Exodus 6 (BOKCV)

1 Kisha BWANA akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.” 2 Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi BWANA. 3 Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao. 4 Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni. 5 Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu. 6 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi BWANA, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu. 7 Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri. 8 Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi BWANA.’ ” 9 Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili. 10 Ndipo BWANA akamwambia Mose, 11 “Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.” 12 Lakini Mose akamwambia BWANA, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?” 13 Ndipo BWANA akanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri. 14 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao: Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni. 15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni. 16 Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. 17 Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei. 18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133. 19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi.Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao. 20 Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. 21 Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri. 22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri. 23 Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora. 25 Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo. 26 Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao BWANA aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” 27 Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni. 28 BWANA aliponena na Mose huko Misri, 29 akamwambia, “Mimi ndimi BWANA. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.” 30 Lakini Mose akamwambia BWANA, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

In Other Versions

Exodus 6 in the ANGEFD

Exodus 6 in the ANTPNG2D

Exodus 6 in the AS21

Exodus 6 in the BAGH

Exodus 6 in the BBPNG

Exodus 6 in the BBT1E

Exodus 6 in the BDS

Exodus 6 in the BEV

Exodus 6 in the BHAD

Exodus 6 in the BIB

Exodus 6 in the BLPT

Exodus 6 in the BNT

Exodus 6 in the BNTABOOT

Exodus 6 in the BNTLV

Exodus 6 in the BOATCB

Exodus 6 in the BOATCB2

Exodus 6 in the BOBCV

Exodus 6 in the BOCNT

Exodus 6 in the BOECS

Exodus 6 in the BOGWICC

Exodus 6 in the BOHCB

Exodus 6 in the BOHCV

Exodus 6 in the BOHLNT

Exodus 6 in the BOHNTLTAL

Exodus 6 in the BOICB

Exodus 6 in the BOILNTAP

Exodus 6 in the BOITCV

Exodus 6 in the BOKCV2

Exodus 6 in the BOKHWOG

Exodus 6 in the BOKSSV

Exodus 6 in the BOLCB

Exodus 6 in the BOLCB2

Exodus 6 in the BOMCV

Exodus 6 in the BONAV

Exodus 6 in the BONCB

Exodus 6 in the BONLT

Exodus 6 in the BONUT2

Exodus 6 in the BOPLNT

Exodus 6 in the BOSCB

Exodus 6 in the BOSNC

Exodus 6 in the BOTLNT

Exodus 6 in the BOVCB

Exodus 6 in the BOYCB

Exodus 6 in the BPBB

Exodus 6 in the BPH

Exodus 6 in the BSB

Exodus 6 in the CCB

Exodus 6 in the CUV

Exodus 6 in the CUVS

Exodus 6 in the DBT

Exodus 6 in the DGDNT

Exodus 6 in the DHNT

Exodus 6 in the DNT

Exodus 6 in the ELBE

Exodus 6 in the EMTV

Exodus 6 in the ESV

Exodus 6 in the FBV

Exodus 6 in the FEB

Exodus 6 in the GGMNT

Exodus 6 in the GNT

Exodus 6 in the HARY

Exodus 6 in the HNT

Exodus 6 in the IRVA

Exodus 6 in the IRVB

Exodus 6 in the IRVG

Exodus 6 in the IRVH

Exodus 6 in the IRVK

Exodus 6 in the IRVM

Exodus 6 in the IRVM2

Exodus 6 in the IRVO

Exodus 6 in the IRVP

Exodus 6 in the IRVT

Exodus 6 in the IRVT2

Exodus 6 in the IRVU

Exodus 6 in the ISVN

Exodus 6 in the JSNT

Exodus 6 in the KAPI

Exodus 6 in the KBT1ETNIK

Exodus 6 in the KBV

Exodus 6 in the KJV

Exodus 6 in the KNFD

Exodus 6 in the LBA

Exodus 6 in the LBLA

Exodus 6 in the LNT

Exodus 6 in the LSV

Exodus 6 in the MAAL

Exodus 6 in the MBV

Exodus 6 in the MBV2

Exodus 6 in the MHNT

Exodus 6 in the MKNFD

Exodus 6 in the MNG

Exodus 6 in the MNT

Exodus 6 in the MNT2

Exodus 6 in the MRS1T

Exodus 6 in the NAA

Exodus 6 in the NASB

Exodus 6 in the NBLA

Exodus 6 in the NBS

Exodus 6 in the NBVTP

Exodus 6 in the NET2

Exodus 6 in the NIV11

Exodus 6 in the NNT

Exodus 6 in the NNT2

Exodus 6 in the NNT3

Exodus 6 in the PDDPT

Exodus 6 in the PFNT

Exodus 6 in the RMNT

Exodus 6 in the SBIAS

Exodus 6 in the SBIBS

Exodus 6 in the SBIBS2

Exodus 6 in the SBICS

Exodus 6 in the SBIDS

Exodus 6 in the SBIGS

Exodus 6 in the SBIHS

Exodus 6 in the SBIIS

Exodus 6 in the SBIIS2

Exodus 6 in the SBIIS3

Exodus 6 in the SBIKS

Exodus 6 in the SBIKS2

Exodus 6 in the SBIMS

Exodus 6 in the SBIOS

Exodus 6 in the SBIPS

Exodus 6 in the SBISS

Exodus 6 in the SBITS

Exodus 6 in the SBITS2

Exodus 6 in the SBITS3

Exodus 6 in the SBITS4

Exodus 6 in the SBIUS

Exodus 6 in the SBIVS

Exodus 6 in the SBT

Exodus 6 in the SBT1E

Exodus 6 in the SCHL

Exodus 6 in the SNT

Exodus 6 in the SUSU

Exodus 6 in the SUSU2

Exodus 6 in the SYNO

Exodus 6 in the TBIAOTANT

Exodus 6 in the TBT1E

Exodus 6 in the TBT1E2

Exodus 6 in the TFTIP

Exodus 6 in the TFTU

Exodus 6 in the TGNTATF3T

Exodus 6 in the THAI

Exodus 6 in the TNFD

Exodus 6 in the TNT

Exodus 6 in the TNTIK

Exodus 6 in the TNTIL

Exodus 6 in the TNTIN

Exodus 6 in the TNTIP

Exodus 6 in the TNTIZ

Exodus 6 in the TOMA

Exodus 6 in the TTENT

Exodus 6 in the UBG

Exodus 6 in the UGV

Exodus 6 in the UGV2

Exodus 6 in the UGV3

Exodus 6 in the VBL

Exodus 6 in the VDCC

Exodus 6 in the YALU

Exodus 6 in the YAPE

Exodus 6 in the YBVTP

Exodus 6 in the ZBP