Ezekiel 37 (BOKCV)

1 Mkono wa BWANA ulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho wa BWANA na kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele. 2 Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana. 3 Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”Nikajibu, “Ee BWANA Mwenyezi, wewe peke yako wajua.” 4 Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno la BWANA! 5 Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. 6 Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ” 7 Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Wakati nilipokuwa ninatabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. 8 Nikatazama, mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini hapakuwepo pumzi ndani yake. 9 Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ” 10 Hivyo nikatabiri kama alivyoniamuru, nayo pumzi ikawaingia, wakawa hai na wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. 11 Ndipo akaniambia: “Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli. Nao wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka na tumaini letu limetoweka, tumekatiliwa mbali.’ 12 Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli. 13 Ndipo ninyi watu wangu, mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo. 14 Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi BWANA nimenena, nami nitalitenda, asema BWANA!’ ” 15 Neno la BWANA likanijia kusema: 16 “Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yosefu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’ 17 Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako. 18 “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’ 19 Waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’ 20 Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika 21 kisha waambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe. 22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili. 23 Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao. 24 “ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu. 25 Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele. 26 Nitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele. 27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 28 Ndipo mataifa watakapojua kwamba Mimi BWANA ndiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”

In Other Versions

Ezekiel 37 in the ANGEFD

Ezekiel 37 in the ANTPNG2D

Ezekiel 37 in the AS21

Ezekiel 37 in the BAGH

Ezekiel 37 in the BBPNG

Ezekiel 37 in the BBT1E

Ezekiel 37 in the BDS

Ezekiel 37 in the BEV

Ezekiel 37 in the BHAD

Ezekiel 37 in the BIB

Ezekiel 37 in the BLPT

Ezekiel 37 in the BNT

Ezekiel 37 in the BNTABOOT

Ezekiel 37 in the BNTLV

Ezekiel 37 in the BOATCB

Ezekiel 37 in the BOATCB2

Ezekiel 37 in the BOBCV

Ezekiel 37 in the BOCNT

Ezekiel 37 in the BOECS

Ezekiel 37 in the BOGWICC

Ezekiel 37 in the BOHCB

Ezekiel 37 in the BOHCV

Ezekiel 37 in the BOHLNT

Ezekiel 37 in the BOHNTLTAL

Ezekiel 37 in the BOICB

Ezekiel 37 in the BOILNTAP

Ezekiel 37 in the BOITCV

Ezekiel 37 in the BOKCV2

Ezekiel 37 in the BOKHWOG

Ezekiel 37 in the BOKSSV

Ezekiel 37 in the BOLCB

Ezekiel 37 in the BOLCB2

