1 Kings 19 (BOKCV)

1 Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.” 3 Eliya aliogopa, na akakimbia kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko, 4 lakini yeye mwenyewe akatembea mwendo wa kutwa nzima katika jangwa. Akafika kwenye mti wa mretemu, akakaa chini yake na kuomba ili afe. Akasema, “Yatosha sasa, BWANA, ondoa roho yangu, kwani mimi si bora kuliko baba zangu.” 5 Kisha akajinyoosha chini ya mti, akalala usingizi.Mara malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka na ule.” 6 Akatazama pande zote, napo hapo karibu na kichwa chake palikuwepo mkate uliookwa kwenye makaa ya moto na gudulia la maji. Akala na kunywa, kisha akajinyoosha tena. 7 Yule malaika wa BWANA akaja tena mara ya pili, akamgusa akamwambia, “Inuka na ule, kwa kuwa safari ni ndefu kwako.” 8 Kwa hiyo akainuka, akala na kunywa. Akiwa ametiwa nguvu na kile chakula, akasafiri siku arobaini usiku na mchana mpaka akafika Horebu, mlima wa Mungu. 9 Huko akaingia katika pango, akalala humo usiku ule.Nalo neno la BWANA likamjia, kusema, “Unafanya nini hapa, Eliya?” 10 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize.” 11 BWANA akasema, “Toka nje ukasimame juu ya mlima mbele za BWANA, kwa kuwa BWANA yu karibu kupita hapo.”Kisha upepo mwingi na wenye nguvu ukapasua milima ile na kuvunjavunja miamba mbele za BWANA, lakini BWANA hakuwamo katika ule upepo. Baada ya upepo palikuwa na tetemeko la nchi, lakini BWANA hakuwamo kwenye lile tetemeko. 12 Baada ya tetemeko la nchi ukaja moto, lakini BWANA hakuwamo katika ule moto. Baada ya moto ikaja sauti ya utulivu ya kunongʼona. 13 Eliya alipoisikia, akafunika uso kwa vazi lake, akatoka na kusimama kwenye mdomo wa pango.Kisha ile sauti ikamwambia, “Eliya, unafanya nini hapa?” 14 Akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya BWANA Mungu Mwenye Nguvu Zote. Waisraeli wamelikataa Agano lako, wamevunja madhabahu zako na kuwaua manabii wako kwa upanga. Ni mimi, mimi peke yangu, niliyebaki, nao sasa wananitafuta ili waniangamize.” 15 BWANA akamwambia, “Rudi kwa njia uliyoijia, uende kwenye Jangwa la Dameski. Wakati utakapofika huko, mtie Hazaeli mafuta awe mfalme wa Aramu 16 Pia mtie mafuta Yehu mwana wa Nimshi awe mfalme wa Israeli, na umtie Elisha mwana wa Shafati kutoka Abel-Mehola mafuta awe nabii badala yako. 17 Yehu atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Hazaeli, naye Elisha atamuua yeyote atakayeutoroka upanga wa Yehu. 18 Hata sasa nimeweka akiba watu elfu saba katika Israeli, wote ambao hawajampigia Baali magoti, na wote ambao midomo yao haijambusu.” 19 Hivyo Eliya akaondoka kutoka huko na kumkuta Elisha mwana wa Shafati. Alikuwa akilima kwa jozi kumi na mbili za maksai, na yeye mwenyewe aliongoza ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akamrushia vazi lake. 20 Kisha Elisha akawaacha maksai wake, akamkimbilia Eliya, akamwambia, “Niruhusu nikawabusu baba yangu na mama yangu, halafu nitafuatana nawe.”Eliya akajibu, “Rudi zako, kwani nimekutendea nini?” 21 Basi Elisha akamwacha Eliya, naye akarudi. Akachukua ile jozi yake ya maksai na kuwachinja. Akaipika ile nyama kwa kutumia miti ya nira kama kuni na kuwapa watu, nao wakala. Kisha akaondoka, akamfuata Eliya, akamtumikia.

