Exodus 18 (BOKCV)
1 Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Mose, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Mose na watu wake wa Israeli, pia jinsi BWANA alivyowatoa Israeli Misri. 2 Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea 3 pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Mose alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” 4 Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.” 5 Yethro, baba mkwe wa Mose, pamoja na wana wawili wa Mose na mkewe, wakamjia Mose huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu. 6 Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Mose, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.” 7 Kwa hiyo Mose akatoka kumlaki baba mkwe wake, akainama na kumbusu. Wakasalimiana, kisha wakaingia hemani. 8 Mose akamwambia baba mkwe wake kuhusu kila kitu BWANA alichomfanyia Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na pia kuhusu shida zote walizokutana nazo njiani na jinsi BWANA alivyowaokoa. 9 Yethro akafurahishwa sana kusikia juu ya mambo yote mazuri BWANA aliyowatendea Waisraeli kuwaokoa kutoka mkono wa Wamisri. 10 Yethro akasema, “Sifa na ziwe kwa BWANA, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri. 11 Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu mingine yote, kwa kuwa amewatendea hivi wale waliowatenda Israeli kwa ujeuri.” 12 Kisha Yethro, baba mkwe wa Mose, akaleta sadaka ya kuteketezwa na dhabihu nyingine kwa Mungu, naye Aroni pamoja na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula pamoja na baba mkwe wa Mose mbele za Mungu. 13 Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. 14 Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?” 15 Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. 16 Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.” 17 Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. 18 Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. 19 Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. 20 Uwafundishe amri na sheria, tena uwaonyeshe namna ya kuishi na kazi zinazowapasa wao kufanya. 21 Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. 22 Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. 23 Kama ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.” 24 Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. 25 Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. 26 Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe. 27 Kisha Mose akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake.
In Other Versions
Exodus 18 in the ANGEFD
Exodus 18 in the ANTPNG2D
Exodus 18 in the AS21
Exodus 18 in the BAGH
Exodus 18 in the BBPNG
Exodus 18 in the BBT1E
Exodus 18 in the BDS
Exodus 18 in the BEV
Exodus 18 in the BHAD
Exodus 18 in the BIB
Exodus 18 in the BLPT
Exodus 18 in the BNT
Exodus 18 in the BNTABOOT
Exodus 18 in the BNTLV
Exodus 18 in the BOATCB
Exodus 18 in the BOATCB2
Exodus 18 in the BOBCV
Exodus 18 in the BOCNT
Exodus 18 in the BOECS
Exodus 18 in the BOGWICC
Exodus 18 in the BOHCB
Exodus 18 in the BOHCV
Exodus 18 in the BOHLNT
Exodus 18 in the BOHNTLTAL
Exodus 18 in the BOICB
Exodus 18 in the BOILNTAP
Exodus 18 in the BOITCV
Exodus 18 in the BOKCV2
Exodus 18 in the BOKHWOG
Exodus 18 in the BOKSSV
Exodus 18 in the BOLCB
Exodus 18 in the BOLCB2
Exodus 18 in the BOMCV
Exodus 18 in the BONAV
Exodus 18 in the BONCB
Exodus 18 in the BONLT
Exodus 18 in the BONUT2
Exodus 18 in the BOPLNT
Exodus 18 in the BOSCB
Exodus 18 in the BOSNC
Exodus 18 in the BOTLNT
Exodus 18 in the BOVCB
Exodus 18 in the BOYCB
Exodus 18 in the BPBB
Exodus 18 in the BPH
Exodus 18 in the BSB
Exodus 18 in the CCB
Exodus 18 in the CUV
Exodus 18 in the CUVS
Exodus 18 in the DBT
Exodus 18 in the DGDNT
Exodus 18 in the DHNT
Exodus 18 in the DNT
Exodus 18 in the ELBE
Exodus 18 in the EMTV
Exodus 18 in the ESV
Exodus 18 in the FBV
Exodus 18 in the FEB
Exodus 18 in the GGMNT
Exodus 18 in the GNT
Exodus 18 in the HARY
Exodus 18 in the HNT
Exodus 18 in the IRVA
Exodus 18 in the IRVB
Exodus 18 in the IRVG
Exodus 18 in the IRVH
Exodus 18 in the IRVK
Exodus 18 in the IRVM
Exodus 18 in the IRVM2
Exodus 18 in the IRVO
Exodus 18 in the IRVP
Exodus 18 in the IRVT
Exodus 18 in the IRVT2
Exodus 18 in the IRVU
Exodus 18 in the ISVN
Exodus 18 in the JSNT
Exodus 18 in the KAPI
Exodus 18 in the KBT1ETNIK
Exodus 18 in the KBV
Exodus 18 in the KJV
Exodus 18 in the KNFD
Exodus 18 in the LBA
Exodus 18 in the LBLA
Exodus 18 in the LNT
Exodus 18 in the LSV
Exodus 18 in the MAAL
Exodus 18 in the MBV
Exodus 18 in the MBV2
Exodus 18 in the MHNT
Exodus 18 in the MKNFD
Exodus 18 in the MNG
Exodus 18 in the MNT
Exodus 18 in the MNT2
Exodus 18 in the MRS1T
Exodus 18 in the NAA
Exodus 18 in the NASB
Exodus 18 in the NBLA
Exodus 18 in the NBS
Exodus 18 in the NBVTP
Exodus 18 in the NET2
Exodus 18 in the NIV11
Exodus 18 in the NNT
Exodus 18 in the NNT2
Exodus 18 in the NNT3
Exodus 18 in the PDDPT
Exodus 18 in the PFNT
Exodus 18 in the RMNT
Exodus 18 in the SBIAS
Exodus 18 in the SBIBS
Exodus 18 in the SBIBS2
Exodus 18 in the SBICS
Exodus 18 in the SBIDS
Exodus 18 in the SBIGS
Exodus 18 in the SBIHS
Exodus 18 in the SBIIS
Exodus 18 in the SBIIS2
Exodus 18 in the SBIIS3
Exodus 18 in the SBIKS
Exodus 18 in the SBIKS2
Exodus 18 in the SBIMS
Exodus 18 in the SBIOS
Exodus 18 in the SBIPS
Exodus 18 in the SBISS
Exodus 18 in the SBITS
Exodus 18 in the SBITS2
Exodus 18 in the SBITS3
Exodus 18 in the SBITS4
Exodus 18 in the SBIUS
Exodus 18 in the SBIVS
Exodus 18 in the SBT
Exodus 18 in the SBT1E
Exodus 18 in the SCHL
Exodus 18 in the SNT
Exodus 18 in the SUSU
Exodus 18 in the SUSU2
Exodus 18 in the SYNO
Exodus 18 in the TBIAOTANT
Exodus 18 in the TBT1E
Exodus 18 in the TBT1E2
Exodus 18 in the TFTIP
Exodus 18 in the TFTU
Exodus 18 in the TGNTATF3T
Exodus 18 in the THAI
Exodus 18 in the TNFD
Exodus 18 in the TNT
Exodus 18 in the TNTIK
Exodus 18 in the TNTIL
Exodus 18 in the TNTIN
Exodus 18 in the TNTIP
Exodus 18 in the TNTIZ
Exodus 18 in the TOMA
Exodus 18 in the TTENT
Exodus 18 in the UBG
Exodus 18 in the UGV
Exodus 18 in the UGV2
Exodus 18 in the UGV3
Exodus 18 in the VBL
Exodus 18 in the VDCC
Exodus 18 in the YALU
Exodus 18 in the YAPE
Exodus 18 in the YBVTP
Exodus 18 in the ZBP