2 Samuel 19 (BOKCV)

1 Yoabu akaambiwa, “Mfalme analia na kumwombolezea Absalomu.” 2 Kwa jeshi lote, ushindi wa siku ile ukageuka kuwa maombolezo, kwa sababu siku ile vikosi vilisikia ikisemwa, “Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe.” 3 Siku ile watu wakaingia mjini kimya kama vile waingiavyo kwa aibu watu waliokimbia kutoka vitani. 4 Mfalme akafunika uso wake akalia kwa sauti, akisema, “Ee mwanangu Absalomu! Ee Absalomu, mwanangu, mwanangu!” 5 Kisha Yoabu akaingia ndani ya nyumba ya mfalme na kusema, “Leo umewaaibisha watu wako wote, waliookoa maisha yako, maisha ya wanao na binti zako, maisha ya wake zako na masuria wako. 6 Unawapenda wale wanaokuchukia, na unawachukia wale wanaokupenda. Leo umeonyesha wazi kwamba majemadari wako na watu wao hawana maana kwako. Naona kwamba ungefurahi kama Absalomu angekuwa hai leo na sisi sote tuwe tumekufa. 7 Sasa utoke nje ukawatie moyo watu wako. Naapa kwa BWANA kwamba ikiwa hutatoka nje, hakuna mtu atakayesalia pamoja nawe ifikapo leo jioni. Hii itakuwa mbaya zaidi kwako kuliko maafa yote yaliyokupata tangu ujana wako hadi sasa.” 8 Kwa hiyo mfalme akaondoka akaketi kitini pake penye lango. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia.Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani kwao. 9 Katika makabila yote ya Israeli, watu walikuwa wanabishana wao kwa wao, wakisema, “Mfalme alituokoa kutoka mikononi mwa adui zetu; ndiye alituokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti. Lakini sasa mfalme ameikimbia nchi kwa sababu ya Absalomu, 10 naye Absalomu, tuliyemtia mafuta atutawale, amekufa vitani. Basi mbona hamsemi lolote kuhusu kumrudisha mfalme?” 11 Mfalme Daudi akapeleka ujumbe huu kwa makuhani Sadoki na Abiathari, kusema: “Waulizeni wazee wa Yuda, ‘Kwa nini mwe wa mwisho kumrudisha mfalme katika jumba lake la kifalme, maadamu kile kinachosemwa katika Israeli yote kimemfikia mfalme katika makao yake? 12 Ninyi ni ndugu zangu, nyama yangu na damu yangu mwenyewe. Kwa hiyo kwa nini mwe wa mwisho kumrudisha mfalme?’ 13 Nanyi mwambieni Amasa, ‘Je, wewe si nyama yangu mwenyewe na damu yangu? Mungu na anishughulikie, tena kwa ukali, kama kuanzia sasa na kuendelea wewe si jemadari wa jeshi langu mahali pa Yoabu.’ ” 14 Aliipata mioyo ya watu wote wa Yuda kama vile walikuwa mtu mmoja. Wakapeleka ujumbe kwa mfalme, kusema, “Rudi, wewe na watu wako wote.” 15 Ndipo mfalme akarudi, akaenda hadi kufikia Mto Yordani.Basi watu wa Yuda walikuwa wamekuja mpaka Gilgali ili kutoka kwenda kumlaki mfalme na kumvusha Mto Yordani. 16 Shimei mwana wa Gera, wa kabila la Benyamini kutoka Bahurimu, akaharakisha kuteremka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki Mfalme Daudi. 17 Pamoja naye walikuwepo Wabenyamini elfu moja wakiwa wamefuatana na Siba, msimamizi wa nyumba ya Sauli, pia wanawe kumi na watano, na watumishi ishirini. Wakaharakisha kwenda Yordani, mahali mfalme alipokuwa. 18 Wakavuka kivuko ili kuwachukua watu wa nyumbani mwa mfalme ili kuwavusha na kufanya kila kitu alichotaka.Shimei mwana wa Gera alipovuka Yordani, akaanguka kifudifudi mbele ya mfalme, 19 na kumwambia, “Bwana wangu na asinihesabie hatia. Usikumbuke jinsi mtumishi wako alivyofanya kosa siku ile bwana wangu mfalme alipoondoka Yerusalemu. Mfalme aliondoe moyoni mwake. 20 Kwa maana mimi mtumishi wako najua nimefanya dhambi, lakini leo nimekuja hapa kama wa kwanza wa nyumba yote ya Yosefu kushuka na kumlaki bwana wangu mfalme.” 21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, Shimei hapaswi kuuawa kwa ajili ya hili? Alimlaani mpakwa mafuta wa BWANA.” 