1 Corinthians 11 (BOKCV)

1 Igeni mfano wangu, kama ninavyouiga mfano wa Kristo. 2 Ninawasifu kwa kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kushika mafundisho niliyowapa. 3 Napenda mfahamu kwamba kichwa cha kila mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu. 4 Kila mwanaume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake. 5 Naye kila mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake, kwani ni sawa na yeye aliyenyoa nywele. 6 Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu kwa mwanamke kukata au kunyoa nywele zake, basi afunike kichwa chake. 7 Haimpasi mwanaume kufunika kichwa chake kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa mwanaume. 8 Kwa maana mwanaume hakutoka kwa mwanamke, bali mwanamke alitoka kwa mwanaume. 9 Wala mwanaume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanaume. 10 Kwa sababu hii na kwa sababu ya malaika, inampasa mwanamke awe na ishara ya mamlaka juu yake. 11 Lakini katika Bwana, mwanamke hajitegemei pasipo mwanaume na mwanaume hajitegemei pasipo mwanamke. 12 Kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanaume, vivyo hivyo mwanaume huzaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vyatoka kwa Mungu. 13 Hukumuni ninyi wenyewe: Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu bila kufunika kichwa chake? 14 Je, maumbile ya asili hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa na nywele ndefu? 15 Lakini mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Kwa maana mwanamke amepewa nywele ndefu ili kumfunika. 16 Kama mtu anataka kubishana juu ya jambo hili, sisi wala makanisa ya Mungu hatutambui desturi nyingine. 17 Basi katika maagizo yafuatayo, siwezi kuwasifu, kwa sababu mkutanikapo si kwa ajili ya faida bali kwa hasara. 18 Kwanza, mnapokutana kama kanisa, nasikia kwamba kuna mgawanyiko miongoni mwenu, nami kwa kiasi fulani nasadiki kuwa ndivyo ilivyo. 19 Bila shaka lazima pawe na tofauti miongoni mwenu ili kuonyesha ni nani anayekubaliwa na Mungu. 20 Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula, 21 kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa. 22 Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha! 23 Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alitwaa mkate, 24 naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema, “Huu ndio mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.” 25 Vivyo hivyo baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.” 26 Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27 Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28 Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29 Kwa maana mtu yeyote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, hula na kunywa hukumu juu yake mwenyewe. 30 Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. 31 Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa. 32 Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. 33 Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane. 34 Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani kwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa.Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.

