Esther 8 (BOKCV)
1 Siku ile ile Mfalme Ahasuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye. 2 Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyangʼanya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani. 3 Esta alimsihi tena mfalme, akianguka miguuni pake na kulia. Akamwomba akomeshe mpango mwovu wa Hamani Mwagagi ambao alikuwa ameupanga dhidi ya Wayahudi. 4 Kisha mfalme alimnyooshea Esta fimbo yake ya utawala ya dhahabu naye aliinuka na kusimama mbele yake. 5 Esta akasema, “Kama ikimpendeza mfalme, nami kama nikipata kibali naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea na kama akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme. 6 Kwa maana nitawezaje kuvumilia kuona maafa yakiwapata watu wangu? Nitawezaje kuvumilia kuona maangamizi ya jamaa yangu?” 7 Mfalme Ahasuero akawajibu Malkia Esta na Mordekai Myahudi, “Kwa sababu Hamani aliwashambulia Wayahudi, nimetoa shamba la Hamani kwa Esta, naye ameangikwa kwenye mti wa kunyongea. 8 Basi andika amri nyingine kwa jina la mfalme kwa ajili ya Wayahudi kama unavyoona vyema, kisha uifunge kwa kutia muhuri kwa pete ya mfalme kwa kuwa hakuna andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme linaloweza kutanguliwa.” 9 Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi. Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao. 10 Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahasuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa njia ya matarishi, ambao waliendesha farasi waendao kasi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme. 11 Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lolote, taifa lolote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali za adui zao. 12 Siku ambayo iliwekwa kwa Wayahudi kufanya hili katika majimbo yote ya Mfalme Ahasuero ilikuwa siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari. 13 Nakala ya tangazo ilikuwa itolewe kama sheria katika kila jimbo na iweze kujulikana kwa watu wa kila taifa, ili kwamba Wayahudi wawe tayari siku hiyo kulipiza kisasi kwa adui zao. 14 Matarishi, wakiwa wamepanda farasi wa kifalme, walitoka mbio wakichochewa na agizo la mfalme. Tangazo lilitolewa pia katika ngome ya mji wa Shushani. 15 Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherehekea kwa furaha. 16 Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima. 17 Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.
In Other Versions
Esther 8 in the ANGEFD
Esther 8 in the ANTPNG2D
Esther 8 in the AS21
Esther 8 in the BAGH
Esther 8 in the BBPNG
Esther 8 in the BBT1E
Esther 8 in the BDS
Esther 8 in the BEV
Esther 8 in the BHAD
Esther 8 in the BIB
Esther 8 in the BLPT
Esther 8 in the BNT
Esther 8 in the BNTABOOT
Esther 8 in the BNTLV
Esther 8 in the BOATCB
Esther 8 in the BOATCB2
Esther 8 in the BOBCV
Esther 8 in the BOCNT
Esther 8 in the BOECS
Esther 8 in the BOGWICC
Esther 8 in the BOHCB
Esther 8 in the BOHCV
Esther 8 in the BOHLNT
Esther 8 in the BOHNTLTAL
Esther 8 in the BOICB
Esther 8 in the BOILNTAP
Esther 8 in the BOITCV
Esther 8 in the BOKCV2
Esther 8 in the BOKHWOG
Esther 8 in the BOKSSV
Esther 8 in the BOLCB
Esther 8 in the BOLCB2
Esther 8 in the BOMCV
Esther 8 in the BONAV
Esther 8 in the BONCB
Esther 8 in the BONLT
Esther 8 in the BONUT2
Esther 8 in the BOPLNT
Esther 8 in the BOSCB
Esther 8 in the BOSNC
Esther 8 in the BOTLNT
Esther 8 in the BOVCB
Esther 8 in the BOYCB
Esther 8 in the BPBB
Esther 8 in the BPH
Esther 8 in the BSB
Esther 8 in the CCB
Esther 8 in the CUV
Esther 8 in the CUVS
Esther 8 in the DBT
Esther 8 in the DGDNT
Esther 8 in the DHNT
Esther 8 in the DNT
Esther 8 in the ELBE
Esther 8 in the EMTV
Esther 8 in the ESV
Esther 8 in the FBV
Esther 8 in the FEB
Esther 8 in the GGMNT
Esther 8 in the GNT
Esther 8 in the HARY
Esther 8 in the HNT
Esther 8 in the IRVA
Esther 8 in the IRVB
Esther 8 in the IRVG
Esther 8 in the IRVH
Esther 8 in the IRVK
Esther 8 in the IRVM
Esther 8 in the IRVM2
Esther 8 in the IRVO
Esther 8 in the IRVP
Esther 8 in the IRVT
Esther 8 in the IRVT2
Esther 8 in the IRVU
Esther 8 in the ISVN
Esther 8 in the JSNT
Esther 8 in the KAPI
Esther 8 in the KBT1ETNIK
Esther 8 in the KBV
Esther 8 in the KJV
Esther 8 in the KNFD
Esther 8 in the LBA
Esther 8 in the LBLA
Esther 8 in the LNT
Esther 8 in the LSV
Esther 8 in the MAAL
Esther 8 in the MBV
Esther 8 in the MBV2
Esther 8 in the MHNT
Esther 8 in the MKNFD
Esther 8 in the MNG
Esther 8 in the MNT
Esther 8 in the MNT2
Esther 8 in the MRS1T
Esther 8 in the NAA
Esther 8 in the NASB
Esther 8 in the NBLA
Esther 8 in the NBS
Esther 8 in the NBVTP
Esther 8 in the NET2
Esther 8 in the NIV11
Esther 8 in the NNT
Esther 8 in the NNT2
Esther 8 in the NNT3
Esther 8 in the PDDPT
Esther 8 in the PFNT
Esther 8 in the RMNT
Esther 8 in the SBIAS
Esther 8 in the SBIBS
Esther 8 in the SBIBS2
Esther 8 in the SBICS
Esther 8 in the SBIDS
Esther 8 in the SBIGS
Esther 8 in the SBIHS
Esther 8 in the SBIIS
Esther 8 in the SBIIS2
Esther 8 in the SBIIS3
Esther 8 in the SBIKS
Esther 8 in the SBIKS2
Esther 8 in the SBIMS
Esther 8 in the SBIOS
Esther 8 in the SBIPS
Esther 8 in the SBISS
Esther 8 in the SBITS
Esther 8 in the SBITS2
Esther 8 in the SBITS3
Esther 8 in the SBITS4
Esther 8 in the SBIUS
Esther 8 in the SBIVS
Esther 8 in the SBT
Esther 8 in the SBT1E
Esther 8 in the SCHL
Esther 8 in the SNT
Esther 8 in the SUSU
Esther 8 in the SUSU2
Esther 8 in the SYNO
Esther 8 in the TBIAOTANT
Esther 8 in the TBT1E
Esther 8 in the TBT1E2
Esther 8 in the TFTIP
Esther 8 in the TFTU
Esther 8 in the TGNTATF3T
Esther 8 in the THAI
Esther 8 in the TNFD
Esther 8 in the TNT
Esther 8 in the TNTIK
Esther 8 in the TNTIL
Esther 8 in the TNTIN
Esther 8 in the TNTIP
Esther 8 in the TNTIZ
Esther 8 in the TOMA
Esther 8 in the TTENT
Esther 8 in the UBG
Esther 8 in the UGV
Esther 8 in the UGV2
Esther 8 in the UGV3
Esther 8 in the VBL
Esther 8 in the VDCC
Esther 8 in the YALU
Esther 8 in the YAPE
Esther 8 in the YBVTP
Esther 8 in the ZBP