22 Daudi akajibu, “Mimi nina nini nanyi, enyi wana wa Seruya? Leo hii mmekuwa adui zangu! Je, leo kuna yeyote atakayeuawa katika Israeli? Je, mimi sijui kuwa leo ndimi mfalme katika Israeli yote?” 23 Basi mfalme akamwambia Shimei, “Hutakufa.” Naye mfalme akamwahidi kwa kiapo. 24 Pia Mefiboshethi mwana wa Sauli akashuka kwenda kumlaki mfalme. Hakuwa amenawa miguu wala kunyoa ndevu zake wala kufua nguo zake tangu siku mfalme alipoondoka Yerusalemu mpaka siku aliporudi ile salama. 25 Wakati alipotoka Yerusalemu kuja kumlaki mfalme, mfalme akamuuliza, “Mefiboshethi, kwa nini hukufuatana nami?” 26 Akasema, “Bwana wangu mfalme, maadamu mimi mtumishi wako ni kiwete, nilisema, ‘Nitandikiwe punda wangu, nimpande, ili niweze kwenda pamoja na mfalme.’ Lakini Siba mtumishi wangu akanisaliti. 27 Naye amemchongea mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme. Bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu, kwa hiyo fanya lolote linalokupendeza. 28 Wazao wote wa baba yangu hawastahili kitu kingine isipokuwa kifo kutoka kwa bwana wangu mfalme, lakini ulimpa mtumishi wako nafasi miongoni mwa wale waliokula mezani pako. Je, ninayo haki gani kumwomba mfalme zaidi ya hayo?” 29 Mfalme akamwambia, “Kwa nini useme zaidi? Naamuru wewe na Siba mgawanye mashamba.” 30 Mefiboshethi akamwambia mfalme, “Mruhusu achukue kila kitu, kwa kuwa sasa bwana wangu mfalme amerudi nyumbani salama.” 31 Barzilai, Mgileadi, pia akashuka kutoka Rogelimu ili kuvuka Yordani pamoja na mfalme na kumsindikiza kutoka huko. 32 Basi Barzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amempatia mfalme mahitaji wakati alipokuwa anaishi huko Mahanaimu, kwa kuwa alikuwa mtu tajiri sana. 33 Mfalme akamwambia Barzilai, “Vuka pamoja nami na ukae nami huko Yerusalemu, nami nitakupatia mahitaji yako.” 34 Lakini Barzilai akamjibu mfalme, “Je, nitaishi miaka mingine mingapi, hata nipande kwenda Yerusalemu pamoja na mfalme? 35 Sasa nina miaka themanini. Je, naweza kutofautisha kati ya lililo jema na lililo baya? Je, mtumishi wako anaweza kujua ladha ya kile anachokula au anachokunywa? Je, bado naweza kusikiliza sauti za waimbaji wa kiume na za wanawake? Kwa nini mtumishi wako aongeze mzigo kwa bwana wangu mfalme? 36 Mtumishi wako atavuka Yordani pamoja na mfalme kwa umbali mfupi tu, lakini kwa nini mfalme anizawadie kwa namna hii? 37 Mruhusu mtumishi wako arudi, ili mimi nikafie katika mji wangu mwenyewe karibu na kaburi la baba yangu na mama yangu. Lakini yupo hapa mtumishi wako Kimhamu. Mruhusu avuke pamoja na bwana wangu mfalme. Mtendee lolote linalokupendeza.” 38 Mfalme akamwambia Barzilai, “Kimhamu atavuka Yordani pamoja nami, nami nitamtendea lolote litakalokupendeza. Nawe kitu chochote unachotaka kutoka kwangu nitakutendea.” 39 Kwa hiyo watu wote wakavuka Yordani, kisha mfalme akavuka. Mfalme akambusu Barzilai na kumbariki; Barzilai akarudi nyumbani kwake. 40 Mfalme alipovuka kwenda Gilgali, Kimhamu akavuka pamoja naye. Vikosi vyote vya Yuda na nusu ya vikosi vya Israeli vilimvusha mfalme. 41 Baada ya kitambo kidogo watu wote wa Israeli wakaja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemrudisha mfalme kwa siri bila kutushirikisha, na kumvusha ngʼambo ya Yordani, yeye na nyumba yake, pamoja na watu wake wote?” 42 Watu wote wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Tulifanya hivi kwa sababu mfalme ni jamaa yetu wa karibu. Kwa nini mnakasirikia jambo hili? Je, tumekula kitu chochote cha mfalme? Je, tumejichukulia kitu chochote kwa ajili yetu wenyewe?” 43 Ndipo watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, “Tunayo haki mara kumi kwa mfalme; sisi tunahusika zaidi na Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mnatudharau? Je, hatukuwa wa kwanza kuzungumza kuhusu kumrudisha mfalme nyumbani?”Lakini watu wa Yuda wakajibu kwa ukali hata zaidi kuliko watu wa Israeli.

