2 Chronicles 26 (BOKCV)
1 Kisha watu wote wa Yuda wakamtwaa Uzia, aliyekuwa na umri wa miaka kumi na sita, nao wakamfanya mfalme mahali pa Amazia baba yake. 2 Ndiye alijenga upya Elathi kuirudisha kwa Yuda baada ya Amazia kulala pamoja na baba zake. 3 Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka hamsini na miwili. Mama yake aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 4 Akatenda yaliyo mema machoni pa Bwana, kama Amazia baba yake alivyofanya. 5 Akamtafuta Mungu katika siku za Zekaria, aliyemwelekeza kumcha Mungu. Wakati wote alipomtafuta BWANA, Mungu alimfanikisha. 6 Alipigana vita dhidi ya Wafilisti na kubomoa kuta za Gathi, Yabne na Ashdodi. Kisha akajenga upya miji karibu na Ashdodi na mahali pengine katikati ya Wafilisti. 7 Mungu akamsaidia dhidi ya Wafilisti na dhidi ya Waarabu walioishi Gur-Baali na dhidi ya Wameuni. 8 Waamoni wakamletea Uzia ushuru, umaarufu wake ukaenea hadi kwenye mpaka wa Misri, kwa sababu alikuwa amekuwa na nguvu sana. 9 Uzia akajenga minara huko Yerusalemu katika Lango la Pembeni, katika Lango la Bondeni na katika pembe, mahali kuta zikutanapo, kisha akaijengea ngome. 10 Akajenga pia minara jangwani na kuchimba visima vingi vya maji, kwa sababu alikuwa na mifugo mingi chini ya vilimani na kwenye nchi tambarare. Alikuwa na watu wanaofanya kazi katika mashamba yake na kwenye mashamba yake ya mizabibu huko vilimani na katika ardhi zenye rutuba, kwa kuwa aliupenda udongo. 11 Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi lililofunzwa vizuri, lililokuwa tayari kwenda vitani kwa vikosi kufuatana na idadi yao kama walivyokusanywa na Yeieli mwandishi na Maaseya msimamizi chini ya maelekezo ya Hanania, mmojawapo wa maafisa wa mfalme. 12 Idadi yote ya viongozi wa jamaa waliowaongoza hawa wapiganaji walikuwa 2,600. 13 Chini ya uongozi wao kulikuwa na jeshi la askari 307,500 watu waliofundishwa kwa ajili ya vita, jeshi lenye nguvu la kumsaidia mfalme dhidi ya adui zake. 14 Uzia akalipatia jeshi lote ngao, mikuki, chapeo, dirii, pinde na mawe ya kombeo. 15 Huko Yerusalemu watu wenye utaalamu mkubwa wakatengeneza mitambo iliyotumika katika minara na kwenye pembe za ulinzi ili kurusha mishale na kuvurumisha mawe makubwa. Sifa zake zikaenea mbali sana kwa sababu alisaidiwa mno mpaka akawa na nguvu sana. 16 Lakini baada ya Uzia kuwa na nguvu sana, majivuno yake yakamsababishia kuanguka. Alikosa uaminifu kwa BWANA Mungu wake, naye akaingia hekaluni mwa BWANA ili afukize uvumba kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba. 17 Azaria kuhani akiwa pamoja na makuhani wengine themanini wa BWANA wenye ujasiri wakamfuata huko ndani. 18 Wakamkabili na kumwambia, “Siyo sawa kwako, Uzia, kumfukizia BWANA uvumba. Hiyo ni kazi ya makuhani, wazao wa Aroni, ambao wamewekwa wakfu ili kufukiza uvumba. Ondoka mahali patakatifu, kwa kuwa umekosa uaminifu nawe hutaheshimiwa na BWANA.” 