Exodus 2 (BOKCV)
1 Basi mtu mmoja wa nyumba ya Lawi akaoa mwanamke Mlawi, 2 naye mwanamke huyo akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Alipoona mtoto huyo ni mzuri, akamficha kwa miezi mitatu. 3 Lakini alipoona hawezi kumficha zaidi, akamtengenezea kisafina cha mafunjo, akakipaka lami. Kisha akamweka huyo mtoto ndani yake, akakificha katikati ya matete kando ya ukingo wa Mto Naili. 4 Dada ya huyo mtoto akasimama mbali ili kuona kitakachompata mtoto. 5 Ndipo binti Farao akateremka mtoni Naili kuoga, nao wahudumu wake wakawa wanatembea ukingoni mwa mto. Binti mfalme akaona kisafina katikati ya manyasi, akamtuma mmoja wa watumwa wake wa kike kukichukua. 6 Alifungua kisafina akaona mtoto ndani yake. Mtoto alikuwa akilia, akamhurumia. Akasema, “Huyu ni mmoja wa watoto wa Kiebrania.” 7 Ndipo dada wa huyo mtoto akamuuliza binti Farao, “Je, niende nikakutafutie mmoja wa wanawake wa Kiebrania akulelee huyu mtoto?” 8 Binti Farao akamjibu, “Ndiyo, nenda.” Yule msichana akaenda akamleta mama wa mtoto. 9 Binti Farao akamwambia, “Mchukue huyu mtoto unisaidie kumlea, nami nitakulipa.” Basi yule mwanamke akamchukua mtoto na kumlea. 10 Mtoto alipokua, akampeleka kwa binti Farao, naye akawa mwanawe. Akamwita jina lake Mose akisema, “Nilimtoa kwenye maji.” 11 Siku moja, baada ya Mose kukua, akaondoka kwenda walikokuwa watu wake, na akachunguza jinsi walivyokuwa wakifanya kazi ngumu. Akamwona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmojawapo wa watu wake. 12 Mose akatazama huku na huko asione mtu yeyote, akamuua yule Mmisri, akamficha mchangani. 13 Kesho yake akatoka, akaona Waebrania wawili wakipigana. Akamuuliza yule aliyekosa, “Mbona unampiga Mwebrania mwenzako?” 14 Yule mtu akamjibu, “Ni nani aliyekufanya mtawala na mwamuzi juu yetu? Je, unataka kuniua kama ulivyomuua yule Mmisri?” Ndipo Mose akaogopa na kuwaza, “Jambo lile nililofanya lazima limefahamika.” 15 Farao aliposikia jambo hili, alijaribu kumuua Mose, lakini Mose akamkimbia Farao na kwenda kuishi katika nchi ya Midiani, akaketi kando ya kisima. 16 Kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja kisimani ili kuchota maji na kujaza hori kwa ajili ya kunyweshea mifugo ya baba yao. 17 Baadhi ya wachungaji wakaja wakawafukuza hao wasichana. Ndipo Mose akainuka, akawasaidia na kunywesha mifugo yao. 18 Hao wasichana waliporudi nyumbani kwa Reueli baba yao, akawauliza, “Imekuwaje leo mmerudi mapema hivyo?” 19 Wakamjibu, “Mmisri mmoja alituokoa kutoka mikononi mwa wachungaji. Pia mtu huyo alituchotea maji na kunywesha mifugo.” 20 Akawauliza binti zake, “Yuko wapi? Mbona mmemwacha? Mkaribisheni ale chakula.” 21 Mose akakubali kukaa kwa huyo mtu, ambaye alimpa Mose binti yake aliyeitwa Sipora amwoe. 22 Sipora alizaa mtoto wa kiume, naye Mose akamwita Gershomu, akisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” 23 Baada ya muda mrefu, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli wakalia kwa huzuni katika utumwa wao, walilia na kilio chao cha kutaka msaada kwa ajili ya utumwa kikamfikia Mungu. 24 Mungu akasikia kilio chao cha huzuni, akakumbuka Agano alilofanya na Abrahamu pamoja na Isaki na Yakobo. 25 Kwa hiyo Mungu akawaangalia Waisraeli na kuwahurumia.
