Genesis 35 (BOKCV)
1 Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.” 2 Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. 3 Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” 4 Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. 5 Kisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo. 6 Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. 7 Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli, kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake. 8 Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi. 9 Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. 10 Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli. 11 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. 12 Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” 13 Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye. 14 Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. 15 Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli. 16 Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. 17 Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” 18 Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni. Lakini babaye akamwita Benyamini. 19 Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). 20 Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli. 21 Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. 22 Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili. Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili: 23 Wana wa Lea walikuwa:Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo,Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni. 24 Wana wa Raheli walikuwa:Yosefu na Benyamini. 25 Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa:Dani na Naftali. 26 Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa:Gadi na Asheri.Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu. 27 Yakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. 28 Isaki aliishi miaka 180. 29 Kisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika.
In Other Versions
Genesis 35 in the ANGEFD
Genesis 35 in the ANTPNG2D
Genesis 35 in the AS21
Genesis 35 in the BAGH
Genesis 35 in the BBPNG
Genesis 35 in the BBT1E
Genesis 35 in the BDS
Genesis 35 in the BEV
Genesis 35 in the BHAD
Genesis 35 in the BIB
Genesis 35 in the BLPT
Genesis 35 in the BNT
Genesis 35 in the BNTABOOT
Genesis 35 in the BNTLV
Genesis 35 in the BOATCB
Genesis 35 in the BOATCB2
Genesis 35 in the BOBCV
Genesis 35 in the BOCNT
Genesis 35 in the BOECS
Genesis 35 in the BOGWICC
Genesis 35 in the BOHCB
Genesis 35 in the BOHCV
Genesis 35 in the BOHLNT
Genesis 35 in the BOHNTLTAL
Genesis 35 in the BOICB
Genesis 35 in the BOILNTAP
Genesis 35 in the BOITCV
Genesis 35 in the BOKCV2
Genesis 35 in the BOKHWOG
Genesis 35 in the BOKSSV
Genesis 35 in the BOLCB
Genesis 35 in the BOLCB2
Genesis 35 in the BOMCV
Genesis 35 in the BONAV
Genesis 35 in the BONCB
Genesis 35 in the BONLT
Genesis 35 in the BONUT2
Genesis 35 in the BOPLNT
Genesis 35 in the BOSCB
Genesis 35 in the BOSNC
Genesis 35 in the BOTLNT
Genesis 35 in the BOVCB
Genesis 35 in the BOYCB
Genesis 35 in the BPBB
Genesis 35 in the BPH
Genesis 35 in the BSB
Genesis 35 in the CCB
Genesis 35 in the CUV
Genesis 35 in the CUVS
Genesis 35 in the DBT
Genesis 35 in the DGDNT
Genesis 35 in the DHNT
Genesis 35 in the DNT
Genesis 35 in the ELBE
Genesis 35 in the EMTV
Genesis 35 in the ESV
Genesis 35 in the FBV
Genesis 35 in the FEB
Genesis 35 in the GGMNT
Genesis 35 in the GNT
Genesis 35 in the HARY
Genesis 35 in the HNT
Genesis 35 in the IRVA
Genesis 35 in the IRVB
Genesis 35 in the IRVG
Genesis 35 in the IRVH
Genesis 35 in the IRVK
Genesis 35 in the IRVM
Genesis 35 in the IRVM2
Genesis 35 in the IRVO
Genesis 35 in the IRVP
Genesis 35 in the IRVT
Genesis 35 in the IRVT2
Genesis 35 in the IRVU
Genesis 35 in the ISVN
Genesis 35 in the JSNT
Genesis 35 in the KAPI
Genesis 35 in the KBT1ETNIK
Genesis 35 in the KBV
Genesis 35 in the KJV
Genesis 35 in the KNFD
Genesis 35 in the LBA
Genesis 35 in the LBLA
Genesis 35 in the LNT
Genesis 35 in the LSV
Genesis 35 in the MAAL
Genesis 35 in the MBV
Genesis 35 in the MBV2
Genesis 35 in the MHNT
Genesis 35 in the MKNFD
Genesis 35 in the MNG
Genesis 35 in the MNT
Genesis 35 in the MNT2
Genesis 35 in the MRS1T
Genesis 35 in the NAA
Genesis 35 in the NASB
Genesis 35 in the NBLA
Genesis 35 in the NBS
Genesis 35 in the NBVTP
Genesis 35 in the NET2
Genesis 35 in the NIV11
Genesis 35 in the NNT
Genesis 35 in the NNT2
Genesis 35 in the NNT3
Genesis 35 in the PDDPT
Genesis 35 in the PFNT
Genesis 35 in the RMNT
Genesis 35 in the SBIAS
Genesis 35 in the SBIBS
Genesis 35 in the SBIBS2
Genesis 35 in the SBICS
Genesis 35 in the SBIDS
Genesis 35 in the SBIGS
Genesis 35 in the SBIHS
Genesis 35 in the SBIIS
Genesis 35 in the SBIIS2
Genesis 35 in the SBIIS3
Genesis 35 in the SBIKS
Genesis 35 in the SBIKS2
Genesis 35 in the SBIMS
Genesis 35 in the SBIOS
Genesis 35 in the SBIPS
Genesis 35 in the SBISS
Genesis 35 in the SBITS
Genesis 35 in the SBITS2
Genesis 35 in the SBITS3
Genesis 35 in the SBITS4
Genesis 35 in the SBIUS
Genesis 35 in the SBIVS
Genesis 35 in the SBT
Genesis 35 in the SBT1E
Genesis 35 in the SCHL
Genesis 35 in the SNT
Genesis 35 in the SUSU
Genesis 35 in the SUSU2
Genesis 35 in the SYNO
Genesis 35 in the TBIAOTANT
Genesis 35 in the TBT1E
Genesis 35 in the TBT1E2
Genesis 35 in the TFTIP
Genesis 35 in the TFTU
Genesis 35 in the TGNTATF3T
Genesis 35 in the THAI
Genesis 35 in the TNFD
Genesis 35 in the TNT
Genesis 35 in the TNTIK
Genesis 35 in the TNTIL
Genesis 35 in the TNTIN
Genesis 35 in the TNTIP
Genesis 35 in the TNTIZ
Genesis 35 in the TOMA
Genesis 35 in the TTENT
Genesis 35 in the UBG
Genesis 35 in the UGV
Genesis 35 in the UGV2
Genesis 35 in the UGV3
Genesis 35 in the VBL
Genesis 35 in the VDCC
Genesis 35 in the YALU
Genesis 35 in the YAPE
Genesis 35 in the YBVTP
Genesis 35 in the ZBP