In Other Versions

1 Kings 19 in the ANGEFD

1 Kings 19 in the ANTPNG2D

1 Kings 19 in the AS21

1 Kings 19 in the BAGH

1 Kings 19 in the BBPNG

1 Kings 19 in the BBT1E

1 Kings 19 in the BDS

1 Kings 19 in the BEV

1 Kings 19 in the BHAD

1 Kings 19 in the BIB

1 Kings 19 in the BLPT

1 Kings 19 in the BNT

1 Kings 19 in the BNTABOOT

1 Kings 19 in the BNTLV

1 Kings 19 in the BOATCB

1 Kings 19 in the BOATCB2

1 Kings 19 in the BOBCV

1 Kings 19 in the BOCNT

1 Kings 19 in the BOECS

1 Kings 19 in the BOGWICC

1 Kings 19 in the BOHCB

1 Kings 19 in the BOHCV

1 Kings 19 in the BOHLNT

1 Kings 19 in the BOHNTLTAL

1 Kings 19 in the BOICB

1 Kings 19 in the BOILNTAP

1 Kings 19 in the BOITCV

1 Kings 19 in the BOKCV2

1 Kings 19 in the BOKHWOG

1 Kings 19 in the BOKSSV

1 Kings 19 in the BOLCB

1 Kings 19 in the BOLCB2

1 Kings 19 in the BOMCV

1 Kings 19 in the BONAV

1 Kings 19 in the BONCB

1 Kings 19 in the BONLT

1 Kings 19 in the BONUT2

1 Kings 19 in the BOPLNT

1 Kings 19 in the BOSCB

1 Kings 19 in the BOSNC

1 Kings 19 in the BOTLNT

1 Kings 19 in the BOVCB

1 Kings 19 in the BOYCB

1 Kings 19 in the BPBB

1 Kings 19 in the BPH

1 Kings 19 in the BSB

1 Kings 19 in the CCB

1 Kings 19 in the CUV

1 Kings 19 in the CUVS

1 Kings 19 in the DBT

1 Kings 19 in the DGDNT

1 Kings 19 in the DHNT

1 Kings 19 in the DNT

1 Kings 19 in the ELBE

1 Kings 19 in the EMTV

1 Kings 19 in the ESV

1 Kings 19 in the FBV

1 Kings 19 in the FEB

1 Kings 19 in the GGMNT

1 Kings 19 in the GNT

1 Kings 19 in the HARY

1 Kings 19 in the HNT

1 Kings 19 in the IRVA

1 Kings 19 in the IRVB

1 Kings 19 in the IRVG

1 Kings 19 in the IRVH

1 Kings 19 in the IRVK

1 Kings 19 in the IRVM

1 Kings 19 in the IRVM2

1 Kings 19 in the IRVO

1 Kings 19 in the IRVP

1 Kings 19 in the IRVT

1 Kings 19 in the IRVT2

1 Kings 19 in the IRVU

1 Kings 19 in the ISVN

1 Kings 19 in the JSNT

1 Kings 19 in the KAPI

1 Kings 19 in the KBT1ETNIK

1 Kings 19 in the KBV

1 Kings 19 in the KJV

1 Kings 19 in the KNFD

1 Kings 19 in the LBA

1 Kings 19 in the LBLA

1 Kings 19 in the LNT

1 Kings 19 in the LSV

1 Kings 19 in the MAAL

1 Kings 19 in the MBV

1 Kings 19 in the MBV2

1 Kings 19 in the MHNT

1 Kings 19 in the MKNFD

1 Kings 19 in the MNG

1 Kings 19 in the MNT

1 Kings 19 in the MNT2

1 Kings 19 in the MRS1T

1 Kings 19 in the NAA

1 Kings 19 in the NASB

1 Kings 19 in the NBLA

1 Kings 19 in the NBS

1 Kings 19 in the NBVTP

1 Kings 19 in the NET2

1 Kings 19 in the NIV11

1 Kings 19 in the NNT

1 Kings 19 in the NNT2

1 Kings 19 in the NNT3

1 Kings 19 in the PDDPT

1 Kings 19 in the PFNT

1 Kings 19 in the RMNT

1 Kings 19 in the SBIAS

1 Kings 19 in the SBIBS

1 Kings 19 in the SBIBS2

1 Kings 19 in the SBICS

1 Kings 19 in the SBIDS

1 Kings 19 in the SBIGS

1 Kings 19 in the SBIHS

1 Kings 19 in the SBIIS

1 Kings 19 in the SBIIS2

1 Kings 19 in the SBIIS3

1 Kings 19 in the SBIKS

1 Kings 19 in the SBIKS2

1 Kings 19 in the SBIMS

1 Kings 19 in the SBIOS

1 Kings 19 in the SBIPS

1 Kings 19 in the SBISS

1 Kings 19 in the SBITS

1 Kings 19 in the SBITS2

1 Kings 19 in the SBITS3

1 Kings 19 in the SBITS4

1 Kings 19 in the SBIUS

1 Kings 19 in the SBIVS

1 Kings 19 in the SBT

1 Kings 19 in the SBT1E

1 Kings 19 in the SCHL

1 Kings 19 in the SNT

1 Kings 19 in the SUSU

1 Kings 19 in the SUSU2

1 Kings 19 in the SYNO

1 Kings 19 in the TBIAOTANT

1 Kings 19 in the TBT1E

1 Kings 19 in the TBT1E2

1 Kings 19 in the TFTIP

1 Kings 19 in the TFTU

1 Kings 19 in the TGNTATF3T

1 Kings 19 in the THAI

1 Kings 19 in the TNFD

1 Kings 19 in the TNT

1 Kings 19 in the TNTIK

1 Kings 19 in the TNTIL

1 Kings 19 in the TNTIN

1 Kings 19 in the TNTIP

1 Kings 19 in the TNTIZ

1 Kings 19 in the TOMA

1 Kings 19 in the TTENT

1 Kings 19 in the UBG

1 Kings 19 in the UGV

1 Kings 19 in the UGV2

1 Kings 19 in the UGV3

1 Kings 19 in the VBL

1 Kings 19 in the VDCC

1 Kings 19 in the YALU

1 Kings 19 in the YAPE

1 Kings 19 in the YBVTP

1 Kings 19 in the ZBP