Psalms 128 (BOKCV)
undefined Wimbo wa kwenda juu. 1 Heri ni wale wote wamchao BWANA,waendao katika njia zake. 2 Utakula matunda ya kazi yako;baraka na mafanikio vitakuwa vyako. 3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaaondani ya nyumba yako;wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeitunikuizunguka meza yako. 4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwamtu amchaye BWANA. 5 BWANA na akubariki kutoka Sayunisiku zote za maisha yako,na uone mafanikio ya Yerusalemu, 6 nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.