Psalms 12 (BOKCV)
undefined Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi. 1 BWANA tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. 2 Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. 3 BWANA na akatilie mbali midomo yote ya hilana kila ulimi uliojaa majivuno, 4 ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” 5 “Kwa sababu ya uonevu wa wanyongena kulia kwa uchungu kwa wahitaji,nitainuka sasa,” asema BWANA.“Nitawalinda kutokana na walewenye nia mbaya juu yao.” 6 Maneno ya BWANA ni safi,kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,iliyosafishwa mara saba. 7 Ee BWANA, utatuweka salamana kutulinda na kizazi hiki milele. 8 Watu waovu huenda wakiringa kila mahaliwakati ambapo yule aliye mbaya sanandiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.