Jeremiah 9 (BOKCV)

1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya majina macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!Ningelia usiku na mchanakwa kuuawa kwa watu wangu. 2 Laiti ningekuwa na nyumbaya kukaa wasafiri jangwani,ningewaacha watu wanguna kwenda mbali nao,kwa kuwa wote ni wazinzi,kundi la watu wadanganyifu. 3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde,ili kurusha uongo;wamekuwa na nguvu katika nchilakini si katika ukweli.Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,hawanitambui mimi,”asema BWANA. 4 “Jihadhari na rafiki zako;usiwaamini ndugu zako.Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,na kila rafiki ni msingiziaji. 5 Rafiki humdanganya rafiki,hakuna yeyote asemaye kweli.Wamefundisha ndimi zao kudanganya,wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi. 6 Unakaa katikati ya udanganyifu;katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”asema BWANA. 7 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,kwani ni nini kingine niwezacho kufanyakwa sababu ya dhambi ya watu wangu? 8 Ndimi zao ni mshale wenye sumu,hunena kwa udanganyifu.Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,lakini moyoni mwake humtegea mtego. 9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”asema BWANA.“Je, nisijilipizie kisasikwa taifa kama hili?” 10 Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milimana kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,milio ya ngʼombe haisikiki.Ndege wa angani wametorokana wanyama wamekimbia. 11 “Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,makao ya mbweha;nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwaili asiwepo atakayeishi humo.” 12 Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa na BWANA awezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita? 13 BWANA akasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu. 14 Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.” 15 Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu. 16 Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.” 17 Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote:“Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,waite wale walio na ustadi kuliko wote. 18 Nao waje upesina kutuombolezea,mpaka macho yetu yafurike machozina vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu. 19 Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!Ni lazima tuihame nchi yetukwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ” 20 Basi, enyi wanawake, sikieni neno la BWANA;fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.Wafundisheni binti zenu kuomboleza;fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo. 21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;imewakatilia mbali watoto katika barabarana vijana waume kutoka viwanja vya miji. 22 Sema, “Hili ndilo asemalo BWANA:“ ‘Maiti za wanaume zitalalakama mavi katika mashamba,kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,wala hakuna anayekusanya.’ ” 23 Hili ndilo asemalo BWANA:“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,wala tajiri ajisifu katika utajiri wake, 24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:kwamba ananifahamu na kunijua mimi,kwamba mimi ndimi BWANA, nitendaye wema,hukumu na haki duniani,kwa kuwa napendezwa na haya,”asema BWANA. 25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asema BWANA, 26 yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”

