Ruth 4 (BOKCV)

1 Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, “Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi.” Naye akakaribia, akaketi. 2 Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, “Ketini hapa.” Nao wakaketi. 3 Kisha akamwambia yule jamaa wa karibu wa kukomboa, “Naomi, aliyerudi hapa kutoka nchi ya Moabu, anauza sehemu ya ardhi iliyokuwa mali ya ndugu yetu Elimeleki. 4 Nami niliwaza nikujulishe wewe na kukuambia uinunue mbele ya hawa waliopo hapa, na mbele ya wazee wa watu wangu. Kama wewe utaikomboa, haya fanya hivyo. Lakini kama hutaikomboa, uniambie, ili nijue. Kwa kuwa hakuna mtu mwingine mwenye haki ya kuikomboa ila wewe na baada yako ni mimi.”Naye akasema, “Nitaikomboa mimi.” 5 Ndipo Boazi akasema “Siku utakaponunua hiyo ardhi kutoka kwa Naomi na Ruthu, Mmoabu, itakubidi kumchukua pia huyo mjane, ili kudumisha jina la marehemu pamoja na mali yake.” 6 Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, “Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza.” 7 (Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.) 8 Basi yule jamaa wa karibu wa kukomboa akamwambia Boazi, “Wewe inunue mwenyewe.” Naye huyo jamaa akavua kiatu chake. 9 Kisha Boazi akawatangazia wazee na watu wote waliokuwepo, “Leo ninyi ni mashahidi kwamba mimi nimenunua kutoka kwa Naomi yote yaliyokuwa mali ya Elimeleki, Kilioni na Maloni. 10 Nimemchukua pia Ruthu, Mmoabu, mjane wa Maloni, awe mke wangu, ili kuendeleza jina la marehemu pamoja na mali zake, ili jina lake marehemu lisitoweke miongoni mwa jamaa yake, wala katika kumbukumbu za mji wake. Leo hivi ninyi ni mashahidi!” 11 Kisha wazee pamoja na watu wote waliokuwa langoni wakasema, “Sisi ni mashahidi. BWANA na amfanye mwanamke huyu aingiaye nyumbani mwako kuwa kama Raheli na kama Lea, wale wanawake wawili ambao pamoja waliijenga nyumba ya Israeli. Nawe ufanikiwe katika Efrathi na uwe mashuhuri katika Bethlehemu. 12 Kupitia kwa watoto ambao BWANA atakupa kutokana na huyu mwanamwali, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda.” 13 Basi Boazi akamwoa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, BWANA akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume. 14 Wanawake wakamwambia Naomi: “Ahimidiwe BWANA, asiyekuacha bila kuwa na jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe mashuhuri katika Israeli yote! 15 Atakurejeshea uhai wako na kukuangalia katika siku za uzee wako. Kwa maana mkweo ambaye anakupenda, na ambaye kwako ni bora zaidi ya watoto wa kiume saba, ndiye alimzaa.” 16 Basi Naomi akamchukua yule mtoto, akampakata na akawa mlezi wake. 17 Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, “Naomi ana mtoto wa kiume.” Wakamwita jina lake Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi. 18 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni, 19 Hesroni akamzaa Ramu,Ramu akamzaa Aminadabu, 20 Aminadabu akamzaa Nashoni,Nashoni akamzaa Salmoni, 21 Salmoni akamzaa Boazi,Boazi akamzaa Obedi, 22 Obedi akamzaa Yese,na Yese akamzaa Daudi.

