Joshua 15 (BOKCV)

1 Mgawo kwa kabila la Yuda, ulienea ukoo kwa ukoo, ukishuka kufikia eneo la Edomu, hadi Jangwa la Sini mwisho kabisa upande wa kusini. 2 Mpaka wao wa kusini ulianzia kwenye ghuba iliyoko kwenye ncha ya kusini mwa Bahari ya Chumvi, 3 ukakatiza kusini mwa Akrabimu, ukaendelea hadi Sini ukaenda hadi kusini mwa Kadesh-Barnea. Tena ukapitia Hesroni ukapanda hadi Adari na ukapinda hadi Karka. 4 Kisha ukaendelea mpaka Azmoni na kuunganika na Kijito cha Misri, na kuishia baharini. Huu ndio mpaka wao wa upande wa kusini. 5 Mpaka wa upande wa mashariki ni Bahari ya Chumvi ukienea mahali Mto Yordani unapoingilia.Mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia penye ghuba ya bahari mahali Mto Yordani unapoingilia, 6 ukapanda hadi Beth-Hogla, na kuendelea kaskazini mwa Beth-Araba hadi kwenye Jiwe la Bohani mwana wa Reubeni. 7 Kisha mpaka ulipanda hadi Debiri kutoka Bonde la Akori na kugeuka kaskazini hadi Gilgali inayotazamana na materemko ya Adumimu, kusini mwa bonde. Ukaendelea sambamba hadi maji ya En-Shemeshi na kutokeza huko En-Rogeli. 8 Kisha ukapanda kwa kufuata Bonde la Ben-Hinomu sambamba na mteremko wa kusini wa mji mkubwa wa Wayebusi (yaani Yerusalemu). Kutoka hapo ukapanda juu ya kilima magharibi ya Bonde la Hinomu mwisho wa ncha ya kaskazini mwa Bonde la Warefai. 9 Kutoka juu ya kilima mpaka ule ukaendelea hadi kwenye chemchemi ya maji ya Neftoa, ukatokea kwenye miji ya Mlima Efroni na kuteremka kuelekea Baala (yaani Kiriath-Yearimu). 10 Kisha ukapinda upande wa magharibi kutoka Baala hadi Mlima Seiri, ukafuatia sambamba mteremko wa kaskazini mwa Mlima Yearimu (yaani Kesaloni), ukaendelea chini hadi Beth-Shemeshi na kukatiza hadi Timna. 11 Ukaelekea hadi kwenye mteremko wa kaskazini mwa Ekroni, ukageuka kuelekea Shikeroni, ukapita hadi Mlima Baala na kufika Yabineeli. Mpaka ule ukaishia baharini. 12 Mpaka wa magharibi ni pwani ya Bahari Kuu. Hii ndiyo mipaka ya watu wa Yuda kwa koo zao. 13 Kwa kufuata maagizo ya BWANA kwake, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune sehemu katika Yuda: Kiriath-Arba, yaani Hebroni (Arba alikuwa baba wa zamani wa Anaki). 14 Kutoka Hebroni Kalebu alifukuza hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, Ahimani na Talmai, wazao wa Anaki. 15 Kutoka hapo akaondoka kupigana dhidi ya watu walioishi Debiri (jina la Debiri hapo kwanza uliitwa Kiriath-Seferi). 16 Kalebu akasema, “Nitamwoza binti yangu Aksa kwa mtu atakayeweza kupigana na kuteka Kiriath-Seferi.” 