Esther 6 (BOKCV)

1 Usiku ule mfalme hakupata usingizi, hivyo akaagiza aletewe kitabu cha kumbukumbu za matukio ya utawala wake, asomewe. 2 Kitabu hicho kilikutwa na kumbukumbu kwamba Mordekai alikuwa amefichua jinsi Bigthana na Tereshi, waliokuwa maafisa wawili wa mfalme, walinzi wa lango walivyokuwa wamepanga hila ya kumuua Mfalme Ahasuero. 3 Mfalme akauliza, “Je, ni heshima na shukrani gani Mordekai alipokea kwa ajili ya jambo hili?”Watumishi wake wakajibu, “Hakuna lolote alilofanyiwa.” 4 Mfalme akasema, “Ni nani yuko uani?” Wakati huo huo Hamani alikuwa ameingia ua wa nje wa jumba la mfalme kusema na mfalme kuhusu kumwangika Mordekai katika mahali pa kuangikia watu alipokuwa amepajenga kwa ajili yake. 5 Watumishi wake wakamjibu, “Hamani amesimama uani.”Mfalme akaamuru, “Mleteni ndani.” 6 Hamani alipoingia, mfalme alimuuliza, “Afanyiwe nini mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu?”Basi Hamani akawaza moyoni mwake, “Ni nani mwingine ambaye mfalme angemheshimu kuliko mimi?” 7 Kwa hiyo akamjibu mfalme, “Kwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu, 8 aletewe joho la kifalme ambalo mfalme ameshalivaa na farasi ambaye mfalme alishampanda, ambaye amevikwa taji ya kifalme kichwani mwake. 9 Kisha joho na farasi vikabidhiwe kwa mmojawapo wa wakuu wa mfalme anayeheshimika sana. Nao wamvike mtu yule ambaye mfalme anapenda kumheshimu, na aongozwe akiwa juu ya farasi kupitia barabara za mji, wakitangaza mbele yake, ‘Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme apenda kumheshimu!’ ” 10 Mfalme akamwamuru Hamani, “Nenda mara moja, chukua joho na farasi na ufanye kama vile ulivyopendekeza kwa Mordekai Myahudi, akaaye langoni mwa mfalme. Usipuuze kufanya kitu chochote ulichoshauri.” 11 Hivyo Hamani akachukua joho na farasi.Akamvika Mordekai, na kumpandisha juu ya farasi akamtembeza katika barabara za mji akitangaza mbele yake, “Hivi ndivyo anavyofanyiwa mtu ambaye mfalme anapenda kumheshimu!” 12 Baadaye Mordekai akarudi kwenye lango la mfalme. Lakini Hamani akakimbia nyumbani, akiwa amejaa huzuni, 13 naye akamweleza Zereshi mkewe pamoja na rafiki zake wote kila kitu ambacho kimempata.Washauri wake pamoja na Zereshi mkewe wakamwambia, “Kwa kuwa Mordekai, ambaye mbele yake umeanza kuanguka ni wa asili ya Kiyahudi, huwezi kushindana naye; kwa hakika utaanguka!” 14 Walipokuwa bado wakizungumza naye, matowashi wa mfalme wakaja na kumharakisha Hamani aende katika karamu aliyoiandaa Esta.

