1 Chronicles 15 (BOKCV)

1 Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake. 2 Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu BWANA aliwachagua kulibeba Sanduku la BWANA na kuhudumu mbele zake milele.” 3 Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la BWANA na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake. 4 Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi: 5 Kutoka wazao wa Kohathi,Urieli kiongozi na ndugu zake 120, 6 Kutoka wazao wa Merari,Asaya kiongozi na ndugu zake 220. 7 Kutoka wazao wa Gershoni,Yoeli kiongozi na ndugu zake 130. 8 Kutoka wazao wa Elisafani,Shemaya kiongozi na ndugu zake 200. 9 Kutoka wazao wa Hebroni,Elieli kiongozi na ndugu zake 80. 10 Kutoka wazao wa Uzieli,Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112. 11 Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu. 12 Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake. 13 Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku la BWANA mara ya kwanza, hata ikasababisha BWANA Mungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.” 14 Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku la BWANA, Mungu wa Israeli. 15 Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno la BWANA. 16 Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi. 17 Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya; 18 hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli. 19 Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba; 20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti ya alamothi, 21 na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti ya sheminithi. 22 Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo. 23 Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku. 24 Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku. 25 Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe. 26 Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano la BWANA, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu. 27 Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi. 28 Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano la BWANA kwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi. 29 Sanduku la Agano la BWANA lilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.

