1 Samuel 22 (BOKCV)

1 Daudi akaondoka Gathi na kukimbilia kwenye pango la Adulamu. Ndugu zake na watu wa nyumba ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakamwendea huko. 2 Wale wote waliokuwa katika dhiki au waliokuwa na madeni au wale ambao hawakuridhika wakamkusanyikia Daudi, naye akawa kiongozi wao. Watu wapatao 400 walikuwa pamoja naye. 3 Kutoka huko Daudi akaenda Mispa huko Moabu na kumwambia mfalme wa Moabu, “Naomba uwaruhusu baba yangu na mama yangu waje kukaa nawe mpaka nijue nini Mungu atakachonifanyia.” 4 Hivyo akawaacha wazazi wake wakae na mfalme wa Moabu, nao wakakaa naye muda wote ambao Daudi alikuwa ngomeni. 5 Ndipo nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae ngomeni. Nenda katika nchi ya Yuda.” Hivyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi. 6 Basi Sauli akasikia kwamba Daudi na watu wake wameonekana. Sauli akiwa na mkuki mkononi, alikuwa ameketi chini ya mti wa mkwaju kwenye kilima huko Gibea, maafisa wake wote wakiwa wamesimama kumzunguka. 7 Sauli akawaambia, “Sikilizeni enyi watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa ninyi nyote mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya ninyi nyote majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia? 8 Je, ndiyo sababu ninyi mkapanga hila mbaya dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu ambaye ameniambia ni lini mwanangu alifanya agano na mwana wa Yese. Hapana hata mmoja wenu anayejishughulisha nami wala anayeniambia kwamba mwanangu amechochea mtumishi wangu kunivizia, kama afanyavyo leo.” 9 Lakini Doegi Mwedomu, ambaye alikuwa akisimama na maafisa wa Sauli, akasema, “Nilimwona mwana wa Yese akija kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu huko Nobu. 10 Ahimeleki akamuuliza BWANA kwa ajili yake; pia akampa vyakula na ule upanga wa Goliathi Mfilisti.” 11 Kisha mfalme akatuma watu wamwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu, na jamaa yote ya baba yake, waliokuwa makuhani huko Nobu, nao wote wakaja kwa mfalme. 12 Sauli akasema, “Sikiliza sasa, mwana wa Ahitubu.”Akajibu, “Naam, bwana wangu.” 13 Sauli akamwambia, “Kwa nini umepanga shauri baya dhidi yangu, wewe na mwana wa Yese, ukampa vyakula na upanga, tena hukumuuliza Mungu kwa ajili yake, na kwa sababu hiyo ameasi dhidi yangu na kunivizia, kama afanyavyo leo?” 14 Ahimeleki akamjibu mfalme, “Ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliye mwaminifu kama Daudi, mkwewe mfalme, kiongozi wa walinzi wako na anayeheshimika sana katika watu wa nyumbani mwako? 15 Je, siku hiyo ilikuwa ndiyo ya kwanza kumwomba Mungu kwa ajili yake? La hasha! Mfalme na usiwashutumu watumishi wako wala yeyote wa jamaa ya baba yake, kwa kuwa mtumishi wako hafahamu lolote kabisa kuhusu jambo hili lote.” 16 Lakini mfalme akasema, “Ahimeleki, hakika utakufa, wewe na jamaa yote ya baba yako.” 17 Ndipo mfalme akawaamuru walinzi wake waliokuwa kando yake: “Geukeni na kuwaua makuhani wa BWANA, kwa sababu nao pia wamejiunga na Daudi. Walijua kuwa alikuwa anakimbia, wala hawakuniambia.”Lakini maafisa wa mfalme hawakuwa radhi kuinua mkono kuwaua makuhani wa BWANA. 18 Kisha mfalme akamwagiza Doegi, “Wewe geuka ukawaue makuhani.” Hivyo basi Doegi Mwedomu, akageuka na kuwaua. Siku ile aliwaua watu themanini na watano wavaao visibau vya kitani. 19 Pia akaupiga Nobu kwa upanga, mji wa makuhani, wakiwemo wanaume na wanawake, watoto wadogo na wale wanyonyao, ngʼombe wake, punda na kondoo. 20 Lakini Abiathari, mwana wa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu, akatoroka, akakimbia na kujiunga na Daudi. 21 Akamwambia Daudi kuwa Sauli amewaua makuhani wa BWANA. 22 Kisha Daudi akamwambia Abiathari: “Siku ile, wakati Doegi Mwedomu alipokuwa pale, nilijua atahakikisha amemwambia Sauli. Mimi ninawajibika kwa vifo vya jamaa ya baba yako yote. 23 Kaa pamoja nami; usiogope. Mtu anayeutafuta uhai wako anautafuta uhai wangu pia. Ukiwa pamoja nami utakuwa salama.”