17 Basi Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, akauteka; hivyo Kalebu akamtoa Aksa binti yake aolewe naye. 18 Siku moja Aksa alipokuja kwa Othnieli, alimsihi Othnieli amwombe baba yake, Kalebu, shamba. Aksa aliposhuka kutoka juu ya punda wake, Kalebu akamuuliza, “Je, wataka nikufanyie nini?” 19 Akamjibu, “Naomba unifanyie jambo moja la hisani. Kwa kuwa umenipa ardhi huko Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Basi Kalebu akampa chemchemi za juu na za chini. 20 Huu ndio urithi wa kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo: 21 Miji ya kusini kabisa ya kabila la Yuda katika Negebu kuelekea mpaka wa Edomu ilikuwa:Kabseeli, Ederi, Yaguri, 22 Kina, Dimona, Adada, 23 Kedeshi, Hazori, Ithnani, 24 Zifu, Telemu, Bealothi, 25 Hazor-Hadata, Kerioth-Hezroni (yaani Hazori), 26 Amamu, Shema, Molada, 27 Hasar-Gada, Heshmoni, Beth-Peleti, 28 Hasar-Shuali, Beer-Sheba, Biziothia, 29 Baala, Iyimu, Esemu, 30 Eltoladi, Kesili, Horma, 31 Siklagi, Madmana, Sansana, 32 Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake. 33 Kwenye shefela ya magharibi:Eshtaoli, Sora, Ashna, 34 Zanoa, En-Ganimu, Tapua, Enamu, 35 Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka, 36 Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. 37 Senani, Hadasha, Migdal-Gadi, 38 Dileani, Mispa, Yoktheeli, 39 Lakishi, Boskathi, Egloni, 40 Kaboni, Lamasi, Kitlishi, 41 Gederothi, Beth-Dagoni, Naama na Makeda; yote ni miji kumi na sita pamoja na vijiji vyake. 42 Libna, Etheri, Ashani, 43 Yifta, Ashna, Nesibu, 44 Keila, Akzibu na Maresha; yote ni miji tisa pamoja na vijiji vyake. 45 Ekroni, pamoja na viunga vyake na vijiji vyake; 46 magharibi ya Ekroni, maeneo yote yaliyokuwa karibu na Ashdodi, pamoja na vijiji vyake; 47 Ashdodi, miji yake na vijiji vyake na Gaza viunga vyake na vijiji vyake, hadi kufikia Kijito cha Misri na Pwani ya Bahari Kuu. 48 Katika nchi ya vilima:Shamiri, Yatiri, Soko, 49 Dana, Kiriath-Sana (yaani Debiri), 50 Anabu, Eshtemoa, Animu, 51 Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja pamoja na vijiji vyake. 52 Arabu, Duma, Ashani, 53 Yanimu, Beth-Tapua, Afeka, 54 Humta, Kiriath-Arba (yaani Hebroni), na Siori; miji tisa pamoja na vijiji vyake. 55 Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta, 56 Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa, 57 Kaini, Gibea na Timna; miji kumi pamoja na vijiji vyake. 58 Halhuli, Beth-Suri, Gedori, 59 Maarathi, Beth-Anothi na Eltekoni; miji sita pamoja na vijiji vyake. 60 Kiriath-Baali (yaani Kiriath-Yearimu) na Raba; miji miwili pamoja na vijiji vyake. 61 Huko jangwani:Beth-Araba, Midini, Sekaka, 62 Nibshani, Mji wa Chumvi, na En-Gedi; miji sita pamoja na vijiji vyake. 63 Yuda hakuweza kuwafukuza Wayebusi, waliokuwa wakiishi Yerusalemu; hadi leo Wayebusi huishi huko pamoja na watu wa Yuda.

