BWANA na kuniokoa kutoka taabu zote.” 25 Ndipo Sauli akamwambia Daudi, “Mwanangu Daudi na ubarikiwe; utafanya mambo makubwa na hakika utashinda.”Basi Daudi akaenda zake, naye Sauli akarudi nyumbani.

In Other Versions

1 Samuel 26 in the ANGEFD

1 Samuel 26 in the ANTPNG2D

1 Samuel 26 in the AS21

1 Samuel 26 in the BAGH

1 Samuel 26 in the BBPNG

1 Samuel 26 in the BBT1E

1 Samuel 26 in the BDS

1 Samuel 26 in the BEV

1 Samuel 26 in the BHAD

1 Samuel 26 in the BIB

1 Samuel 26 in the BLPT

1 Samuel 26 in the BNT

1 Samuel 26 in the BNTABOOT

1 Samuel 26 in the BNTLV

1 Samuel 26 in the BOATCB

1 Samuel 26 in the BOATCB2

1 Samuel 26 in the BOBCV

1 Samuel 26 in the BOCNT

1 Samuel 26 in the BOECS

1 Samuel 26 in the BOGWICC

1 Samuel 26 in the BOHCB

1 Samuel 26 in the BOHCV

1 Samuel 26 in the BOHLNT

1 Samuel 26 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 26 in the BOICB

1 Samuel 26 in the BOILNTAP

1 Samuel 26 in the BOITCV

1 Samuel 26 in the BOKCV2

1 Samuel 26 in the BOKHWOG

1 Samuel 26 in the BOKSSV

1 Samuel 26 in the BOLCB

1 Samuel 26 in the BOLCB2

1 Samuel 26 in the BOMCV

1 Samuel 26 in the BONAV

1 Samuel 26 in the BONCB

1 Samuel 26 in the BONLT

1 Samuel 26 in the BONUT2

1 Samuel 26 in the BOPLNT

1 Samuel 26 in the BOSCB

1 Samuel 26 in the BOSNC

1 Samuel 26 in the BOTLNT

1 Samuel 26 in the BOVCB

1 Samuel 26 in the BOYCB

1 Samuel 26 in the BPBB

1 Samuel 26 in the BPH

1 Samuel 26 in the BSB

1 Samuel 26 in the CCB

1 Samuel 26 in the CUV

1 Samuel 26 in the CUVS

1 Samuel 26 in the DBT

1 Samuel 26 in the DGDNT

1 Samuel 26 in the DHNT

1 Samuel 26 in the DNT

1 Samuel 26 in the ELBE

1 Samuel 26 in the EMTV

1 Samuel 26 in the ESV

1 Samuel 26 in the FBV

1 Samuel 26 in the FEB

1 Samuel 26 in the GGMNT

1 Samuel 26 in the GNT

1 Samuel 26 in the HARY

1 Samuel 26 in the HNT

1 Samuel 26 in the IRVA

1 Samuel 26 in the IRVB

1 Samuel 26 in the IRVG

1 Samuel 26 in the IRVH

1 Samuel 26 in the IRVK

1 Samuel 26 in the IRVM

1 Samuel 26 in the IRVM2

1 Samuel 26 in the IRVO

1 Samuel 26 in the IRVP

1 Samuel 26 in the IRVT

1 Samuel 26 in the IRVT2

1 Samuel 26 in the IRVU

1 Samuel 26 in the ISVN

1 Samuel 26 in the JSNT

1 Samuel 26 in the KAPI

1 Samuel 26 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 26 in the KBV

1 Samuel 26 in the KJV

1 Samuel 26 in the KNFD

1 Samuel 26 in the LBA

1 Samuel 26 in the LBLA

1 Samuel 26 in the LNT

1 Samuel 26 in the LSV

1 Samuel 26 in the MAAL

1 Samuel 26 in the MBV

1 Samuel 26 in the MBV2

1 Samuel 26 in the MHNT

1 Samuel 26 in the MKNFD

1 Samuel 26 in the MNG

1 Samuel 26 in the MNT

1 Samuel 26 in the MNT2

1 Samuel 26 in the MRS1T

1 Samuel 26 in the NAA

1 Samuel 26 in the NASB

1 Samuel 26 in the NBLA

1 Samuel 26 in the NBS

1 Samuel 26 in the NBVTP

1 Samuel 26 in the NET2

1 Samuel 26 in the NIV11

1 Samuel 26 in the NNT

1 Samuel 26 in the NNT2

1 Samuel 26 in the NNT3

1 Samuel 26 in the PDDPT

1 Samuel 26 in the PFNT

1 Samuel 26 in the RMNT

1 Samuel 26 in the SBIAS

1 Samuel 26 in the SBIBS

1 Samuel 26 in the SBIBS2

1 Samuel 26 in the SBICS

1 Samuel 26 in the SBIDS

1 Samuel 26 in the SBIGS

1 Samuel 26 in the SBIHS

1 Samuel 26 in the SBIIS

1 Samuel 26 in the SBIIS2

1 Samuel 26 in the SBIIS3

1 Samuel 26 in the SBIKS

1 Samuel 26 in the SBIKS2

1 Samuel 26 in the SBIMS

1 Samuel 26 in the SBIOS

1 Samuel 26 in the SBIPS

1 Samuel 26 in the SBISS

1 Samuel 26 in the SBITS

1 Samuel 26 in the SBITS2

1 Samuel 26 in the SBITS3

1 Samuel 26 in the SBITS4

1 Samuel 26 in the SBIUS

1 Samuel 26 in the SBIVS

1 Samuel 26 in the SBT

1 Samuel 26 in the SBT1E

1 Samuel 26 in the SCHL

1 Samuel 26 in the SNT

1 Samuel 26 in the SUSU

1 Samuel 26 in the SUSU2

1 Samuel 26 in the SYNO

1 Samuel 26 in the TBIAOTANT

1 Samuel 26 in the TBT1E

1 Samuel 26 in the TBT1E2

1 Samuel 26 in the TFTIP

1 Samuel 26 in the TFTU

1 Samuel 26 in the TGNTATF3T

1 Samuel 26 in the THAI

1 Samuel 26 in the TNFD

1 Samuel 26 in the TNT

1 Samuel 26 in the TNTIK

1 Samuel 26 in the TNTIL

1 Samuel 26 in the TNTIN

1 Samuel 26 in the TNTIP

1 Samuel 26 in the TNTIZ

1 Samuel 26 in the TOMA

1 Samuel 26 in the TTENT

1 Samuel 26 in the UBG

1 Samuel 26 in the UGV

1 Samuel 26 in the UGV2

1 Samuel 26 in the UGV3

1 Samuel 26 in the VBL

1 Samuel 26 in the VDCC

1 Samuel 26 in the YALU

1 Samuel 26 in the YAPE

1 Samuel 26 in the YBVTP

1 Samuel 26 in the ZBP