Exodus 40 (BOKCV)

1 Kisha BWANA akamwambia Mose: 2 “Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza. 3 Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake. 4 Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake. 5 Weka madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba mbele ya Sanduku la Ushuhuda kisha uweke pazia kwenye lango la Maskani ya Mungu. 6 “Weka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa mbele ya lango la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania; 7 weka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, na uweke maji ndani yake. 8 Fanyiza ua kuzunguka maskani na uweke pazia penye ingilio la ua. 9 “Chukua mafuta ya upako, ipake Maskani ya Mungu pamoja na kila kitu kilichomo ndani yake; iweke wakfu pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani mwake, nayo itakuwa takatifu. 10 Kisha yapake mafuta hayo madhabahu ya kuteketezea sadaka pamoja na vifaa vyake vyote; weka wakfu madhabahu nayo yatakuwa takatifu sana. 11 Paka sinia mafuta pamoja na kishikilio chake na uviweke wakfu. 12 “Mlete Aroni na wanawe kwenye ingilio la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. 13 Kisha mvike Aroni yale mavazi matakatifu, umtie mafuta na kumweka wakfu ili apate kunitumikia katikati ya ukuhani. 14 Walete wanawe na uwavike makoti. 15 Kisha watie mafuta kama ulivyomtia baba yao, ili nao pia wanitumikie katika kazi ya ukuhani. Kutiwa mafuta kwao kutakuwa kwa ajili ya ukuhani utakaoendelea kwa vizazi vyote vijavyo.” 16 Mose akafanya kila kitu sawa kama vile BWANA alivyomwagiza. 17 Kwa hiyo Maskani ya Mungu ilisimikwa katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, katika mwaka wa pili. 18 Mose alipoweka wakfu Maskani ya Mungu, aliweka vitako mahali pake, akasimamisha mihimili, akatia mataruma na kusimamisha nguzo. 19 Kisha akalitandaza hema juu ya Maskani ya Mungu na kuifunika hema, kama BWANA alivyomwagiza. 20 Akachukua ule Ushuhuda na kuuweka ndani ya Sanduku la Agano, akaweka ile mipiko ya kubebea hilo Sanduku na kuweka kiti cha rehema juu yake. 21 Kisha Mose akalileta Sanduku ndani ya Maskani ya Mungu, akatundika pazia ili kulifunika Sanduku la Ushuhuda, kama BWANA alivyomwagiza. 22 Mose akaweka meza ndani ya Hema la Kukutania, upande wa kaskazini ya Maskani ya Mungu nje ya pazia 23 na kupanga mikate juu yake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwagiza. 24 Akaweka kinara cha taa ndani ya Hema la Kukutania mkabala na meza upande wa kusini mwa Maskani ya Mungu 25 na kuziweka taa mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwagiza. 26 Mose akaweka madhabahu ya dhahabu ndani ya Hema la Kukutania mbele ya pazia 27 na kufukiza uvumba wenye harufu nzuri, kama BWANA alivyomwagiza. 28 Kisha akaweka pazia kwenye ingilio la Maskani ya Mungu. 29 Mose akaweka madhabahu ya sadaka za kuteketezwa karibu na ingilio la Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka kama BWANA alivyomwagiza. 30 Akaweka sinia kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, akaweka maji ndani yake kwa ajili ya kunawia, 31 Naye Mose, Aroni na wanawe wakayatumia kwa kunawia mikono na miguu yao. 32 Wakanawa kila walipoingia katika Hema la Kukutania au walipoikaribia madhabahu kama BWANA alivyomwagiza Mose. 33 Kisha Mose akafanya ua kuizunguka Maskani ya Mungu na madhabahu, pia akaweka pazia kwenye ingilio la huo ua. Hivyo Mose akaikamilisha kazi. 34 Ndipo wingu likafunika Hema la Kukutania, na utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. 35 Mose hakuweza kuingia ndani ya Hema la Kukutania kwa sababu wingu lilikuwa limetua juu ya Hema, nao utukufu wa BWANA ukaijaza Maskani ya Mungu. 36 Katika safari yote ya Waisraeli, kila wakati wingu lilipoinuka kutoka juu ya Maskani ya Mungu, wangeondoka; 37 lakini kama wingu halikuinuka, hawakuondoka, mpaka siku lilipoinuka. 38 Kwa hiyo wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani mchana, na moto ulikuwa katika hilo wingu wakati wa usiku, machoni pa nyumba yote ya Israeli siku zote za safari zao.

