Joshua 13 (BOKCV)

1 Yoshua alipokuwa mzee na umri wake ukiwa umesogea sana, BWANA akamwambia, “Wewe ni mzee sana, na bado kumesalia sehemu kubwa sana za nchi ambazo ni za kutwaliwa. 2 “Nchi iliyosalia ni hii: maeneo yote ya Wafilisti na Wageshuri: 3 kutoka Mto Shihori ulioko mashariki mwa Misri, kuelekea kaskazini kwenye eneo la Ekroni, ambayo yote ilihesabika kama ya Wakanaani (maeneo yale matano ya watawala wa Kifilisti, ambayo ni Gaza, Ashdodi, Ashkeloni, Gathi na Ekroni: ndiyo nchi ya Waavi); 4 kuanzia kusini, nchi yote ya Wakanaani, kuanzia Ara ambayo ni ya Wasidoni, ikienea hadi Afeki, na eneo la Waamori, 5 eneo la Wagebali; Lebanoni yote kuelekea mashariki, kuanzia Baal-Gadi chini ya Mlima Hermoni hadi Lebo-Hamathi. 6 “Na kuhusu wakaaji wote katika maeneo ya milima, kuanzia Lebanoni hadi Misrefoth-Maimu, pamoja na eneo lote la Wasidoni, mimi mwenyewe nitawafukuza watoke mbele ya Waisraeli. Hakikisha umegawa nchi hii kwa Israeli kuwa urithi, kama nilivyokuagiza, 7 sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.” 8 Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa BWANA alivyowagawia. 9 Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, likijumlisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni, 10 nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamoni. 11 Vilevile ilijumlisha Gileadi, eneo la Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote ikienea hadi Saleka: 12 yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao. 13 Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii. 14 Lakini kwa kabila la Lawi, Mose hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa BWANA, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi. 15 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo: 16 Eneo la Aroeri lililo ukingoni mwa Bonde la Arnoni, na kuanzia mji ulio katikati ya bonde, pia uwanda wote wa juu kupita Medeba 17 hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, 18 Yahasa, Kedemothi, Mefaathi, 19 Kiriathaimu, Sibma, Sereth-Shahari juu ya kilima kilicho katika bonde, 20 Beth-Peori, materemko ya Pisga na Beth-Yeshimothi: 21 miji yote ya uwanda wa juu na eneo lote la utawala wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni. Mose alikuwa amemshinda Sihoni, pia watawala wakuu wa Wamidiani, ambao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba, waliokuwa wameungana na Sihoni, ambao waliishi katika nchi ile. 22 Pamoja na wale waliouawa katika vita, Waisraeli walikuwa wamemuua kwa upanga Balaamu mwana wa Beori aliyekuwa mchawi. 23 Mpaka wa Wareubeni ulikuwa ni ukingo wa Mto Yordani. Miji hii na vijiji vyake ndiyo iliyokuwa urithi wa Wareubeni ukoo kwa ukoo. 24 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo: 25 Nchi ya Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Amoni iliyoenea hadi Aroeri, karibu na Raba; 26 na kuanzia Heshboni mpaka Ramath-Mispa na Betonimu, na kutoka Mahanaimu hadi eneo la Debiri; 27 na katika bonde, Beth-Haramu, Beth-Nimra, Sukothi na Safoni na sehemu iliyobaki ya eneo la utawala wa Sihoni mfalme wa Heshboni (upande wa mashariki mwa Mto Yordani, eneo inayoishia kwenye Bahari ya Kinerethi). 28 Miji hii na vijiji vyake ilikuwa urithi wa kabila la Gadi ukoo kwa ukoo. 29 Haya ndiyo maeneo ambayo Mose alikuwa amewapa hiyo nusu ya kabila la Manase, yaani kwa nusu ya jamaa ya uzao wa Manase, ukoo kwa ukoo: 30 Eneo lililoenea kuanzia Mahanaimu, na kujumlisha Bashani yote, ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, makazi yote ya Yairi huko Bashani, miji sitini, 31 nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo. 32 Huu ndio urithi alioupeana Mose wakati alipokuwa katika tambarare za Moabu, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko. 33 Lakini kwa kabila la Walawi, Mose hakuwapa urithi; BWANA Mungu, Mungu wa Israeli ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

