2 Kings 21 (BOKCV)

1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka hamsini na mitano. Mama yake aliitwa Hefsiba. 2 Akafanya maovu machoni pa BWANA, akafuata desturi za machukizo za mataifa ambayo BWANA aliyafukuza mbele ya Waisraeli. 3 Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Baali na kutengeneza nguzo ya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu. 4 Akajenga madhabahu katika Hekalu la BWANA, ambamo BWANA alikuwa amesema, “Katika Yerusalemu nitaliweka Jina langu.” 5 Katika nyua zote mbili za Hekalu la BWANA, akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la angani. 6 Akamtoa kafara mwanawe mwenyewe katika moto, akafanya uchawi na uaguzi, na akataka shauri kwa wapiga ramli na kwa mizimu. Akafanya maovu mengi sana machoni mwa BWANA na kumghadhibisha. 7 Akachukua nguzo ya Ashera aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu, ambalo BWANA alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele. 8 Sitaifanya tena miguu ya Waisraeli itangetange kutoka nchi niliyowapa baba zao, ikiwa watakuwa waangalifu kufanya kila kitu nilichowaamuru, na kuishika Sheria yote ambayo walipewa na Mose mtumishi wangu.” 9 Lakini hawa watu hawakusikiliza. Manase akawapotosha, hivyo kwamba walifanya maovu mengi kuliko mataifa ambayo BWANA aliyaangamiza mbele ya Waisraeli. 10 BWANA akasema kupitia watumishi wake manabii: 11 “Manase mfalme wa Yuda ametenda dhambi hizi za kuchukiza. Amefanya maovu mengi kuliko Waamori waliokuwepo kabla yake, na ameiongoza Yuda katika dhambi kwa sanamu zake. 12 Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA, Mungu wa Israeli: Nitaleta maafa makubwa juu ya Yerusalemu na Yuda, kiasi kwamba masikio ya kila mmoja atakayesikia habari zake yatawasha. 13 Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kamba ya kupimia iliyotumika dhidi ya Samaria, na timazi iliyotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu. Nitaifutilia mbali Yerusalemu kama mtu afutaye sahani, nikiifuta na kuifunikiza. 14 Nitawakataa mabaki wa urithi wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao. Watapokonywa mali zao na kutekwa nyara na adui zao wote, 15 kwa sababu wametenda uovu machoni pangu na kunighadhibisha tangu siku baba zao walipotoka Misri mpaka siku ya leo.” 16 Zaidi ya hayo, Manase pia alimwaga damu nyingi isiyo na hatia, hivi kwamba aliijaza Yerusalemu kutoka mwanzo hadi mwisho, mbali na dhambi ambayo alikuwa amesababisha Yuda kufanya, na hivyo wakatenda maovu machoni pa BWANA. 17 Matukio mengine ya utawala wa Manase, na yote aliyoyafanya, pamoja na dhambi alizotenda, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 18 Manase akalala pamoja na baba zake na akazikwa katika bustani ya jumba lake la kifalme, katika bustani ya Uza. Naye Amoni mwanawe akawa mfalme baada yake. 19 Amoni alikuwa na miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka miwili. Mamaye aliitwa Meshulemethi binti Haruzi, kutoka Yotba. 20 Akatenda maovu machoni mwa BWANA, kama baba yake Manase alivyofanya. 21 Akaenenda katika njia zote za baba yake, akaabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu na kuzisujudia. 22 Akamwacha BWANA, Mungu wa baba zake, wala hakuenenda katika njia za BWANA. 23 Watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, nao wakamuulia kwake nyumbani. 24 Kisha watu wa nchi wakawaua wale wote waliokuwa wamefanya hila dhidi ya Mfalme Amoni. Wakamfanya Yosia mwanawe kuwa mfalme mahali pake. 25 Matukio mengine ya utawala wa Amoni na yale aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 26 Akazikwa kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza. Naye Yosia mwanawe akawa mfalme baada yake.