In Other Versions
Exodus 2 in the ANGEFD
Exodus 2 in the ANTPNG2D
Exodus 2 in the AS21
Exodus 2 in the BAGH
Exodus 2 in the BBPNG
Exodus 2 in the BBT1E
Exodus 2 in the BDS
Exodus 2 in the BEV
Exodus 2 in the BHAD
Exodus 2 in the BIB
Exodus 2 in the BLPT
Exodus 2 in the BNT
Exodus 2 in the BNTABOOT
Exodus 2 in the BNTLV
Exodus 2 in the BOATCB
Exodus 2 in the BOATCB2
Exodus 2 in the BOBCV
Exodus 2 in the BOCNT
Exodus 2 in the BOECS
Exodus 2 in the BOGWICC
Exodus 2 in the BOHCB
Exodus 2 in the BOHCV
Exodus 2 in the BOHLNT
Exodus 2 in the BOHNTLTAL
Exodus 2 in the BOICB
Exodus 2 in the BOILNTAP
Exodus 2 in the BOITCV
Exodus 2 in the BOKCV2
Exodus 2 in the BOKHWOG
Exodus 2 in the BOKSSV
Exodus 2 in the BOLCB
Exodus 2 in the BOLCB2
Exodus 2 in the BOMCV
Exodus 2 in the BONAV
Exodus 2 in the BONCB
Exodus 2 in the BONLT
Exodus 2 in the BONUT2
Exodus 2 in the BOPLNT
Exodus 2 in the BOSCB
Exodus 2 in the BOSNC
Exodus 2 in the BOTLNT
Exodus 2 in the BOVCB
Exodus 2 in the BOYCB
Exodus 2 in the BPBB
Exodus 2 in the BPH
Exodus 2 in the BSB
Exodus 2 in the CCB
Exodus 2 in the CUV
Exodus 2 in the CUVS
Exodus 2 in the DBT
Exodus 2 in the DGDNT
Exodus 2 in the DHNT
Exodus 2 in the DNT
Exodus 2 in the ELBE
Exodus 2 in the EMTV
Exodus 2 in the ESV
Exodus 2 in the FBV
Exodus 2 in the FEB
Exodus 2 in the GGMNT
Exodus 2 in the GNT
Exodus 2 in the HARY
Exodus 2 in the HNT
Exodus 2 in the IRVA
Exodus 2 in the IRVB
Exodus 2 in the IRVG
Exodus 2 in the IRVH
Exodus 2 in the IRVK
Exodus 2 in the IRVM
Exodus 2 in the IRVM2
Exodus 2 in the IRVO
Exodus 2 in the IRVP
Exodus 2 in the IRVT
Exodus 2 in the IRVT2
Exodus 2 in the IRVU
Exodus 2 in the ISVN
Exodus 2 in the JSNT
Exodus 2 in the KAPI
Exodus 2 in the KBT1ETNIK
Exodus 2 in the KBV
Exodus 2 in the KJV
Exodus 2 in the KNFD
Exodus 2 in the LBA
Exodus 2 in the LBLA
Exodus 2 in the LNT
Exodus 2 in the LSV
Exodus 2 in the MAAL
Exodus 2 in the MBV
Exodus 2 in the MBV2
Exodus 2 in the MHNT
Exodus 2 in the MKNFD
Exodus 2 in the MNG
Exodus 2 in the MNT
Exodus 2 in the MNT2
Exodus 2 in the MRS1T
Exodus 2 in the NAA
Exodus 2 in the NASB
Exodus 2 in the NBLA
Exodus 2 in the NBS
Exodus 2 in the NBVTP
Exodus 2 in the NET2
Exodus 2 in the NIV11
Exodus 2 in the NNT
Exodus 2 in the NNT2
Exodus 2 in the NNT3
Exodus 2 in the PDDPT
Exodus 2 in the PFNT
Exodus 2 in the RMNT
Exodus 2 in the SBIAS
Exodus 2 in the SBIBS
Exodus 2 in the SBIBS2
Exodus 2 in the SBICS
Exodus 2 in the SBIDS
Exodus 2 in the SBIGS
Exodus 2 in the SBIHS
Exodus 2 in the SBIIS
Exodus 2 in the SBIIS2
Exodus 2 in the SBIIS3
Exodus 2 in the SBIKS
Exodus 2 in the SBIKS2
Exodus 2 in the SBIMS
Exodus 2 in the SBIOS
Exodus 2 in the SBIPS
Exodus 2 in the SBISS
Exodus 2 in the SBITS
Exodus 2 in the SBITS2
Exodus 2 in the SBITS3
Exodus 2 in the SBITS4
Exodus 2 in the SBIUS
Exodus 2 in the SBIVS
Exodus 2 in the SBT
Exodus 2 in the SBT1E
Exodus 2 in the SCHL
Exodus 2 in the SNT
Exodus 2 in the SUSU
Exodus 2 in the SUSU2
Exodus 2 in the SYNO
Exodus 2 in the TBIAOTANT
Exodus 2 in the TBT1E
Exodus 2 in the TBT1E2
Exodus 2 in the TFTIP
Exodus 2 in the TFTU
Exodus 2 in the TGNTATF3T
Exodus 2 in the THAI
Exodus 2 in the TNFD
Exodus 2 in the TNT
Exodus 2 in the TNTIK
Exodus 2 in the TNTIL
Exodus 2 in the TNTIN
Exodus 2 in the TNTIP
Exodus 2 in the TNTIZ
Exodus 2 in the TOMA
Exodus 2 in the TTENT
Exodus 2 in the UBG
Exodus 2 in the UGV
Exodus 2 in the UGV2
Exodus 2 in the UGV3
Exodus 2 in the VBL
Exodus 2 in the VDCC
Exodus 2 in the YALU
Exodus 2 in the YAPE
Exodus 2 in the YBVTP
Exodus 2 in the ZBP