In Other Versions

Exodus 40 in the ANGEFD

Exodus 40 in the ANTPNG2D

Exodus 40 in the AS21

Exodus 40 in the BAGH

Exodus 40 in the BBPNG

Exodus 40 in the BBT1E

Exodus 40 in the BDS

Exodus 40 in the BEV

Exodus 40 in the BHAD

Exodus 40 in the BIB

Exodus 40 in the BLPT

Exodus 40 in the BNT

Exodus 40 in the BNTABOOT

Exodus 40 in the BNTLV

Exodus 40 in the BOATCB

Exodus 40 in the BOATCB2

Exodus 40 in the BOBCV

Exodus 40 in the BOCNT

Exodus 40 in the BOECS

Exodus 40 in the BOGWICC

Exodus 40 in the BOHCB

Exodus 40 in the BOHCV

Exodus 40 in the BOHLNT

Exodus 40 in the BOHNTLTAL

Exodus 40 in the BOICB

Exodus 40 in the BOILNTAP

Exodus 40 in the BOITCV

Exodus 40 in the BOKCV2

Exodus 40 in the BOKHWOG

Exodus 40 in the BOKSSV

Exodus 40 in the BOLCB

Exodus 40 in the BOLCB2

Exodus 40 in the BOMCV

Exodus 40 in the BONAV

Exodus 40 in the BONCB

Exodus 40 in the BONLT

Exodus 40 in the BONUT2

Exodus 40 in the BOPLNT

Exodus 40 in the BOSCB

Exodus 40 in the BOSNC

Exodus 40 in the BOTLNT

Exodus 40 in the BOVCB

Exodus 40 in the BOYCB

Exodus 40 in the BPBB

Exodus 40 in the BPH

Exodus 40 in the BSB

Exodus 40 in the CCB

Exodus 40 in the CUV

Exodus 40 in the CUVS

Exodus 40 in the DBT

Exodus 40 in the DGDNT

Exodus 40 in the DHNT

Exodus 40 in the DNT

Exodus 40 in the ELBE

Exodus 40 in the EMTV

Exodus 40 in the ESV

Exodus 40 in the FBV

Exodus 40 in the FEB

Exodus 40 in the GGMNT

Exodus 40 in the GNT

Exodus 40 in the HARY

Exodus 40 in the HNT

Exodus 40 in the IRVA

Exodus 40 in the IRVB

Exodus 40 in the IRVG

Exodus 40 in the IRVH

Exodus 40 in the IRVK

Exodus 40 in the IRVM

Exodus 40 in the IRVM2

Exodus 40 in the IRVO

Exodus 40 in the IRVP

Exodus 40 in the IRVT

Exodus 40 in the IRVT2

Exodus 40 in the IRVU

Exodus 40 in the ISVN

Exodus 40 in the JSNT

Exodus 40 in the KAPI

Exodus 40 in the KBT1ETNIK

Exodus 40 in the KBV

Exodus 40 in the KJV

Exodus 40 in the KNFD

Exodus 40 in the LBA

Exodus 40 in the LBLA

Exodus 40 in the LNT

Exodus 40 in the LSV

Exodus 40 in the MAAL

Exodus 40 in the MBV

Exodus 40 in the MBV2

Exodus 40 in the MHNT

Exodus 40 in the MKNFD

Exodus 40 in the MNG

Exodus 40 in the MNT

Exodus 40 in the MNT2

Exodus 40 in the MRS1T

Exodus 40 in the NAA

Exodus 40 in the NASB

Exodus 40 in the NBLA

Exodus 40 in the NBS

Exodus 40 in the NBVTP

Exodus 40 in the NET2

Exodus 40 in the NIV11

Exodus 40 in the NNT

Exodus 40 in the NNT2

Exodus 40 in the NNT3

Exodus 40 in the PDDPT

Exodus 40 in the PFNT

Exodus 40 in the RMNT

Exodus 40 in the SBIAS

Exodus 40 in the SBIBS

Exodus 40 in the SBIBS2

Exodus 40 in the SBICS

Exodus 40 in the SBIDS

Exodus 40 in the SBIGS

Exodus 40 in the SBIHS

Exodus 40 in the SBIIS

Exodus 40 in the SBIIS2

Exodus 40 in the SBIIS3

Exodus 40 in the SBIKS

Exodus 40 in the SBIKS2

Exodus 40 in the SBIMS

Exodus 40 in the SBIOS

Exodus 40 in the SBIPS

Exodus 40 in the SBISS

Exodus 40 in the SBITS

Exodus 40 in the SBITS2

Exodus 40 in the SBITS3

Exodus 40 in the SBITS4

Exodus 40 in the SBIUS

Exodus 40 in the SBIVS

Exodus 40 in the SBT

Exodus 40 in the SBT1E

Exodus 40 in the SCHL

Exodus 40 in the SNT

Exodus 40 in the SUSU

Exodus 40 in the SUSU2

Exodus 40 in the SYNO

Exodus 40 in the TBIAOTANT

Exodus 40 in the TBT1E

Exodus 40 in the TBT1E2

Exodus 40 in the TFTIP

Exodus 40 in the TFTU

Exodus 40 in the TGNTATF3T

Exodus 40 in the THAI

Exodus 40 in the TNFD

Exodus 40 in the TNT

Exodus 40 in the TNTIK

Exodus 40 in the TNTIL

Exodus 40 in the TNTIN

Exodus 40 in the TNTIP

Exodus 40 in the TNTIZ

Exodus 40 in the TOMA

Exodus 40 in the TTENT

Exodus 40 in the UBG

Exodus 40 in the UGV

Exodus 40 in the UGV2

Exodus 40 in the UGV3

Exodus 40 in the VBL

Exodus 40 in the VDCC

Exodus 40 in the YALU

Exodus 40 in the YAPE

Exodus 40 in the YBVTP

Exodus 40 in the ZBP