1 Chronicles 28 (BOKCV)

1 Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari. 2 Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano la BWANA kwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga. 3 Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’ 4 “Hata hivyo, BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote. 5 Miongoni mwa wanangu wote, naye BWANA amenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA juu ya Israeli. 6 Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. 7 Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’ 8 “Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili la BWANA naye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri za BWANA Mungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele. 9 “Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana BWANA huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele. 10 Angalia basi, kwa maana BWANA amekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.” 11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho. 12 Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu la BWANA na vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu. 13 Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu la BWANA. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu. 14 Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali. 15 Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara; 16 uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha; 17 uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha; 18 na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano la BWANA. 19 Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwa BWANA ulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.” 20 Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana BWANA aliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la BWANA itakapokamilika. 21 Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”

In Other Versions

1 Chronicles 28 in the ANGEFD

1 Chronicles 28 in the ANTPNG2D

1 Chronicles 28 in the AS21

1 Chronicles 28 in the BAGH

1 Chronicles 28 in the BBPNG

1 Chronicles 28 in the BBT1E

1 Chronicles 28 in the BDS

1 Chronicles 28 in the BEV

1 Chronicles 28 in the BHAD

1 Chronicles 28 in the BIB

1 Chronicles 28 in the BLPT

1 Chronicles 28 in the BNT

1 Chronicles 28 in the BNTABOOT

1 Chronicles 28 in the BNTLV

1 Chronicles 28 in the BOATCB

1 Chronicles 28 in the BOATCB2

1 Chronicles 28 in the BOBCV

1 Chronicles 28 in the BOCNT

1 Chronicles 28 in the BOECS

1 Chronicles 28 in the BOGWICC

1 Chronicles 28 in the BOHCB

1 Chronicles 28 in the BOHCV

1 Chronicles 28 in the BOHLNT

1 Chronicles 28 in the BOHNTLTAL

1 Chronicles 28 in the BOICB

1 Chronicles 28 in the BOILNTAP

1 Chronicles 28 in the BOITCV

1 Chronicles 28 in the BOKCV2

1 Chronicles 28 in the BOKHWOG

1 Chronicles 28 in the BOKSSV

1 Chronicles 28 in the BOLCB

1 Chronicles 28 in the BOLCB2

1 Chronicles 28 in the BOMCV

1 Chronicles 28 in the BONAV

1 Chronicles 28 in the BONCB

1 Chronicles 28 in the BONLT

1 Chronicles 28 in the BONUT2

1 Chronicles 28 in the BOPLNT

1 Chronicles 28 in the BOSCB

1 Chronicles 28 in the BOSNC

1 Chronicles 28 in the BOTLNT

1 Chronicles 28 in the BOVCB

1 Chronicles 28 in the BOYCB

1 Chronicles 28 in the BPBB

1 Chronicles 28 in the BPH

1 Chronicles 28 in the BSB

1 Chronicles 28 in the CCB

