Exodus 25 (BOKCV)

1 BWANA akamwambia Mose, 2 “Waambie Waisraeli waniletee sadaka. Utapokea sadaka kwa niaba yangu kutoka kwa kila mtu ambaye moyo wake wapenda kutoa. 3 Hizi ndizo sadaka utakazozipokea kutoka kwao: dhahabu, fedha na shaba; 4 nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu, pamoja na kitani safi; singa za mbuzi; 5 ngozi za kondoo dume zilizopakwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo; mbao za mshita; 6 mafuta ya zeituni kwa ajili ya taa; vikolezi kwa ajili ya mafuta ya upako, pamoja na uvumba wa harufu nzuri; 7 na vito vya shohamu na vito vingine vya thamani vya kuweka kwenye kisibau na kile kifuko cha kifuani. 8 “Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 9 Tengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha. 10 “Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, upana wa dhiraa moja na nusu, na kimo cha dhiraa moja na nusu. 11 Utalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12 Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13 Kisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14 Utaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15 Hiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. 16 Kisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa. 17 “Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. 18 Tengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 19 Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 20 Makerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. 21 Weka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. 22 Hapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli. 23 “Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili, upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. 24 Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 25 Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne, na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. 26 Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 27 Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. 28 Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. 29 Tengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. 30 Utaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima. 31 “Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja. 32 Matawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 33 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa. 34 Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. 35 Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. 36 Matovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi. 37 “Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake. 38 Mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi. 39 Utatumia talanta moja ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote. 40 Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

In Other Versions

Exodus 25 in the ANGEFD

Exodus 25 in the ANTPNG2D

Exodus 25 in the AS21

Exodus 25 in the BAGH

Exodus 25 in the BBPNG

Exodus 25 in the BBT1E

Exodus 25 in the BDS

Exodus 25 in the BEV

Exodus 25 in the BHAD

Exodus 25 in the BIB

Exodus 25 in the BLPT

Exodus 25 in the BNT

Exodus 25 in the BNTABOOT

Exodus 25 in the BNTLV

Exodus 25 in the BOATCB

Exodus 25 in the BOATCB2

Exodus 25 in the BOBCV

Exodus 25 in the BOCNT

Exodus 25 in the BOECS

Exodus 25 in the BOGWICC

Exodus 25 in the BOHCB

Exodus 25 in the BOHCV

Exodus 25 in the BOHLNT

Exodus 25 in the BOHNTLTAL

Exodus 25 in the BOICB

Exodus 25 in the BOILNTAP

Exodus 25 in the BOITCV

Exodus 25 in the BOKCV2

Exodus 25 in the BOKHWOG

Exodus 25 in the BOKSSV

Exodus 25 in the BOLCB

Exodus 25 in the BOLCB2

Exodus 25 in the BOMCV

Exodus 25 in the BONAV

Exodus 25 in the BONCB

Exodus 25 in the BONLT

Exodus 25 in the BONUT2

Exodus 25 in the BOPLNT

Exodus 25 in the BOSCB

Exodus 25 in the BOSNC

Exodus 25 in the BOTLNT

Exodus 25 in the BOVCB

Exodus 25 in the BOYCB

Exodus 25 in the BPBB

Exodus 25 in the BPH

Exodus 25 in the BSB

Exodus 25 in the CCB

Exodus 25 in the CUV

Exodus 25 in the CUVS

Exodus 25 in the DBT

Exodus 25 in the DGDNT

Exodus 25 in the DHNT

Exodus 25 in the DNT

Exodus 25 in the ELBE

Exodus 25 in the EMTV

Exodus 25 in the ESV

Exodus 25 in the FBV

Exodus 25 in the FEB

Exodus 25 in the GGMNT

Exodus 25 in the GNT

Exodus 25 in the HARY

Exodus 25 in the HNT

Exodus 25 in the IRVA

Exodus 25 in the IRVB

Exodus 25 in the IRVG

Exodus 25 in the IRVH

Exodus 25 in the IRVK

Exodus 25 in the IRVM

Exodus 25 in the IRVM2

Exodus 25 in the IRVO

Exodus 25 in the IRVP

Exodus 25 in the IRVT

Exodus 25 in the IRVT2

Exodus 25 in the IRVU

Exodus 25 in the ISVN

Exodus 25 in the JSNT

Exodus 25 in the KAPI

Exodus 25 in the KBT1ETNIK

Exodus 25 in the KBV

Exodus 25 in the KJV

Exodus 25 in the KNFD

Exodus 25 in the LBA

Exodus 25 in the LBLA

Exodus 25 in the LNT

Exodus 25 in the LSV

Exodus 25 in the MAAL

Exodus 25 in the MBV

Exodus 25 in the MBV2

Exodus 25 in the MHNT

Exodus 25 in the MKNFD

Exodus 25 in the MNG

Exodus 25 in the MNT

Exodus 25 in the MNT2

Exodus 25 in the MRS1T

Exodus 25 in the NAA

Exodus 25 in the NASB

Exodus 25 in the NBLA

Exodus 25 in the NBS

Exodus 25 in the NBVTP

Exodus 25 in the NET2

Exodus 25 in the NIV11

Exodus 25 in the NNT

Exodus 25 in the NNT2

Exodus 25 in the NNT3

Exodus 25 in the PDDPT

Exodus 25 in the PFNT

Exodus 25 in the RMNT

Exodus 25 in the SBIAS

Exodus 25 in the SBIBS

Exodus 25 in the SBIBS2

Exodus 25 in the SBICS

Exodus 25 in the SBIDS

Exodus 25 in the SBIGS

Exodus 25 in the SBIHS

Exodus 25 in the SBIIS

Exodus 25 in the SBIIS2

Exodus 25 in the SBIIS3

Exodus 25 in the SBIKS

Exodus 25 in the SBIKS2

Exodus 25 in the SBIMS

Exodus 25 in the SBIOS

Exodus 25 in the SBIPS

Exodus 25 in the SBISS

Exodus 25 in the SBITS

Exodus 25 in the SBITS2

Exodus 25 in the SBITS3

Exodus 25 in the SBITS4

Exodus 25 in the SBIUS

Exodus 25 in the SBIVS

Exodus 25 in the SBT

Exodus 25 in the SBT1E

Exodus 25 in the SCHL

Exodus 25 in the SNT

Exodus 25 in the SUSU

Exodus 25 in the SUSU2

Exodus 25 in the SYNO

Exodus 25 in the TBIAOTANT

Exodus 25 in the TBT1E

Exodus 25 in the TBT1E2

Exodus 25 in the TFTIP

Exodus 25 in the TFTU

Exodus 25 in the TGNTATF3T

Exodus 25 in the THAI

Exodus 25 in the TNFD

Exodus 25 in the TNT

Exodus 25 in the TNTIK

Exodus 25 in the TNTIL

Exodus 25 in the TNTIN

Exodus 25 in the TNTIP

Exodus 25 in the TNTIZ

Exodus 25 in the TOMA

Exodus 25 in the TTENT

Exodus 25 in the UBG

Exodus 25 in the UGV

Exodus 25 in the UGV2

Exodus 25 in the UGV3

Exodus 25 in the VBL

Exodus 25 in the VDCC

Exodus 25 in the YALU

Exodus 25 in the YAPE

Exodus 25 in the YBVTP

Exodus 25 in the ZBP