2 Samuel 1 (BOKCV)
1 Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alipokuwa amerudi kutoka kuwashinda Waamaleki, Daudi alikaa siku mbili huko Siklagi. 2 Siku ya tatu akaja mtu mwenye nguo zilizoraruka na mavumbi kichwani mwake kutoka kwenye kambi ya Sauli. Alipomjia Daudi, akajitupa chini ili kumpa heshima. 3 Daudi akamuuliza, “Wewe umetoka wapi?”Akamjibu, “Nimetoroka kutoka kambi ya Waisraeli.” 4 Daudi akamuuliza, “Ni nini kilichotokea? Niambie.”Akasema, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wao walianguka na kufa. Naye Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa.” 5 Ndipo Daudi akamwambia huyo kijana aliyemletea taarifa, “Je, umefahamuje kwamba Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?” 6 Yule kijana akasema, “Nilijipata huko Mlima Gilboa, naye Sauli alikuwa huko akiegemea mkuki wake, na magari ya vita na wapanda farasi wa upande wa adui wakawa wamemkaribia sana. 7 Alipogeuka na kuniona, akaniita, nami nikasema, ‘Je, nifanye nini?’ 8 “Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’“Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki.’ 9 “Kisha akaniambia, ‘Nikaribie mimi na uniue! Niko katika maumivu makali ya kifo, lakini bado ningali hai.’ 10 “Kwa hiyo nikamkaribia nikamuua, kwa sababu nilijua kwamba baada ya kuanguka hangeweza kupona. Nami nikachukua lile taji lililokuwa kichwani mwake na utepe uliokuwa mkononi mwake nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.” 11 Ndipo Daudi pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye wakazishika nguo zao na kuzirarua. 12 Wakaomboleza, wakalia pia na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli na Yonathani mwanawe, kwa ajili ya jeshi la BWANA na nyumba ya Israeli, kwa sababu wameanguka kwa upanga. 13 Daudi akamwambia yule kijana aliyemletea taarifa, “Wewe ni mwenyeji wa wapi?”Akamjibu, “Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.” 14 Daudi akamuuliza, “Kwa nini hukuogopa kuinua mkono wako ili kumwangamiza mpakwa mafuta wa BWANA?” 15 Kisha Daudi akamwita mmoja wa watu wake na kumwambia, “Nenda ukamuue!” Kwa hiyo akampiga, naye akafa. 16 Kwa maana Daudi alikuwa amemwambia, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako mwenyewe. Kinywa chako mwenyewe kimeshuhudia dhidi yako uliposema, ‘Nilimuua mpakwa mafuta wa BWANA.’ ” 17 Daudi akafanya maombolezo haya kuhusu Sauli na Yonathani mwanawe, 18 naye akaagiza kwamba watu wa Yuda wafundishwe ombolezo hili la upinde (ambalo limeandikwa katika Kitabu cha Yashari): 19 “Walio fahari yako, ee Israeli, wameuawa juu ya mahali pako palipoinuka.Jinsi wenye nguvu walivyoanguka! 20 “Msilisimulie hili katika Gathi,msilitangaze hili katikabarabara za Ashkeloni,binti za Wafilisti wasije wakafurahia,binti za hao wasiotahiriwawasije wakashangilia. 21 “Enyi milima ya Gilboa,msipate umande wala mvua,wala mashamba yazaayo sadaka ya nafaka.Kwa maana huko ndiko ngao ya mwenye nguvu iliponajisiwa,ngao ya Sauli haitapakwa tena mafuta. 22 Kutokana na damu ya waliouawa,kutokana na miili ya wenye nguvu,ule upinde wa Yonathani haukugeuka nyuma.Upanga wa Sauli haukurudi bure. 23 “Sauli na Yonathani,maishani walipendwa na kuneemeka,na katika kifo hawakutengana.Walikuwa wepesi kuliko tai,walikuwa na nguvu kuliko simba. 24 “Enyi binti za Israeli,lieni kwa ajili ya Sauli,ambaye aliwavika nguonyekundu na maridadi,ambaye aliremba mavazi yenukwa mapambo ya dhahabu. 25 “Tazama jinsi mashujaawalivyoanguka vitani!Yonathani ameuawamahali pako palipoinuka. 26 Nahuzunika kwa ajili yako,Yonathani ndugu yangu,kwangu ulikuwa mpendwa sana.Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,wa ajabu zaidi kuliko ule wa wanawake. 27 “Tazama jinsi mashujaa walivyoanguka!Silaha za vita zimeangamia!”