1 Chronicles 28 in the CUV

1 Chronicles 28 in the CUVS

1 Chronicles 28 in the DBT

1 Chronicles 28 in the DGDNT

1 Chronicles 28 in the DHNT

1 Chronicles 28 in the DNT

1 Chronicles 28 in the ELBE

1 Chronicles 28 in the EMTV

1 Chronicles 28 in the ESV

1 Chronicles 28 in the FBV

1 Chronicles 28 in the FEB

1 Chronicles 28 in the GGMNT

1 Chronicles 28 in the GNT

1 Chronicles 28 in the HARY

1 Chronicles 28 in the HNT

1 Chronicles 28 in the IRVA

1 Chronicles 28 in the IRVB

1 Chronicles 28 in the IRVG

1 Chronicles 28 in the IRVH

1 Chronicles 28 in the IRVK

1 Chronicles 28 in the IRVM

1 Chronicles 28 in the IRVM2

1 Chronicles 28 in the IRVO

1 Chronicles 28 in the IRVP

1 Chronicles 28 in the IRVT

1 Chronicles 28 in the IRVT2

1 Chronicles 28 in the IRVU

1 Chronicles 28 in the ISVN

1 Chronicles 28 in the JSNT

1 Chronicles 28 in the KAPI

1 Chronicles 28 in the KBT1ETNIK

1 Chronicles 28 in the KBV

1 Chronicles 28 in the KJV

1 Chronicles 28 in the KNFD

1 Chronicles 28 in the LBA

1 Chronicles 28 in the LBLA

1 Chronicles 28 in the LNT

1 Chronicles 28 in the LSV

1 Chronicles 28 in the MAAL

1 Chronicles 28 in the MBV

1 Chronicles 28 in the MBV2

1 Chronicles 28 in the MHNT

1 Chronicles 28 in the MKNFD

1 Chronicles 28 in the MNG

1 Chronicles 28 in the MNT

1 Chronicles 28 in the MNT2

1 Chronicles 28 in the MRS1T

1 Chronicles 28 in the NAA

1 Chronicles 28 in the NASB

1 Chronicles 28 in the NBLA

1 Chronicles 28 in the NBS

1 Chronicles 28 in the NBVTP

1 Chronicles 28 in the NET2

1 Chronicles 28 in the NIV11

1 Chronicles 28 in the NNT

1 Chronicles 28 in the NNT2

1 Chronicles 28 in the NNT3

1 Chronicles 28 in the PDDPT

1 Chronicles 28 in the PFNT

1 Chronicles 28 in the RMNT

1 Chronicles 28 in the SBIAS

1 Chronicles 28 in the SBIBS

1 Chronicles 28 in the SBIBS2

1 Chronicles 28 in the SBICS

1 Chronicles 28 in the SBIDS

1 Chronicles 28 in the SBIGS

1 Chronicles 28 in the SBIHS

1 Chronicles 28 in the SBIIS

1 Chronicles 28 in the SBIIS2

1 Chronicles 28 in the SBIIS3

1 Chronicles 28 in the SBIKS

1 Chronicles 28 in the SBIKS2

1 Chronicles 28 in the SBIMS

1 Chronicles 28 in the SBIOS

1 Chronicles 28 in the SBIPS

1 Chronicles 28 in the SBISS

1 Chronicles 28 in the SBITS

1 Chronicles 28 in the SBITS2

1 Chronicles 28 in the SBITS3

1 Chronicles 28 in the SBITS4

1 Chronicles 28 in the SBIUS

1 Chronicles 28 in the SBIVS

1 Chronicles 28 in the SBT

1 Chronicles 28 in the SBT1E

1 Chronicles 28 in the SCHL

1 Chronicles 28 in the SNT

1 Chronicles 28 in the SUSU

1 Chronicles 28 in the SUSU2

1 Chronicles 28 in the SYNO

1 Chronicles 28 in the TBIAOTANT

1 Chronicles 28 in the TBT1E

1 Chronicles 28 in the TBT1E2

1 Chronicles 28 in the TFTIP

1 Chronicles 28 in the TFTU

1 Chronicles 28 in the TGNTATF3T

1 Chronicles 28 in the THAI

1 Chronicles 28 in the TNFD

1 Chronicles 28 in the TNT

1 Chronicles 28 in the TNTIK

1 Chronicles 28 in the TNTIL

1 Chronicles 28 in the TNTIN

1 Chronicles 28 in the TNTIP

1 Chronicles 28 in the TNTIZ

1 Chronicles 28 in the TOMA

1 Chronicles 28 in the TTENT

1 Chronicles 28 in the UBG

1 Chronicles 28 in the UGV

1 Chronicles 28 in the UGV2

1 Chronicles 28 in the UGV3

1 Chronicles 28 in the VBL

1 Chronicles 28 in the VDCC

1 Chronicles 28 in the YALU

1 Chronicles 28 in the YAPE

1 Chronicles 28 in the YBVTP

1 Chronicles 28 in the ZBP