In Other Versions

Esther 6 in the ANGEFD

Esther 6 in the ANTPNG2D

Esther 6 in the AS21

Esther 6 in the BAGH

Esther 6 in the BBPNG

Esther 6 in the BBT1E

Esther 6 in the BDS

Esther 6 in the BEV

Esther 6 in the BHAD

Esther 6 in the BIB

Esther 6 in the BLPT

Esther 6 in the BNT

Esther 6 in the BNTABOOT

Esther 6 in the BNTLV

Esther 6 in the BOATCB

Esther 6 in the BOATCB2

Esther 6 in the BOBCV

Esther 6 in the BOCNT

Esther 6 in the BOECS

Esther 6 in the BOGWICC

Esther 6 in the BOHCB

Esther 6 in the BOHCV

Esther 6 in the BOHLNT

Esther 6 in the BOHNTLTAL

Esther 6 in the BOICB

Esther 6 in the BOILNTAP

Esther 6 in the BOITCV

Esther 6 in the BOKCV2

Esther 6 in the BOKHWOG

Esther 6 in the BOKSSV

Esther 6 in the BOLCB

Esther 6 in the BOLCB2

Esther 6 in the BOMCV

Esther 6 in the BONAV

Esther 6 in the BONCB

Esther 6 in the BONLT

Esther 6 in the BONUT2

Esther 6 in the BOPLNT

Esther 6 in the BOSCB

Esther 6 in the BOSNC

Esther 6 in the BOTLNT

Esther 6 in the BOVCB

Esther 6 in the BOYCB

Esther 6 in the BPBB

Esther 6 in the BPH

Esther 6 in the BSB

Esther 6 in the CCB

Esther 6 in the CUV

Esther 6 in the CUVS

Esther 6 in the DBT

Esther 6 in the DGDNT

Esther 6 in the DHNT

Esther 6 in the DNT

Esther 6 in the ELBE

Esther 6 in the EMTV

Esther 6 in the ESV

Esther 6 in the FBV

Esther 6 in the FEB

Esther 6 in the GGMNT

Esther 6 in the GNT

Esther 6 in the HARY

Esther 6 in the HNT

Esther 6 in the IRVA

Esther 6 in the IRVB

Esther 6 in the IRVG

Esther 6 in the IRVH

Esther 6 in the IRVK

Esther 6 in the IRVM

Esther 6 in the IRVM2

Esther 6 in the IRVO

Esther 6 in the IRVP

Esther 6 in the IRVT

Esther 6 in the IRVT2

Esther 6 in the IRVU

Esther 6 in the ISVN

Esther 6 in the JSNT

Esther 6 in the KAPI

Esther 6 in the KBT1ETNIK

Esther 6 in the KBV

Esther 6 in the KJV

Esther 6 in the KNFD

Esther 6 in the LBA

Esther 6 in the LBLA

Esther 6 in the LNT

Esther 6 in the LSV

Esther 6 in the MAAL

Esther 6 in the MBV

Esther 6 in the MBV2

Esther 6 in the MHNT

Esther 6 in the MKNFD

Esther 6 in the MNG

Esther 6 in the MNT

Esther 6 in the MNT2

Esther 6 in the MRS1T

Esther 6 in the NAA

Esther 6 in the NASB

Esther 6 in the NBLA

Esther 6 in the NBS

Esther 6 in the NBVTP

Esther 6 in the NET2

Esther 6 in the NIV11

Esther 6 in the NNT

Esther 6 in the NNT2

Esther 6 in the NNT3

Esther 6 in the PDDPT

Esther 6 in the PFNT

Esther 6 in the RMNT

Esther 6 in the SBIAS

Esther 6 in the SBIBS

Esther 6 in the SBIBS2

Esther 6 in the SBICS

Esther 6 in the SBIDS

Esther 6 in the SBIGS

Esther 6 in the SBIHS

Esther 6 in the SBIIS

Esther 6 in the SBIIS2

Esther 6 in the SBIIS3

Esther 6 in the SBIKS

Esther 6 in the SBIKS2

Esther 6 in the SBIMS

Esther 6 in the SBIOS

Esther 6 in the SBIPS

Esther 6 in the SBISS

Esther 6 in the SBITS

Esther 6 in the SBITS2

Esther 6 in the SBITS3

Esther 6 in the SBITS4

Esther 6 in the SBIUS

Esther 6 in the SBIVS

Esther 6 in the SBT

Esther 6 in the SBT1E

Esther 6 in the SCHL

Esther 6 in the SNT

Esther 6 in the SUSU

Esther 6 in the SUSU2

Esther 6 in the SYNO

Esther 6 in the TBIAOTANT

Esther 6 in the TBT1E

Esther 6 in the TBT1E2

Esther 6 in the TFTIP

Esther 6 in the TFTU

Esther 6 in the TGNTATF3T

Esther 6 in the THAI

Esther 6 in the TNFD

Esther 6 in the TNT

Esther 6 in the TNTIK

Esther 6 in the TNTIL

Esther 6 in the TNTIN

Esther 6 in the TNTIP

Esther 6 in the TNTIZ

Esther 6 in the TOMA

Esther 6 in the TTENT

Esther 6 in the UBG

Esther 6 in the UGV

Esther 6 in the UGV2

Esther 6 in the UGV3

Esther 6 in the VBL

Esther 6 in the VDCC

Esther 6 in the YALU

Esther 6 in the YAPE

Esther 6 in the YBVTP

Esther 6 in the ZBP