In Other Versions

2 Samuel 19 in the ANGEFD

2 Samuel 19 in the ANTPNG2D

2 Samuel 19 in the AS21

2 Samuel 19 in the BAGH

2 Samuel 19 in the BBPNG

2 Samuel 19 in the BBT1E

2 Samuel 19 in the BDS

2 Samuel 19 in the BEV

2 Samuel 19 in the BHAD

2 Samuel 19 in the BIB

2 Samuel 19 in the BLPT

2 Samuel 19 in the BNT

2 Samuel 19 in the BNTABOOT

2 Samuel 19 in the BNTLV

2 Samuel 19 in the BOATCB

2 Samuel 19 in the BOATCB2

2 Samuel 19 in the BOBCV

2 Samuel 19 in the BOCNT

2 Samuel 19 in the BOECS

2 Samuel 19 in the BOGWICC

2 Samuel 19 in the BOHCB

2 Samuel 19 in the BOHCV

2 Samuel 19 in the BOHLNT

2 Samuel 19 in the BOHNTLTAL

2 Samuel 19 in the BOICB

2 Samuel 19 in the BOILNTAP

2 Samuel 19 in the BOITCV

2 Samuel 19 in the BOKCV2

2 Samuel 19 in the BOKHWOG

2 Samuel 19 in the BOKSSV

2 Samuel 19 in the BOLCB

2 Samuel 19 in the BOLCB2

2 Samuel 19 in the BOMCV

2 Samuel 19 in the BONAV

2 Samuel 19 in the BONCB

2 Samuel 19 in the BONLT

2 Samuel 19 in the BONUT2

2 Samuel 19 in the BOPLNT

2 Samuel 19 in the BOSCB

2 Samuel 19 in the BOSNC

2 Samuel 19 in the BOTLNT

2 Samuel 19 in the BOVCB

2 Samuel 19 in the BOYCB

2 Samuel 19 in the BPBB

2 Samuel 19 in the BPH

2 Samuel 19 in the BSB

2 Samuel 19 in the CCB

2 Samuel 19 in the CUV

2 Samuel 19 in the CUVS

2 Samuel 19 in the DBT

2 Samuel 19 in the DGDNT

2 Samuel 19 in the DHNT

2 Samuel 19 in the DNT

2 Samuel 19 in the ELBE

2 Samuel 19 in the EMTV

2 Samuel 19 in the ESV

2 Samuel 19 in the FBV

2 Samuel 19 in the FEB

2 Samuel 19 in the GGMNT

2 Samuel 19 in the GNT

2 Samuel 19 in the HARY

2 Samuel 19 in the HNT

2 Samuel 19 in the IRVA

2 Samuel 19 in the IRVB

2 Samuel 19 in the IRVG

2 Samuel 19 in the IRVH

2 Samuel 19 in the IRVK

2 Samuel 19 in the IRVM

2 Samuel 19 in the IRVM2

2 Samuel 19 in the IRVO

2 Samuel 19 in the IRVP

2 Samuel 19 in the IRVT

2 Samuel 19 in the IRVT2

2 Samuel 19 in the IRVU

2 Samuel 19 in the ISVN

2 Samuel 19 in the JSNT

2 Samuel 19 in the KAPI

2 Samuel 19 in the KBT1ETNIK

2 Samuel 19 in the KBV

2 Samuel 19 in the KJV