In Other Versions

Jeremiah 9 in the ANGEFD

Jeremiah 9 in the ANTPNG2D

Jeremiah 9 in the AS21

Jeremiah 9 in the BAGH

Jeremiah 9 in the BBPNG

Jeremiah 9 in the BBT1E

Jeremiah 9 in the BDS

Jeremiah 9 in the BEV

Jeremiah 9 in the BHAD

Jeremiah 9 in the BIB

Jeremiah 9 in the BLPT

Jeremiah 9 in the BNT

Jeremiah 9 in the BNTABOOT

Jeremiah 9 in the BNTLV

Jeremiah 9 in the BOATCB

Jeremiah 9 in the BOATCB2

Jeremiah 9 in the BOBCV

Jeremiah 9 in the BOCNT

Jeremiah 9 in the BOECS

Jeremiah 9 in the BOGWICC

Jeremiah 9 in the BOHCB

Jeremiah 9 in the BOHCV

Jeremiah 9 in the BOHLNT

Jeremiah 9 in the BOHNTLTAL

Jeremiah 9 in the BOICB

Jeremiah 9 in the BOILNTAP

Jeremiah 9 in the BOITCV

Jeremiah 9 in the BOKCV2

Jeremiah 9 in the BOKHWOG

Jeremiah 9 in the BOKSSV

Jeremiah 9 in the BOLCB

Jeremiah 9 in the BOLCB2

Jeremiah 9 in the BOMCV

Jeremiah 9 in the BONAV

Jeremiah 9 in the BONCB

Jeremiah 9 in the BONLT

Jeremiah 9 in the BONUT2

Jeremiah 9 in the BOPLNT

Jeremiah 9 in the BOSCB

Jeremiah 9 in the BOSNC

Jeremiah 9 in the BOTLNT

Jeremiah 9 in the BOVCB

Jeremiah 9 in the BOYCB

Jeremiah 9 in the BPBB

Jeremiah 9 in the BPH

Jeremiah 9 in the BSB

Jeremiah 9 in the CCB

Jeremiah 9 in the CUV

Jeremiah 9 in the CUVS

Jeremiah 9 in the DBT

Jeremiah 9 in the DGDNT

Jeremiah 9 in the DHNT

Jeremiah 9 in the DNT

Jeremiah 9 in the ELBE

Jeremiah 9 in the EMTV

Jeremiah 9 in the ESV

Jeremiah 9 in the FBV

Jeremiah 9 in the FEB

Jeremiah 9 in the GGMNT

Jeremiah 9 in the GNT

Jeremiah 9 in the HARY

Jeremiah 9 in the HNT

Jeremiah 9 in the IRVA

Jeremiah 9 in the IRVB

Jeremiah 9 in the IRVG

Jeremiah 9 in the IRVH

Jeremiah 9 in the IRVK

Jeremiah 9 in the IRVM

Jeremiah 9 in the IRVM2

Jeremiah 9 in the IRVO

Jeremiah 9 in the IRVP

Jeremiah 9 in the IRVT

Jeremiah 9 in the IRVT2

Jeremiah 9 in the IRVU

Jeremiah 9 in the ISVN

Jeremiah 9 in the JSNT

Jeremiah 9 in the KAPI

Jeremiah 9 in the KBT1ETNIK

Jeremiah 9 in the KBV

Jeremiah 9 in the KJV

Jeremiah 9 in the KNFD

Jeremiah 9 in the LBA

Jeremiah 9 in the LBLA

Jeremiah 9 in the LNT

Jeremiah 9 in the LSV

Jeremiah 9 in the MAAL

Jeremiah 9 in the MBV

Jeremiah 9 in the MBV2

Jeremiah 9 in the MHNT

Jeremiah 9 in the MKNFD

Jeremiah 9 in the MNG

Jeremiah 9 in the MNT

Jeremiah 9 in the MNT2

Jeremiah 9 in the MRS1T

Jeremiah 9 in the NAA

Jeremiah 9 in the NASB

Jeremiah 9 in the NBLA

Jeremiah 9 in the NBS

Jeremiah 9 in the NBVTP

Jeremiah 9 in the NET2

Jeremiah 9 in the NIV11

Jeremiah 9 in the NNT

Jeremiah 9 in the NNT2

Jeremiah 9 in the NNT3

Jeremiah 9 in the PDDPT

Jeremiah 9 in the PFNT

Jeremiah 9 in the RMNT

Jeremiah 9 in the SBIAS

Jeremiah 9 in the SBIBS

Jeremiah 9 in the SBIBS2

Jeremiah 9 in the SBICS

Jeremiah 9 in the SBIDS

Jeremiah 9 in the SBIGS

Jeremiah 9 in the SBIHS

Jeremiah 9 in the SBIIS

Jeremiah 9 in the SBIIS2

Jeremiah 9 in the SBIIS3

Jeremiah 9 in the SBIKS

Jeremiah 9 in the SBIKS2

Jeremiah 9 in the SBIMS

Jeremiah 9 in the SBIOS

Jeremiah 9 in the SBIPS

Jeremiah 9 in the SBISS

Jeremiah 9 in the SBITS

Jeremiah 9 in the SBITS2

Jeremiah 9 in the SBITS3

Jeremiah 9 in the SBITS4

Jeremiah 9 in the SBIUS

Jeremiah 9 in the SBIVS

Jeremiah 9 in the SBT

Jeremiah 9 in the SBT1E

Jeremiah 9 in the SCHL

Jeremiah 9 in the SNT

Jeremiah 9 in the SUSU

Jeremiah 9 in the SUSU2

Jeremiah 9 in the SYNO

Jeremiah 9 in the TBIAOTANT

Jeremiah 9 in the TBT1E

Jeremiah 9 in the TBT1E2

Jeremiah 9 in the TFTIP

Jeremiah 9 in the TFTU

Jeremiah 9 in the TGNTATF3T

Jeremiah 9 in the THAI

Jeremiah 9 in the TNFD

Jeremiah 9 in the TNT

Jeremiah 9 in the TNTIK

Jeremiah 9 in the TNTIL

Jeremiah 9 in the TNTIN

Jeremiah 9 in the TNTIP

Jeremiah 9 in the TNTIZ

Jeremiah 9 in the TOMA

Jeremiah 9 in the TTENT

Jeremiah 9 in the UBG

Jeremiah 9 in the UGV

Jeremiah 9 in the UGV2

Jeremiah 9 in the UGV3

Jeremiah 9 in the VBL

Jeremiah 9 in the VDCC

Jeremiah 9 in the YALU

Jeremiah 9 in the YAPE

Jeremiah 9 in the YBVTP

Jeremiah 9 in the ZBP