Daniel 10 (BOKCV)
1 Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, Danieli (ambaye aliitwa Belteshaza) alipewa ufunuo. Ujumbe wake ulikuwa kweli, nao ulihusu vita vikubwa. Ufahamu wa ujumbe ulimjia katika maono. 2 Wakati huo, mimi Danieli nikaomboleza kwa majuma matatu. 3 Sikula chakula kizuri; nyama wala divai havikugusa midomo yangu; nami sikujipaka mafuta kamwe mpaka majuma matatu yalipotimia. 4 Kwenye siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa nimesimama kwenye ukingo wa mto mkubwa Hidekeli, 5 nikatazama juu, na mbele yangu alikuwepo mtu aliyevaa mavazi ya kitani na mshipi wa dhahabu safi kutoka ufazi kiunoni mwake. 6 Mwili wake ulikuwa kama kito cha zabarajadi safi, uso wake kama umeme wa radi, macho yake kama mwali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mngʼao wa shaba iliyosuguliwa sana, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu. 7 Mimi Danieli, ni mimi peke yangu niliyeona hayo maono; watu waliokuwa pamoja nami hawakuyaona, lakini waligubikwa na hofu kuu, hata wakakimbia na kujificha. 8 Kwa hiyo niliachwa peke yangu, nikikodolea macho maono hayo makubwa; sikubakiwa na nguvu, na rangi ya uso wangu ikabadilika kama aliyekufa, nikakosa nguvu. 9 Kisha nikamsikia akisema, nami nilipokuwa nikimsikiliza, nikalala kifudifudi, nikapatwa na usingizi mzito. 10 Mkono ulinigusa, ukaninyanyua, na kuniweka nikipiga magoti na mikono yangu ikashika chini, huku nikiwa bado ninatetemeka. 11 Akasema, “Danieli, wewe mtu upendwaye sana, fikiri kwa makini maneno ninayokwenda kunena nawe sasa; simama wima, kwa maana sasa nimetumwa kwako.” Naye aliponiambia haya, nikasimama nikitetemeka. 12 Ndipo akaendelea kusema, “Danieli, usiogope. Tangu siku ya kwanza ulipotia moyo wako ili kupata ufahamu na kujinyenyekeza mbele ya Mungu wako, maneno yako yalisikiwa, nami nimekuja ili kujibu maneno yako. 13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga kwa siku ishirini na moja. Ndipo Mikaeli, mmoja wa malaika wakuu, alikuja kunisaidia, kwa sababu nilikuwa nimezuiliwa huko na mfalme wa Uajemi. 14 Sasa nimekuja kukuelezea mambo yatakayowatokea watu wako wakati ujao, kwa maana maono hayo yanahusu wakati ambao haujaja bado.” 15 Alipokuwa akinielezea haya, nilisujudu uso wangu ukiwa umeelekea chini, nikawa bubu. 16 Ndipo mmoja aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa midomo yangu, nami nikafungua kinywa changu, nikaanza kunena. Nikamwambia yule aliyesimama mbele yangu, “Nimepatwa na huzuni kubwa kwa sababu ya maono haya, bwana wangu, nami nimeishiwa nguvu. 17 Bwana wangu, mimi mtumishi wako nitawezaje kuzungumza na wewe? Nguvu zangu zimeniishia hata ninashindwa kupumua.” 18 Tena yule aliyeonekana kama mwanadamu akanigusa na kunitia nguvu. 19 Akasema, “Ee mtu upendwaye sana, usiogope. Amani iwe kwako! Uwe na nguvu sasa; jipe nguvu.”Alipozungumza nami, nilipata nguvu, nikasema, “Nena, bwana wangu, kwa kuwa umenipa nguvu.” 20 Kwa hiyo akasema, “Je, unajua kwa nini nimekujia? Sasa hivi nitarudi kupigana dhidi ya mkuu wa Uajemi, nami nikienda, mkuu wa Uyunani atakuja. 21 Lakini kwanza nitakuambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Kweli. (Hakuna hata mmoja anayenisaidia dhidi yao isipokuwa Mikaeli, mkuu wenu.
