Genesis 22 (BOKCV)

1 Baadaye Mungu akamjaribu Abrahamu. Akamwambia, “Abrahamu!”Abrahamu akajibu, “Mimi hapa.” 2 Kisha Mungu akamwambia, “Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, Isaki umpendaye, uende katika nchi ya Moria. Mtoe huko kama sadaka ya kuteketezwa juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.” 3 Abrahamu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaki mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia. 4 Siku ya tatu Abrahamu akainua macho, akapaona mahali pale kwa mbali. 5 Akawaambia watumishi wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, wakati mimi na kijana tunakwenda kule. Tutakwenda kuabudu na kisha tutawarudia.” 6 Abrahamu akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, akamtwika Isaki mwanawe, yeye mwenyewe akachukua moto na kisu. Walipokuwa wakienda pamoja, 7 Isaki akanena akamwambia Abrahamu baba yake, “Baba yangu!”Abrahamu akaitika, “Mimi hapa, mwanangu.”Isaki akasema, “Moto na kuni zipo, Je, yuko wapi mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?” 8 Abrahamu akajibu, “Mwanangu, Mungu mwenyewe atajipatia mwana-kondoo kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa.” Nao hawa wawili wakaendelea mbele pamoja. 9 Walipofika mahali pale alipokuwa ameambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu hapo, akaziweka kuni juu yake. Akamfunga Isaki mwanawe na akamlaza kwenye madhabahu, juu ya zile kuni. 10 Kisha akanyoosha mkono wake na akachukua kisu ili amchinje mwanawe. 11 Lakini malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, “Abrahamu! Abrahamu!”Akajibu, “Mimi hapa.” 12 Akamwambia, “Usimdhuru kijana, wala usimtendee jambo lolote. Sasa ninajua kwamba unamcha Mungu, kwa sababu hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee.” 13 Abrahamu akainua macho yake, akaona kondoo dume amenaswa pembe zake nyuma yake katika kichaka. Akaenda akamchukua huyo kondoo dume, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe. 14 Abrahamu akapaita mahali pale Yehova-Yire. Mpaka siku ya leo inasemekana, “Katika mlima wa BWANA itapatikana.” 15 Basi malaika wa BWANA akamwita Abrahamu kutoka mbinguni mara ya pili, 16 akasema, “Ninaapa kwa nafsi yangu, asema BWANA, kwamba kwa sababu umefanya jambo hili na hukunizuilia mwanao, mwana wako wa pekee, 17 hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao, 18 na kupitia uzao wako mataifa yote duniani yatabarikiwa, kwa sababu umenitii.” 19 Ndipo Abrahamu akawarudia watumishi wake, wakaondoka wakaenda wote pamoja mpaka Beer-Sheba. Abrahamu akaishi huko Beer-Sheba. 20 Baada ya muda, Abrahamu akaambiwa, “Milka pia amepata watoto, amemzalia ndugu yako Nahori wana: 21 Usi mzaliwa wake wa kwanza, Buzi nduguye, Kemueli (baba wa Aramu), 22 Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu na Bethueli.” 23 Bethueli akamzaa Rebeka. Milka alimzalia Nahori nduguye Abrahamu hao wana wanane. 24 Suria wake Nahori aliyeitwa Reuma pia alikuwa na wana: Teba, Gahamu, Tahashi na Maaka.

