1 Thessalonians 4 (BOKCV)
1 Hatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Yesu kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo. 2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Yesu. 3 Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, 4 ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, 5 si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. 6 Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. 7 Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu. 8 Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu. 9 Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. 10 Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda. 11 Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza, 12 ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote. 13 Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. 14 Kwa kuwa tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake. 15 Kulingana na neno la Bwana mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia waliolala mauti. 16 Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Kristo watafufuka kwanza. 17 Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18 Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.
In Other Versions
1 Thessalonians 4 in the ANGEFD
1 Thessalonians 4 in the ANTPNG2D
1 Thessalonians 4 in the BBPNG
1 Thessalonians 4 in the BBT1E
1 Thessalonians 4 in the BNTABOOT
1 Thessalonians 4 in the BNTLV
1 Thessalonians 4 in the BOATCB
1 Thessalonians 4 in the BOATCB2
1 Thessalonians 4 in the BOBCV
1 Thessalonians 4 in the BOCNT
1 Thessalonians 4 in the BOECS
1 Thessalonians 4 in the BOGWICC
1 Thessalonians 4 in the BOHCB
1 Thessalonians 4 in the BOHCV
1 Thessalonians 4 in the BOHLNT
1 Thessalonians 4 in the BOHNTLTAL
1 Thessalonians 4 in the BOICB
1 Thessalonians 4 in the BOILNTAP
1 Thessalonians 4 in the BOITCV
1 Thessalonians 4 in the BOKCV2
1 Thessalonians 4 in the BOKHWOG
1 Thessalonians 4 in the BOKSSV
1 Thessalonians 4 in the BOLCB
1 Thessalonians 4 in the BOLCB2
1 Thessalonians 4 in the BOMCV
1 Thessalonians 4 in the BONAV
1 Thessalonians 4 in the BONCB
1 Thessalonians 4 in the BONLT
1 Thessalonians 4 in the BONUT2
1 Thessalonians 4 in the BOPLNT
1 Thessalonians 4 in the BOSCB
1 Thessalonians 4 in the BOSNC
1 Thessalonians 4 in the BOTLNT
1 Thessalonians 4 in the BOVCB
1 Thessalonians 4 in the BOYCB
1 Thessalonians 4 in the DGDNT
1 Thessalonians 4 in the GGMNT
1 Thessalonians 4 in the IRVM2
1 Thessalonians 4 in the IRVT2
1 Thessalonians 4 in the KBT1ETNIK
1 Thessalonians 4 in the MKNFD
1 Thessalonians 4 in the MRS1T
1 Thessalonians 4 in the NBVTP
1 Thessalonians 4 in the NIV11
1 Thessalonians 4 in the PDDPT
1 Thessalonians 4 in the SBIAS
1 Thessalonians 4 in the SBIBS
1 Thessalonians 4 in the SBIBS2
1 Thessalonians 4 in the SBICS
1 Thessalonians 4 in the SBIDS
1 Thessalonians 4 in the SBIGS
1 Thessalonians 4 in the SBIHS
1 Thessalonians 4 in the SBIIS
1 Thessalonians 4 in the SBIIS2
1 Thessalonians 4 in the SBIIS3
1 Thessalonians 4 in the SBIKS
1 Thessalonians 4 in the SBIKS2
1 Thessalonians 4 in the SBIMS
1 Thessalonians 4 in the SBIOS
1 Thessalonians 4 in the SBIPS
1 Thessalonians 4 in the SBISS
1 Thessalonians 4 in the SBITS
1 Thessalonians 4 in the SBITS2
1 Thessalonians 4 in the SBITS3
1 Thessalonians 4 in the SBITS4
1 Thessalonians 4 in the SBIUS
1 Thessalonians 4 in the SBIVS
1 Thessalonians 4 in the SBT1E
1 Thessalonians 4 in the SUSU2
1 Thessalonians 4 in the TBIAOTANT
1 Thessalonians 4 in the TBT1E
1 Thessalonians 4 in the TBT1E2
1 Thessalonians 4 in the TFTIP
1 Thessalonians 4 in the TGNTATF3T
1 Thessalonians 4 in the TNTIK
1 Thessalonians 4 in the TNTIL
1 Thessalonians 4 in the TNTIN
1 Thessalonians 4 in the TNTIP
1 Thessalonians 4 in the TNTIZ
1 Thessalonians 4 in the TTENT