2 Kings 12 (BOKCV)

1 Katika mwaka wa saba wa utawala wa Yehu, Yoashi alianza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka arobaini. Jina la mama yake aliitwa Sibia, kutoka Beer-Sheba. 2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA miaka yote ambayo Yehoyada kuhani alikuwa akimwelekeza. 3 Hata hivyo mahali pa juu pa kuabudia hapakuondolewa. Watu waliendelea kutoa kafara na kufukiza uvumba huko. 4 Yoashi akawaambia makuhani, “Kusanyeni fedha zote ambazo zitaletwa kama sadaka takatifu kwenye Hekalu la BWANA, yaani fedha zilizokusanywa kama kodi, fedha zilizopokelewa kutokana na nadhiri za watu binafsi, na fedha zilizoletwa kwa hiari hekaluni. 5 Kila kuhani na apokee fedha kutoka kwa mmoja wa watunza hazina, nazo zitumike kukarabati uharibifu wowote unaoonekana katika Hekalu.” 6 Lakini ikawa kufikia mwaka wa ishirini na tatu wa utawala wake Mfalme Yoashi, makuhani walikuwa bado hawajalikarabati Hekalu. 7 Kwa hiyo Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na makuhani wengine, akawauliza, “Kwa nini hamtengenezi uharibifu uliofanyika hekaluni? Msichukue fedha zaidi kutoka kwa watunza hazina wenu kwa ajili ya matumizi yenu, lakini kuanzia sasa ni lazima fedha yote itumike kwa ajili ya kukarabati Hekalu.” 8 Makuhani wakakubali kuwa hawatakusanya tena fedha kutoka kwa watu na kwamba hawatakarabati Hekalu wenyewe. 9 Yehoyada kuhani akachukua kisanduku na akatoboa tundu kwenye kifuniko chake. Akakiweka kando ya madhabahu upande wa kulia unapoingia hekaluni mwa BWANA. Makuhani waliolinda ingilio wakaweka ndani ya kisanduku fedha zote ambazo zililetwa katika Hekalu la BWANA. 10 Kila mara walipoona kuwa kuna kiasi kikubwa cha fedha ndani ya kisanduku, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu walikuja, wakazihesabu fedha hizo zilizoletwa katika Hekalu la BWANA, na kuziweka katika mifuko. 11 Wakiisha kuthibitisha kiasi cha hizo fedha, waliwapa watu walioteuliwa kusimamia kazi katika Hekalu. Kwa fedha hizo, wakawalipa wale watu waliofanya kazi katika Hekalu la BWANA: yaani, maseremala na wajenzi, 12 waashi na wakata mawe. Walinunua mbao na mawe ya kuchongwa kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu la BWANA, na kulipia gharama nyingine zote za kulitengeneza. 13 Fedha zilizoletwa kwenye Hekalu hazikutumiwa kutengenezea masinia ya fedha, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, tarumbeta wala vyombo vingine vyovyote vya dhahabu au fedha kwa ajili ya Hekalu la BWANA; 14 zililipwa kwa wafanyakazi, ambao walizitumia kwa kukarabati Hekalu. 15 Wao hawakudai kupewa hesabu ya fedha kutoka kwa wale waliowapa ili kuwalipa wafanyakazi, kwa sababu walifanya kwa uaminifu wote. 16 Fedha zilizopatikana kutokana na sadaka za hatia na sadaka za dhambi hazikuletwa katika Hekalu la BWANA; zilikuwa mali ya makuhani. 17 Wakati huu Hazaeli mfalme wa Aramu akapanda kuishambulia Gathi, akaiteka. Kisha akageuka ili kuishambulia Yerusalemu. 18 Lakini Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vyombo vyote vitakatifu vilivyowekwa wakfu na baba zake, yaani Yehoshafati, Yehoramu na Ahazia, wafalme wa Yuda, zawadi ambazo yeye mwenyewe alikuwa ameziweka wakfu pamoja na dhahabu yote iliyokutwa katika hazina za Hekalu la BWANA na katika jumba la kifalme, akazipeleka kwa Hazaeli mfalme wa Aramu, ambaye hatimaye aliondoka Yerusalemu. 19 Kwa matukio mengine ya utawala wa Yoashi na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 20 Maafisa wake wakafanya shauri baya dhidi yake, nao wakamuulia Yoashi huko Beth-Milo, kwenye barabara iteremkayo kuelekea Sila. 21 Maafisa waliomuua walikuwa Yozabadi mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri. Akafa na akazikwa pamoja na baba zake katika Mji wa Daudi. Naye Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

