2 Samuel 5 (BOKCV)
1 Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye BWANA alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ” 3 Wazee wote wa Israeli wakamwendea Mfalme Daudi huko Hebroni, mfalme akafanya mapatano nao huko Hebroni mbele za BWANA, nao wakamtia Daudi mafuta kuwa mfalme wa Israeli. 4 Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. 5 Huko Hebroni alitawala Yuda kwa miaka saba na miezi sita, na katika Yerusalemu alitawala Israeli yote na Yuda kwa miaka thelathini na mitatu. 6 Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.” 7 Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi. 8 Siku ile, Daudi akasema, “Yeyote ambaye atawashinda Wayebusi, atatumia huo mfereji kuwafikia hao ‘viwete na vipofu’ ambao ni adui za Daudi.” Ndiyo sababu wanasema, “ ‘Vipofu na viwete’ hawataingia kwenye jumba la ufalme.” 9 Ndipo Daudi akafanya makao ndani ya ngome na kuiita Mji wa Daudi. Akajenga eneo linalozunguka kuanzia Milo kuelekea ndani. 10 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye. 11 Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, maseremala na waashi, nao wakajenga jumba la kifalme kwa ajili ya Daudi. 12 Naye Daudi akafahamu kuwa BWANA amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na ameinua ufalme wake kwa ajili ya Israeli, watu wake. 13 Baada ya Daudi kuondoka Hebroni, akajitwalia masuria zaidi na wake huko Yerusalemu, nao wana na binti wengi walizaliwa kwake. 14 Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 15 Ibihari, Elishua, Nefegi, Yafia, 16 Elishama, Eliada na Elifeleti. 17 Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 18 Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 19 kwa hiyo Daudi akamuuliza BWANA, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?” BWANA akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.” 20 Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, BWANA amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu. 21 Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua. 22 Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. 23 Kwa hiyo Daudi akamuuliza BWANA, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 24 Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa BWANA ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” 25 Basi Daudi akafanya kama BWANA alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba hadi Gezeri.
In Other Versions
2 Samuel 5 in the ANGEFD
2 Samuel 5 in the ANTPNG2D
2 Samuel 5 in the AS21
2 Samuel 5 in the BAGH
2 Samuel 5 in the BBPNG
2 Samuel 5 in the BBT1E
2 Samuel 5 in the BDS
2 Samuel 5 in the BEV
2 Samuel 5 in the BHAD
2 Samuel 5 in the BIB
2 Samuel 5 in the BLPT
2 Samuel 5 in the BNT
2 Samuel 5 in the BNTABOOT
2 Samuel 5 in the BNTLV
2 Samuel 5 in the BOATCB
2 Samuel 5 in the BOATCB2
2 Samuel 5 in the BOBCV
2 Samuel 5 in the BOCNT
2 Samuel 5 in the BOECS
2 Samuel 5 in the BOGWICC
2 Samuel 5 in the BOHCB
2 Samuel 5 in the BOHCV
2 Samuel 5 in the BOHLNT
2 Samuel 5 in the BOHNTLTAL
2 Samuel 5 in the BOICB
2 Samuel 5 in the BOILNTAP
2 Samuel 5 in the BOITCV
2 Samuel 5 in the BOKCV2
2 Samuel 5 in the BOKHWOG
