Joshua 4 (BOKCV)

1 Wakati taifa lote lilipokwisha kuvuka Mto Yordani, BWANA akamwambia Yoshua, 2 “Chagua watu kumi na wawili miongoni mwa watu, kila kabila mtu mmoja, 3 nawe uwaambie wachukue mawe kumi na mawili katikati ya Mto Yordani, palepale makuhani waliposimama, wayachukue na kuyaweka mahali mtakapokaa usiku huu wa leo.” 4 Basi Yoshua akawaita watu kumi na wawili ambao alikuwa amewachagua kutoka miongoni mwa Waisraeli, mtu mmoja kutoka kila kabila, 5 naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la BWANA Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli, 6 kuwa kama ishara katikati yenu. Siku zijazo, wakati watoto wenu watakapowauliza, ‘Ni nini maana ya mawe haya?’ 7 waambieni kwamba maji ya Mto Yordani yaliyokuwa yakitiririka yalitindika mbele ya Sanduku la Agano la BWANA. Wakati lilipovuka Yordani, maji ya Yordani yalitindika. Mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.” 8 Hivyo Waisraeli wakafanya kama Yoshua alivyowaagiza. Wakachukua mawe kumi na mawili kutoka katikati ya Mto Yordani, kulingana na hesabu ya kabila za Waisraeli kama BWANA alivyomwambia Yoshua, nao wakayabeba hadi kambini mwao, mahali walipoyatua chini. 9 Yoshua akayasimamisha yale mawe kumi na mawili ambayo yalikuwa katikati ya Mto Yordani, mahali pale ambapo miguu ya makuhani waliobeba Sanduku la Agano iliposimama. Nayo yako huko mpaka leo. 10 Makuhani waliobeba lile Sanduku walibakia wakiwa wamesimama katikati ya Mto Yordani mpaka kila kitu BWANA alichomwamuru Yoshua kilipokuwa kimefanywa na watu, sawasawa na vile Mose alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Watu wakafanya haraka kuvuka, 11 na mara tu watu wote walipokwisha kuvuka, Sanduku la BWANA na makuhani wakavuka watu wakiwa wanatazama. 12 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakavuka mbele ya Waisraeli, wakiwa wamevaa silaha, kama Mose alivyowaamuru. 13 Kiasi cha watu 40,000 waliojiandaa kwa vita walivuka mbele za BWANA hadi nchi tambarare za Yeriko kwa ajili ya vita. 14 Siku ile BWANA akamtukuza Yoshua mbele ya Israeli yote, nao wakamheshimu siku zote za maisha yake, kama vile walivyomheshimu Mose. 15 Basi BWANA akamwambia Yoshua, 16 “Waamuru hao makuhani wanaolibeba Sanduku la Ushuhuda, wapande kutoka ndani ya Mto Yordani.” 17 Kwa hiyo Yoshua akawaamuru hao makuhani akisema, “Pandeni kutoka ndani ya Mto Yordani.” 18 Nao makuhani wakapanda kutoka ndani ya Mto Yordani wakilibeba hilo Sanduku la Agano la BWANA. Mara tu walipoiweka miguu yao penye kingo, nje ya mto, maji ya Yordani yakarudi kufurika kama ilivyokuwa kabla. 19 Siku ya kumi ya mwezi wa kwanza watu walipanda kutoka Yordani na kupiga kambi huko Gilgali, kwenye mpaka wa mashariki ya Yeriko. 20 Naye Yoshua akayasimamisha huko Gilgali yale mawe kumi na mawili ambayo walikuwa wameyachukua katikati ya Mto Yordani. 21 Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’ 22 Basi waambieni, ‘Israeli ilivukia mahali pakavu katika Mto Yordani.’ 23 Kwa maana BWANA Mungu wenu alikausha maji ya Yordani mbele yenu, hadi mlipomaliza kuvuka. BWANA Mungu wenu alifanya haya kwa Mto Yordani sawasawa na kile alichoifanyia Bahari ya Shamu wakati alipoikausha mbele yetu hadi tulipomaliza kuvuka. 24 Alifanya hivi ili kwamba mataifa yote ya dunia yapate kujua kuwa mkono wa BWANA ni wenye nguvu, na ili kwamba kila wakati mpate kumcha BWANA Mungu wenu.”