In Other Versions
Daniel 10 in the ANGEFD
Daniel 10 in the ANTPNG2D
Daniel 10 in the AS21
Daniel 10 in the BAGH
Daniel 10 in the BBPNG
Daniel 10 in the BBT1E
Daniel 10 in the BDS
Daniel 10 in the BEV
Daniel 10 in the BHAD
Daniel 10 in the BIB
Daniel 10 in the BLPT
Daniel 10 in the BNT
Daniel 10 in the BNTABOOT
Daniel 10 in the BNTLV
Daniel 10 in the BOATCB
Daniel 10 in the BOATCB2
Daniel 10 in the BOBCV
Daniel 10 in the BOCNT
Daniel 10 in the BOECS
Daniel 10 in the BOGWICC
Daniel 10 in the BOHCB
Daniel 10 in the BOHCV
Daniel 10 in the BOHLNT
Daniel 10 in the BOHNTLTAL
Daniel 10 in the BOICB
Daniel 10 in the BOILNTAP
Daniel 10 in the BOITCV
Daniel 10 in the BOKCV2
Daniel 10 in the BOKHWOG
Daniel 10 in the BOKSSV
Daniel 10 in the BOLCB
Daniel 10 in the BOLCB2
Daniel 10 in the BOMCV
Daniel 10 in the BONAV
Daniel 10 in the BONCB
Daniel 10 in the BONLT
Daniel 10 in the BONUT2
Daniel 10 in the BOPLNT
Daniel 10 in the BOSCB
Daniel 10 in the BOSNC
Daniel 10 in the BOTLNT
Daniel 10 in the BOVCB
Daniel 10 in the BOYCB
Daniel 10 in the BPBB
Daniel 10 in the BPH
Daniel 10 in the BSB
Daniel 10 in the CCB
Daniel 10 in the CUV
Daniel 10 in the CUVS
Daniel 10 in the DBT
Daniel 10 in the DGDNT
Daniel 10 in the DHNT
Daniel 10 in the DNT
Daniel 10 in the ELBE
Daniel 10 in the EMTV
Daniel 10 in the ESV
Daniel 10 in the FBV
Daniel 10 in the FEB
Daniel 10 in the GGMNT
Daniel 10 in the GNT
Daniel 10 in the HARY
Daniel 10 in the HNT
Daniel 10 in the IRVA
Daniel 10 in the IRVB
Daniel 10 in the IRVG
Daniel 10 in the IRVH
Daniel 10 in the IRVK
Daniel 10 in the IRVM
Daniel 10 in the IRVM2
Daniel 10 in the IRVO
Daniel 10 in the IRVP
Daniel 10 in the IRVT
Daniel 10 in the IRVT2
Daniel 10 in the IRVU
Daniel 10 in the ISVN
Daniel 10 in the JSNT
Daniel 10 in the KAPI
Daniel 10 in the KBT1ETNIK
Daniel 10 in the KBV
Daniel 10 in the KJV
Daniel 10 in the KNFD
Daniel 10 in the LBA
Daniel 10 in the LBLA
Daniel 10 in the LNT
Daniel 10 in the LSV
Daniel 10 in the MAAL
Daniel 10 in the MBV
Daniel 10 in the MBV2
Daniel 10 in the MHNT
Daniel 10 in the MKNFD
Daniel 10 in the MNG
Daniel 10 in the MNT
Daniel 10 in the MNT2
Daniel 10 in the MRS1T
Daniel 10 in the NAA
Daniel 10 in the NASB
Daniel 10 in the NBLA
Daniel 10 in the NBS
Daniel 10 in the NBVTP
Daniel 10 in the NET2
Daniel 10 in the NIV11
Daniel 10 in the NNT
Daniel 10 in the NNT2
Daniel 10 in the NNT3
Daniel 10 in the PDDPT
Daniel 10 in the PFNT
Daniel 10 in the RMNT
Daniel 10 in the SBIAS
Daniel 10 in the SBIBS
Daniel 10 in the SBIBS2
Daniel 10 in the SBICS
Daniel 10 in the SBIDS
Daniel 10 in the SBIGS
Daniel 10 in the SBIHS
Daniel 10 in the SBIIS
Daniel 10 in the SBIIS2
Daniel 10 in the SBIIS3
Daniel 10 in the SBIKS
Daniel 10 in the SBIKS2
Daniel 10 in the SBIMS
Daniel 10 in the SBIOS
Daniel 10 in the SBIPS
Daniel 10 in the SBISS
Daniel 10 in the SBITS
Daniel 10 in the SBITS2
Daniel 10 in the SBITS3
Daniel 10 in the SBITS4
Daniel 10 in the SBIUS
Daniel 10 in the SBIVS
Daniel 10 in the SBT
Daniel 10 in the SBT1E
Daniel 10 in the SCHL
Daniel 10 in the SNT
Daniel 10 in the SUSU
Daniel 10 in the SUSU2
Daniel 10 in the SYNO
Daniel 10 in the TBIAOTANT
Daniel 10 in the TBT1E
Daniel 10 in the TBT1E2
Daniel 10 in the TFTIP
Daniel 10 in the TFTU
Daniel 10 in the TGNTATF3T
Daniel 10 in the THAI
Daniel 10 in the TNFD
Daniel 10 in the TNT
Daniel 10 in the TNTIK
Daniel 10 in the TNTIL
Daniel 10 in the TNTIN
Daniel 10 in the TNTIP
Daniel 10 in the TNTIZ
Daniel 10 in the TOMA
Daniel 10 in the TTENT
Daniel 10 in the UBG
Daniel 10 in the UGV
Daniel 10 in the UGV2
Daniel 10 in the UGV3
Daniel 10 in the VBL
Daniel 10 in the VDCC
Daniel 10 in the YALU
Daniel 10 in the YAPE
Daniel 10 in the YBVTP
Daniel 10 in the ZBP