1 Samuel 8 (BOKCV)

1 Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. 2 Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba. 3 Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki. 4 Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 5 Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.” 6 Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba BWANA. 7 Naye BWANA akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanakuambia. Si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao. 8 Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe. 9 Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.” 10 Samweli akawaambia wale watu waliokuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya BWANA. 11 Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. 12 Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. 13 Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. 14 Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. 15 Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake. 16 Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike, na ngʼombe wenu walio wazuri sana na punda kwa matumizi yake mwenyewe. 17 Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. 18 Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye BWANA hatawajibu.” 19 Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. 20 Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.” 21 Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za BWANA. 22 BWANA akamjibu, “Wasikilize na uwape mfalme.”Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, “Kila mmoja arudi mjini kwake.”

In Other Versions

1 Samuel 8 in the ANGEFD

1 Samuel 8 in the ANTPNG2D

1 Samuel 8 in the AS21

1 Samuel 8 in the BAGH

1 Samuel 8 in the BBPNG

1 Samuel 8 in the BBT1E

1 Samuel 8 in the BDS

1 Samuel 8 in the BEV

1 Samuel 8 in the BHAD

1 Samuel 8 in the BIB

1 Samuel 8 in the BLPT

1 Samuel 8 in the BNT

1 Samuel 8 in the BNTABOOT

1 Samuel 8 in the BNTLV

1 Samuel 8 in the BOATCB

1 Samuel 8 in the BOATCB2

1 Samuel 8 in the BOBCV

1 Samuel 8 in the BOCNT

1 Samuel 8 in the BOECS

1 Samuel 8 in the BOGWICC

1 Samuel 8 in the BOHCB

1 Samuel 8 in the BOHCV

1 Samuel 8 in the BOHLNT

1 Samuel 8 in the BOHNTLTAL

1 Samuel 8 in the BOICB

1 Samuel 8 in the BOILNTAP

1 Samuel 8 in the BOITCV

1 Samuel 8 in the BOKCV2

1 Samuel 8 in the BOKHWOG

1 Samuel 8 in the BOKSSV

1 Samuel 8 in the BOLCB

1 Samuel 8 in the BOLCB2

1 Samuel 8 in the BOMCV

1 Samuel 8 in the BONAV

1 Samuel 8 in the BONCB

1 Samuel 8 in the BONLT

1 Samuel 8 in the BONUT2

1 Samuel 8 in the BOPLNT

1 Samuel 8 in the BOSCB

1 Samuel 8 in the BOSNC

1 Samuel 8 in the BOTLNT

1 Samuel 8 in the BOVCB

1 Samuel 8 in the BOYCB

1 Samuel 8 in the BPBB

1 Samuel 8 in the BPH

1 Samuel 8 in the BSB

1 Samuel 8 in the CCB

1 Samuel 8 in the CUV

1 Samuel 8 in the CUVS

1 Samuel 8 in the DBT

1 Samuel 8 in the DGDNT

1 Samuel 8 in the DHNT

1 Samuel 8 in the DNT

1 Samuel 8 in the ELBE

1 Samuel 8 in the EMTV

1 Samuel 8 in the ESV

1 Samuel 8 in the FBV

1 Samuel 8 in the FEB

1 Samuel 8 in the GGMNT

1 Samuel 8 in the GNT

1 Samuel 8 in the HARY

1 Samuel 8 in the HNT

1 Samuel 8 in the IRVA

1 Samuel 8 in the IRVB

1 Samuel 8 in the IRVG

1 Samuel 8 in the IRVH

1 Samuel 8 in the IRVK

1 Samuel 8 in the IRVM

1 Samuel 8 in the IRVM2

1 Samuel 8 in the IRVO

1 Samuel 8 in the IRVP

1 Samuel 8 in the IRVT

1 Samuel 8 in the IRVT2

1 Samuel 8 in the IRVU

1 Samuel 8 in the ISVN

1 Samuel 8 in the JSNT

1 Samuel 8 in the KAPI

1 Samuel 8 in the KBT1ETNIK

1 Samuel 8 in the KBV

1 Samuel 8 in the KJV

1 Samuel 8 in the KNFD

1 Samuel 8 in the LBA

1 Samuel 8 in the LBLA

1 Samuel 8 in the LNT

1 Samuel 8 in the LSV

1 Samuel 8 in the MAAL

1 Samuel 8 in the MBV

1 Samuel 8 in the MBV2

1 Samuel 8 in the MHNT

1 Samuel 8 in the MKNFD

1 Samuel 8 in the MNG

1 Samuel 8 in the MNT

1 Samuel 8 in the MNT2

1 Samuel 8 in the MRS1T

1 Samuel 8 in the NAA

1 Samuel 8 in the NASB

1 Samuel 8 in the NBLA

1 Samuel 8 in the NBS

1 Samuel 8 in the NBVTP

1 Samuel 8 in the NET2

1 Samuel 8 in the NIV11

1 Samuel 8 in the NNT

1 Samuel 8 in the NNT2

1 Samuel 8 in the NNT3

1 Samuel 8 in the PDDPT

1 Samuel 8 in the PFNT

1 Samuel 8 in the RMNT

1 Samuel 8 in the SBIAS

1 Samuel 8 in the SBIBS

1 Samuel 8 in the SBIBS2

1 Samuel 8 in the SBICS

1 Samuel 8 in the SBIDS

1 Samuel 8 in the SBIGS

1 Samuel 8 in the SBIHS

1 Samuel 8 in the SBIIS

1 Samuel 8 in the SBIIS2

1 Samuel 8 in the SBIIS3

1 Samuel 8 in the SBIKS

1 Samuel 8 in the SBIKS2

1 Samuel 8 in the SBIMS

1 Samuel 8 in the SBIOS

1 Samuel 8 in the SBIPS

1 Samuel 8 in the SBISS

1 Samuel 8 in the SBITS

1 Samuel 8 in the SBITS2

1 Samuel 8 in the SBITS3

1 Samuel 8 in the SBITS4

1 Samuel 8 in the SBIUS

1 Samuel 8 in the SBIVS

1 Samuel 8 in the SBT

1 Samuel 8 in the SBT1E

1 Samuel 8 in the SCHL

1 Samuel 8 in the SNT

1 Samuel 8 in the SUSU

1 Samuel 8 in the SUSU2

1 Samuel 8 in the SYNO

1 Samuel 8 in the TBIAOTANT

1 Samuel 8 in the TBT1E

1 Samuel 8 in the TBT1E2

1 Samuel 8 in the TFTIP

1 Samuel 8 in the TFTU

1 Samuel 8 in the TGNTATF3T

1 Samuel 8 in the THAI

1 Samuel 8 in the TNFD

1 Samuel 8 in the TNT

1 Samuel 8 in the TNTIK

1 Samuel 8 in the TNTIL

1 Samuel 8 in the TNTIN

1 Samuel 8 in the TNTIP

1 Samuel 8 in the TNTIZ

1 Samuel 8 in the TOMA

1 Samuel 8 in the TTENT

1 Samuel 8 in the UBG

1 Samuel 8 in the UGV

1 Samuel 8 in the UGV2

1 Samuel 8 in the UGV3

1 Samuel 8 in the VBL

1 Samuel 8 in the VDCC

1 Samuel 8 in the YALU

1 Samuel 8 in the YAPE

1 Samuel 8 in the YBVTP

1 Samuel 8 in the ZBP