Exodus 19 (BOKCV)
1 Mnamo mwezi wa tatu baada ya Waisraeli kuondoka Misri, siku kama iyo hiyo, wakafika katika Jangwa la Sinai. 2 Baada ya kuondoka Refidimu, waliingia katika Jangwa la Sinai na Israeli wakapiga kambi pale jangwani mbele ya mlima. 3 Kisha Mose akakwea kwenda kwa Mungu, naye BWANA akamwita kutoka kwenye ule mlima akasema, “Hivi ndivyo utakavyosema na nyumba ya Yakobo na utakachowaambia watu wa Israeli: 4 ‘Ninyi wenyewe mmeona nililofanya huko Misri, jinsi nilivyowabeba kwenye mbawa za tai na kuwaleta kwangu. 5 Sasa kama mkinitii kikamilifu na kutunza Agano langu, basi ninyi mtakuwa mali yangu ya thamani kubwa miongoni mwa mataifa yote. Ijapokuwa dunia yote ni mali yangu, 6 ninyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani na taifa takatifu.’ Haya ndiyo maneno utakayosema kwa wana wa Israeli.” 7 Kwa hiyo Mose akarudi, akawaita wazee wa watu na kuwaambia maneno yote ambayo BWANA alikuwa amemwamuru ayaseme. 8 Watu wote wakajibu kwa pamoja, “Tutafanya kila kitu BWANA alichokisema.” Naye Mose akarudisha majibu yao kwa BWANA. 9 BWANA akamwambia Mose, “Nitakujia katika wingu zito, ili watu wanisikie nikinena nawe na kila mara waweke tumaini lao kwako.” Kisha Mose akamwambia BWANA yale ambayo watu walikuwa wamesema. 10 Naye BWANA akamwambia Mose, “Nenda kwa watu ukawaweke wakfu leo na kesho. Waambie wafue nguo zao 11 na wawe tayari siku ya tatu, kwa sababu siku hiyo, BWANA atashuka juu ya mlima Sinai machoni pa watu wote. 12 Weka mipaka kuzunguka mlima kwa ajili ya watu, uwaambie, ‘Mwe waangalifu, msije mkapanda mlimani au kuugusa. Yeyote atakayeugusa mlima hakika atauawa. 13 Hakika atapigwa mawe au kupigwa mishale; mkono wa mtu hautamgusa. Akiwa mwanadamu au mnyama, hataruhusiwa kuishi.’ Ila tu wakati baragumu itakapopigwa kwa mfululizo, ndipo watu wote watakapopanda mlimani.” 14 Baada ya Mose kushuka kutoka mlimani akawaendea watu na kuwaweka wakfu, wakafua nguo zao. 15 Kisha akawaambia watu, “Jitayarisheni kwa ajili ya siku ya tatu. Mwanaume yeyote asimkaribie mwanamke.” 16 Asubuhi ya siku ya tatu kulikuwa na ngurumo na radi pamoja na wingu nene juu ya mlima na mlio mkubwa sana wa tarumbeta. Kila mmoja aliyekuwa kambini akatetemeka. 17 Kisha Mose akawaongoza watu kutoka kambini kukutana na Mungu, nao wakasimama chini ya mlima. 18 Mlima Sinai ulikuwa umefunikwa na moshi, kwa sababu BWANA alishuka juu yake katika moto. Moshi wa moto huo ulipanda juu kama moshi kutoka kwenye tanuru kubwa na mlima wote ukatetemeka kwa nguvu nyingi, 19 nayo sauti ya tarumbeta ikawa kubwa zaidi na zaidi. Kisha Mose akazungumza na sauti ya BWANA ikamjibu. 20 BWANA akashuka juu ya Mlima Sinai na akamwita Mose apande juu mlimani. Kwa hiyo Mose akapanda juu, 21 naye BWANA akamwambia Mose, “Shuka ukawaonye watu ili wasijipenyeze kutafuta kumwona BWANA na wengi wao wakafa. 22 Hata makuhani, watakaomkaribia BWANA ni lazima wajiweke wakfu, la sivyo BWANA atawaadhibu.” 23 Mose akamwambia BWANA, “Watu hawawezi kupanda mlima Sinai kwa sababu wewe mwenyewe ulituonya ukisema, ‘Wekeni mipaka kuuzunguka mlima na kuutenga kama patakatifu.’ ” 24 BWANA akajibu, “Shuka ukamlete Aroni pamoja nawe. Lakini makuhani pamoja na watu wasije wakalazimisha kuja kwa BWANA, nisije nikawaadhibu.” 25 Basi Mose akashuka kwa watu na kuwaambia lile aliloambiwa.