In Other Versions

Joshua 4 in the ANGEFD

Joshua 4 in the ANTPNG2D

Joshua 4 in the AS21

Joshua 4 in the BAGH

Joshua 4 in the BBPNG

Joshua 4 in the BBT1E

Joshua 4 in the BDS

Joshua 4 in the BEV

Joshua 4 in the BHAD

Joshua 4 in the BIB

Joshua 4 in the BLPT

Joshua 4 in the BNT

Joshua 4 in the BNTABOOT

Joshua 4 in the BNTLV

Joshua 4 in the BOATCB

Joshua 4 in the BOATCB2

Joshua 4 in the BOBCV

Joshua 4 in the BOCNT

Joshua 4 in the BOECS

Joshua 4 in the BOGWICC

Joshua 4 in the BOHCB

Joshua 4 in the BOHCV

Joshua 4 in the BOHLNT

Joshua 4 in the BOHNTLTAL

Joshua 4 in the BOICB

Joshua 4 in the BOILNTAP

Joshua 4 in the BOITCV

Joshua 4 in the BOKCV2

Joshua 4 in the BOKHWOG

Joshua 4 in the BOKSSV

Joshua 4 in the BOLCB

Joshua 4 in the BOLCB2

Joshua 4 in the BOMCV

Joshua 4 in the BONAV

Joshua 4 in the BONCB

Joshua 4 in the BONLT

Joshua 4 in the BONUT2

Joshua 4 in the BOPLNT

Joshua 4 in the BOSCB

Joshua 4 in the BOSNC

Joshua 4 in the BOTLNT

Joshua 4 in the BOVCB

Joshua 4 in the BOYCB

Joshua 4 in the BPBB

Joshua 4 in the BPH

Joshua 4 in the BSB

Joshua 4 in the CCB

Joshua 4 in the CUV

Joshua 4 in the CUVS

Joshua 4 in the DBT

Joshua 4 in the DGDNT

Joshua 4 in the DHNT

Joshua 4 in the DNT

Joshua 4 in the ELBE

Joshua 4 in the EMTV

Joshua 4 in the ESV

Joshua 4 in the FBV

Joshua 4 in the FEB

Joshua 4 in the GGMNT

Joshua 4 in the GNT

Joshua 4 in the HARY

Joshua 4 in the HNT

Joshua 4 in the IRVA

Joshua 4 in the IRVB

Joshua 4 in the IRVG

Joshua 4 in the IRVH

Joshua 4 in the IRVK

Joshua 4 in the IRVM

Joshua 4 in the IRVM2

Joshua 4 in the IRVO

Joshua 4 in the IRVP

Joshua 4 in the IRVT

Joshua 4 in the IRVT2

Joshua 4 in the IRVU

Joshua 4 in the ISVN

Joshua 4 in the JSNT

Joshua 4 in the KAPI

Joshua 4 in the KBT1ETNIK

Joshua 4 in the KBV

Joshua 4 in the KJV

Joshua 4 in the KNFD

Joshua 4 in the LBA

Joshua 4 in the LBLA

Joshua 4 in the LNT

Joshua 4 in the LSV

Joshua 4 in the MAAL

Joshua 4 in the MBV

Joshua 4 in the MBV2

Joshua 4 in the MHNT

Joshua 4 in the MKNFD

Joshua 4 in the MNG

Joshua 4 in the MNT

Joshua 4 in the MNT2

Joshua 4 in the MRS1T

Joshua 4 in the NAA

Joshua 4 in the NASB

Joshua 4 in the NBLA

Joshua 4 in the NBS

Joshua 4 in the NBVTP

Joshua 4 in the NET2

Joshua 4 in the NIV11

Joshua 4 in the NNT

Joshua 4 in the NNT2

Joshua 4 in the NNT3

Joshua 4 in the PDDPT

Joshua 4 in the PFNT

Joshua 4 in the RMNT

Joshua 4 in the SBIAS

Joshua 4 in the SBIBS

Joshua 4 in the SBIBS2

Joshua 4 in the SBICS

Joshua 4 in the SBIDS

Joshua 4 in the SBIGS

Joshua 4 in the SBIHS

Joshua 4 in the SBIIS

Joshua 4 in the SBIIS2

Joshua 4 in the SBIIS3

Joshua 4 in the SBIKS

Joshua 4 in the SBIKS2

Joshua 4 in the SBIMS

Joshua 4 in the SBIOS

Joshua 4 in the SBIPS

Joshua 4 in the SBISS

Joshua 4 in the SBITS

Joshua 4 in the SBITS2

Joshua 4 in the SBITS3

Joshua 4 in the SBITS4

Joshua 4 in the SBIUS

Joshua 4 in the SBIVS

Joshua 4 in the SBT

Joshua 4 in the SBT1E

Joshua 4 in the SCHL

Joshua 4 in the SNT

Joshua 4 in the SUSU

Joshua 4 in the SUSU2

Joshua 4 in the SYNO

Joshua 4 in the TBIAOTANT

Joshua 4 in the TBT1E

Joshua 4 in the TBT1E2

Joshua 4 in the TFTIP

Joshua 4 in the TFTU

Joshua 4 in the TGNTATF3T

Joshua 4 in the THAI

Joshua 4 in the TNFD

Joshua 4 in the TNT

Joshua 4 in the TNTIK

Joshua 4 in the TNTIL

Joshua 4 in the TNTIN

Joshua 4 in the TNTIP

Joshua 4 in the TNTIZ

Joshua 4 in the TOMA

Joshua 4 in the TTENT

Joshua 4 in the UBG

Joshua 4 in the UGV

Joshua 4 in the UGV2

Joshua 4 in the UGV3

Joshua 4 in the VBL

Joshua 4 in the VDCC

Joshua 4 in the YALU

Joshua 4 in the YAPE

Joshua 4 in the YBVTP

Joshua 4 in the ZBP