In Other Versions

Ruth 4 in the ANGEFD

Ruth 4 in the ANTPNG2D

Ruth 4 in the AS21

Ruth 4 in the BAGH

Ruth 4 in the BBPNG

Ruth 4 in the BBT1E

Ruth 4 in the BDS

Ruth 4 in the BEV

Ruth 4 in the BHAD

Ruth 4 in the BIB

Ruth 4 in the BLPT

Ruth 4 in the BNT

Ruth 4 in the BNTABOOT

Ruth 4 in the BNTLV

Ruth 4 in the BOATCB

Ruth 4 in the BOATCB2

Ruth 4 in the BOBCV

Ruth 4 in the BOCNT

Ruth 4 in the BOECS

Ruth 4 in the BOGWICC

Ruth 4 in the BOHCB

Ruth 4 in the BOHCV

Ruth 4 in the BOHLNT

Ruth 4 in the BOHNTLTAL

Ruth 4 in the BOICB

Ruth 4 in the BOILNTAP

Ruth 4 in the BOITCV

Ruth 4 in the BOKCV2

Ruth 4 in the BOKHWOG

Ruth 4 in the BOKSSV

Ruth 4 in the BOLCB

Ruth 4 in the BOLCB2

Ruth 4 in the BOMCV

Ruth 4 in the BONAV

Ruth 4 in the BONCB

Ruth 4 in the BONLT

Ruth 4 in the BONUT2

Ruth 4 in the BOPLNT

Ruth 4 in the BOSCB

Ruth 4 in the BOSNC

Ruth 4 in the BOTLNT

Ruth 4 in the BOVCB

Ruth 4 in the BOYCB

Ruth 4 in the BPBB

Ruth 4 in the BPH

Ruth 4 in the BSB

Ruth 4 in the CCB

Ruth 4 in the CUV

Ruth 4 in the CUVS

Ruth 4 in the DBT

Ruth 4 in the DGDNT

Ruth 4 in the DHNT

Ruth 4 in the DNT

Ruth 4 in the ELBE

Ruth 4 in the EMTV

Ruth 4 in the ESV

Ruth 4 in the FBV

Ruth 4 in the FEB

Ruth 4 in the GGMNT

Ruth 4 in the GNT

Ruth 4 in the HARY

Ruth 4 in the HNT

Ruth 4 in the IRVA

Ruth 4 in the IRVB

Ruth 4 in the IRVG

Ruth 4 in the IRVH

Ruth 4 in the IRVK

Ruth 4 in the IRVM

Ruth 4 in the IRVM2

Ruth 4 in the IRVO

Ruth 4 in the IRVP

Ruth 4 in the IRVT

Ruth 4 in the IRVT2

Ruth 4 in the IRVU

Ruth 4 in the ISVN

Ruth 4 in the JSNT

Ruth 4 in the KAPI

Ruth 4 in the KBT1ETNIK

Ruth 4 in the KBV

Ruth 4 in the KJV

Ruth 4 in the KNFD

Ruth 4 in the LBA

Ruth 4 in the LBLA

Ruth 4 in the LNT

Ruth 4 in the LSV

Ruth 4 in the MAAL

Ruth 4 in the MBV

Ruth 4 in the MBV2

Ruth 4 in the MHNT

Ruth 4 in the MKNFD

Ruth 4 in the MNG

Ruth 4 in the MNT

Ruth 4 in the MNT2

Ruth 4 in the MRS1T

Ruth 4 in the NAA

Ruth 4 in the NASB

Ruth 4 in the NBLA

Ruth 4 in the NBS

Ruth 4 in the NBVTP

Ruth 4 in the NET2

Ruth 4 in the NIV11

Ruth 4 in the NNT

Ruth 4 in the NNT2

Ruth 4 in the NNT3

Ruth 4 in the PDDPT

Ruth 4 in the PFNT

Ruth 4 in the RMNT

Ruth 4 in the SBIAS

Ruth 4 in the SBIBS

Ruth 4 in the SBIBS2

Ruth 4 in the SBICS

Ruth 4 in the SBIDS

Ruth 4 in the SBIGS

Ruth 4 in the SBIHS

Ruth 4 in the SBIIS

Ruth 4 in the SBIIS2

Ruth 4 in the SBIIS3

Ruth 4 in the SBIKS

Ruth 4 in the SBIKS2

Ruth 4 in the SBIMS

Ruth 4 in the SBIOS

Ruth 4 in the SBIPS

Ruth 4 in the SBISS

Ruth 4 in the SBITS

Ruth 4 in the SBITS2

Ruth 4 in the SBITS3

Ruth 4 in the SBITS4

Ruth 4 in the SBIUS

Ruth 4 in the SBIVS

Ruth 4 in the SBT

Ruth 4 in the SBT1E

Ruth 4 in the SCHL

Ruth 4 in the SNT

Ruth 4 in the SUSU

Ruth 4 in the SUSU2

Ruth 4 in the SYNO

Ruth 4 in the TBIAOTANT

Ruth 4 in the TBT1E

Ruth 4 in the TBT1E2

Ruth 4 in the TFTIP

Ruth 4 in the TFTU

Ruth 4 in the TGNTATF3T

Ruth 4 in the THAI

Ruth 4 in the TNFD

Ruth 4 in the TNT

Ruth 4 in the TNTIK

Ruth 4 in the TNTIL

Ruth 4 in the TNTIN

Ruth 4 in the TNTIP

Ruth 4 in the TNTIZ

Ruth 4 in the TOMA

Ruth 4 in the TTENT

Ruth 4 in the UBG

Ruth 4 in the UGV

Ruth 4 in the UGV2

Ruth 4 in the UGV3

Ruth 4 in the VBL

Ruth 4 in the VDCC

Ruth 4 in the YALU

Ruth 4 in the YAPE

Ruth 4 in the YBVTP

Ruth 4 in the ZBP