In Other Versions
Exodus 19 in the ANGEFD
Exodus 19 in the ANTPNG2D
Exodus 19 in the AS21
Exodus 19 in the BAGH
Exodus 19 in the BBPNG
Exodus 19 in the BBT1E
Exodus 19 in the BDS
Exodus 19 in the BEV
Exodus 19 in the BHAD
Exodus 19 in the BIB
Exodus 19 in the BLPT
Exodus 19 in the BNT
Exodus 19 in the BNTABOOT
Exodus 19 in the BNTLV
Exodus 19 in the BOATCB
Exodus 19 in the BOATCB2
Exodus 19 in the BOBCV
Exodus 19 in the BOCNT
Exodus 19 in the BOECS
Exodus 19 in the BOGWICC
Exodus 19 in the BOHCB
Exodus 19 in the BOHCV
Exodus 19 in the BOHLNT
Exodus 19 in the BOHNTLTAL
Exodus 19 in the BOICB
Exodus 19 in the BOILNTAP
Exodus 19 in the BOITCV
Exodus 19 in the BOKCV2
Exodus 19 in the BOKHWOG
Exodus 19 in the BOKSSV
Exodus 19 in the BOLCB
Exodus 19 in the BOLCB2
Exodus 19 in the BOMCV
Exodus 19 in the BONAV
Exodus 19 in the BONCB
Exodus 19 in the BONLT
Exodus 19 in the BONUT2
Exodus 19 in the BOPLNT
Exodus 19 in the BOSCB
Exodus 19 in the BOSNC
Exodus 19 in the BOTLNT
Exodus 19 in the BOVCB
Exodus 19 in the BOYCB
Exodus 19 in the BPBB
Exodus 19 in the BPH
Exodus 19 in the BSB
Exodus 19 in the CCB
Exodus 19 in the CUV
Exodus 19 in the CUVS
Exodus 19 in the DBT
Exodus 19 in the DGDNT
Exodus 19 in the DHNT
Exodus 19 in the DNT
Exodus 19 in the ELBE
Exodus 19 in the EMTV
Exodus 19 in the ESV
Exodus 19 in the FBV
Exodus 19 in the FEB
Exodus 19 in the GGMNT
Exodus 19 in the GNT
Exodus 19 in the HARY
Exodus 19 in the HNT
Exodus 19 in the IRVA
Exodus 19 in the IRVB
Exodus 19 in the IRVG
Exodus 19 in the IRVH
Exodus 19 in the IRVK
Exodus 19 in the IRVM
Exodus 19 in the IRVM2
Exodus 19 in the IRVO
Exodus 19 in the IRVP
Exodus 19 in the IRVT
Exodus 19 in the IRVT2
Exodus 19 in the IRVU
Exodus 19 in the ISVN
Exodus 19 in the JSNT
Exodus 19 in the KAPI
Exodus 19 in the KBT1ETNIK
Exodus 19 in the KBV
Exodus 19 in the KJV
Exodus 19 in the KNFD
Exodus 19 in the LBA
Exodus 19 in the LBLA
Exodus 19 in the LNT
Exodus 19 in the LSV
Exodus 19 in the MAAL
Exodus 19 in the MBV
Exodus 19 in the MBV2
Exodus 19 in the MHNT
Exodus 19 in the MKNFD
Exodus 19 in the MNG
Exodus 19 in the MNT
Exodus 19 in the MNT2
Exodus 19 in the MRS1T
Exodus 19 in the NAA
Exodus 19 in the NASB
Exodus 19 in the NBLA
Exodus 19 in the NBS
Exodus 19 in the NBVTP
Exodus 19 in the NET2
Exodus 19 in the NIV11
Exodus 19 in the NNT
Exodus 19 in the NNT2
Exodus 19 in the NNT3
Exodus 19 in the PDDPT
Exodus 19 in the PFNT
Exodus 19 in the RMNT
Exodus 19 in the SBIAS
Exodus 19 in the SBIBS
Exodus 19 in the SBIBS2
Exodus 19 in the SBICS
Exodus 19 in the SBIDS
Exodus 19 in the SBIGS
Exodus 19 in the SBIHS
Exodus 19 in the SBIIS
Exodus 19 in the SBIIS2
Exodus 19 in the SBIIS3
Exodus 19 in the SBIKS
Exodus 19 in the SBIKS2
Exodus 19 in the SBIMS
Exodus 19 in the SBIOS
Exodus 19 in the SBIPS
Exodus 19 in the SBISS
Exodus 19 in the SBITS
Exodus 19 in the SBITS2
Exodus 19 in the SBITS3
Exodus 19 in the SBITS4
Exodus 19 in the SBIUS
Exodus 19 in the SBIVS
Exodus 19 in the SBT
Exodus 19 in the SBT1E
Exodus 19 in the SCHL
Exodus 19 in the SNT
Exodus 19 in the SUSU
Exodus 19 in the SUSU2
Exodus 19 in the SYNO
Exodus 19 in the TBIAOTANT
Exodus 19 in the TBT1E
Exodus 19 in the TBT1E2
Exodus 19 in the TFTIP
Exodus 19 in the TFTU
Exodus 19 in the TGNTATF3T
Exodus 19 in the THAI
Exodus 19 in the TNFD
Exodus 19 in the TNT
Exodus 19 in the TNTIK
Exodus 19 in the TNTIL
Exodus 19 in the TNTIN
Exodus 19 in the TNTIP
Exodus 19 in the TNTIZ
Exodus 19 in the TOMA
Exodus 19 in the TTENT
Exodus 19 in the UBG
Exodus 19 in the UGV
Exodus 19 in the UGV2
Exodus 19 in the UGV3
Exodus 19 in the VBL
Exodus 19 in the VDCC
Exodus 19 in the YALU
Exodus 19 in the YAPE
Exodus 19 in the YBVTP
Exodus 19 in the ZBP