In Other Versions

Joshua 15 in the ANGEFD

Joshua 15 in the ANTPNG2D

Joshua 15 in the AS21

Joshua 15 in the BAGH

Joshua 15 in the BBPNG

Joshua 15 in the BBT1E

Joshua 15 in the BDS

Joshua 15 in the BEV

Joshua 15 in the BHAD

Joshua 15 in the BIB

Joshua 15 in the BLPT

Joshua 15 in the BNT

Joshua 15 in the BNTABOOT

Joshua 15 in the BNTLV

Joshua 15 in the BOATCB

Joshua 15 in the BOATCB2

Joshua 15 in the BOBCV

Joshua 15 in the BOCNT

Joshua 15 in the BOECS

Joshua 15 in the BOGWICC

Joshua 15 in the BOHCB

Joshua 15 in the BOHCV

Joshua 15 in the BOHLNT

Joshua 15 in the BOHNTLTAL

Joshua 15 in the BOICB

Joshua 15 in the BOILNTAP

Joshua 15 in the BOITCV

Joshua 15 in the BOKCV2

Joshua 15 in the BOKHWOG

Joshua 15 in the BOKSSV

Joshua 15 in the BOLCB

Joshua 15 in the BOLCB2

Joshua 15 in the BOMCV

Joshua 15 in the BONAV

Joshua 15 in the BONCB

Joshua 15 in the BONLT

Joshua 15 in the BONUT2

Joshua 15 in the BOPLNT

Joshua 15 in the BOSCB

Joshua 15 in the BOSNC

Joshua 15 in the BOTLNT

Joshua 15 in the BOVCB

Joshua 15 in the BOYCB

Joshua 15 in the BPBB

Joshua 15 in the BPH

Joshua 15 in the BSB

Joshua 15 in the CCB

Joshua 15 in the CUV

Joshua 15 in the CUVS

Joshua 15 in the DBT

Joshua 15 in the DGDNT

Joshua 15 in the DHNT

Joshua 15 in the DNT

Joshua 15 in the ELBE

Joshua 15 in the EMTV

Joshua 15 in the ESV

Joshua 15 in the FBV

Joshua 15 in the FEB

Joshua 15 in the GGMNT

Joshua 15 in the GNT

Joshua 15 in the HARY

Joshua 15 in the HNT

Joshua 15 in the IRVA

Joshua 15 in the IRVB

Joshua 15 in the IRVG

Joshua 15 in the IRVH

Joshua 15 in the IRVK

Joshua 15 in the IRVM

Joshua 15 in the IRVM2

Joshua 15 in the IRVO

Joshua 15 in the IRVP

Joshua 15 in the IRVT

Joshua 15 in the IRVT2

Joshua 15 in the IRVU

Joshua 15 in the ISVN

Joshua 15 in the JSNT

Joshua 15 in the KAPI

Joshua 15 in the KBT1ETNIK

Joshua 15 in the KBV

Joshua 15 in the KJV

Joshua 15 in the KNFD

Joshua 15 in the LBA

Joshua 15 in the LBLA

Joshua 15 in the LNT

Joshua 15 in the LSV

Joshua 15 in the MAAL

Joshua 15 in the MBV

Joshua 15 in the MBV2

Joshua 15 in the MHNT

Joshua 15 in the MKNFD

Joshua 15 in the MNG

Joshua 15 in the MNT

Joshua 15 in the MNT2

Joshua 15 in the MRS1T

Joshua 15 in the NAA

Joshua 15 in the NASB

Joshua 15 in the NBLA

Joshua 15 in the NBS

Joshua 15 in the NBVTP

Joshua 15 in the NET2

Joshua 15 in the NIV11

Joshua 15 in the NNT

Joshua 15 in the NNT2

Joshua 15 in the NNT3

Joshua 15 in the PDDPT

Joshua 15 in the PFNT

Joshua 15 in the RMNT

Joshua 15 in the SBIAS

Joshua 15 in the SBIBS

Joshua 15 in the SBIBS2

Joshua 15 in the SBICS

Joshua 15 in the SBIDS

Joshua 15 in the SBIGS

Joshua 15 in the SBIHS

Joshua 15 in the SBIIS

Joshua 15 in the SBIIS2

Joshua 15 in the SBIIS3

Joshua 15 in the SBIKS

Joshua 15 in the SBIKS2

Joshua 15 in the SBIMS

Joshua 15 in the SBIOS

Joshua 15 in the SBIPS

Joshua 15 in the SBISS

Joshua 15 in the SBITS

Joshua 15 in the SBITS2

Joshua 15 in the SBITS3

Joshua 15 in the SBITS4

Joshua 15 in the SBIUS

Joshua 15 in the SBIVS

Joshua 15 in the SBT

Joshua 15 in the SBT1E

Joshua 15 in the SCHL

Joshua 15 in the SNT

Joshua 15 in the SUSU

Joshua 15 in the SUSU2

Joshua 15 in the SYNO

Joshua 15 in the TBIAOTANT

Joshua 15 in the TBT1E

Joshua 15 in the TBT1E2

Joshua 15 in the TFTIP

Joshua 15 in the TFTU

Joshua 15 in the TGNTATF3T

Joshua 15 in the THAI

Joshua 15 in the TNFD

Joshua 15 in the TNT

Joshua 15 in the TNTIK

Joshua 15 in the TNTIL

Joshua 15 in the TNTIN

Joshua 15 in the TNTIP

Joshua 15 in the TNTIZ

Joshua 15 in the TOMA

Joshua 15 in the TTENT

Joshua 15 in the UBG

Joshua 15 in the UGV

Joshua 15 in the UGV2

Joshua 15 in the UGV3

Joshua 15 in the VBL

Joshua 15 in the VDCC

Joshua 15 in the YALU

Joshua 15 in the YAPE

Joshua 15 in the YBVTP

Joshua 15 in the ZBP