2 Kings 11 (BOKCV)
1 Wakati Athalia mamaye Ahazia alipoona kuwa mwanawe amekufa, akainuka na kuiangamiza jamaa yote ya mfalme. 2 Lakini Yehosheba, binti wa Mfalme Yehoramu, aliyekuwa pia dada yake Ahazia, akamtwaa Yoashi mwana wa Ahazia kwa siri kutoka miongoni mwa wana wa mfalme waliokuwa karibu kuuawa. Akamweka Yoashi pamoja na yaya wake ndani ya chumba cha kulala na kumficha humo ili Athalia asimwone; kwa hiyo hakuuawa. 3 Alibaki amefichwa pamoja na yaya wake katika Hekalu la BWANA kwa muda wa miaka sita wakati Athalia alikuwa akitawala nchi. 4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada akatumania wakuu wa vikundi vya mamia, na Wakari, na walinzi, nao wakaletwa kwake katika Hekalu la BWANA. Alifanya agano nao na kuwaapisha katika Hekalu la BWANA. Ndipo akawaonyesha mwana wa mfalme. 5 Akawaamuru akisema, “Hivi ndivyo iwapasavyo kufanya: Ninyi ambao mko makundi matatu mnaoingia zamu siku ya Sabato, theluthi yenu inayolinda jumba la kifalme, 6 theluthi nyingine Lango la Suri, na theluthi nyingine lango lililo nyuma ya walinzi, ambao hupeana zamu kulinda Hekalu, 7 nanyi ambao mko katika makundi mengine mawili ambao kwa kawaida hupumzika Sabato, wote mtalinda Hekalu kwa ajili ya mfalme. 8 Jipangeni kumzunguka mfalme, kila mtu akiwa na silaha yake mkononi. Yeyote anayesogelea safu zenu lazima auawe. Kaeni karibu na mfalme popote aendapo.” 9 Wakuu wa vikosi vya mamia wakafanya kama vile kuhani Yehoyada aliagiza. Kila mmoja akawachukua watu wake, wale waliokuwa wakiingia zamu siku ya Sabato na wale waliokuwa wakienda mapumziko, nao wakaja kwa kuhani Yehoyada. 10 Ndipo akawapa wale wakuu mikuki na ngao zilizokuwa za Mfalme Daudi, zilizokuwa ndani ya Hekalu la BWANA. 11 Wale walinzi, kila mmoja akiwa na silaha yake mkononi mwake, wakajipanga kumzunguka mfalme, karibu na madhabahu na Hekalu, kuanzia upande wa kusini hadi upande wa kaskazini mwa Hekalu. 12 Yehoyada akamtoa mwana wa mfalme na kumvika taji, akampa nakala ya agano, na kumtangaza kuwa mfalme. Wakamtia mafuta, nao watu wakapiga makofi na kupaza sauti, wakisema, “Mfalme aishi maisha marefu!” 13 Athalia aliposikia kelele iliyofanywa na walinzi pamoja na watu, akawaendea watu pale penye Hekalu la BWANA. 14 Akaangalia, na tazama alikuwako mfalme, akiwa amesimama karibu na nguzo, kama ilivyokuwa desturi. Maafisa na wapiga tarumbeta walikuwa pembeni mwa mfalme, nao watu wote wa nchi walikuwa wakifurahi na kupiga tarumbeta. Ndipo Athalia akararua mavazi yake na kulia, “Uhaini! Uhaini!” 15 Kuhani Yehoyada akawaagiza majemadari wa vikosi vya mamia, waliokuwa viongozi wa jeshi, “Mleteni nje kati ya safu, na mkamuue kwa upanga yeyote anayemfuata.” Kwa kuwa kuhani alikuwa amesema, “Hatauawa ndani ya Hekalu la BWANA.” 16 Basi wakamkamata Athalia, na alipofika mahali ambapo farasi huingilia katika viwanja vya jumba la mfalme, wakamuulia hapo. 17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya BWANA na mfalme na watu kwamba watakuwa watu wa BWANA. Akafanya pia agano kati ya mfalme na watu. 18 Watu wote wa nchi wakaenda kwenye hekalu la Baali na kulibomoa. Wakavunjavunja madhabahu na sanamu, na kumuua Matani kuhani wa Baali mbele ya hayo madhabahu.Kisha Yehoyada kuhani akawaweka walinzi kwenye Hekalu la BWANA. 19 Pamoja naye akawachukua majemadari wa mamia, Wakari, walinzi na watu wote wa nchi, nao kwa pamoja wakamteremsha mfalme kutoka Hekalu la BWANA na kwenda kwenye jumba la mfalme, wakiingilia njia ya lango la walinzi. Ndipo mfalme akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi, 20 nao watu wote wa nchi wakafurahi. Mji ukatulia, kwa sababu Athalia alikuwa ameuawa kwa upanga nyumbani kwa mfalme. 21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.