In Other Versions

1 Samuel 22 in the ANGEFD

1 Samuel 22 in the ANTPNG2D

1 Samuel 22 in the AS21

1 Samuel 22 in the BAGH

1 Samuel 22 in the BBPNG

1 Samuel 22 in the BBT1E

1 Samuel 22 in the BDS

1 Samuel 22 in the BEV

1 Samuel 22 in the BHAD

1 Samuel 22 in the BIB

1 Samuel 22 in the BLPT

1 Samuel 22 in the BNT

1 Samuel 22 in the BNTABOOT

1 Samuel 22 in the BNTLV

1 Samuel 22 in the BOATCB

1 Samuel 22 in the BOATCB2

1 Samuel 22 in the BOBCV

1 Samuel 22 in the BOCNT

1 Samuel 22 in the BOECS

1 Samuel 22 in the BOGWICC

1 Samuel 22 in the BOHCB

1 Samuel 22 in the BOHCV

1 Samuel 22 in the BOHLNT

1 Samuel 22 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 22 in the BOICB

1 Samuel 22 in the BOILNTAP

1 Samuel 22 in the BOITCV

1 Samuel 22 in the BOKCV2

1 Samuel 22 in the BOKHWOG

1 Samuel 22 in the BOKSSV

1 Samuel 22 in the BOLCB

1 Samuel 22 in the BOLCB2

1 Samuel 22 in the BOMCV

1 Samuel 22 in the BONAV

1 Samuel 22 in the BONCB

1 Samuel 22 in the BONLT

1 Samuel 22 in the BONUT2

1 Samuel 22 in the BOPLNT

1 Samuel 22 in the BOSCB

1 Samuel 22 in the BOSNC

1 Samuel 22 in the BOTLNT

1 Samuel 22 in the BOVCB

1 Samuel 22 in the BOYCB

1 Samuel 22 in the BPBB

1 Samuel 22 in the BPH

1 Samuel 22 in the BSB

1 Samuel 22 in the CCB

1 Samuel 22 in the CUV

1 Samuel 22 in the CUVS

1 Samuel 22 in the DBT

1 Samuel 22 in the DGDNT

1 Samuel 22 in the DHNT

1 Samuel 22 in the DNT

1 Samuel 22 in the ELBE

1 Samuel 22 in the EMTV

1 Samuel 22 in the ESV

1 Samuel 22 in the FBV

1 Samuel 22 in the FEB

1 Samuel 22 in the GGMNT

1 Samuel 22 in the GNT

1 Samuel 22 in the HARY

1 Samuel 22 in the HNT

1 Samuel 22 in the IRVA

1 Samuel 22 in the IRVB

1 Samuel 22 in the IRVG

1 Samuel 22 in the IRVH

1 Samuel 22 in the IRVK

1 Samuel 22 in the IRVM

1 Samuel 22 in the IRVM2

1 Samuel 22 in the IRVO

1 Samuel 22 in the IRVP

1 Samuel 22 in the IRVT

1 Samuel 22 in the IRVT2

1 Samuel 22 in the IRVU

1 Samuel 22 in the ISVN

1 Samuel 22 in the JSNT

1 Samuel 22 in the KAPI

1 Samuel 22 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 22 in the KBV

1 Samuel 22 in the KJV

1 Samuel 22 in the KNFD

1 Samuel 22 in the LBA

1 Samuel 22 in the LBLA

1 Samuel 22 in the LNT

1 Samuel 22 in the LSV

1 Samuel 22 in the MAAL

1 Samuel 22 in the MBV

1 Samuel 22 in the MBV2

1 Samuel 22 in the MHNT

1 Samuel 22 in the MKNFD

1 Samuel 22 in the MNG

1 Samuel 22 in the MNT

1 Samuel 22 in the MNT2

1 Samuel 22 in the MRS1T

1 Samuel 22 in the NAA

1 Samuel 22 in the NASB

1 Samuel 22 in the NBLA

1 Samuel 22 in the NBS

1 Samuel 22 in the NBVTP

1 Samuel 22 in the NET2

1 Samuel 22 in the NIV11

1 Samuel 22 in the NNT

1 Samuel 22 in the NNT2

1 Samuel 22 in the NNT3

1 Samuel 22 in the PDDPT

1 Samuel 22 in the PFNT

1 Samuel 22 in the RMNT

1 Samuel 22 in the SBIAS

1 Samuel 22 in the SBIBS

1 Samuel 22 in the SBIBS2

1 Samuel 22 in the SBICS

1 Samuel 22 in the SBIDS

1 Samuel 22 in the SBIGS

1 Samuel 22 in the SBIHS

1 Samuel 22 in the SBIIS

1 Samuel 22 in the SBIIS2

1 Samuel 22 in the SBIIS3

1 Samuel 22 in the SBIKS

1 Samuel 22 in the SBIKS2

1 Samuel 22 in the SBIMS

1 Samuel 22 in the SBIOS

1 Samuel 22 in the SBIPS

1 Samuel 22 in the SBISS

1 Samuel 22 in the SBITS

1 Samuel 22 in the SBITS2

1 Samuel 22 in the SBITS3

1 Samuel 22 in the SBITS4

1 Samuel 22 in the SBIUS

1 Samuel 22 in the SBIVS

1 Samuel 22 in the SBT

1 Samuel 22 in the SBT1E

1 Samuel 22 in the SCHL

1 Samuel 22 in the SNT

1 Samuel 22 in the SUSU

1 Samuel 22 in the SUSU2

1 Samuel 22 in the SYNO

1 Samuel 22 in the TBIAOTANT

1 Samuel 22 in the TBT1E

1 Samuel 22 in the TBT1E2

1 Samuel 22 in the TFTIP

1 Samuel 22 in the TFTU

1 Samuel 22 in the TGNTATF3T

1 Samuel 22 in the THAI

1 Samuel 22 in the TNFD

1 Samuel 22 in the TNT

1 Samuel 22 in the TNTIK

1 Samuel 22 in the TNTIL

1 Samuel 22 in the TNTIN

1 Samuel 22 in the TNTIP

1 Samuel 22 in the TNTIZ

1 Samuel 22 in the TOMA

1 Samuel 22 in the TTENT

1 Samuel 22 in the UBG

1 Samuel 22 in the UGV

1 Samuel 22 in the UGV2

1 Samuel 22 in the UGV3

1 Samuel 22 in the VBL

1 Samuel 22 in the VDCC

1 Samuel 22 in the YALU

1 Samuel 22 in the YAPE

1 Samuel 22 in the YBVTP

1 Samuel 22 in the ZBP