Jeremiah 41 (BOKCV)

1 Katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme na pia alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa. Walipokuwa wakila pamoja huko, 2 Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi. 3 Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari wa Kikaldayo waliokuwa huko. 4 Siku moja baada ya kuuawa kwa siri kwa Gedalia, kabla mtu yeyote hajafahamu jambo hilo, 5 watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya BWANA. 6 Ishmaeli mwana wa Nethania akaondoka Mispa ili kwenda kuwalaki, huku akilia alipokuwa akienda. Alipokutana nao, akasema, “Karibuni kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.” 7 Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu waliokuwa pamoja naye wakawachinja na kuwatupa ndani ya kisima. 8 Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine. 9 Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti. 10 Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao: walikuwa binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni. 11 Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye waliposikia juu ya uhalifu wote ambao Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa ameufanya, 12 waliwachukua watu wao wote kwenda kupigana na Ishmaeli mwana wa Nethania. Wakakutana naye karibu na bwawa kubwa huko Gibeoni. 13 Ikawa watu wote waliokuwa na Ishmaeli walipomwona Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa pamoja naye, wakafurahi. 14 Watu wote ambao Ishmaeli alikuwa amewachukua mateka huko Mispa wakageuka na kumfuata Yohanani mwana wa Karea. 15 Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na watu wake wanane wakamtoroka Yohanani na kukimbilia kwa Waamoni. 16 Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu: walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni. 17 Kisha wakaenda mbele na kutua Geruth-Kimhamu karibu na Bethlehemu wakiwa njiani kwenda Misri 18 ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye alikuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

In Other Versions

Jeremiah 41 in the ANGEFD

Jeremiah 41 in the ANTPNG2D

Jeremiah 41 in the AS21

Jeremiah 41 in the BAGH

Jeremiah 41 in the BBPNG

Jeremiah 41 in the BBT1E

Jeremiah 41 in the BDS

Jeremiah 41 in the BEV

Jeremiah 41 in the BHAD

Jeremiah 41 in the BIB

Jeremiah 41 in the BLPT

Jeremiah 41 in the BNT

Jeremiah 41 in the BNTABOOT

Jeremiah 41 in the BNTLV

Jeremiah 41 in the BOATCB

Jeremiah 41 in the BOATCB2

Jeremiah 41 in the BOBCV

Jeremiah 41 in the BOCNT

Jeremiah 41 in the BOECS

Jeremiah 41 in the BOGWICC

Jeremiah 41 in the BOHCB

Jeremiah 41 in the BOHCV

Jeremiah 41 in the BOHLNT

Jeremiah 41 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 41 in the BOICB

