Genesis 2 (BOKCV)
1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. 2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. 3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. 4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. BWANA Mungu alipoziumba mbingu na dunia, 5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa BWANA Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, 6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: 7 BWANA Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. 8 Basi BWANA Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. 9 BWANA Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya. 10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. 11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. 12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. 14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati. 15 BWANA Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. 16 BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, 17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.” 18 BWANA Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” 19 Basi BWANA Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. 20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini.Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. 21 Hivyo BWANA Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. 22 Kisha BWANA Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. 23 Huyo mwanaume akasema,“Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yanguna nyama ya nyama yangu,ataitwa ‘mwanamke,’kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” 24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. 25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu.
In Other Versions
Genesis 2 in the ANGEFD
Genesis 2 in the ANTPNG2D
Genesis 2 in the AS21
Genesis 2 in the BAGH
Genesis 2 in the BBPNG
Genesis 2 in the BBT1E
Genesis 2 in the BDS
Genesis 2 in the BEV
Genesis 2 in the BHAD
Genesis 2 in the BIB
Genesis 2 in the BLPT
Genesis 2 in the BNT
Genesis 2 in the BNTABOOT
Genesis 2 in the BNTLV
Genesis 2 in the BOATCB
Genesis 2 in the BOATCB2
Genesis 2 in the BOBCV
Genesis 2 in the BOCNT
Genesis 2 in the BOECS
Genesis 2 in the BOGWICC
Genesis 2 in the BOHCB
Genesis 2 in the BOHCV
Genesis 2 in the BOHLNT
Genesis 2 in the BOHNTLTAL
Genesis 2 in the BOICB
Genesis 2 in the BOILNTAP
Genesis 2 in the BOITCV
Genesis 2 in the BOKCV2
Genesis 2 in the BOKHWOG
Genesis 2 in the BOKSSV
Genesis 2 in the BOLCB
Genesis 2 in the BOLCB2
Genesis 2 in the BOMCV
Genesis 2 in the BONAV
Genesis 2 in the BONCB
Genesis 2 in the BONLT
Genesis 2 in the BONUT2
Genesis 2 in the BOPLNT
Genesis 2 in the BOSCB
Genesis 2 in the BOSNC
Genesis 2 in the BOTLNT
Genesis 2 in the BOVCB
Genesis 2 in the BOYCB
Genesis 2 in the BPBB
Genesis 2 in the BPH
Genesis 2 in the BSB
Genesis 2 in the CCB
Genesis 2 in the CUV
Genesis 2 in the CUVS
Genesis 2 in the DBT
Genesis 2 in the DGDNT
Genesis 2 in the DHNT
Genesis 2 in the DNT
Genesis 2 in the ELBE
Genesis 2 in the EMTV
Genesis 2 in the ESV
Genesis 2 in the FBV
Genesis 2 in the FEB
Genesis 2 in the GGMNT
Genesis 2 in the GNT
Genesis 2 in the HARY
Genesis 2 in the HNT
Genesis 2 in the IRVA
Genesis 2 in the IRVB
Genesis 2 in the IRVG
Genesis 2 in the IRVH
Genesis 2 in the IRVK
Genesis 2 in the IRVM
Genesis 2 in the IRVM2
Genesis 2 in the IRVO
Genesis 2 in the IRVP
Genesis 2 in the IRVT
Genesis 2 in the IRVT2
Genesis 2 in the IRVU
Genesis 2 in the ISVN
Genesis 2 in the JSNT
Genesis 2 in the KAPI
Genesis 2 in the KBT1ETNIK
Genesis 2 in the KBV
Genesis 2 in the KJV
Genesis 2 in the KNFD
Genesis 2 in the LBA
Genesis 2 in the LBLA
Genesis 2 in the LNT
Genesis 2 in the LSV
Genesis 2 in the MAAL
Genesis 2 in the MBV
Genesis 2 in the MBV2
Genesis 2 in the MHNT
Genesis 2 in the MKNFD
Genesis 2 in the MNG
Genesis 2 in the MNT
Genesis 2 in the MNT2
Genesis 2 in the MRS1T
Genesis 2 in the NAA
Genesis 2 in the NASB
Genesis 2 in the NBLA
Genesis 2 in the NBS
Genesis 2 in the NBVTP
Genesis 2 in the NET2
Genesis 2 in the NIV11
Genesis 2 in the NNT
Genesis 2 in the NNT2
Genesis 2 in the NNT3
Genesis 2 in the PDDPT
Genesis 2 in the PFNT
Genesis 2 in the RMNT
Genesis 2 in the SBIAS
Genesis 2 in the SBIBS
Genesis 2 in the SBIBS2
Genesis 2 in the SBICS
Genesis 2 in the SBIDS
Genesis 2 in the SBIGS
Genesis 2 in the SBIHS
Genesis 2 in the SBIIS
Genesis 2 in the SBIIS2
Genesis 2 in the SBIIS3
Genesis 2 in the SBIKS
Genesis 2 in the SBIKS2
Genesis 2 in the SBIMS
Genesis 2 in the SBIOS
Genesis 2 in the SBIPS
Genesis 2 in the SBISS
Genesis 2 in the SBITS
Genesis 2 in the SBITS2
Genesis 2 in the SBITS3
Genesis 2 in the SBITS4
Genesis 2 in the SBIUS
Genesis 2 in the SBIVS
Genesis 2 in the SBT
Genesis 2 in the SBT1E
Genesis 2 in the SCHL
Genesis 2 in the SNT
Genesis 2 in the SUSU
Genesis 2 in the SUSU2
Genesis 2 in the SYNO
Genesis 2 in the TBIAOTANT
Genesis 2 in the TBT1E
Genesis 2 in the TBT1E2
Genesis 2 in the TFTIP
Genesis 2 in the TFTU
Genesis 2 in the TGNTATF3T
Genesis 2 in the THAI
Genesis 2 in the TNFD
Genesis 2 in the TNT
Genesis 2 in the TNTIK
Genesis 2 in the TNTIL
Genesis 2 in the TNTIN
Genesis 2 in the TNTIP
Genesis 2 in the TNTIZ
Genesis 2 in the TOMA
Genesis 2 in the TTENT
Genesis 2 in the UBG
Genesis 2 in the UGV
Genesis 2 in the UGV2
Genesis 2 in the UGV3
Genesis 2 in the VBL
Genesis 2 in the VDCC
Genesis 2 in the YALU
Genesis 2 in the YAPE
Genesis 2 in the YBVTP
Genesis 2 in the ZBP