Genesis 8 (BOKCV)
1 Mungu akamkumbuka Noa na wanyama wote wa porini na wa kufugwa waliokuwa naye ndani ya safina, akatuma upepo ukavuma katika dunia, nayo maji yakaondoka. 2 Zile chemchemi zilizo chini sana ya ardhi pamoja na malango ya mafuriko ya mbinguni yakawa yamefungwa nayo mvua ikawa imekoma kunyesha kutoka angani. 3 Maji yakaendelea kupungua taratibu katika nchi. Kunako mwisho wa siku ya 150, maji yalikuwa yamepungua, 4 katika siku ya kumi na saba ya mwezi wa saba, safina ikatua katika milima ya Ararati. 5 Maji yakaendelea kupungua hadi mwezi wa kumi, na siku ya kwanza ya mwezi wa kumi, vilele vya milima vikaonekana. 6 Baada ya siku arobaini Noa akafungua dirisha alilokuwa amelifanya katika safina 7 na akamtoa kunguru, akawa akiruka kwenda na kurudi mpaka maji yalipokwisha kukauka juu ya nchi. 8 Kisha akamtoa hua ili aone kama maji yameondoka juu ya uso wa ardhi. 9 Lakini hua hakupata mahali pa kutua kwa kuwa maji yalienea juu ya uso wa dunia yote, kwa hiyo akarudi kwa Noa ndani ya safina. Noa akanyoosha mkono akamchukua yule hua akamrudisha ndani ya safina. 10 Noa akangojea siku saba zaidi kisha akamtoa tena hua kutoka safina. 11 Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia. 12 Akangojea siku saba zaidi na akamtuma tena hua, lakini wakati huu hua hakurudi tena kwa Noa. 13 Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka. 14 Katika siku ya ishirini na saba ya mwezi wa pili dunia ilikuwa imekauka kabisa. 15 Ndipo Mungu akamwambia Noa, 16 “Toka ndani ya safina, wewe na mkeo na wanao na wake zao. 17 Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.” 18 Kwa hiyo Noa akatoka nje pamoja na mkewe, wanawe na wake zao. 19 Wanyama wote na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi na ndege wote, kila kitu kiendacho juu ya nchi, aina moja baada ya nyingine vikatoka katika safina, kila aina ya kiumbe, kimoja baada ya kingine. 20 Kisha Noa akamjengea BWANA madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. 21 BWANA akasikia harufu nzuri ya kupendeza, naye akasema moyoni mwake, “Kamwe sitailaani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, hata ingawa kila mwelekeo wa moyo wake ni mbaya tangu ujana. Kamwe sitaangamiza tena viumbe hai vyote kama nilivyofanya. 22 “Kwa muda dunia idumupo,wakati wa kupanda na wa kuvuna,wakati wa baridi na wa joto,wakati wa kiangazi na wa masika,usiku na mchanakamwe havitakoma.”
In Other Versions
Genesis 8 in the ANGEFD
Genesis 8 in the ANTPNG2D
Genesis 8 in the AS21
Genesis 8 in the BAGH
Genesis 8 in the BBPNG
Genesis 8 in the BBT1E
Genesis 8 in the BDS
Genesis 8 in the BEV
Genesis 8 in the BHAD
Genesis 8 in the BIB
Genesis 8 in the BLPT
Genesis 8 in the BNT
Genesis 8 in the BNTABOOT
Genesis 8 in the BNTLV
Genesis 8 in the BOATCB
Genesis 8 in the BOATCB2
Genesis 8 in the BOBCV
Genesis 8 in the BOCNT
Genesis 8 in the BOECS
Genesis 8 in the BOGWICC
Genesis 8 in the BOHCB
Genesis 8 in the BOHCV
Genesis 8 in the BOHLNT
Genesis 8 in the BOHNTLTAL
Genesis 8 in the BOICB
Genesis 8 in the BOILNTAP
Genesis 8 in the BOITCV