In Other Versions

1 Chronicles 15 in the ANGEFD

1 Chronicles 15 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 15 in the AS21

1 Chronicles 15 in the BAGH

1 Chronicles 15 in the BBPNG

1 Chronicles 15 in the BBT1E

1 Chronicles 15 in the BDS

1 Chronicles 15 in the BEV

1 Chronicles 15 in the BHAD

1 Chronicles 15 in the BIB

1 Chronicles 15 in the BLPT

1 Chronicles 15 in the BNT

1 Chronicles 15 in the BNTABOOT

1 Chronicles 15 in the BNTLV

1 Chronicles 15 in the BOATCB

1 Chronicles 15 in the BOATCB2

1 Chronicles 15 in the BOBCV

1 Chronicles 15 in the BOCNT

1 Chronicles 15 in the BOECS

1 Chronicles 15 in the BOGWICC

1 Chronicles 15 in the BOHCB

1 Chronicles 15 in the BOHCV

1 Chronicles 15 in the BOHLNT

1 Chronicles 15 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 15 in the BOICB

1 Chronicles 15 in the BOILNTAP

1 Chronicles 15 in the BOITCV

1 Chronicles 15 in the BOKCV2

1 Chronicles 15 in the BOKHWOG

1 Chronicles 15 in the BOKSSV

1 Chronicles 15 in the BOLCB

1 Chronicles 15 in the BOLCB2

1 Chronicles 15 in the BOMCV

1 Chronicles 15 in the BONAV

1 Chronicles 15 in the BONCB

1 Chronicles 15 in the BONLT

1 Chronicles 15 in the BONUT2

1 Chronicles 15 in the BOPLNT

1 Chronicles 15 in the BOSCB

1 Chronicles 15 in the BOSNC

1 Chronicles 15 in the BOTLNT

1 Chronicles 15 in the BOVCB

1 Chronicles 15 in the BOYCB

1 Chronicles 15 in the BPBB

1 Chronicles 15 in the BPH

1 Chronicles 15 in the BSB

1 Chronicles 15 in the CCB

1 Chronicles 15 in the CUV

1 Chronicles 15 in the CUVS

1 Chronicles 15 in the DBT

1 Chronicles 15 in the DGDNT

1 Chronicles 15 in the DHNT

1 Chronicles 15 in the DNT

1 Chronicles 15 in the ELBE

1 Chronicles 15 in the EMTV

1 Chronicles 15 in the ESV

1 Chronicles 15 in the FBV

1 Chronicles 15 in the FEB

1 Chronicles 15 in the GGMNT

1 Chronicles 15 in the GNT

1 Chronicles 15 in the HARY

1 Chronicles 15 in the HNT

1 Chronicles 15 in the IRVA

1 Chronicles 15 in the IRVB

1 Chronicles 15 in the IRVG

1 Chronicles 15 in the IRVH

1 Chronicles 15 in the IRVK

1 Chronicles 15 in the IRVM

1 Chronicles 15 in the IRVM2

1 Chronicles 15 in the IRVO

1 Chronicles 15 in the IRVP

1 Chronicles 15 in the IRVT

1 Chronicles 15 in the IRVT2

1 Chronicles 15 in the IRVU

1 Chronicles 15 in the ISVN

1 Chronicles 15 in the JSNT

1 Chronicles 15 in the KAPI

1 Chronicles 15 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 15 in the KBV

1 Chronicles 15 in the KJV

1 Chronicles 15 in the KNFD

1 Chronicles 15 in the LBA

1 Chronicles 15 in the LBLA

1 Chronicles 15 in the LNT

1 Chronicles 15 in the LSV

1 Chronicles 15 in the MAAL

1 Chronicles 15 in the MBV

1 Chronicles 15 in the MBV2

1 Chronicles 15 in the MHNT

1 Chronicles 15 in the MKNFD

1 Chronicles 15 in the MNG

1 Chronicles 15 in the MNT

1 Chronicles 15 in the MNT2

1 Chronicles 15 in the MRS1T

1 Chronicles 15 in the NAA

1 Chronicles 15 in the NASB

1 Chronicles 15 in the NBLA

1 Chronicles 15 in the NBS

1 Chronicles 15 in the NBVTP

1 Chronicles 15 in the NET2

1 Chronicles 15 in the NIV11

1 Chronicles 15 in the NNT

1 Chronicles 15 in the NNT2

1 Chronicles 15 in the NNT3

1 Chronicles 15 in the PDDPT

1 Chronicles 15 in the PFNT

1 Chronicles 15 in the RMNT

1 Chronicles 15 in the SBIAS

1 Chronicles 15 in the SBIBS

1 Chronicles 15 in the SBIBS2

1 Chronicles 15 in the SBICS

1 Chronicles 15 in the SBIDS

1 Chronicles 15 in the SBIGS

1 Chronicles 15 in the SBIHS

1 Chronicles 15 in the SBIIS

1 Chronicles 15 in the SBIIS2

1 Chronicles 15 in the SBIIS3

1 Chronicles 15 in the SBIKS

1 Chronicles 15 in the SBIKS2

1 Chronicles 15 in the SBIMS

1 Chronicles 15 in the SBIOS

1 Chronicles 15 in the SBIPS

1 Chronicles 15 in the SBISS

1 Chronicles 15 in the SBITS

1 Chronicles 15 in the SBITS2

1 Chronicles 15 in the SBITS3

1 Chronicles 15 in the SBITS4

1 Chronicles 15 in the SBIUS

1 Chronicles 15 in the SBIVS

1 Chronicles 15 in the SBT

1 Chronicles 15 in the SBT1E

1 Chronicles 15 in the SCHL

1 Chronicles 15 in the SNT

1 Chronicles 15 in the SUSU

1 Chronicles 15 in the SUSU2

1 Chronicles 15 in the SYNO

1 Chronicles 15 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 15 in the TBT1E

1 Chronicles 15 in the TBT1E2

1 Chronicles 15 in the TFTIP

1 Chronicles 15 in the TFTU

1 Chronicles 15 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 15 in the THAI

1 Chronicles 15 in the TNFD

1 Chronicles 15 in the TNT

1 Chronicles 15 in the TNTIK

1 Chronicles 15 in the TNTIL

1 Chronicles 15 in the TNTIN

1 Chronicles 15 in the TNTIP

1 Chronicles 15 in the TNTIZ

1 Chronicles 15 in the TOMA

1 Chronicles 15 in the TTENT

1 Chronicles 15 in the UBG

1 Chronicles 15 in the UGV

1 Chronicles 15 in the UGV2

1 Chronicles 15 in the UGV3

1 Chronicles 15 in the VBL

1 Chronicles 15 in the VDCC

1 Chronicles 15 in the YALU

1 Chronicles 15 in the YAPE

1 Chronicles 15 in the YBVTP

1 Chronicles 15 in the ZBP