2 Chronicles 29 (BOKCV)

1 Hezekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka ishirini na tisa. Mama yake aliitwa Abiya binti Zekaria. 2 Akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA kama Daudi baba yake alivyofanya. 3 Katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa kwanza wa utawala wa alifungua milango ya Hekalu la BWANA, na kuikarabati. 4 Akawaingiza makuhani na Walawi ndani na kuwakutanisha katika uwanja upande wa mashariki 5 na kusema: “Nisikilizeni mimi, enyi Walawi! Jitakaseni nafsi zenu sasa, mkaitakase na nyumba ya BWANA, Mungu wa baba zenu. Ondoeni uchafu wote kutoka mahali patakatifu. 6 Baba zetu hawakuwa waaminifu, walifanya maovu machoni pa BWANA Mungu wetu na wakamwacha yeye. Wakageuza nyuso zao mbali na Maskani ya BWANA wakamgeuzia visogo vyao. 7 Pia walifunga milango ya ukumbi wa Hekalu na kuzima taa zake. Hawakufukiza uvumba wala kutoa sadaka yoyote ya kuteketezwa katika mahali patakatifu kwa Mungu wa Israeli. 8 Kwa hiyo, hasira ya BWANA ikashuka juu ya Yuda na Yerusalemu, naye akawa amewafanya kitu cha kutisha, cha kushangaza na kitu cha kufanyia mzaha kama mnavyoona kwa macho yenu wenyewe. 9 Hii ndiyo sababu baba zetu wameanguka kwa upanga na ndiyo sababu wana wetu na binti zetu, pia wake zetu wamekuwa mateka. 10 Sasa ninadhamiria moyoni mwangu kuweka Agano na BWANA, Mungu wa Israeli, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nasi. 11 Wanangu, basi msipuuze jambo hili sasa, kwa kuwa BWANA amewachagua ninyi msimame mbele zake na kumtumikia, mkawe watumishi wake na mkamfukizie uvumba.” 12 Ndipo Walawi wafuatao wakaanza kazi:Kutoka kwa Wakohathi,Mahathi mwana wa Amasai na Yoeli mwana wa Azaria;kutoka kwa Wamerari,Kishi mwana wa Abdi na Azaria mwana wa Yahaleleli;kutoka kwa Wagershoni,Yoa mwana wa Zima na Edeni mwana wa Yoa; 13 kutoka kwa wana wa Elisafani,Shimri na Yeieli;kutoka kwa wana wa Asafu,Zekaria na Matania; 14 kutoka kwa wana wa Hemani,Yehieli na Shimei;kutoka kwa wana wa Yeduthuni,Shemaya na Uzieli. 15 Walipomaliza kuwakusanya ndugu zao na kujiweka wakfu, wakaingia ndani ili kutakasa Hekalu la BWANA, kama vile mfalme alivyokuwa ameagiza, kwa kufuata neno la BWANA. 16 Makuhani wakaingia patakatifu pa Hekalu la BWANA ili kupatakasa. Wakatoa nje penye ua wa Hekalu la Mungu kila kitu kichafu walichokikuta kwenye Hekalu la BWANA. Walawi wakavichukua na kuvipeleka nje katika Bonde la Kidroni. 17 Walianza kazi ya utakaso siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza na kufikia siku ya nane ya mwezi huo wakawa wamefikia kwenye ukumbi wa BWANA. Kwa siku zingine nane wakalitakasa Hekalu lenyewe la BWANA wakakamilisha katika siku ya kumi na sita ya mwezi huo wa kwanza. 18 Kisha wakaingia ndani kwa Mfalme Hezekia kutoa habari na kusema: “Tumelitakasa Hekalu lote la BWANA, madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa pamoja na vyombo vyake vyote, meza ya kupanga mikate iliyowekwa wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote. 19 Tumeviandaa na kuvitakasa vyombo vyote vile ambavyo Mfalme Ahazi, kwa kukosa uaminifu kwake, aliviondoa wakati alipokuwa mfalme. Sasa viko mbele ya madhabahu ya BWANA.” 20 Ndipo Mfalme Hezekia akainuka asubuhi na mapema, akakusanya pamoja maafisa wa mji wakakwea hekaluni mwa BWANA. 