Ezekiel 37 in the BOMCV

Ezekiel 37 in the BONAV

Ezekiel 37 in the BONCB

Ezekiel 37 in the BONLT

Ezekiel 37 in the BONUT2

Ezekiel 37 in the BOPLNT

Ezekiel 37 in the BOSCB

Ezekiel 37 in the BOSNC

Ezekiel 37 in the BOTLNT

Ezekiel 37 in the BOVCB

Ezekiel 37 in the BOYCB

Ezekiel 37 in the BPBB

Ezekiel 37 in the BPH

Ezekiel 37 in the BSB

Ezekiel 37 in the CCB

Ezekiel 37 in the CUV

Ezekiel 37 in the CUVS

Ezekiel 37 in the DBT

Ezekiel 37 in the DGDNT

Ezekiel 37 in the DHNT

Ezekiel 37 in the DNT

Ezekiel 37 in the ELBE

Ezekiel 37 in the EMTV

Ezekiel 37 in the ESV

Ezekiel 37 in the FBV

Ezekiel 37 in the FEB

Ezekiel 37 in the GGMNT

Ezekiel 37 in the GNT

Ezekiel 37 in the HARY

Ezekiel 37 in the HNT

Ezekiel 37 in the IRVA

Ezekiel 37 in the IRVB

Ezekiel 37 in the IRVG

Ezekiel 37 in the IRVH

Ezekiel 37 in the IRVK

Ezekiel 37 in the IRVM

Ezekiel 37 in the IRVM2

Ezekiel 37 in the IRVO

Ezekiel 37 in the IRVP

Ezekiel 37 in the IRVT

Ezekiel 37 in the IRVT2

Ezekiel 37 in the IRVU

Ezekiel 37 in the ISVN

Ezekiel 37 in the JSNT

Ezekiel 37 in the KAPI

Ezekiel 37 in the KBT1ETNIK

Ezekiel 37 in the KBV

Ezekiel 37 in the KJV

Ezekiel 37 in the KNFD

Ezekiel 37 in the LBA

Ezekiel 37 in the LBLA

Ezekiel 37 in the LNT

Ezekiel 37 in the LSV

Ezekiel 37 in the MAAL

Ezekiel 37 in the MBV

Ezekiel 37 in the MBV2

Ezekiel 37 in the MHNT

Ezekiel 37 in the MKNFD

Ezekiel 37 in the MNG

Ezekiel 37 in the MNT

Ezekiel 37 in the MNT2

Ezekiel 37 in the MRS1T

Ezekiel 37 in the NAA

Ezekiel 37 in the NASB

Ezekiel 37 in the NBLA

Ezekiel 37 in the NBS

Ezekiel 37 in the NBVTP

Ezekiel 37 in the NET2

Ezekiel 37 in the NIV11

Ezekiel 37 in the NNT

Ezekiel 37 in the NNT2

Ezekiel 37 in the NNT3

Ezekiel 37 in the PDDPT

Ezekiel 37 in the PFNT

Ezekiel 37 in the RMNT

Ezekiel 37 in the SBIAS

Ezekiel 37 in the SBIBS

Ezekiel 37 in the SBIBS2

Ezekiel 37 in the SBICS

Ezekiel 37 in the SBIDS

Ezekiel 37 in the SBIGS

Ezekiel 37 in the SBIHS

Ezekiel 37 in the SBIIS

Ezekiel 37 in the SBIIS2

Ezekiel 37 in the SBIIS3

Ezekiel 37 in the SBIKS

Ezekiel 37 in the SBIKS2

Ezekiel 37 in the SBIMS

Ezekiel 37 in the SBIOS

Ezekiel 37 in the SBIPS

Ezekiel 37 in the SBISS

Ezekiel 37 in the SBITS

Ezekiel 37 in the SBITS2

Ezekiel 37 in the SBITS3

Ezekiel 37 in the SBITS4

Ezekiel 37 in the SBIUS

Ezekiel 37 in the SBIVS

Ezekiel 37 in the SBT

Ezekiel 37 in the SBT1E

Ezekiel 37 in the SCHL

Ezekiel 37 in the SNT

Ezekiel 37 in the SUSU

Ezekiel 37 in the SUSU2

Ezekiel 37 in the SYNO

Ezekiel 37 in the TBIAOTANT

Ezekiel 37 in the TBT1E

Ezekiel 37 in the TBT1E2

Ezekiel 37 in the TFTIP

Ezekiel 37 in the TFTU

Ezekiel 37 in the TGNTATF3T

Ezekiel 37 in the THAI

Ezekiel 37 in the TNFD

Ezekiel 37 in the TNT

Ezekiel 37 in the TNTIK

Ezekiel 37 in the TNTIL

Ezekiel 37 in the TNTIN

Ezekiel 37 in the TNTIP

Ezekiel 37 in the TNTIZ

Ezekiel 37 in the TOMA

Ezekiel 37 in the TTENT

Ezekiel 37 in the UBG

Ezekiel 37 in the UGV

Ezekiel 37 in the UGV2

Ezekiel 37 in the UGV3

Ezekiel 37 in the VBL

Ezekiel 37 in the VDCC

Ezekiel 37 in the YALU

Ezekiel 37 in the YAPE

Ezekiel 37 in the YBVTP

Ezekiel 37 in the ZBP