In Other Versions
2 Kings 11 in the ANGEFD
2 Kings 11 in the ANTPNG2D
2 Kings 11 in the AS21
2 Kings 11 in the BAGH
2 Kings 11 in the BBPNG
2 Kings 11 in the BBT1E
2 Kings 11 in the BDS
2 Kings 11 in the BEV
2 Kings 11 in the BHAD
2 Kings 11 in the BIB
2 Kings 11 in the BLPT
2 Kings 11 in the BNT
2 Kings 11 in the BNTABOOT
2 Kings 11 in the BNTLV
2 Kings 11 in the BOATCB
2 Kings 11 in the BOATCB2
2 Kings 11 in the BOBCV
2 Kings 11 in the BOCNT
2 Kings 11 in the BOECS
2 Kings 11 in the BOGWICC
2 Kings 11 in the BOHCB
2 Kings 11 in the BOHCV
2 Kings 11 in the BOHLNT
2 Kings 11 in the BOHNTLTAL
2 Kings 11 in the BOICB
2 Kings 11 in the BOILNTAP
2 Kings 11 in the BOITCV
2 Kings 11 in the BOKCV2
2 Kings 11 in the BOKHWOG
2 Kings 11 in the BOKSSV
2 Kings 11 in the BOLCB
2 Kings 11 in the BOLCB2
2 Kings 11 in the BOMCV
2 Kings 11 in the BONAV
2 Kings 11 in the BONCB
2 Kings 11 in the BONLT
2 Kings 11 in the BONUT2
2 Kings 11 in the BOPLNT
2 Kings 11 in the BOSCB
2 Kings 11 in the BOSNC
2 Kings 11 in the BOTLNT
2 Kings 11 in the BOVCB
2 Kings 11 in the BOYCB
2 Kings 11 in the BPBB
2 Kings 11 in the BPH
2 Kings 11 in the BSB
2 Kings 11 in the CCB
2 Kings 11 in the CUV
2 Kings 11 in the CUVS
2 Kings 11 in the DBT
2 Kings 11 in the DGDNT
2 Kings 11 in the DHNT
2 Kings 11 in the DNT
2 Kings 11 in the ELBE
2 Kings 11 in the EMTV
2 Kings 11 in the ESV
2 Kings 11 in the FBV
2 Kings 11 in the FEB
2 Kings 11 in the GGMNT
2 Kings 11 in the GNT
2 Kings 11 in the HARY
2 Kings 11 in the HNT
2 Kings 11 in the IRVA
2 Kings 11 in the IRVB
2 Kings 11 in the IRVG
2 Kings 11 in the IRVH
2 Kings 11 in the IRVK
2 Kings 11 in the IRVM
2 Kings 11 in the IRVM2
2 Kings 11 in the IRVO
2 Kings 11 in the IRVP
2 Kings 11 in the IRVT
2 Kings 11 in the IRVT2
2 Kings 11 in the IRVU
2 Kings 11 in the ISVN
2 Kings 11 in the JSNT
2 Kings 11 in the KAPI
2 Kings 11 in the KBT1ETNIK
2 Kings 11 in the KBV
2 Kings 11 in the KJV
2 Kings 11 in the KNFD
2 Kings 11 in the LBA
2 Kings 11 in the LBLA
2 Kings 11 in the LNT
2 Kings 11 in the LSV
2 Kings 11 in the MAAL
2 Kings 11 in the MBV
2 Kings 11 in the MBV2
2 Kings 11 in the MHNT
2 Kings 11 in the MKNFD
2 Kings 11 in the MNG
2 Kings 11 in the MNT
2 Kings 11 in the MNT2
2 Kings 11 in the MRS1T
2 Kings 11 in the NAA
2 Kings 11 in the NASB
2 Kings 11 in the NBLA
2 Kings 11 in the NBS
2 Kings 11 in the NBVTP
2 Kings 11 in the NET2
2 Kings 11 in the NIV11
2 Kings 11 in the NNT
2 Kings 11 in the NNT2
2 Kings 11 in the NNT3
2 Kings 11 in the PDDPT
2 Kings 11 in the PFNT
2 Kings 11 in the RMNT
2 Kings 11 in the SBIAS
2 Kings 11 in the SBIBS
2 Kings 11 in the SBIBS2
2 Kings 11 in the SBICS
2 Kings 11 in the SBIDS
2 Kings 11 in the SBIGS
2 Kings 11 in the SBIHS
2 Kings 11 in the SBIIS
2 Kings 11 in the SBIIS2
2 Kings 11 in the SBIIS3
2 Kings 11 in the SBIKS
2 Kings 11 in the SBIKS2
2 Kings 11 in the SBIMS
2 Kings 11 in the SBIOS
2 Kings 11 in the SBIPS
2 Kings 11 in the SBISS
2 Kings 11 in the SBITS
2 Kings 11 in the SBITS2
2 Kings 11 in the SBITS3
2 Kings 11 in the SBITS4
2 Kings 11 in the SBIUS
2 Kings 11 in the SBIVS
2 Kings 11 in the SBT
2 Kings 11 in the SBT1E
2 Kings 11 in the SCHL
2 Kings 11 in the SNT
2 Kings 11 in the SUSU
2 Kings 11 in the SUSU2
2 Kings 11 in the SYNO
2 Kings 11 in the TBIAOTANT
2 Kings 11 in the TBT1E
2 Kings 11 in the TBT1E2
2 Kings 11 in the TFTIP
2 Kings 11 in the TFTU
2 Kings 11 in the TGNTATF3T
2 Kings 11 in the THAI
2 Kings 11 in the TNFD
2 Kings 11 in the TNT
2 Kings 11 in the TNTIK
2 Kings 11 in the TNTIL
2 Kings 11 in the TNTIN
2 Kings 11 in the TNTIP
2 Kings 11 in the TNTIZ
2 Kings 11 in the TOMA
2 Kings 11 in the TTENT
2 Kings 11 in the UBG
2 Kings 11 in the UGV
2 Kings 11 in the UGV2
2 Kings 11 in the UGV3
2 Kings 11 in the VBL
2 Kings 11 in the VDCC
2 Kings 11 in the YALU
2 Kings 11 in the YAPE
2 Kings 11 in the YBVTP
2 Kings 11 in the ZBP