21 Wakaleta mafahali saba, kondoo dume saba, wana-kondoo dume saba na mabeberu saba kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya ufalme, kwa ajili ya mahali patakatifu na kwa ajili ya Yuda. Mfalme akawaamuru makuhani, wazao wa Aroni, kuvitoa vitu hivyo sadaka katika madhabahu ya BWANA. 22 Hivyo wakachinja wale mafahali, nao makuhani wakachukua ile damu na kuinyunyiza kwenye madhabahu, halafu wakawachinja wale kondoo dume saba na kunyunyiza hiyo damu yao kwenye madhabahu, kisha wakawachinja wale wana-kondoo dume na kunyunyiza damu yao kwenye madhabahu. 23 Wale mabeberu waliokuwa kwa ajili ya sadaka ya dhambi wakaletwa mbele ya mfalme na kusanyiko nao wakaweka mikono yao juu hao mabeberu. 24 Ndipo makuhani wakawachinja hao mabeberu na kuweka damu yao kwenye madhabahu kwa ajili ya sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli yote, kwa sababu mfalme alikuwa ameamuru hiyo sadaka ya kuteketezwa na hiyo sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli yote. 25 Akawaweka Walawi kwenye Hekalu la BWANA wakiwa na matoazi, vinubi na zeze kama ilivyoagizwa na Daudi na Gadi mwonaji wa mfalme pamoja na nabii Nathani kwani hili lilikuwa limeamriwa na BWANA kupitia manabii wake. 26 Hivyo Walawi wakasimama tayari wakiwa na ala za uimbaji za Daudi na makuhani walikuwa na tarumbeta zao. 27 Hezekia akatoa amri ya kutoa sadaka ya kuteketezwa madhabahuni. Walipoanza kutoa sadaka, wakaanza pia kumwimbia BWANA pamoja na tarumbeta na zile ala za uimbaji za Daudi mfalme wa Israeli. 28 Kusanyiko lote wakaabudu kwa kusujudu, wakati waimbaji wakiwa wanaimba na wenye tarumbeta wakipiga tarumbeta zao. Yote haya yaliendelea mpaka walipomaliza kutoa ile dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa. 29 Kutoa sadaka kulipomalizika, mfalme na kila mtu aliyekuwepo pamoja naye wakapiga magoti na kuabudu. 30 Mfalme Hezekia na maafisa wake wakawaamuru Walawi kumsifu BWANA kwa maneno ya Daudi na ya Asafu mwonaji. Hivyo wakaimba sifa kwa furaha nao wakainamisha vichwa vyao na kuabudu. 31 Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu kwa BWANA. Njooni mlete dhabihu na sadaka za shukrani Hekaluni mwa BWANA.” Hivyo kusanyiko likaleta dhabihu na sadaka za shukrani, nao wote waliokuwa na mioyo ya hiari wakaleta sadaka za kuteketezwa. 32 Idadi ya sadaka za kuteketezwa zilizoletwa na kusanyiko zilikuwa mafahali sabini, kondoo dume 100 na wana-kondoo dume 200. Wote hawa walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa BWANA. 33 Wanyama waliowekwa wakfu kwa sadaka ya kuteketezwa walikuwa mafahali 600, pamoja na kondoo na mbuzi 3,000. 34 Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuweza kuchuna wale wanyama wote wa sadaka za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao Walawi wakawasaidia mpaka kazi ile ikakamilika na mpaka makuhani wengine walipowekwa wakfu, kwa kuwa Walawi walikuwa makini kujiweka wakfu kuliko walivyokuwa makuhani. 35 Kulikuwa na sadaka nyingi za kuteketezwa, pamoja na mafuta ya wanyama ya sadaka za amani na sadaka za kinywaji ambazo ziliambatana na sadaka za kuteketezwa.Kwa hiyo huduma ya Hekalu la BWANA ikarudishwa kwa upya. 36 Hezekia pamoja na watu wote wakafurahi kwa sababu ya lile Mungu alilolifanya kwa ajili ya watu wake, kwa kuwa lilitendeka papo hapo.