In Other Versions

1 Corinthians 11 in the ANGEFD

1 Corinthians 11 in the ANTPNG2D

1 Corinthians 11 in the AS21

1 Corinthians 11 in the BAGH

1 Corinthians 11 in the BBPNG

1 Corinthians 11 in the BBT1E

1 Corinthians 11 in the BDS

1 Corinthians 11 in the BEV

1 Corinthians 11 in the BHAD

1 Corinthians 11 in the BIB

1 Corinthians 11 in the BLPT

1 Corinthians 11 in the BNT

1 Corinthians 11 in the BNTABOOT

1 Corinthians 11 in the BNTLV

1 Corinthians 11 in the BOATCB

1 Corinthians 11 in the BOATCB2

1 Corinthians 11 in the BOBCV

1 Corinthians 11 in the BOCNT

1 Corinthians 11 in the BOECS

1 Corinthians 11 in the BOGWICC

1 Corinthians 11 in the BOHCB

1 Corinthians 11 in the BOHCV

1 Corinthians 11 in the BOHLNT

1 Corinthians 11 in the BOHNTLTAL

1 Corinthians 11 in the BOICB

1 Corinthians 11 in the BOILNTAP

1 Corinthians 11 in the BOITCV

1 Corinthians 11 in the BOKCV2

1 Corinthians 11 in the BOKHWOG

1 Corinthians 11 in the BOKSSV

1 Corinthians 11 in the BOLCB

1 Corinthians 11 in the BOLCB2

1 Corinthians 11 in the BOMCV

1 Corinthians 11 in the BONAV

1 Corinthians 11 in the BONCB

1 Corinthians 11 in the BONLT

1 Corinthians 11 in the BONUT2

1 Corinthians 11 in the BOPLNT

1 Corinthians 11 in the BOSCB

1 Corinthians 11 in the BOSNC

1 Corinthians 11 in the BOTLNT

1 Corinthians 11 in the BOVCB

1 Corinthians 11 in the BOYCB

1 Corinthians 11 in the BPBB

1 Corinthians 11 in the BPH

1 Corinthians 11 in the BSB

1 Corinthians 11 in the CCB

1 Corinthians 11 in the CUV

1 Corinthians 11 in the CUVS

1 Corinthians 11 in the DBT

1 Corinthians 11 in the DGDNT

1 Corinthians 11 in the DHNT

1 Corinthians 11 in the DNT

1 Corinthians 11 in the ELBE

1 Corinthians 11 in the EMTV

1 Corinthians 11 in the ESV

1 Corinthians 11 in the FBV

1 Corinthians 11 in the FEB

1 Corinthians 11 in the GGMNT

1 Corinthians 11 in the GNT

1 Corinthians 11 in the HARY

1 Corinthians 11 in the HNT

1 Corinthians 11 in the IRVA

1 Corinthians 11 in the IRVB

1 Corinthians 11 in the IRVG

1 Corinthians 11 in the IRVH

1 Corinthians 11 in the IRVK

1 Corinthians 11 in the IRVM

1 Corinthians 11 in the IRVM2

1 Corinthians 11 in the IRVO

1 Corinthians 11 in the IRVP

1 Corinthians 11 in the IRVT

1 Corinthians 11 in the IRVT2

1 Corinthians 11 in the IRVU

1 Corinthians 11 in the ISVN

1 Corinthians 11 in the JSNT

1 Corinthians 11 in the KAPI

1 Corinthians 11 in the KBT1ETNIK

1 Corinthians 11 in the KBV

1 Corinthians 11 in the KJV

1 Corinthians 11 in the KNFD

1 Corinthians 11 in the LBA

1 Corinthians 11 in the LBLA

1 Corinthians 11 in the LNT

1 Corinthians 11 in the LSV

1 Corinthians 11 in the MAAL

1 Corinthians 11 in the MBV

1 Corinthians 11 in the MBV2

1 Corinthians 11 in the MHNT

1 Corinthians 11 in the MKNFD

1 Corinthians 11 in the MNG

1 Corinthians 11 in the MNT

1 Corinthians 11 in the MNT2

1 Corinthians 11 in the MRS1T

1 Corinthians 11 in the NAA

1 Corinthians 11 in the NASB

1 Corinthians 11 in the NBLA

1 Corinthians 11 in the NBS

1 Corinthians 11 in the NBVTP

1 Corinthians 11 in the NET2

1 Corinthians 11 in the NIV11

1 Corinthians 11 in the NNT

1 Corinthians 11 in the NNT2

1 Corinthians 11 in the NNT3

1 Corinthians 11 in the PDDPT

1 Corinthians 11 in the PFNT

1 Corinthians 11 in the RMNT

1 Corinthians 11 in the SBIAS

1 Corinthians 11 in the SBIBS

1 Corinthians 11 in the SBIBS2

1 Corinthians 11 in the SBICS

1 Corinthians 11 in the SBIDS

1 Corinthians 11 in the SBIGS

1 Corinthians 11 in the SBIHS

1 Corinthians 11 in the SBIIS

1 Corinthians 11 in the SBIIS2

1 Corinthians 11 in the SBIIS3

1 Corinthians 11 in the SBIKS

1 Corinthians 11 in the SBIKS2

1 Corinthians 11 in the SBIMS

1 Corinthians 11 in the SBIOS

1 Corinthians 11 in the SBIPS

1 Corinthians 11 in the SBISS

1 Corinthians 11 in the SBITS

1 Corinthians 11 in the SBITS2

1 Corinthians 11 in the SBITS3

1 Corinthians 11 in the SBITS4

1 Corinthians 11 in the SBIUS

1 Corinthians 11 in the SBIVS

1 Corinthians 11 in the SBT

1 Corinthians 11 in the SBT1E

1 Corinthians 11 in the SCHL

1 Corinthians 11 in the SNT

1 Corinthians 11 in the SUSU

1 Corinthians 11 in the SUSU2

1 Corinthians 11 in the SYNO

1 Corinthians 11 in the TBIAOTANT

1 Corinthians 11 in the TBT1E

1 Corinthians 11 in the TBT1E2

1 Corinthians 11 in the TFTIP

1 Corinthians 11 in the TFTU

1 Corinthians 11 in the TGNTATF3T

1 Corinthians 11 in the THAI

1 Corinthians 11 in the TNFD

1 Corinthians 11 in the TNT

1 Corinthians 11 in the TNTIK

1 Corinthians 11 in the TNTIL

1 Corinthians 11 in the TNTIN

1 Corinthians 11 in the TNTIP

1 Corinthians 11 in the TNTIZ

1 Corinthians 11 in the TOMA

1 Corinthians 11 in the TTENT

1 Corinthians 11 in the UBG

1 Corinthians 11 in the UGV

1 Corinthians 11 in the UGV2

1 Corinthians 11 in the UGV3

1 Corinthians 11 in the VBL

1 Corinthians 11 in the VDCC

1 Corinthians 11 in the YALU

1 Corinthians 11 in the YAPE

1 Corinthians 11 in the YBVTP

1 Corinthians 11 in the ZBP