Jeremiah 41 in the BOILNTAP

Jeremiah 41 in the BOITCV

Jeremiah 41 in the BOKCV2

Jeremiah 41 in the BOKHWOG

Jeremiah 41 in the BOKSSV

Jeremiah 41 in the BOLCB

Jeremiah 41 in the BOLCB2

Jeremiah 41 in the BOMCV

Jeremiah 41 in the BONAV

Jeremiah 41 in the BONCB

Jeremiah 41 in the BONLT

Jeremiah 41 in the BONUT2

Jeremiah 41 in the BOPLNT

Jeremiah 41 in the BOSCB

Jeremiah 41 in the BOSNC

Jeremiah 41 in the BOTLNT

Jeremiah 41 in the BOVCB

Jeremiah 41 in the BOYCB

Jeremiah 41 in the BPBB

Jeremiah 41 in the BPH

Jeremiah 41 in the BSB

Jeremiah 41 in the CCB

Jeremiah 41 in the CUV

Jeremiah 41 in the CUVS

Jeremiah 41 in the DBT

Jeremiah 41 in the DGDNT

Jeremiah 41 in the DHNT

Jeremiah 41 in the DNT

Jeremiah 41 in the ELBE

Jeremiah 41 in the EMTV

Jeremiah 41 in the ESV

Jeremiah 41 in the FBV

Jeremiah 41 in the FEB

Jeremiah 41 in the GGMNT

Jeremiah 41 in the GNT

Jeremiah 41 in the HARY

Jeremiah 41 in the HNT

Jeremiah 41 in the IRVA

Jeremiah 41 in the IRVB

Jeremiah 41 in the IRVG

Jeremiah 41 in the IRVH

Jeremiah 41 in the IRVK

Jeremiah 41 in the IRVM

Jeremiah 41 in the IRVM2

Jeremiah 41 in the IRVO

Jeremiah 41 in the IRVP

Jeremiah 41 in the IRVT

Jeremiah 41 in the IRVT2

Jeremiah 41 in the IRVU

Jeremiah 41 in the ISVN

Jeremiah 41 in the JSNT

Jeremiah 41 in the KAPI

Jeremiah 41 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 41 in the KBV

Jeremiah 41 in the KJV

Jeremiah 41 in the KNFD

Jeremiah 41 in the LBA

Jeremiah 41 in the LBLA

Jeremiah 41 in the LNT

Jeremiah 41 in the LSV

Jeremiah 41 in the MAAL

Jeremiah 41 in the MBV

Jeremiah 41 in the MBV2

Jeremiah 41 in the MHNT

Jeremiah 41 in the MKNFD

Jeremiah 41 in the MNG

Jeremiah 41 in the MNT

Jeremiah 41 in the MNT2

Jeremiah 41 in the MRS1T

Jeremiah 41 in the NAA

Jeremiah 41 in the NASB

Jeremiah 41 in the NBLA

Jeremiah 41 in the NBS

Jeremiah 41 in the NBVTP

Jeremiah 41 in the NET2

Jeremiah 41 in the NIV11

Jeremiah 41 in the NNT

Jeremiah 41 in the NNT2

Jeremiah 41 in the NNT3

Jeremiah 41 in the PDDPT

Jeremiah 41 in the PFNT

Jeremiah 41 in the RMNT

Jeremiah 41 in the SBIAS

Jeremiah 41 in the SBIBS

Jeremiah 41 in the SBIBS2

Jeremiah 41 in the SBICS

Jeremiah 41 in the SBIDS

Jeremiah 41 in the SBIGS

Jeremiah 41 in the SBIHS

Jeremiah 41 in the SBIIS

Jeremiah 41 in the SBIIS2

Jeremiah 41 in the SBIIS3

Jeremiah 41 in the SBIKS

Jeremiah 41 in the SBIKS2

Jeremiah 41 in the SBIMS

Jeremiah 41 in the SBIOS

Jeremiah 41 in the SBIPS

Jeremiah 41 in the SBISS

Jeremiah 41 in the SBITS

Jeremiah 41 in the SBITS2

Jeremiah 41 in the SBITS3

Jeremiah 41 in the SBITS4

Jeremiah 41 in the SBIUS

Jeremiah 41 in the SBIVS

Jeremiah 41 in the SBT

Jeremiah 41 in the SBT1E

Jeremiah 41 in the SCHL

Jeremiah 41 in the SNT

Jeremiah 41 in the SUSU

Jeremiah 41 in the SUSU2

Jeremiah 41 in the SYNO

Jeremiah 41 in the TBIAOTANT

Jeremiah 41 in the TBT1E

Jeremiah 41 in the TBT1E2

Jeremiah 41 in the TFTIP

Jeremiah 41 in the TFTU

Jeremiah 41 in the TGNTATF3T

Jeremiah 41 in the THAI

Jeremiah 41 in the TNFD

Jeremiah 41 in the TNT

Jeremiah 41 in the TNTIK

Jeremiah 41 in the TNTIL

Jeremiah 41 in the TNTIN

Jeremiah 41 in the TNTIP

Jeremiah 41 in the TNTIZ

Jeremiah 41 in the TOMA

Jeremiah 41 in the TTENT

Jeremiah 41 in the UBG

Jeremiah 41 in the UGV

Jeremiah 41 in the UGV2

Jeremiah 41 in the UGV3

Jeremiah 41 in the VBL

Jeremiah 41 in the VDCC

Jeremiah 41 in the YALU

Jeremiah 41 in the YAPE

Jeremiah 41 in the YBVTP

Jeremiah 41 in the ZBP