1 Chronicles 21 (BOKCV)

1 Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli. 2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.” 3 Yoabu akajibu, “BWANA na aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?” 4 Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu. 5 Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000. 6 Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme. 7 Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli. 8 Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.” 9 BWANA akamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi, 10 “Nenda ukamwambie Daudi, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ” 11 Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndilo BWANA asemalo: ‘Chagua: 12 miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa BWANA, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika wa BWANA akiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.” 13 Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa BWANA kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.” 14 Basi BWANA akatuma tauni katika Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa. 15 Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo, BWANA akaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa BWANA alikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi. 16 Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika wa BWANA akiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi. 17 Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? Ee BWANA, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.” 18 Kisha malaika wa BWANA akamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengea BWANA madhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi. 19 Kwa hiyo Daudi akakwea, akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina la BWANA. 20 Arauna alipokuwa akipura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano. 21 Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akiuinamisha uso wake ardhini. 22 Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu ya BWANA tauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.” 23 Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.” 24 Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili ya BWANA au kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.” 25 Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600 kwa ajili ya ule uwanja. 26 Kisha Daudi akamjengea BWANA madhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Akamwita BWANA naye BWANA akajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. 27 Kisha BWANA akanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake. 28 Wakati huo, Daudi alipoona kwamba BWANA amemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko. 29 Maskani ya BWANA ambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni. 30 Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumuuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika wa BWANA.

