2 Chronicles 36 (BOKCV)

1 Watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia na kumfanya mfalme mahali pa baba yake huko Yerusalemu. 2 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, akatawala huko Yerusalemu kwa miezi mitatu. 3 Mfalme wa Misri akamwondoa madarakani huko Yerusalemu na akatoza Yuda kodi ya talanta 100 za fedha na talanta moja ya dhahabu. 4 Mfalme wa Misri akamweka Eliakimu, nduguye Yehoahazi, kuwa mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu na kubadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu. Lakini Neko akamchukua Yehoahazi, Nduguye Eliakimu akampeleka Misri. 5 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni pa BWANA Mungu wake. 6 Nebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli. 7 Nebukadneza akachukua pia vyombo kutoka Hekalu la BWANA na kuviweka katika hekalu lake huko Babeli. 8 Matukio mengine ya utawala wa Yehoyakimu, machukizo aliyoyafanya na yote yaliyoonekana dhidi yake, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda. Naye Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake. 9 Yehoyakini alikuwa na miaka kumi na minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miezi mitatu na siku kumi. Akafanya yaliyo maovu machoni pa BWANA. 10 Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu, nao wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka Hekalu la BWANA. Naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu. 11 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. 12 Alifanya maovu machoni pa BWANA Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la BWANA. 13 Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukia BWANA, Mungu wa Israeli. 14 Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la BWANA alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu. 15 BWANA, Mungu wa baba zao, akawapelekea neno kupitia wajumbe wake tena na tena, kwa sababu alikuwa anawahurumia watu wake pamoja na mahali pa maskani yake. 16 Lakini waliwadhihaki wajumbe wa BWANA wakayadharau maneno yake na kuwacheka manabii wake mpaka ghadhabu ya BWANA ikawa kubwa dhidi ya watu wake na hakukuwa na namna ya kuituliza. 17 Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza. 18 Akavichukua kwenda Babeli vyombo vyote kutoka Hekalu la Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za Hekalu la BWANA pamoja na hazina za mfalme na za maafisa wake. 19 Wakalichoma Hekalu la Mungu na kuzibomoa kuta za Yerusalemu, wakachoma moto majumba yote ya kifalme na kuharibu kila kitu chake cha thamani. 20 Wale watu walionusurika kuuawa kwa upanga wakachukuliwa kwenda uhamishoni Babeli. Nao wakawa watumishi wake na wa wanawe mpaka wakati wa utawala wa ufalme wa Uajemi ulifika. 21 Nchi ikaendelea kufurahia pumziko lake la Sabato, wakati wote wa kufanywa kwake ukiwa ilipumzika mpaka ile miaka sabini ilipotimia katika kutimiza neno la BWANA lililonenwa na Yeremia. 22 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la BWANA lililosemwa na nabii Yeremia, BWANA aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi: 23 “Hili ndilo asemalo Koreshi mfalme wa Uajemi:“ ‘BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote duniani, na ameniagiza kumjengea Hekalu huko Yerusalemu katika Yuda. Yeyote wa watu wake miongoni mwenu, Mungu wake na awe pamoja naye, wacha huyo mtu na apande.’ ”