In Other Versions

2 Kings 21 in the ANGEFD

2 Kings 21 in the ANTPNG2D

2 Kings 21 in the AS21

2 Kings 21 in the BAGH

2 Kings 21 in the BBPNG

2 Kings 21 in the BBT1E

2 Kings 21 in the BDS

2 Kings 21 in the BEV

2 Kings 21 in the BHAD

2 Kings 21 in the BIB

2 Kings 21 in the BLPT

2 Kings 21 in the BNT

2 Kings 21 in the BNTABOOT

2 Kings 21 in the BNTLV

2 Kings 21 in the BOATCB

2 Kings 21 in the BOATCB2

2 Kings 21 in the BOBCV

2 Kings 21 in the BOCNT

2 Kings 21 in the BOECS

2 Kings 21 in the BOGWICC

2 Kings 21 in the BOHCB

2 Kings 21 in the BOHCV

2 Kings 21 in the BOHLNT

2 Kings 21 in the BOHNTLTAL

2 Kings 21 in the BOICB

2 Kings 21 in the BOILNTAP

2 Kings 21 in the BOITCV

2 Kings 21 in the BOKCV2

2 Kings 21 in the BOKHWOG

2 Kings 21 in the BOKSSV

2 Kings 21 in the BOLCB

2 Kings 21 in the BOLCB2

2 Kings 21 in the BOMCV

2 Kings 21 in the BONAV

2 Kings 21 in the BONCB

2 Kings 21 in the BONLT

2 Kings 21 in the BONUT2

2 Kings 21 in the BOPLNT

2 Kings 21 in the BOSCB

2 Kings 21 in the BOSNC

2 Kings 21 in the BOTLNT

2 Kings 21 in the BOVCB

2 Kings 21 in the BOYCB

2 Kings 21 in the BPBB

2 Kings 21 in the BPH

2 Kings 21 in the BSB

2 Kings 21 in the CCB

2 Kings 21 in the CUV

2 Kings 21 in the CUVS

2 Kings 21 in the DBT

2 Kings 21 in the DGDNT

2 Kings 21 in the DHNT

2 Kings 21 in the DNT

2 Kings 21 in the ELBE

2 Kings 21 in the EMTV

2 Kings 21 in the ESV

2 Kings 21 in the FBV

2 Kings 21 in the FEB

2 Kings 21 in the GGMNT

2 Kings 21 in the GNT

2 Kings 21 in the HARY

2 Kings 21 in the HNT

2 Kings 21 in the IRVA

2 Kings 21 in the IRVB

2 Kings 21 in the IRVG

2 Kings 21 in the IRVH

2 Kings 21 in the IRVK

2 Kings 21 in the IRVM

2 Kings 21 in the IRVM2

2 Kings 21 in the IRVO

2 Kings 21 in the IRVP

2 Kings 21 in the IRVT

2 Kings 21 in the IRVT2

2 Kings 21 in the IRVU

2 Kings 21 in the ISVN

2 Kings 21 in the JSNT

2 Kings 21 in the KAPI

2 Kings 21 in the KBT1ETNIK

2 Kings 21 in the KBV

2 Kings 21 in the KJV

2 Kings 21 in the KNFD

2 Kings 21 in the LBA

2 Kings 21 in the LBLA

2 Kings 21 in the LNT

2 Kings 21 in the LSV

2 Kings 21 in the MAAL

2 Kings 21 in the MBV

2 Kings 21 in the MBV2

2 Kings 21 in the MHNT

2 Kings 21 in the MKNFD

2 Kings 21 in the MNG

2 Kings 21 in the MNT

2 Kings 21 in the MNT2

2 Kings 21 in the MRS1T

2 Kings 21 in the NAA

2 Kings 21 in the NASB

2 Kings 21 in the NBLA

2 Kings 21 in the NBS

2 Kings 21 in the NBVTP

2 Kings 21 in the NET2

2 Kings 21 in the NIV11

2 Kings 21 in the NNT

2 Kings 21 in the NNT2

2 Kings 21 in the NNT3

2 Kings 21 in the PDDPT

2 Kings 21 in the PFNT

2 Kings 21 in the RMNT

2 Kings 21 in the SBIAS

2 Kings 21 in the SBIBS

2 Kings 21 in the SBIBS2

2 Kings 21 in the SBICS

2 Kings 21 in the SBIDS

2 Kings 21 in the SBIGS

2 Kings 21 in the SBIHS

2 Kings 21 in the SBIIS

2 Kings 21 in the SBIIS2

2 Kings 21 in the SBIIS3

2 Kings 21 in the SBIKS

2 Kings 21 in the SBIKS2

2 Kings 21 in the SBIMS

2 Kings 21 in the SBIOS

2 Kings 21 in the SBIPS

2 Kings 21 in the SBISS

2 Kings 21 in the SBITS

2 Kings 21 in the SBITS2

2 Kings 21 in the SBITS3

2 Kings 21 in the SBITS4

2 Kings 21 in the SBIUS

2 Kings 21 in the SBIVS

2 Kings 21 in the SBT

2 Kings 21 in the SBT1E

2 Kings 21 in the SCHL

2 Kings 21 in the SNT

2 Kings 21 in the SUSU

2 Kings 21 in the SUSU2

2 Kings 21 in the SYNO

2 Kings 21 in the TBIAOTANT

2 Kings 21 in the TBT1E

2 Kings 21 in the TBT1E2

2 Kings 21 in the TFTIP

2 Kings 21 in the TFTU

2 Kings 21 in the TGNTATF3T

2 Kings 21 in the THAI

2 Kings 21 in the TNFD

2 Kings 21 in the TNT

2 Kings 21 in the TNTIK

2 Kings 21 in the TNTIL

2 Kings 21 in the TNTIN

2 Kings 21 in the TNTIP

2 Kings 21 in the TNTIZ

2 Kings 21 in the TOMA

2 Kings 21 in the TTENT

2 Kings 21 in the UBG

2 Kings 21 in the UGV

2 Kings 21 in the UGV2

2 Kings 21 in the UGV3

2 Kings 21 in the VBL

2 Kings 21 in the VDCC

2 Kings 21 in the YALU

2 Kings 21 in the YAPE

2 Kings 21 in the YBVTP

2 Kings 21 in the ZBP