In Other Versions
2 Samuel 1 in the ANGEFD
2 Samuel 1 in the ANTPNG2D
2 Samuel 1 in the AS21
2 Samuel 1 in the BAGH
2 Samuel 1 in the BBPNG
2 Samuel 1 in the BBT1E
2 Samuel 1 in the BDS
2 Samuel 1 in the BEV
2 Samuel 1 in the BHAD
2 Samuel 1 in the BIB
2 Samuel 1 in the BLPT
2 Samuel 1 in the BNT
2 Samuel 1 in the BNTABOOT
2 Samuel 1 in the BNTLV
2 Samuel 1 in the BOATCB
2 Samuel 1 in the BOATCB2
2 Samuel 1 in the BOBCV
2 Samuel 1 in the BOCNT
2 Samuel 1 in the BOECS
2 Samuel 1 in the BOGWICC
2 Samuel 1 in the BOHCB
2 Samuel 1 in the BOHCV
2 Samuel 1 in the BOHLNT
2 Samuel 1 in the BOHNTLTAL
2 Samuel 1 in the BOICB
2 Samuel 1 in the BOILNTAP
2 Samuel 1 in the BOITCV
2 Samuel 1 in the BOKCV2
2 Samuel 1 in the BOKHWOG
2 Samuel 1 in the BOKSSV
2 Samuel 1 in the BOLCB
2 Samuel 1 in the BOLCB2
2 Samuel 1 in the BOMCV
2 Samuel 1 in the BONAV
2 Samuel 1 in the BONCB
2 Samuel 1 in the BONLT
2 Samuel 1 in the BONUT2
2 Samuel 1 in the BOPLNT
2 Samuel 1 in the BOSCB
2 Samuel 1 in the BOSNC
2 Samuel 1 in the BOTLNT
2 Samuel 1 in the BOVCB
2 Samuel 1 in the BOYCB
2 Samuel 1 in the BPBB
2 Samuel 1 in the BPH
2 Samuel 1 in the BSB
2 Samuel 1 in the CCB
2 Samuel 1 in the CUV
2 Samuel 1 in the CUVS
2 Samuel 1 in the DBT
2 Samuel 1 in the DGDNT
2 Samuel 1 in the DHNT
2 Samuel 1 in the DNT
2 Samuel 1 in the ELBE
2 Samuel 1 in the EMTV
2 Samuel 1 in the ESV
2 Samuel 1 in the FBV
2 Samuel 1 in the FEB
2 Samuel 1 in the GGMNT
2 Samuel 1 in the GNT
2 Samuel 1 in the HARY
2 Samuel 1 in the HNT
2 Samuel 1 in the IRVA
2 Samuel 1 in the IRVB
2 Samuel 1 in the IRVG
2 Samuel 1 in the IRVH
2 Samuel 1 in the IRVK
2 Samuel 1 in the IRVM
2 Samuel 1 in the IRVM2
2 Samuel 1 in the IRVO
2 Samuel 1 in the IRVP
2 Samuel 1 in the IRVT
2 Samuel 1 in the IRVT2
2 Samuel 1 in the IRVU
2 Samuel 1 in the ISVN
2 Samuel 1 in the JSNT
2 Samuel 1 in the KAPI
2 Samuel 1 in the KBT1ETNIK
2 Samuel 1 in the KBV
2 Samuel 1 in the KJV
2 Samuel 1 in the KNFD
2 Samuel 1 in the LBA
2 Samuel 1 in the LBLA
2 Samuel 1 in the LNT
2 Samuel 1 in the LSV
2 Samuel 1 in the MAAL
2 Samuel 1 in the MBV
2 Samuel 1 in the MBV2
2 Samuel 1 in the MHNT
2 Samuel 1 in the MKNFD
2 Samuel 1 in the MNG
2 Samuel 1 in the MNT
2 Samuel 1 in the MNT2
2 Samuel 1 in the MRS1T
2 Samuel 1 in the NAA
2 Samuel 1 in the NASB
2 Samuel 1 in the NBLA
2 Samuel 1 in the NBS
2 Samuel 1 in the NBVTP
2 Samuel 1 in the NET2
2 Samuel 1 in the NIV11
2 Samuel 1 in the NNT
2 Samuel 1 in the NNT2
2 Samuel 1 in the NNT3
2 Samuel 1 in the PDDPT
2 Samuel 1 in the PFNT
2 Samuel 1 in the RMNT
2 Samuel 1 in the SBIAS
2 Samuel 1 in the SBIBS
2 Samuel 1 in the SBIBS2
2 Samuel 1 in the SBICS
2 Samuel 1 in the SBIDS
2 Samuel 1 in the SBIGS
2 Samuel 1 in the SBIHS
2 Samuel 1 in the SBIIS
2 Samuel 1 in the SBIIS2
2 Samuel 1 in the SBIIS3
2 Samuel 1 in the SBIKS
2 Samuel 1 in the SBIKS2
2 Samuel 1 in the SBIMS
2 Samuel 1 in the SBIOS
2 Samuel 1 in the SBIPS
2 Samuel 1 in the SBISS
2 Samuel 1 in the SBITS
2 Samuel 1 in the SBITS2
2 Samuel 1 in the SBITS3
2 Samuel 1 in the SBITS4
2 Samuel 1 in the SBIUS
2 Samuel 1 in the SBIVS
2 Samuel 1 in the SBT
2 Samuel 1 in the SBT1E
2 Samuel 1 in the SCHL
2 Samuel 1 in the SNT
2 Samuel 1 in the SUSU
2 Samuel 1 in the SUSU2
2 Samuel 1 in the SYNO
2 Samuel 1 in the TBIAOTANT
2 Samuel 1 in the TBT1E
2 Samuel 1 in the TBT1E2
2 Samuel 1 in the TFTIP
2 Samuel 1 in the TFTU
2 Samuel 1 in the TGNTATF3T
2 Samuel 1 in the THAI
2 Samuel 1 in the TNFD
2 Samuel 1 in the TNT
2 Samuel 1 in the TNTIK
2 Samuel 1 in the TNTIL
2 Samuel 1 in the TNTIN
2 Samuel 1 in the TNTIP
2 Samuel 1 in the TNTIZ
2 Samuel 1 in the TOMA
2 Samuel 1 in the TTENT
2 Samuel 1 in the UBG
2 Samuel 1 in the UGV
2 Samuel 1 in the UGV2
2 Samuel 1 in the UGV3
2 Samuel 1 in the VBL
2 Samuel 1 in the VDCC
2 Samuel 1 in the YALU
2 Samuel 1 in the YAPE
2 Samuel 1 in the YBVTP
2 Samuel 1 in the ZBP