Ezekiel 13 (BOKCV)
1 Neno la BWANA likanijia kusema: 2 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wa Israeli wanaotabiri sasa. Waambie hao ambao hutabiri kutokana na mawazo yao wenyewe: ‘Sikia neno la BWANA! 3 Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ole wao manabii wapumbavu wafuatao roho yao wenyewe na wala hawajaona chochote! 4 Manabii wako, ee Israeli, ni kama mbweha katikati ya magofu. 5 Hamjakwea kwenda kuziba mahali palipobomoka katika ukuta ili kuukarabati kwa ajili ya nyumba ya Israeli, ili kwamba isimame imara kwenye vita katika siku ya BWANA. 6 Maono yao ni ya uongo na ubashiri wao ni wa udanganyifu. Wao husema, “BWANA amesema,” wakati BWANA hakuwatuma, bado wakitarajia maneno yao kutimizwa. 7 Je, hamjaona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu hapo msemapo, “BWANA asema,” lakini Mimi sijasema? 8 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ya uongo wa maneno yenu na kwa madanganyo ya maono yenu, Mimi ni kinyume na ninyi, asema BWANA Mwenyezi. 9 Mkono wangu utakuwa dhidi ya manabii ambao huona maono ya uongo na kusema ubashiri wa udanganyifu. Hawatakuwa katika baraza la watu wangu au kuandikwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli wala hawataingia katika nchi ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA Mwenyezi. 10 “ ‘Kwa sababu ni kweli wanapotosha watu wangu, wakisema, “Amani,” wakati ambapo hakuna amani, pia kwa sababu, wakati ukuta dhaifu unapojengwa, wanaufunika kwa kupaka chokaa, 11 kwa hiyo waambie hao wanaoupaka chokaa isiyokorogwa vyema kwamba ukuta huo utaanguka. Mvua kubwa ya mafuriko itanyesha, nami nitaleta mvua ya mawe inyeshe kwa nguvu, nao upepo wa dhoruba utavuma juu yake. 12 Wakati ukuta utakapoanguka, je, watu hawatawauliza, “Iko wapi chokaa mliyopaka ukuta?” 13 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Katika ghadhabu yangu nitauachia upepo wa dhoruba, pia katika hasira yangu mvua ya mawe na mvua ya mafuriko itanyesha ikiwa na ghadhabu ya kuangamiza. 14 Nitaubomoa ukuta mlioupaka chokaa na kuuangusha chini ili msingi wake uachwe wazi. Utakapoanguka, mtaangamizwa ndani yake, nanyi mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA. 15 Hivyo ndivyo nitakavyoitimiza ghadhabu yangu dhidi ya huo ukuta na dhidi yao walioupaka chokaa. Nitawaambia ninyi, “Ukuta umebomoka na vivyo hivyo wale walioupaka chokaa, 16 wale manabii wa Israeli waliotabiri juu ya Yerusalemu na kuona maono ya amani kwa ajili yake wakati kulipokuwa hakuna amani, asema BWANA Mwenyezi.” ’ 17 “Sasa, mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya binti za watu wako wanaotabiri mambo kutoka mawazo yao wenyewe. Tabiri dhidi yao 18 na useme, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ole wao wanawake washonao hirizi za uchawi juu ya viwiko vyao vyote na kutengeneza shela za urefu wa aina mbalimbali kwa ajili ya kufunika vichwa vyao kwa makusudi ya kuwanasa watu. Je, mtatega uhai wa watu wangu lakini ninyi mponye wa kwenu? 19 Ninyi mmeninajisi miongoni mwa watu wangu kwa ajili ya konzi chache za shayiri na chembe za mkate. Kwa kuwaambia uongo watu wangu, wale ambao husikiliza uongo, mmewaua wale watu ambao wasingekufa na kuwaacha hai wale ambao wasingeishi. 20 “ ‘Kwa hiyo hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na hizo hirizi zenu za uchawi ambazo kwa hizo mnawatega watu kama ndege, nami nitazirarua kutoka mikononi mwenu, nitawaweka huru watu wale mliowatega kama ndege. 21 Nitazirarua shela zenu na kuwaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu, nao hawatakuwa tena mawindo ya nguvu zenu. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA. 22 Kwa sababu mliwavunja moyo wenye haki kwa uongo wenu, wakati mimi sikuwaletea huzuni na kwa kuwa mliwatia moyo waovu ili wasiziache njia zao mbaya na hivyo kuokoa maisha yao, 23 kwa hiyo hamtaona tena maono ya uongo wala kufanya ubashiri. Nitawaokoa watu wangu kutoka mikononi mwenu. Nanyi ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimi BWANA.’ ”
