2 Chronicles 5 (BOKCV)

1 Hivyo Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la BWANA, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu. 2 Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la BWANA kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 3 Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba. 4 Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano, 5 nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo, 6 naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa. 7 Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la BWANA hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. 8 Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea. 9 Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 10 Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo BWANA alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri. 11 Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao. 12 Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta. 13 Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru BWANA, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu BWANA wakisema:“Yeye ni mwema;upendo wake unadumu milele.”Ndipo Hekalu la BWANA likajazwa na wingu, 14 nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa BWANA ulijaza Hekalu la Mungu.

In Other Versions

2 Chronicles 5 in the ANGEFD

2 Chronicles 5 in the ANTPNG2D

2 Chronicles 5 in the AS21

2 Chronicles 5 in the BAGH

2 Chronicles 5 in the BBPNG

2 Chronicles 5 in the BBT1E

2 Chronicles 5 in the BDS

2 Chronicles 5 in the BEV

2 Chronicles 5 in the BHAD

2 Chronicles 5 in the BIB

2 Chronicles 5 in the BLPT

2 Chronicles 5 in the BNT

2 Chronicles 5 in the BNTABOOT

2 Chronicles 5 in the BNTLV

2 Chronicles 5 in the BOATCB

2 Chronicles 5 in the BOATCB2

2 Chronicles 5 in the BOBCV

2 Chronicles 5 in the BOCNT

2 Chronicles 5 in the BOECS

2 Chronicles 5 in the BOGWICC

2 Chronicles 5 in the BOHCB

2 Chronicles 5 in the BOHCV

2 Chronicles 5 in the BOHLNT

2 Chronicles 5 in the BOHNTLTAL

2 Chronicles 5 in the BOICB

2 Chronicles 5 in the BOILNTAP

2 Chronicles 5 in the BOITCV

2 Chronicles 5 in the BOKCV2

2 Chronicles 5 in the BOKHWOG

2 Chronicles 5 in the BOKSSV

2 Chronicles 5 in the BOLCB

2 Chronicles 5 in the BOLCB2

2 Chronicles 5 in the BOMCV

2 Chronicles 5 in the BONAV

2 Chronicles 5 in the BONCB

2 Chronicles 5 in the BONLT

2 Chronicles 5 in the BONUT2

2 Chronicles 5 in the BOPLNT

2 Chronicles 5 in the BOSCB

2 Chronicles 5 in the BOSNC

2 Chronicles 5 in the BOTLNT

2 Chronicles 5 in the BOVCB

2 Chronicles 5 in the BOYCB

2 Chronicles 5 in the BPBB

2 Chronicles 5 in the BPH

2 Chronicles 5 in the BSB

2 Chronicles 5 in the CCB

2 Chronicles 5 in the CUV

2 Chronicles 5 in the CUVS

2 Chronicles 5 in the DBT

2 Chronicles 5 in the DGDNT

2 Chronicles 5 in the DHNT

2 Chronicles 5 in the DNT

2 Chronicles 5 in the ELBE

2 Chronicles 5 in the EMTV

2 Chronicles 5 in the ESV

2 Chronicles 5 in the FBV

2 Chronicles 5 in the FEB

2 Chronicles 5 in the GGMNT

2 Chronicles 5 in the GNT

2 Chronicles 5 in the HARY

2 Chronicles 5 in the HNT

2 Chronicles 5 in the IRVA

2 Chronicles 5 in the IRVB

2 Chronicles 5 in the IRVG

2 Chronicles 5 in the IRVH

2 Chronicles 5 in the IRVK

2 Chronicles 5 in the IRVM

2 Chronicles 5 in the IRVM2

2 Chronicles 5 in the IRVO

2 Chronicles 5 in the IRVP

2 Chronicles 5 in the IRVT

2 Chronicles 5 in the IRVT2

2 Chronicles 5 in the IRVU

2 Chronicles 5 in the ISVN

2 Chronicles 5 in the JSNT

2 Chronicles 5 in the KAPI

2 Chronicles 5 in the KBT1ETNIK

2 Chronicles 5 in the KBV

2 Chronicles 5 in the KJV

2 Chronicles 5 in the KNFD

2 Chronicles 5 in the LBA

2 Chronicles 5 in the LBLA

2 Chronicles 5 in the LNT

2 Chronicles 5 in the LSV

2 Chronicles 5 in the MAAL

2 Chronicles 5 in the MBV

2 Chronicles 5 in the MBV2

2 Chronicles 5 in the MHNT

2 Chronicles 5 in the MKNFD

2 Chronicles 5 in the MNG

2 Chronicles 5 in the MNT

2 Chronicles 5 in the MNT2

2 Chronicles 5 in the MRS1T

2 Chronicles 5 in the NAA

2 Chronicles 5 in the NASB

2 Chronicles 5 in the NBLA

2 Chronicles 5 in the NBS

2 Chronicles 5 in the NBVTP

2 Chronicles 5 in the NET2

2 Chronicles 5 in the NIV11

2 Chronicles 5 in the NNT

2 Chronicles 5 in the NNT2

2 Chronicles 5 in the NNT3

2 Chronicles 5 in the PDDPT

2 Chronicles 5 in the PFNT

2 Chronicles 5 in the RMNT

2 Chronicles 5 in the SBIAS

2 Chronicles 5 in the SBIBS

2 Chronicles 5 in the SBIBS2

2 Chronicles 5 in the SBICS

2 Chronicles 5 in the SBIDS

2 Chronicles 5 in the SBIGS

2 Chronicles 5 in the SBIHS

2 Chronicles 5 in the SBIIS

2 Chronicles 5 in the SBIIS2

2 Chronicles 5 in the SBIIS3

2 Chronicles 5 in the SBIKS

2 Chronicles 5 in the SBIKS2

2 Chronicles 5 in the SBIMS

2 Chronicles 5 in the SBIOS

2 Chronicles 5 in the SBIPS

2 Chronicles 5 in the SBISS

2 Chronicles 5 in the SBITS

2 Chronicles 5 in the SBITS2

2 Chronicles 5 in the SBITS3

2 Chronicles 5 in the SBITS4

2 Chronicles 5 in the SBIUS

2 Chronicles 5 in the SBIVS

2 Chronicles 5 in the SBT

2 Chronicles 5 in the SBT1E

2 Chronicles 5 in the SCHL

2 Chronicles 5 in the SNT

2 Chronicles 5 in the SUSU

2 Chronicles 5 in the SUSU2

2 Chronicles 5 in the SYNO

2 Chronicles 5 in the TBIAOTANT

2 Chronicles 5 in the TBT1E

2 Chronicles 5 in the TBT1E2

2 Chronicles 5 in the TFTIP

2 Chronicles 5 in the TFTU

2 Chronicles 5 in the TGNTATF3T

2 Chronicles 5 in the THAI

2 Chronicles 5 in the TNFD

2 Chronicles 5 in the TNT

2 Chronicles 5 in the TNTIK

2 Chronicles 5 in the TNTIL

2 Chronicles 5 in the TNTIN

2 Chronicles 5 in the TNTIP

2 Chronicles 5 in the TNTIZ

2 Chronicles 5 in the TOMA

2 Chronicles 5 in the TTENT

2 Chronicles 5 in the UBG

2 Chronicles 5 in the UGV

2 Chronicles 5 in the UGV2

2 Chronicles 5 in the UGV3

2 Chronicles 5 in the VBL

2 Chronicles 5 in the VDCC

2 Chronicles 5 in the YALU

2 Chronicles 5 in the YAPE

2 Chronicles 5 in the YBVTP

2 Chronicles 5 in the ZBP