Psalms 150 (BOKCV)
1 Msifuni BWANA. Msifuni Mungu katika patakatifu pake,msifuni katika mbingu zake kuu. 2 Msifuni kwa matendo yake makuu,msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake. 3 Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,msifuni kwa kinubi na zeze, 4 msifuni kwa matari na kucheza,msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi, 5 msifuni kwa matoazi yaliayo,msifuni kwa matoazi yavumayo sana. 6 Kila chenye pumzi na kimsifu BWANA. Msifuni BWANA!