19 Uzia, ambaye alikuwa na chetezo mkononi mwake tayari kufukiza uvumba, akakasirika. Alipokuwa anawaghadhibikia makuhani mbele ya madhabahu ya kufukizia uvumba katika Hekalu la BWANA, ukoma ukamtokea penye kipaji chake cha uso. 20 Azaria kuhani mkuu pamoja na makuhani wengine wote walipomtazama wakaona kwamba alikuwa na ukoma penye kipaji chake cha uso wakaharakisha kumtoa nje. Naam, hata yeye mwenyewe alikuwa anatamani kuondoka kwa sababu BWANA alikuwa amempiga. 21 Mfalme Uzia alikuwa na ukoma mpaka siku ya kufa kwake. Akatengwa katika nyumba ya pekee akiwa mwenye ukoma, naye akawa ametengwa kutoka Hekalu la BWANA. Yothamu mwanawe akawa msimamizi wa jumba la mfalme, pia akawaongoza watu wa nchi. 22 Matukio mengine ya utawala wa Uzia, kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yameandikwa na nabii Isaya mwana wa Amozi. 23 Uzia akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa karibu nao katika shamba la kuzikia lililokuwa mali ya wafalme, kwa kuwa watu walisema, “Alikuwa na ukoma.” Yothamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
In Other Versions
2 Chronicles 26 in the ANGEFD
2 Chronicles 26 in the ANTPNG2D
2 Chronicles 26 in the AS21
2 Chronicles 26 in the BAGH
2 Chronicles 26 in the BBPNG
2 Chronicles 26 in the BBT1E
2 Chronicles 26 in the BDS
2 Chronicles 26 in the BEV
2 Chronicles 26 in the BHAD
2 Chronicles 26 in the BIB
2 Chronicles 26 in the BLPT
2 Chronicles 26 in the BNT
2 Chronicles 26 in the BNTABOOT
2 Chronicles 26 in the BNTLV
2 Chronicles 26 in the BOATCB
2 Chronicles 26 in the BOATCB2
2 Chronicles 26 in the BOBCV
2 Chronicles 26 in the BOCNT
2 Chronicles 26 in the BOECS
2 Chronicles 26 in the BOGWICC
2 Chronicles 26 in the BOHCB
2 Chronicles 26 in the BOHCV
2 Chronicles 26 in the BOHLNT
2 Chronicles 26 in the BOHNTLTAL
2 Chronicles 26 in the BOICB
2 Chronicles 26 in the BOILNTAP
2 Chronicles 26 in the BOITCV
2 Chronicles 26 in the BOKCV2
2 Chronicles 26 in the BOKHWOG
2 Chronicles 26 in the BOKSSV
2 Chronicles 26 in the BOLCB
2 Chronicles 26 in the BOLCB2
2 Chronicles 26 in the BOMCV
2 Chronicles 26 in the BONAV
2 Chronicles 26 in the BONCB
2 Chronicles 26 in the BONLT
2 Chronicles 26 in the BONUT2
2 Chronicles 26 in the BOPLNT
2 Chronicles 26 in the BOSCB
2 Chronicles 26 in the BOSNC
2 Chronicles 26 in the BOTLNT
2 Chronicles 26 in the BOVCB
2 Chronicles 26 in the BOYCB
2 Chronicles 26 in the BPBB
2 Chronicles 26 in the BPH
2 Chronicles 26 in the BSB
2 Chronicles 26 in the CCB
2 Chronicles 26 in the CUV
2 Chronicles 26 in the CUVS
2 Chronicles 26 in the DBT
2 Chronicles 26 in the DGDNT
2 Chronicles 26 in the DHNT
2 Chronicles 26 in the DNT
2 Chronicles 26 in the ELBE
2 Chronicles 26 in the EMTV
2 Chronicles 26 in the ESV
2 Chronicles 26 in the FBV
2 Chronicles 26 in the FEB
2 Chronicles 26 in the GGMNT
2 Chronicles 26 in the GNT
2 Chronicles 26 in the HARY