In Other Versions

Genesis 22 in the ANGEFD

Genesis 22 in the ANTPNG2D

Genesis 22 in the AS21

Genesis 22 in the BAGH

Genesis 22 in the BBPNG

Genesis 22 in the BBT1E

Genesis 22 in the BDS

Genesis 22 in the BEV

Genesis 22 in the BHAD

Genesis 22 in the BIB

Genesis 22 in the BLPT

Genesis 22 in the BNT

Genesis 22 in the BNTABOOT

Genesis 22 in the BNTLV

Genesis 22 in the BOATCB

Genesis 22 in the BOATCB2

Genesis 22 in the BOBCV

Genesis 22 in the BOCNT

Genesis 22 in the BOECS

Genesis 22 in the BOGWICC

Genesis 22 in the BOHCB

Genesis 22 in the BOHCV

Genesis 22 in the BOHLNT

Genesis 22 in the BOHNTLTAL

Genesis 22 in the BOICB

Genesis 22 in the BOILNTAP

Genesis 22 in the BOITCV

Genesis 22 in the BOKCV2

Genesis 22 in the BOKHWOG

Genesis 22 in the BOKSSV

Genesis 22 in the BOLCB

Genesis 22 in the BOLCB2

Genesis 22 in the BOMCV

Genesis 22 in the BONAV

Genesis 22 in the BONCB

Genesis 22 in the BONLT

Genesis 22 in the BONUT2

Genesis 22 in the BOPLNT

Genesis 22 in the BOSCB

Genesis 22 in the BOSNC

Genesis 22 in the BOTLNT

Genesis 22 in the BOVCB

Genesis 22 in the BOYCB

Genesis 22 in the BPBB

Genesis 22 in the BPH

Genesis 22 in the BSB

Genesis 22 in the CCB

Genesis 22 in the CUV

Genesis 22 in the CUVS

Genesis 22 in the DBT

Genesis 22 in the DGDNT

Genesis 22 in the DHNT

Genesis 22 in the DNT

Genesis 22 in the ELBE

Genesis 22 in the EMTV

Genesis 22 in the ESV

Genesis 22 in the FBV

Genesis 22 in the FEB

Genesis 22 in the GGMNT

Genesis 22 in the GNT

Genesis 22 in the HARY

Genesis 22 in the HNT

Genesis 22 in the IRVA

Genesis 22 in the IRVB

Genesis 22 in the IRVG

Genesis 22 in the IRVH

Genesis 22 in the IRVK

Genesis 22 in the IRVM

Genesis 22 in the IRVM2

Genesis 22 in the IRVO

Genesis 22 in the IRVP

Genesis 22 in the IRVT

Genesis 22 in the IRVT2

Genesis 22 in the IRVU

Genesis 22 in the ISVN

Genesis 22 in the JSNT

Genesis 22 in the KAPI

Genesis 22 in the KBT1ETNIK

Genesis 22 in the KBV

Genesis 22 in the KJV

Genesis 22 in the KNFD

Genesis 22 in the LBA

Genesis 22 in the LBLA

Genesis 22 in the LNT

Genesis 22 in the LSV

Genesis 22 in the MAAL

Genesis 22 in the MBV

Genesis 22 in the MBV2

Genesis 22 in the MHNT

Genesis 22 in the MKNFD

Genesis 22 in the MNG

Genesis 22 in the MNT

Genesis 22 in the MNT2

Genesis 22 in the MRS1T

Genesis 22 in the NAA

Genesis 22 in the NASB

Genesis 22 in the NBLA

Genesis 22 in the NBS

Genesis 22 in the NBVTP

Genesis 22 in the NET2

Genesis 22 in the NIV11

Genesis 22 in the NNT

Genesis 22 in the NNT2

Genesis 22 in the NNT3

Genesis 22 in the PDDPT

Genesis 22 in the PFNT

Genesis 22 in the RMNT

Genesis 22 in the SBIAS

Genesis 22 in the SBIBS

Genesis 22 in the SBIBS2

Genesis 22 in the SBICS

Genesis 22 in the SBIDS

Genesis 22 in the SBIGS

Genesis 22 in the SBIHS

Genesis 22 in the SBIIS

Genesis 22 in the SBIIS2

Genesis 22 in the SBIIS3

Genesis 22 in the SBIKS

Genesis 22 in the SBIKS2

Genesis 22 in the SBIMS

Genesis 22 in the SBIOS

Genesis 22 in the SBIPS

Genesis 22 in the SBISS

Genesis 22 in the SBITS

Genesis 22 in the SBITS2

Genesis 22 in the SBITS3

Genesis 22 in the SBITS4

Genesis 22 in the SBIUS

Genesis 22 in the SBIVS

Genesis 22 in the SBT

Genesis 22 in the SBT1E

Genesis 22 in the SCHL

Genesis 22 in the SNT

Genesis 22 in the SUSU

Genesis 22 in the SUSU2

Genesis 22 in the SYNO

Genesis 22 in the TBIAOTANT

Genesis 22 in the TBT1E

Genesis 22 in the TBT1E2

Genesis 22 in the TFTIP

Genesis 22 in the TFTU

Genesis 22 in the TGNTATF3T

Genesis 22 in the THAI

Genesis 22 in the TNFD

Genesis 22 in the TNT

Genesis 22 in the TNTIK

Genesis 22 in the TNTIL

Genesis 22 in the TNTIN

Genesis 22 in the TNTIP

Genesis 22 in the TNTIZ

Genesis 22 in the TOMA

Genesis 22 in the TTENT

Genesis 22 in the UBG

Genesis 22 in the UGV

Genesis 22 in the UGV2

Genesis 22 in the UGV3

Genesis 22 in the VBL

Genesis 22 in the VDCC

Genesis 22 in the YALU

Genesis 22 in the YAPE

Genesis 22 in the YBVTP

Genesis 22 in the ZBP