In Other Versions

2 Kings 12 in the ANGEFD

2 Kings 12 in the ANTPNG2D

2 Kings 12 in the AS21

2 Kings 12 in the BAGH

2 Kings 12 in the BBPNG

2 Kings 12 in the BBT1E

2 Kings 12 in the BDS

2 Kings 12 in the BEV

2 Kings 12 in the BHAD

2 Kings 12 in the BIB

2 Kings 12 in the BLPT

2 Kings 12 in the BNT

2 Kings 12 in the BNTABOOT

2 Kings 12 in the BNTLV

2 Kings 12 in the BOATCB

2 Kings 12 in the BOATCB2

2 Kings 12 in the BOBCV

2 Kings 12 in the BOCNT

2 Kings 12 in the BOECS

2 Kings 12 in the BOGWICC

2 Kings 12 in the BOHCB

2 Kings 12 in the BOHCV

2 Kings 12 in the BOHLNT

2 Kings 12 in the BOHNTLTAL

2 Kings 12 in the BOICB

2 Kings 12 in the BOILNTAP

2 Kings 12 in the BOITCV

2 Kings 12 in the BOKCV2

2 Kings 12 in the BOKHWOG

2 Kings 12 in the BOKSSV

2 Kings 12 in the BOLCB

2 Kings 12 in the BOLCB2

2 Kings 12 in the BOMCV

2 Kings 12 in the BONAV

2 Kings 12 in the BONCB

2 Kings 12 in the BONLT

2 Kings 12 in the BONUT2

2 Kings 12 in the BOPLNT

2 Kings 12 in the BOSCB

2 Kings 12 in the BOSNC

2 Kings 12 in the BOTLNT

2 Kings 12 in the BOVCB

2 Kings 12 in the BOYCB

2 Kings 12 in the BPBB

2 Kings 12 in the BPH

2 Kings 12 in the BSB

2 Kings 12 in the CCB

2 Kings 12 in the CUV

2 Kings 12 in the CUVS

2 Kings 12 in the DBT

2 Kings 12 in the DGDNT

2 Kings 12 in the DHNT

2 Kings 12 in the DNT

2 Kings 12 in the ELBE

2 Kings 12 in the EMTV

2 Kings 12 in the ESV

2 Kings 12 in the FBV

2 Kings 12 in the FEB

2 Kings 12 in the GGMNT

2 Kings 12 in the GNT

2 Kings 12 in the HARY

2 Kings 12 in the HNT

2 Kings 12 in the IRVA

2 Kings 12 in the IRVB

2 Kings 12 in the IRVG

2 Kings 12 in the IRVH

2 Kings 12 in the IRVK

2 Kings 12 in the IRVM

2 Kings 12 in the IRVM2

2 Kings 12 in the IRVO

2 Kings 12 in the IRVP

2 Kings 12 in the IRVT

2 Kings 12 in the IRVT2

2 Kings 12 in the IRVU

2 Kings 12 in the ISVN

2 Kings 12 in the JSNT

2 Kings 12 in the KAPI

2 Kings 12 in the KBT1ETNIK

2 Kings 12 in the KBV

2 Kings 12 in the KJV

2 Kings 12 in the KNFD

2 Kings 12 in the LBA

2 Kings 12 in the LBLA

2 Kings 12 in the LNT

2 Kings 12 in the LSV

2 Kings 12 in the MAAL

2 Kings 12 in the MBV

2 Kings 12 in the MBV2

2 Kings 12 in the MHNT

2 Kings 12 in the MKNFD

2 Kings 12 in the MNG

2 Kings 12 in the MNT

2 Kings 12 in the MNT2

2 Kings 12 in the MRS1T

2 Kings 12 in the NAA

2 Kings 12 in the NASB

2 Kings 12 in the NBLA

2 Kings 12 in the NBS

2 Kings 12 in the NBVTP

2 Kings 12 in the NET2

2 Kings 12 in the NIV11

2 Kings 12 in the NNT

2 Kings 12 in the NNT2

2 Kings 12 in the NNT3

2 Kings 12 in the PDDPT

2 Kings 12 in the PFNT

2 Kings 12 in the RMNT

2 Kings 12 in the SBIAS

2 Kings 12 in the SBIBS

2 Kings 12 in the SBIBS2

2 Kings 12 in the SBICS

2 Kings 12 in the SBIDS

2 Kings 12 in the SBIGS

2 Kings 12 in the SBIHS

2 Kings 12 in the SBIIS

2 Kings 12 in the SBIIS2

2 Kings 12 in the SBIIS3

2 Kings 12 in the SBIKS

2 Kings 12 in the SBIKS2

2 Kings 12 in the SBIMS

2 Kings 12 in the SBIOS

2 Kings 12 in the SBIPS

2 Kings 12 in the SBISS

2 Kings 12 in the SBITS

2 Kings 12 in the SBITS2

2 Kings 12 in the SBITS3

2 Kings 12 in the SBITS4

2 Kings 12 in the SBIUS

2 Kings 12 in the SBIVS

2 Kings 12 in the SBT

2 Kings 12 in the SBT1E

2 Kings 12 in the SCHL

2 Kings 12 in the SNT

2 Kings 12 in the SUSU

2 Kings 12 in the SUSU2

2 Kings 12 in the SYNO

2 Kings 12 in the TBIAOTANT

2 Kings 12 in the TBT1E

2 Kings 12 in the TBT1E2

2 Kings 12 in the TFTIP

2 Kings 12 in the TFTU

2 Kings 12 in the TGNTATF3T

2 Kings 12 in the THAI

2 Kings 12 in the TNFD

2 Kings 12 in the TNT

2 Kings 12 in the TNTIK

2 Kings 12 in the TNTIL

2 Kings 12 in the TNTIN

2 Kings 12 in the TNTIP

2 Kings 12 in the TNTIZ

2 Kings 12 in the TOMA

2 Kings 12 in the TTENT

2 Kings 12 in the UBG

2 Kings 12 in the UGV

2 Kings 12 in the UGV2

2 Kings 12 in the UGV3

2 Kings 12 in the VBL

2 Kings 12 in the VDCC

2 Kings 12 in the YALU

2 Kings 12 in the YAPE

2 Kings 12 in the YBVTP

2 Kings 12 in the ZBP