Genesis 8 in the BOKCV2
Genesis 8 in the BOKHWOG
Genesis 8 in the BOKSSV
Genesis 8 in the BOLCB
Genesis 8 in the BOLCB2
Genesis 8 in the BOMCV
Genesis 8 in the BONAV
Genesis 8 in the BONCB
Genesis 8 in the BONLT
Genesis 8 in the BONUT2
Genesis 8 in the BOPLNT
Genesis 8 in the BOSCB
Genesis 8 in the BOSNC
Genesis 8 in the BOTLNT
Genesis 8 in the BOVCB
Genesis 8 in the BOYCB
Genesis 8 in the BPBB
Genesis 8 in the BPH
Genesis 8 in the BSB
Genesis 8 in the CCB
Genesis 8 in the CUV
Genesis 8 in the CUVS
Genesis 8 in the DBT
Genesis 8 in the DGDNT
Genesis 8 in the DHNT
Genesis 8 in the DNT
Genesis 8 in the ELBE
Genesis 8 in the EMTV
Genesis 8 in the ESV
Genesis 8 in the FBV
Genesis 8 in the FEB
Genesis 8 in the GGMNT
Genesis 8 in the GNT
Genesis 8 in the HARY
Genesis 8 in the HNT
Genesis 8 in the IRVA
Genesis 8 in the IRVB
Genesis 8 in the IRVG
Genesis 8 in the IRVH
Genesis 8 in the IRVK
Genesis 8 in the IRVM
Genesis 8 in the IRVM2
Genesis 8 in the IRVO
Genesis 8 in the IRVP
Genesis 8 in the IRVT
Genesis 8 in the IRVT2
Genesis 8 in the IRVU
Genesis 8 in the ISVN
Genesis 8 in the JSNT
Genesis 8 in the KAPI
Genesis 8 in the KBT1ETNIK
Genesis 8 in the KBV
Genesis 8 in the KJV
Genesis 8 in the KNFD
Genesis 8 in the LBA
Genesis 8 in the LBLA
Genesis 8 in the LNT
Genesis 8 in the LSV
Genesis 8 in the MAAL
Genesis 8 in the MBV
Genesis 8 in the MBV2
Genesis 8 in the MHNT
Genesis 8 in the MKNFD
Genesis 8 in the MNG
Genesis 8 in the MNT
Genesis 8 in the MNT2
Genesis 8 in the MRS1T
Genesis 8 in the NAA
Genesis 8 in the NASB
Genesis 8 in the NBLA
Genesis 8 in the NBS
Genesis 8 in the NBVTP
Genesis 8 in the NET2
Genesis 8 in the NIV11
Genesis 8 in the NNT
Genesis 8 in the NNT2
Genesis 8 in the NNT3
Genesis 8 in the PDDPT
Genesis 8 in the PFNT
Genesis 8 in the RMNT
Genesis 8 in the SBIAS
Genesis 8 in the SBIBS
Genesis 8 in the SBIBS2
Genesis 8 in the SBICS
Genesis 8 in the SBIDS
Genesis 8 in the SBIGS
Genesis 8 in the SBIHS
Genesis 8 in the SBIIS
Genesis 8 in the SBIIS2
Genesis 8 in the SBIIS3
Genesis 8 in the SBIKS
Genesis 8 in the SBIKS2
Genesis 8 in the SBIMS
Genesis 8 in the SBIOS
Genesis 8 in the SBIPS
Genesis 8 in the SBISS
Genesis 8 in the SBITS
Genesis 8 in the SBITS2
Genesis 8 in the SBITS3
Genesis 8 in the SBITS4
Genesis 8 in the SBIUS
Genesis 8 in the SBIVS
Genesis 8 in the SBT
Genesis 8 in the SBT1E
Genesis 8 in the SCHL
Genesis 8 in the SNT
Genesis 8 in the SUSU
Genesis 8 in the SUSU2
Genesis 8 in the SYNO
Genesis 8 in the TBIAOTANT
Genesis 8 in the TBT1E
Genesis 8 in the TBT1E2
Genesis 8 in the TFTIP
Genesis 8 in the TFTU
Genesis 8 in the TGNTATF3T
Genesis 8 in the THAI
Genesis 8 in the TNFD
Genesis 8 in the TNT
Genesis 8 in the TNTIK
Genesis 8 in the TNTIL
Genesis 8 in the TNTIN
Genesis 8 in the TNTIP
Genesis 8 in the TNTIZ
Genesis 8 in the TOMA
Genesis 8 in the TTENT
Genesis 8 in the UBG
Genesis 8 in the UGV
Genesis 8 in the UGV2
Genesis 8 in the UGV3
Genesis 8 in the VBL
Genesis 8 in the VDCC
Genesis 8 in the YALU
Genesis 8 in the YAPE
Genesis 8 in the YBVTP
Genesis 8 in the ZBP