In Other Versions

2 Chronicles 36 in the ANGEFD

2 Chronicles 36 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 36 in the AS21

2 Chronicles 36 in the BAGH

2 Chronicles 36 in the BBPNG

2 Chronicles 36 in the BBT1E

2 Chronicles 36 in the BDS

2 Chronicles 36 in the BEV

2 Chronicles 36 in the BHAD

2 Chronicles 36 in the BIB

2 Chronicles 36 in the BLPT

2 Chronicles 36 in the BNT

2 Chronicles 36 in the BNTABOOT

2 Chronicles 36 in the BNTLV

2 Chronicles 36 in the BOATCB

2 Chronicles 36 in the BOATCB2

2 Chronicles 36 in the BOBCV

2 Chronicles 36 in the BOCNT

2 Chronicles 36 in the BOECS

2 Chronicles 36 in the BOGWICC

2 Chronicles 36 in the BOHCB

2 Chronicles 36 in the BOHCV

2 Chronicles 36 in the BOHLNT

2 Chronicles 36 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 36 in the BOICB

2 Chronicles 36 in the BOILNTAP

2 Chronicles 36 in the BOITCV

2 Chronicles 36 in the BOKCV2

2 Chronicles 36 in the BOKHWOG

2 Chronicles 36 in the BOKSSV

2 Chronicles 36 in the BOLCB

2 Chronicles 36 in the BOLCB2

2 Chronicles 36 in the BOMCV

2 Chronicles 36 in the BONAV

2 Chronicles 36 in the BONCB

2 Chronicles 36 in the BONLT

2 Chronicles 36 in the BONUT2

2 Chronicles 36 in the BOPLNT

2 Chronicles 36 in the BOSCB

2 Chronicles 36 in the BOSNC

2 Chronicles 36 in the BOTLNT

2 Chronicles 36 in the BOVCB

2 Chronicles 36 in the BOYCB

2 Chronicles 36 in the BPBB

2 Chronicles 36 in the BPH

2 Chronicles 36 in the BSB

2 Chronicles 36 in the CCB

2 Chronicles 36 in the CUV

2 Chronicles 36 in the CUVS

2 Chronicles 36 in the DBT

2 Chronicles 36 in the DGDNT

2 Chronicles 36 in the DHNT

2 Chronicles 36 in the DNT

2 Chronicles 36 in the ELBE

2 Chronicles 36 in the EMTV

2 Chronicles 36 in the ESV

2 Chronicles 36 in the FBV

2 Chronicles 36 in the FEB

2 Chronicles 36 in the GGMNT

2 Chronicles 36 in the GNT

2 Chronicles 36 in the HARY

2 Chronicles 36 in the HNT

2 Chronicles 36 in the IRVA

2 Chronicles 36 in the IRVB

2 Chronicles 36 in the IRVG

2 Chronicles 36 in the IRVH

2 Chronicles 36 in the IRVK

2 Chronicles 36 in the IRVM

2 Chronicles 36 in the IRVM2

2 Chronicles 36 in the IRVO

2 Chronicles 36 in the IRVP

2 Chronicles 36 in the IRVT

2 Chronicles 36 in the IRVT2

2 Chronicles 36 in the IRVU

2 Chronicles 36 in the ISVN

2 Chronicles 36 in the JSNT

2 Chronicles 36 in the KAPI

2 Chronicles 36 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 36 in the KBV

2 Chronicles 36 in the KJV

2 Chronicles 36 in the KNFD

2 Chronicles 36 in the LBA

2 Chronicles 36 in the LBLA

2 Chronicles 36 in the LNT

2 Chronicles 36 in the LSV

2 Chronicles 36 in the MAAL

2 Chronicles 36 in the MBV

2 Chronicles 36 in the MBV2

2 Chronicles 36 in the MHNT

2 Chronicles 36 in the MKNFD

2 Chronicles 36 in the MNG

2 Chronicles 36 in the MNT

2 Chronicles 36 in the MNT2

2 Chronicles 36 in the MRS1T

2 Chronicles 36 in the NAA

2 Chronicles 36 in the NASB

2 Chronicles 36 in the NBLA

2 Chronicles 36 in the NBS

2 Chronicles 36 in the NBVTP

2 Chronicles 36 in the NET2

2 Chronicles 36 in the NIV11

2 Chronicles 36 in the NNT

2 Chronicles 36 in the NNT2

2 Chronicles 36 in the NNT3

2 Chronicles 36 in the PDDPT

2 Chronicles 36 in the PFNT

2 Chronicles 36 in the RMNT

2 Chronicles 36 in the SBIAS

2 Chronicles 36 in the SBIBS

2 Chronicles 36 in the SBIBS2

2 Chronicles 36 in the SBICS

2 Chronicles 36 in the SBIDS

2 Chronicles 36 in the SBIGS

2 Chronicles 36 in the SBIHS

2 Chronicles 36 in the SBIIS

2 Chronicles 36 in the SBIIS2

2 Chronicles 36 in the SBIIS3

2 Chronicles 36 in the SBIKS

2 Chronicles 36 in the SBIKS2

2 Chronicles 36 in the SBIMS

2 Chronicles 36 in the SBIOS

2 Chronicles 36 in the SBIPS

2 Chronicles 36 in the SBISS

2 Chronicles 36 in the SBITS

2 Chronicles 36 in the SBITS2

2 Chronicles 36 in the SBITS3

2 Chronicles 36 in the SBITS4

2 Chronicles 36 in the SBIUS

2 Chronicles 36 in the SBIVS

2 Chronicles 36 in the SBT

2 Chronicles 36 in the SBT1E

2 Chronicles 36 in the SCHL

2 Chronicles 36 in the SNT

2 Chronicles 36 in the SUSU

2 Chronicles 36 in the SUSU2

2 Chronicles 36 in the SYNO

2 Chronicles 36 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 36 in the TBT1E

2 Chronicles 36 in the TBT1E2

2 Chronicles 36 in the TFTIP

2 Chronicles 36 in the TFTU

2 Chronicles 36 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 36 in the THAI

2 Chronicles 36 in the TNFD

2 Chronicles 36 in the TNT

2 Chronicles 36 in the TNTIK

2 Chronicles 36 in the TNTIL

2 Chronicles 36 in the TNTIN

2 Chronicles 36 in the TNTIP

2 Chronicles 36 in the TNTIZ

2 Chronicles 36 in the TOMA

2 Chronicles 36 in the TTENT

2 Chronicles 36 in the UBG

2 Chronicles 36 in the UGV

2 Chronicles 36 in the UGV2

2 Chronicles 36 in the UGV3

2 Chronicles 36 in the VBL

2 Chronicles 36 in the VDCC

2 Chronicles 36 in the YALU

2 Chronicles 36 in the YAPE

2 Chronicles 36 in the YBVTP

2 Chronicles 36 in the ZBP