In Other Versions

1 Chronicles 21 in the ANGEFD

1 Chronicles 21 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 21 in the AS21

1 Chronicles 21 in the BAGH

1 Chronicles 21 in the BBPNG

1 Chronicles 21 in the BBT1E

1 Chronicles 21 in the BDS

1 Chronicles 21 in the BEV

1 Chronicles 21 in the BHAD

1 Chronicles 21 in the BIB

1 Chronicles 21 in the BLPT

1 Chronicles 21 in the BNT

1 Chronicles 21 in the BNTABOOT

1 Chronicles 21 in the BNTLV

1 Chronicles 21 in the BOATCB

1 Chronicles 21 in the BOATCB2

1 Chronicles 21 in the BOBCV

1 Chronicles 21 in the BOCNT

1 Chronicles 21 in the BOECS

1 Chronicles 21 in the BOGWICC

1 Chronicles 21 in the BOHCB

1 Chronicles 21 in the BOHCV

1 Chronicles 21 in the BOHLNT

1 Chronicles 21 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 21 in the BOICB

1 Chronicles 21 in the BOILNTAP

1 Chronicles 21 in the BOITCV

1 Chronicles 21 in the BOKCV2

1 Chronicles 21 in the BOKHWOG

1 Chronicles 21 in the BOKSSV

1 Chronicles 21 in the BOLCB

1 Chronicles 21 in the BOLCB2

1 Chronicles 21 in the BOMCV

1 Chronicles 21 in the BONAV

1 Chronicles 21 in the BONCB

1 Chronicles 21 in the BONLT

1 Chronicles 21 in the BONUT2

1 Chronicles 21 in the BOPLNT

1 Chronicles 21 in the BOSCB

1 Chronicles 21 in the BOSNC

1 Chronicles 21 in the BOTLNT

1 Chronicles 21 in the BOVCB

1 Chronicles 21 in the BOYCB

1 Chronicles 21 in the BPBB

1 Chronicles 21 in the BPH

1 Chronicles 21 in the BSB

1 Chronicles 21 in the CCB

1 Chronicles 21 in the CUV

1 Chronicles 21 in the CUVS

1 Chronicles 21 in the DBT

1 Chronicles 21 in the DGDNT

1 Chronicles 21 in the DHNT

1 Chronicles 21 in the DNT

1 Chronicles 21 in the ELBE

1 Chronicles 21 in the EMTV

1 Chronicles 21 in the ESV

1 Chronicles 21 in the FBV

1 Chronicles 21 in the FEB

1 Chronicles 21 in the GGMNT

1 Chronicles 21 in the GNT

1 Chronicles 21 in the HARY

1 Chronicles 21 in the HNT

1 Chronicles 21 in the IRVA

1 Chronicles 21 in the IRVB

1 Chronicles 21 in the IRVG

1 Chronicles 21 in the IRVH

1 Chronicles 21 in the IRVK

1 Chronicles 21 in the IRVM

1 Chronicles 21 in the IRVM2

1 Chronicles 21 in the IRVO

1 Chronicles 21 in the IRVP

1 Chronicles 21 in the IRVT

1 Chronicles 21 in the IRVT2

1 Chronicles 21 in the IRVU

1 Chronicles 21 in the ISVN

1 Chronicles 21 in the JSNT

1 Chronicles 21 in the KAPI

1 Chronicles 21 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 21 in the KBV

1 Chronicles 21 in the KJV

1 Chronicles 21 in the KNFD

1 Chronicles 21 in the LBA

1 Chronicles 21 in the LBLA

1 Chronicles 21 in the LNT

1 Chronicles 21 in the LSV

1 Chronicles 21 in the MAAL

1 Chronicles 21 in the MBV

1 Chronicles 21 in the MBV2

1 Chronicles 21 in the MHNT

1 Chronicles 21 in the MKNFD

1 Chronicles 21 in the MNG

1 Chronicles 21 in the MNT

1 Chronicles 21 in the MNT2

1 Chronicles 21 in the MRS1T

1 Chronicles 21 in the NAA

1 Chronicles 21 in the NASB

1 Chronicles 21 in the NBLA

1 Chronicles 21 in the NBS

1 Chronicles 21 in the NBVTP

1 Chronicles 21 in the NET2

1 Chronicles 21 in the NIV11

1 Chronicles 21 in the NNT

1 Chronicles 21 in the NNT2

1 Chronicles 21 in the NNT3

1 Chronicles 21 in the PDDPT

1 Chronicles 21 in the PFNT

1 Chronicles 21 in the RMNT

1 Chronicles 21 in the SBIAS

1 Chronicles 21 in the SBIBS

1 Chronicles 21 in the SBIBS2

1 Chronicles 21 in the SBICS

1 Chronicles 21 in the SBIDS

1 Chronicles 21 in the SBIGS

1 Chronicles 21 in the SBIHS

1 Chronicles 21 in the SBIIS

1 Chronicles 21 in the SBIIS2

1 Chronicles 21 in the SBIIS3

1 Chronicles 21 in the SBIKS

1 Chronicles 21 in the SBIKS2

1 Chronicles 21 in the SBIMS

1 Chronicles 21 in the SBIOS

1 Chronicles 21 in the SBIPS

1 Chronicles 21 in the SBISS

1 Chronicles 21 in the SBITS

1 Chronicles 21 in the SBITS2

1 Chronicles 21 in the SBITS3

1 Chronicles 21 in the SBITS4

1 Chronicles 21 in the SBIUS

1 Chronicles 21 in the SBIVS

1 Chronicles 21 in the SBT

1 Chronicles 21 in the SBT1E

1 Chronicles 21 in the SCHL

1 Chronicles 21 in the SNT

1 Chronicles 21 in the SUSU

1 Chronicles 21 in the SUSU2

1 Chronicles 21 in the SYNO

1 Chronicles 21 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 21 in the TBT1E

1 Chronicles 21 in the TBT1E2

1 Chronicles 21 in the TFTIP

1 Chronicles 21 in the TFTU

1 Chronicles 21 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 21 in the THAI

1 Chronicles 21 in the TNFD

1 Chronicles 21 in the TNT

1 Chronicles 21 in the TNTIK

1 Chronicles 21 in the TNTIL

1 Chronicles 21 in the TNTIN

1 Chronicles 21 in the TNTIP

1 Chronicles 21 in the TNTIZ

1 Chronicles 21 in the TOMA

1 Chronicles 21 in the TTENT

1 Chronicles 21 in the UBG

1 Chronicles 21 in the UGV

1 Chronicles 21 in the UGV2

1 Chronicles 21 in the UGV3

1 Chronicles 21 in the VBL

1 Chronicles 21 in the VDCC

1 Chronicles 21 in the YALU

1 Chronicles 21 in the YAPE

1 Chronicles 21 in the YBVTP

1 Chronicles 21 in the ZBP