In Other Versions

2 Chronicles 29 in the ANGEFD

2 Chronicles 29 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 29 in the AS21

2 Chronicles 29 in the BAGH

2 Chronicles 29 in the BBPNG

2 Chronicles 29 in the BBT1E

2 Chronicles 29 in the BDS

2 Chronicles 29 in the BEV

2 Chronicles 29 in the BHAD

2 Chronicles 29 in the BIB

2 Chronicles 29 in the BLPT

2 Chronicles 29 in the BNT

2 Chronicles 29 in the BNTABOOT

2 Chronicles 29 in the BNTLV

2 Chronicles 29 in the BOATCB

2 Chronicles 29 in the BOATCB2

2 Chronicles 29 in the BOBCV

2 Chronicles 29 in the BOCNT

2 Chronicles 29 in the BOECS

2 Chronicles 29 in the BOGWICC

2 Chronicles 29 in the BOHCB

2 Chronicles 29 in the BOHCV

2 Chronicles 29 in the BOHLNT

2 Chronicles 29 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 29 in the BOICB

2 Chronicles 29 in the BOILNTAP

2 Chronicles 29 in the BOITCV

2 Chronicles 29 in the BOKCV2

2 Chronicles 29 in the BOKHWOG

2 Chronicles 29 in the BOKSSV

2 Chronicles 29 in the BOLCB

2 Chronicles 29 in the BOLCB2

2 Chronicles 29 in the BOMCV

2 Chronicles 29 in the BONAV

2 Chronicles 29 in the BONCB

2 Chronicles 29 in the BONLT

2 Chronicles 29 in the BONUT2

2 Chronicles 29 in the BOPLNT

2 Chronicles 29 in the BOSCB

2 Chronicles 29 in the BOSNC

2 Chronicles 29 in the BOTLNT

2 Chronicles 29 in the BOVCB

2 Chronicles 29 in the BOYCB

2 Chronicles 29 in the BPBB

2 Chronicles 29 in the BPH

2 Chronicles 29 in the BSB

2 Chronicles 29 in the CCB

2 Chronicles 29 in the CUV

2 Chronicles 29 in the CUVS

2 Chronicles 29 in the DBT

2 Chronicles 29 in the DGDNT

2 Chronicles 29 in the DHNT

2 Chronicles 29 in the DNT

2 Chronicles 29 in the ELBE

2 Chronicles 29 in the EMTV

2 Chronicles 29 in the ESV

2 Chronicles 29 in the FBV

2 Chronicles 29 in the FEB

2 Chronicles 29 in the GGMNT

2 Chronicles 29 in the GNT

2 Chronicles 29 in the HARY

2 Chronicles 29 in the HNT

2 Chronicles 29 in the IRVA

2 Chronicles 29 in the IRVB

2 Chronicles 29 in the IRVG

2 Chronicles 29 in the IRVH

2 Chronicles 29 in the IRVK

2 Chronicles 29 in the IRVM

2 Chronicles 29 in the IRVM2

2 Chronicles 29 in the IRVO

2 Chronicles 29 in the IRVP

2 Chronicles 29 in the IRVT

2 Chronicles 29 in the IRVT2

2 Chronicles 29 in the IRVU

2 Chronicles 29 in the ISVN

2 Chronicles 29 in the JSNT

2 Chronicles 29 in the KAPI

2 Chronicles 29 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 29 in the KBV

2 Chronicles 29 in the KJV

2 Chronicles 29 in the KNFD

2 Chronicles 29 in the LBA

2 Chronicles 29 in the LBLA

2 Chronicles 29 in the LNT

2 Chronicles 29 in the LSV

2 Chronicles 29 in the MAAL

2 Chronicles 29 in the MBV

2 Chronicles 29 in the MBV2

2 Chronicles 29 in the MHNT

2 Chronicles 29 in the MKNFD

2 Chronicles 29 in the MNG

2 Chronicles 29 in the MNT

2 Chronicles 29 in the MNT2

2 Chronicles 29 in the MRS1T

2 Chronicles 29 in the NAA

2 Chronicles 29 in the NASB

2 Chronicles 29 in the NBLA

2 Chronicles 29 in the NBS

2 Chronicles 29 in the NBVTP

2 Chronicles 29 in the NET2

2 Chronicles 29 in the NIV11

2 Chronicles 29 in the NNT

2 Chronicles 29 in the NNT2

2 Chronicles 29 in the NNT3

2 Chronicles 29 in the PDDPT

2 Chronicles 29 in the PFNT

2 Chronicles 29 in the RMNT

2 Chronicles 29 in the SBIAS

2 Chronicles 29 in the SBIBS

2 Chronicles 29 in the SBIBS2

2 Chronicles 29 in the SBICS

2 Chronicles 29 in the SBIDS

2 Chronicles 29 in the SBIGS

2 Chronicles 29 in the SBIHS

2 Chronicles 29 in the SBIIS

2 Chronicles 29 in the SBIIS2

2 Chronicles 29 in the SBIIS3

2 Chronicles 29 in the SBIKS

2 Chronicles 29 in the SBIKS2

2 Chronicles 29 in the SBIMS

2 Chronicles 29 in the SBIOS

2 Chronicles 29 in the SBIPS

2 Chronicles 29 in the SBISS

2 Chronicles 29 in the SBITS

2 Chronicles 29 in the SBITS2

2 Chronicles 29 in the SBITS3

2 Chronicles 29 in the SBITS4

2 Chronicles 29 in the SBIUS

2 Chronicles 29 in the SBIVS

2 Chronicles 29 in the SBT

2 Chronicles 29 in the SBT1E

2 Chronicles 29 in the SCHL

2 Chronicles 29 in the SNT

2 Chronicles 29 in the SUSU

2 Chronicles 29 in the SUSU2

2 Chronicles 29 in the SYNO

2 Chronicles 29 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 29 in the TBT1E

2 Chronicles 29 in the TBT1E2

2 Chronicles 29 in the TFTIP

2 Chronicles 29 in the TFTU

2 Chronicles 29 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 29 in the THAI

2 Chronicles 29 in the TNFD

2 Chronicles 29 in the TNT

2 Chronicles 29 in the TNTIK

2 Chronicles 29 in the TNTIL

2 Chronicles 29 in the TNTIN

2 Chronicles 29 in the TNTIP

2 Chronicles 29 in the TNTIZ

2 Chronicles 29 in the TOMA

2 Chronicles 29 in the TTENT

2 Chronicles 29 in the UBG

2 Chronicles 29 in the UGV

2 Chronicles 29 in the UGV2

2 Chronicles 29 in the UGV3

2 Chronicles 29 in the VBL

2 Chronicles 29 in the VDCC

2 Chronicles 29 in the YALU

2 Chronicles 29 in the YAPE

2 Chronicles 29 in the YBVTP

2 Chronicles 29 in the ZBP