2 Chronicles 26 in the HNT
2 Chronicles 26 in the IRVA
2 Chronicles 26 in the IRVB
2 Chronicles 26 in the IRVG
2 Chronicles 26 in the IRVH
2 Chronicles 26 in the IRVK
2 Chronicles 26 in the IRVM
2 Chronicles 26 in the IRVM2
2 Chronicles 26 in the IRVO
2 Chronicles 26 in the IRVP
2 Chronicles 26 in the IRVT
2 Chronicles 26 in the IRVT2
2 Chronicles 26 in the IRVU
2 Chronicles 26 in the ISVN
2 Chronicles 26 in the JSNT
2 Chronicles 26 in the KAPI
2 Chronicles 26 in the KBT1ETNIK
2 Chronicles 26 in the KBV
2 Chronicles 26 in the KJV
2 Chronicles 26 in the KNFD
2 Chronicles 26 in the LBA
2 Chronicles 26 in the LBLA
2 Chronicles 26 in the LNT
2 Chronicles 26 in the LSV
2 Chronicles 26 in the MAAL
2 Chronicles 26 in the MBV
2 Chronicles 26 in the MBV2
2 Chronicles 26 in the MHNT
2 Chronicles 26 in the MKNFD
2 Chronicles 26 in the MNG
2 Chronicles 26 in the MNT
2 Chronicles 26 in the MNT2
2 Chronicles 26 in the MRS1T
2 Chronicles 26 in the NAA
2 Chronicles 26 in the NASB
2 Chronicles 26 in the NBLA
2 Chronicles 26 in the NBS
2 Chronicles 26 in the NBVTP
2 Chronicles 26 in the NET2
2 Chronicles 26 in the NIV11
2 Chronicles 26 in the NNT
2 Chronicles 26 in the NNT2
2 Chronicles 26 in the NNT3
2 Chronicles 26 in the PDDPT
2 Chronicles 26 in the PFNT
2 Chronicles 26 in the RMNT
2 Chronicles 26 in the SBIAS
2 Chronicles 26 in the SBIBS
2 Chronicles 26 in the SBIBS2
2 Chronicles 26 in the SBICS
2 Chronicles 26 in the SBIDS
2 Chronicles 26 in the SBIGS
2 Chronicles 26 in the SBIHS
2 Chronicles 26 in the SBIIS
2 Chronicles 26 in the SBIIS2
2 Chronicles 26 in the SBIIS3
2 Chronicles 26 in the SBIKS
2 Chronicles 26 in the SBIKS2
2 Chronicles 26 in the SBIMS
2 Chronicles 26 in the SBIOS
2 Chronicles 26 in the SBIPS
2 Chronicles 26 in the SBISS
2 Chronicles 26 in the SBITS
2 Chronicles 26 in the SBITS2
2 Chronicles 26 in the SBITS3
2 Chronicles 26 in the SBITS4
2 Chronicles 26 in the SBIUS
2 Chronicles 26 in the SBIVS
2 Chronicles 26 in the SBT
2 Chronicles 26 in the SBT1E
2 Chronicles 26 in the SCHL
2 Chronicles 26 in the SNT
2 Chronicles 26 in the SUSU
2 Chronicles 26 in the SUSU2
2 Chronicles 26 in the SYNO
2 Chronicles 26 in the TBIAOTANT
2 Chronicles 26 in the TBT1E
2 Chronicles 26 in the TBT1E2
2 Chronicles 26 in the TFTIP
2 Chronicles 26 in the TFTU
2 Chronicles 26 in the TGNTATF3T
2 Chronicles 26 in the THAI
2 Chronicles 26 in the TNFD
2 Chronicles 26 in the TNT
2 Chronicles 26 in the TNTIK
2 Chronicles 26 in the TNTIL
2 Chronicles 26 in the TNTIN
2 Chronicles 26 in the TNTIP
2 Chronicles 26 in the TNTIZ
2 Chronicles 26 in the TOMA
2 Chronicles 26 in the TTENT
2 Chronicles 26 in the UBG
2 Chronicles 26 in the UGV
2 Chronicles 26 in the UGV2
2 Chronicles 26 in the UGV3
2 Chronicles 26 in the VBL
2 Chronicles 26 in the VDCC
2 Chronicles 26 in the YALU
2 Chronicles 26 in the YAPE
2 Chronicles 26 in the YBVTP
2 Chronicles 26 in the ZBP