2 Samuel 5 in the BOKSSV
2 Samuel 5 in the BOLCB
2 Samuel 5 in the BOLCB2
2 Samuel 5 in the BOMCV
2 Samuel 5 in the BONAV
2 Samuel 5 in the BONCB
2 Samuel 5 in the BONLT
2 Samuel 5 in the BONUT2
2 Samuel 5 in the BOPLNT
2 Samuel 5 in the BOSCB
2 Samuel 5 in the BOSNC
2 Samuel 5 in the BOTLNT
2 Samuel 5 in the BOVCB
2 Samuel 5 in the BOYCB
2 Samuel 5 in the BPBB
2 Samuel 5 in the BPH
2 Samuel 5 in the BSB
2 Samuel 5 in the CCB
2 Samuel 5 in the CUV
2 Samuel 5 in the CUVS
2 Samuel 5 in the DBT
2 Samuel 5 in the DGDNT
2 Samuel 5 in the DHNT
2 Samuel 5 in the DNT
2 Samuel 5 in the ELBE
2 Samuel 5 in the EMTV
2 Samuel 5 in the ESV
2 Samuel 5 in the FBV
2 Samuel 5 in the FEB
2 Samuel 5 in the GGMNT
2 Samuel 5 in the GNT
2 Samuel 5 in the HARY
2 Samuel 5 in the HNT
2 Samuel 5 in the IRVA
2 Samuel 5 in the IRVB
2 Samuel 5 in the IRVG
2 Samuel 5 in the IRVH
2 Samuel 5 in the IRVK
2 Samuel 5 in the IRVM
2 Samuel 5 in the IRVM2
2 Samuel 5 in the IRVO
2 Samuel 5 in the IRVP
2 Samuel 5 in the IRVT
2 Samuel 5 in the IRVT2
2 Samuel 5 in the IRVU
2 Samuel 5 in the ISVN
2 Samuel 5 in the JSNT
2 Samuel 5 in the KAPI
2 Samuel 5 in the KBT1ETNIK
2 Samuel 5 in the KBV
2 Samuel 5 in the KJV
2 Samuel 5 in the KNFD
2 Samuel 5 in the LBA
2 Samuel 5 in the LBLA
2 Samuel 5 in the LNT
2 Samuel 5 in the LSV
2 Samuel 5 in the MAAL
2 Samuel 5 in the MBV
2 Samuel 5 in the MBV2
2 Samuel 5 in the MHNT
2 Samuel 5 in the MKNFD
2 Samuel 5 in the MNG
2 Samuel 5 in the MNT
2 Samuel 5 in the MNT2
2 Samuel 5 in the MRS1T
2 Samuel 5 in the NAA
2 Samuel 5 in the NASB
2 Samuel 5 in the NBLA
2 Samuel 5 in the NBS
2 Samuel 5 in the NBVTP
2 Samuel 5 in the NET2
2 Samuel 5 in the NIV11
2 Samuel 5 in the NNT
2 Samuel 5 in the NNT2
2 Samuel 5 in the NNT3
2 Samuel 5 in the PDDPT
2 Samuel 5 in the PFNT
2 Samuel 5 in the RMNT
2 Samuel 5 in the SBIAS
2 Samuel 5 in the SBIBS
2 Samuel 5 in the SBIBS2
2 Samuel 5 in the SBICS
2 Samuel 5 in the SBIDS
2 Samuel 5 in the SBIGS
2 Samuel 5 in the SBIHS
2 Samuel 5 in the SBIIS
2 Samuel 5 in the SBIIS2
2 Samuel 5 in the SBIIS3
2 Samuel 5 in the SBIKS
2 Samuel 5 in the SBIKS2
2 Samuel 5 in the SBIMS
2 Samuel 5 in the SBIOS
2 Samuel 5 in the SBIPS
2 Samuel 5 in the SBISS
2 Samuel 5 in the SBITS
2 Samuel 5 in the SBITS2
2 Samuel 5 in the SBITS3
2 Samuel 5 in the SBITS4
2 Samuel 5 in the SBIUS
2 Samuel 5 in the SBIVS
2 Samuel 5 in the SBT
2 Samuel 5 in the SBT1E
2 Samuel 5 in the SCHL
2 Samuel 5 in the SNT
2 Samuel 5 in the SUSU
2 Samuel 5 in the SUSU2
2 Samuel 5 in the SYNO
2 Samuel 5 in the TBIAOTANT
2 Samuel 5 in the TBT1E
2 Samuel 5 in the TBT1E2
2 Samuel 5 in the TFTIP
2 Samuel 5 in the TFTU
2 Samuel 5 in the TGNTATF3T
2 Samuel 5 in the THAI
2 Samuel 5 in the TNFD
2 Samuel 5 in the TNT
2 Samuel 5 in the TNTIK
2 Samuel 5 in the TNTIL
2 Samuel 5 in the TNTIN
2 Samuel 5 in the TNTIP
2 Samuel 5 in the TNTIZ
2 Samuel 5 in the TOMA
2 Samuel 5 in the TTENT
2 Samuel 5 in the UBG
2 Samuel 5 in the UGV
2 Samuel 5 in the UGV2
2 Samuel 5 in the UGV3
2 Samuel 5 in the VBL
2 Samuel 5 in the VDCC
2 Samuel 5 in the YALU
2 Samuel 5 in the YAPE
2 Samuel 5 in the YBVTP
2 Samuel 5 in the ZBP