1 John 3 (BOKCV)

1 Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 2 Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua ya kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. 3 Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu. 4 Kila mtu atendaye dhambi afanya uasi, kwa kuwa dhambi ni uasi. 5 Lakini mwajua ya kuwa yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi, wala ndani yake hamna dhambi. 6 Kila mtu akaaye ndani yake hatendi dhambi. Kila mtu atendaye dhambi hakumwona yeye wala hakumtambua. 7 Watoto wapendwa, mtu yeyote asiwadanganye. Kila mtu atendaye haki ana haki, kama yeye alivyo na haki. 8 Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili aziangamize kazi za ibilisi. 9 Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu. 10 Kwa jinsi hii tunaweza kujua dhahiri watoto wa Mungu na pia watoto wa ibilisi. Yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake. 11 Hili ndilo neno mlilolisikia tangu mwanzo: Kwamba imetupasa tupendane sisi kwa sisi. 12 Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki. 13 Ndugu zangu, ninyi msistaajabu kama ulimwengu ukiwachukia. 14 Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini. 15 Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. 16 Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Yesu Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu. 17 Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo? 18 Watoto wapendwa, tusipende kwa maneno au kwa ulimi bali kwa tendo na kweli. 19 Basi hivi ndivyo tutakavyoweza kujua ya kuwa sisi tu wa kweli na hivyo twaithibitisha mioyo yetu mbele za Mungu 20 kila mara mioyo yetu inapotuhukumu. Kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, naye anajua kila kitu. 21 Wapendwa, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri mbele za Mungu, 22 lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza. 23 Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru. 24 Wale wote wanaozishika amri zake hukaa ndani yake na yeye ndani yao. Hivi ndivyo tunavyojua kwamba anakaa ndani yetu. Nasi twajua hili kwa njia ya Roho yule aliyetupa.

In Other Versions

1 John 3 in the ANGEFD

1 John 3 in the ANTPNG2D

1 John 3 in the AS21

1 John 3 in the BAGH

1 John 3 in the BBPNG

1 John 3 in the BBT1E

1 John 3 in the BDS

1 John 3 in the BEV

1 John 3 in the BHAD

1 John 3 in the BIB

1 John 3 in the BLPT

1 John 3 in the BNT

1 John 3 in the BNTABOOT

1 John 3 in the BNTLV

1 John 3 in the BOATCB

1 John 3 in the BOATCB2

1 John 3 in the BOBCV

1 John 3 in the BOCNT

1 John 3 in the BOECS

1 John 3 in the BOGWICC

1 John 3 in the BOHCB

1 John 3 in the BOHCV

1 John 3 in the BOHLNT

1 John 3 in the BOHNTLTAL

1 John 3 in the BOICB

1 John 3 in the BOILNTAP

1 John 3 in the BOITCV

1 John 3 in the BOKCV2

1 John 3 in the BOKHWOG

1 John 3 in the BOKSSV

1 John 3 in the BOLCB

1 John 3 in the BOLCB2

1 John 3 in the BOMCV

1 John 3 in the BONAV

1 John 3 in the BONCB

1 John 3 in the BONLT

1 John 3 in the BONUT2

1 John 3 in the BOPLNT

1 John 3 in the BOSCB

1 John 3 in the BOSNC

1 John 3 in the BOTLNT

1 John 3 in the BOVCB

1 John 3 in the BOYCB

1 John 3 in the BPBB

1 John 3 in the BPH

1 John 3 in the BSB

1 John 3 in the CCB

1 John 3 in the CUV

1 John 3 in the CUVS

1 John 3 in the DBT

1 John 3 in the DGDNT

1 John 3 in the DHNT

1 John 3 in the DNT

1 John 3 in the ELBE

1 John 3 in the EMTV

1 John 3 in the ESV

1 John 3 in the FBV

1 John 3 in the FEB

1 John 3 in the GGMNT

1 John 3 in the GNT

1 John 3 in the HARY

1 John 3 in the HNT

1 John 3 in the IRVA

1 John 3 in the IRVB

1 John 3 in the IRVG

1 John 3 in the IRVH

1 John 3 in the IRVK

1 John 3 in the IRVM

1 John 3 in the IRVM2

1 John 3 in the IRVO

1 John 3 in the IRVP

1 John 3 in the IRVT

1 John 3 in the IRVT2

1 John 3 in the IRVU

1 John 3 in the ISVN

1 John 3 in the JSNT

1 John 3 in the KAPI

1 John 3 in the KBT1ETNIK

1 John 3 in the KBV

1 John 3 in the KJV

1 John 3 in the KNFD

1 John 3 in the LBA

1 John 3 in the LBLA

1 John 3 in the LNT

1 John 3 in the LSV

1 John 3 in the MAAL

1 John 3 in the MBV

1 John 3 in the MBV2

1 John 3 in the MHNT

1 John 3 in the MKNFD

1 John 3 in the MNG

1 John 3 in the MNT

1 John 3 in the MNT2

1 John 3 in the MRS1T

1 John 3 in the NAA

1 John 3 in the NASB

1 John 3 in the NBLA

1 John 3 in the NBS

1 John 3 in the NBVTP

1 John 3 in the NET2

1 John 3 in the NIV11

1 John 3 in the NNT

1 John 3 in the NNT2

1 John 3 in the NNT3

1 John 3 in the PDDPT

1 John 3 in the PFNT

1 John 3 in the RMNT

1 John 3 in the SBIAS

1 John 3 in the SBIBS

1 John 3 in the SBIBS2

1 John 3 in the SBICS

1 John 3 in the SBIDS

1 John 3 in the SBIGS

1 John 3 in the SBIHS

1 John 3 in the SBIIS

1 John 3 in the SBIIS2

1 John 3 in the SBIIS3

1 John 3 in the SBIKS

1 John 3 in the SBIKS2

1 John 3 in the SBIMS

1 John 3 in the SBIOS

1 John 3 in the SBIPS

1 John 3 in the SBISS

1 John 3 in the SBITS

1 John 3 in the SBITS2

1 John 3 in the SBITS3

1 John 3 in the SBITS4

1 John 3 in the SBIUS

1 John 3 in the SBIVS

1 John 3 in the SBT

1 John 3 in the SBT1E

1 John 3 in the SCHL

1 John 3 in the SNT

1 John 3 in the SUSU

1 John 3 in the SUSU2

1 John 3 in the SYNO

1 John 3 in the TBIAOTANT

1 John 3 in the TBT1E

1 John 3 in the TBT1E2

1 John 3 in the TFTIP

1 John 3 in the TFTU

1 John 3 in the TGNTATF3T

1 John 3 in the THAI

1 John 3 in the TNFD

1 John 3 in the TNT

1 John 3 in the TNTIK

1 John 3 in the TNTIL

1 John 3 in the TNTIN

1 John 3 in the TNTIP

1 John 3 in the TNTIZ

1 John 3 in the TOMA

1 John 3 in the TTENT

1 John 3 in the UBG

1 John 3 in the UGV

1 John 3 in the UGV2

1 John 3 in the UGV3

1 John 3 in the VBL

1 John 3 in the VDCC

1 John 3 in the YALU

1 John 3 in the YAPE

1 John 3 in the YBVTP

1 John 3 in the ZBP