In Other Versions

Joshua 13 in the ANGEFD

Joshua 13 in the ANTPNG2D

Joshua 13 in the AS21

Joshua 13 in the BAGH

Joshua 13 in the BBPNG

Joshua 13 in the BBT1E

Joshua 13 in the BDS

Joshua 13 in the BEV

Joshua 13 in the BHAD

Joshua 13 in the BIB

Joshua 13 in the BLPT

Joshua 13 in the BNT

Joshua 13 in the BNTABOOT

Joshua 13 in the BNTLV

Joshua 13 in the BOATCB

Joshua 13 in the BOATCB2

Joshua 13 in the BOBCV

Joshua 13 in the BOCNT

Joshua 13 in the BOECS

Joshua 13 in the BOGWICC

Joshua 13 in the BOHCB

Joshua 13 in the BOHCV

Joshua 13 in the BOHLNT

Joshua 13 in the BOHNTLTAL

Joshua 13 in the BOICB

Joshua 13 in the BOILNTAP

Joshua 13 in the BOITCV

Joshua 13 in the BOKCV2

Joshua 13 in the BOKHWOG

Joshua 13 in the BOKSSV

Joshua 13 in the BOLCB

Joshua 13 in the BOLCB2

Joshua 13 in the BOMCV

Joshua 13 in the BONAV

Joshua 13 in the BONCB

Joshua 13 in the BONLT

Joshua 13 in the BONUT2

Joshua 13 in the BOPLNT

Joshua 13 in the BOSCB

Joshua 13 in the BOSNC

Joshua 13 in the BOTLNT

Joshua 13 in the BOVCB

Joshua 13 in the BOYCB

Joshua 13 in the BPBB

Joshua 13 in the BPH

Joshua 13 in the BSB

Joshua 13 in the CCB

Joshua 13 in the CUV

Joshua 13 in the CUVS

Joshua 13 in the DBT

Joshua 13 in the DGDNT

Joshua 13 in the DHNT

Joshua 13 in the DNT

Joshua 13 in the ELBE

Joshua 13 in the EMTV

Joshua 13 in the ESV

Joshua 13 in the FBV

Joshua 13 in the FEB

Joshua 13 in the GGMNT

Joshua 13 in the GNT

Joshua 13 in the HARY

Joshua 13 in the HNT

Joshua 13 in the IRVA

Joshua 13 in the IRVB

Joshua 13 in the IRVG

Joshua 13 in the IRVH

Joshua 13 in the IRVK

Joshua 13 in the IRVM

Joshua 13 in the IRVM2

Joshua 13 in the IRVO

Joshua 13 in the IRVP

Joshua 13 in the IRVT

Joshua 13 in the IRVT2

Joshua 13 in the IRVU

Joshua 13 in the ISVN

Joshua 13 in the JSNT

Joshua 13 in the KAPI

Joshua 13 in the KBT1ETNIK

Joshua 13 in the KBV

Joshua 13 in the KJV

Joshua 13 in the KNFD

Joshua 13 in the LBA

Joshua 13 in the LBLA

Joshua 13 in the LNT

Joshua 13 in the LSV

Joshua 13 in the MAAL

Joshua 13 in the MBV

Joshua 13 in the MBV2

Joshua 13 in the MHNT

Joshua 13 in the MKNFD

Joshua 13 in the MNG

Joshua 13 in the MNT

Joshua 13 in the MNT2

Joshua 13 in the MRS1T

Joshua 13 in the NAA

Joshua 13 in the NASB

Joshua 13 in the NBLA

Joshua 13 in the NBS

Joshua 13 in the NBVTP

Joshua 13 in the NET2

Joshua 13 in the NIV11

Joshua 13 in the NNT

Joshua 13 in the NNT2

Joshua 13 in the NNT3

Joshua 13 in the PDDPT

Joshua 13 in the PFNT

Joshua 13 in the RMNT

Joshua 13 in the SBIAS

Joshua 13 in the SBIBS

Joshua 13 in the SBIBS2

Joshua 13 in the SBICS

Joshua 13 in the SBIDS

Joshua 13 in the SBIGS

Joshua 13 in the SBIHS

Joshua 13 in the SBIIS

Joshua 13 in the SBIIS2

Joshua 13 in the SBIIS3

Joshua 13 in the SBIKS

Joshua 13 in the SBIKS2

Joshua 13 in the SBIMS

Joshua 13 in the SBIOS

Joshua 13 in the SBIPS

Joshua 13 in the SBISS

Joshua 13 in the SBITS

Joshua 13 in the SBITS2

Joshua 13 in the SBITS3

Joshua 13 in the SBITS4

Joshua 13 in the SBIUS

Joshua 13 in the SBIVS

Joshua 13 in the SBT

Joshua 13 in the SBT1E

Joshua 13 in the SCHL

Joshua 13 in the SNT

Joshua 13 in the SUSU

Joshua 13 in the SUSU2

Joshua 13 in the SYNO

Joshua 13 in the TBIAOTANT

Joshua 13 in the TBT1E

Joshua 13 in the TBT1E2

Joshua 13 in the TFTIP

Joshua 13 in the TFTU

Joshua 13 in the TGNTATF3T

Joshua 13 in the THAI

Joshua 13 in the TNFD

Joshua 13 in the TNT

Joshua 13 in the TNTIK

Joshua 13 in the TNTIL

Joshua 13 in the TNTIN

Joshua 13 in the TNTIP

Joshua 13 in the TNTIZ

Joshua 13 in the TOMA

Joshua 13 in the TTENT

Joshua 13 in the UBG

Joshua 13 in the UGV

Joshua 13 in the UGV2

Joshua 13 in the UGV3

Joshua 13 in the VBL

Joshua 13 in the VDCC

Joshua 13 in the YALU

Joshua 13 in the YAPE

Joshua 13 in the YBVTP

Joshua 13 in the ZBP