2 Samuel 19 in the KNFD

2 Samuel 19 in the LBA

2 Samuel 19 in the LBLA

2 Samuel 19 in the LNT

2 Samuel 19 in the LSV

2 Samuel 19 in the MAAL

2 Samuel 19 in the MBV

2 Samuel 19 in the MBV2

2 Samuel 19 in the MHNT

2 Samuel 19 in the MKNFD

2 Samuel 19 in the MNG

2 Samuel 19 in the MNT

2 Samuel 19 in the MNT2

2 Samuel 19 in the MRS1T

2 Samuel 19 in the NAA

2 Samuel 19 in the NASB

2 Samuel 19 in the NBLA

2 Samuel 19 in the NBS

2 Samuel 19 in the NBVTP

2 Samuel 19 in the NET2

2 Samuel 19 in the NIV11

2 Samuel 19 in the NNT

2 Samuel 19 in the NNT2

2 Samuel 19 in the NNT3

2 Samuel 19 in the PDDPT

2 Samuel 19 in the PFNT

2 Samuel 19 in the RMNT

2 Samuel 19 in the SBIAS

2 Samuel 19 in the SBIBS

2 Samuel 19 in the SBIBS2

2 Samuel 19 in the SBICS

2 Samuel 19 in the SBIDS

2 Samuel 19 in the SBIGS

2 Samuel 19 in the SBIHS

2 Samuel 19 in the SBIIS

2 Samuel 19 in the SBIIS2

2 Samuel 19 in the SBIIS3

2 Samuel 19 in the SBIKS

2 Samuel 19 in the SBIKS2

2 Samuel 19 in the SBIMS

2 Samuel 19 in the SBIOS

2 Samuel 19 in the SBIPS

2 Samuel 19 in the SBISS

2 Samuel 19 in the SBITS

2 Samuel 19 in the SBITS2

2 Samuel 19 in the SBITS3

2 Samuel 19 in the SBITS4

2 Samuel 19 in the SBIUS

2 Samuel 19 in the SBIVS

2 Samuel 19 in the SBT

2 Samuel 19 in the SBT1E

2 Samuel 19 in the SCHL

2 Samuel 19 in the SNT

2 Samuel 19 in the SUSU

2 Samuel 19 in the SUSU2

2 Samuel 19 in the SYNO

2 Samuel 19 in the TBIAOTANT

2 Samuel 19 in the TBT1E

2 Samuel 19 in the TBT1E2

2 Samuel 19 in the TFTIP

2 Samuel 19 in the TFTU

2 Samuel 19 in the TGNTATF3T

2 Samuel 19 in the THAI

2 Samuel 19 in the TNFD

2 Samuel 19 in the TNT

2 Samuel 19 in the TNTIK

2 Samuel 19 in the TNTIL

2 Samuel 19 in the TNTIN

2 Samuel 19 in the TNTIP

2 Samuel 19 in the TNTIZ

2 Samuel 19 in the TOMA

2 Samuel 19 in the TTENT

2 Samuel 19 in the UBG

2 Samuel 19 in the UGV

2 Samuel 19 in the UGV2

2 Samuel 19 in the UGV3

2 Samuel 19 in the VBL

2 Samuel 19 in the VDCC

2 Samuel 19 in the YALU

2 Samuel 19 in the YAPE

2 Samuel 19 in the YBVTP

2 Samuel 19 in the ZBP