In Other Versions
Ezekiel 13 in the ANGEFD
Ezekiel 13 in the ANTPNG2D
Ezekiel 13 in the AS21
Ezekiel 13 in the BAGH
Ezekiel 13 in the BBPNG
Ezekiel 13 in the BBT1E
Ezekiel 13 in the BDS
Ezekiel 13 in the BEV
Ezekiel 13 in the BHAD
Ezekiel 13 in the BIB
Ezekiel 13 in the BLPT
Ezekiel 13 in the BNT
Ezekiel 13 in the BNTABOOT
Ezekiel 13 in the BNTLV
Ezekiel 13 in the BOATCB
Ezekiel 13 in the BOATCB2
Ezekiel 13 in the BOBCV
Ezekiel 13 in the BOCNT
Ezekiel 13 in the BOECS
Ezekiel 13 in the BOGWICC
Ezekiel 13 in the BOHCB
Ezekiel 13 in the BOHCV
Ezekiel 13 in the BOHLNT
Ezekiel 13 in the BOHNTLTAL
Ezekiel 13 in the BOICB
Ezekiel 13 in the BOILNTAP
Ezekiel 13 in the BOITCV
Ezekiel 13 in the BOKCV2
Ezekiel 13 in the BOKHWOG
Ezekiel 13 in the BOKSSV
Ezekiel 13 in the BOLCB
Ezekiel 13 in the BOLCB2
Ezekiel 13 in the BOMCV
Ezekiel 13 in the BONAV
Ezekiel 13 in the BONCB
Ezekiel 13 in the BONLT
Ezekiel 13 in the BONUT2
Ezekiel 13 in the BOPLNT
Ezekiel 13 in the BOSCB
Ezekiel 13 in the BOSNC
Ezekiel 13 in the BOTLNT
Ezekiel 13 in the BOVCB
Ezekiel 13 in the BOYCB
Ezekiel 13 in the BPBB
Ezekiel 13 in the BPH
Ezekiel 13 in the BSB
Ezekiel 13 in the CCB
Ezekiel 13 in the CUV
Ezekiel 13 in the CUVS
Ezekiel 13 in the DBT
Ezekiel 13 in the DGDNT
Ezekiel 13 in the DHNT
Ezekiel 13 in the DNT
Ezekiel 13 in the ELBE
Ezekiel 13 in the EMTV
Ezekiel 13 in the ESV
Ezekiel 13 in the FBV
Ezekiel 13 in the FEB
Ezekiel 13 in the GGMNT
Ezekiel 13 in the GNT
Ezekiel 13 in the HARY
Ezekiel 13 in the HNT
Ezekiel 13 in the IRVA
Ezekiel 13 in the IRVB
Ezekiel 13 in the IRVG
Ezekiel 13 in the IRVH
Ezekiel 13 in the IRVK
Ezekiel 13 in the IRVM
Ezekiel 13 in the IRVM2
Ezekiel 13 in the IRVO
Ezekiel 13 in the IRVP
Ezekiel 13 in the IRVT
Ezekiel 13 in the IRVT2
Ezekiel 13 in the IRVU
Ezekiel 13 in the ISVN
Ezekiel 13 in the JSNT
Ezekiel 13 in the KAPI
Ezekiel 13 in the KBT1ETNIK
Ezekiel 13 in the KBV
Ezekiel 13 in the KJV
Ezekiel 13 in the KNFD
Ezekiel 13 in the LBA
Ezekiel 13 in the LBLA
Ezekiel 13 in the LNT
Ezekiel 13 in the LSV
Ezekiel 13 in the MAAL
Ezekiel 13 in the MBV
Ezekiel 13 in the MBV2
Ezekiel 13 in the MHNT
Ezekiel 13 in the MKNFD
Ezekiel 13 in the MNG
Ezekiel 13 in the MNT
Ezekiel 13 in the MNT2
Ezekiel 13 in the MRS1T
Ezekiel 13 in the NAA
Ezekiel 13 in the NASB
Ezekiel 13 in the NBLA
Ezekiel 13 in the NBS
Ezekiel 13 in the NBVTP
Ezekiel 13 in the NET2
Ezekiel 13 in the NIV11
Ezekiel 13 in the NNT
Ezekiel 13 in the NNT2
Ezekiel 13 in the NNT3
Ezekiel 13 in the PDDPT
Ezekiel 13 in the PFNT
Ezekiel 13 in the RMNT
Ezekiel 13 in the SBIAS
Ezekiel 13 in the SBIBS
Ezekiel 13 in the SBIBS2
Ezekiel 13 in the SBICS
Ezekiel 13 in the SBIDS
Ezekiel 13 in the SBIGS
Ezekiel 13 in the SBIHS
Ezekiel 13 in the SBIIS
Ezekiel 13 in the SBIIS2
Ezekiel 13 in the SBIIS3
Ezekiel 13 in the SBIKS
Ezekiel 13 in the SBIKS2
Ezekiel 13 in the SBIMS
Ezekiel 13 in the SBIOS
Ezekiel 13 in the SBIPS
Ezekiel 13 in the SBISS
Ezekiel 13 in the SBITS
Ezekiel 13 in the SBITS2
Ezekiel 13 in the SBITS3
Ezekiel 13 in the SBITS4
Ezekiel 13 in the SBIUS
Ezekiel 13 in the SBIVS
Ezekiel 13 in the SBT
Ezekiel 13 in the SBT1E
Ezekiel 13 in the SCHL
Ezekiel 13 in the SNT
Ezekiel 13 in the SUSU
Ezekiel 13 in the SUSU2
Ezekiel 13 in the SYNO
Ezekiel 13 in the TBIAOTANT
Ezekiel 13 in the TBT1E
Ezekiel 13 in the TBT1E2
Ezekiel 13 in the TFTIP
Ezekiel 13 in the TFTU
Ezekiel 13 in the TGNTATF3T
Ezekiel 13 in the THAI
Ezekiel 13 in the TNFD
Ezekiel 13 in the TNT
Ezekiel 13 in the TNTIK
Ezekiel 13 in the TNTIL
Ezekiel 13 in the TNTIN
Ezekiel 13 in the TNTIP
Ezekiel 13 in the TNTIZ
Ezekiel 13 in the TOMA
Ezekiel 13 in the TTENT
Ezekiel 13 in the UBG
Ezekiel 13 in the UGV
Ezekiel 13 in the UGV2
Ezekiel 13 in the UGV3
Ezekiel 13 in the VBL
Ezekiel 13 in the VDCC
Ezekiel 13 in the YALU
Ezekiel 13 in the YAPE
Ezekiel 13 in the YBVTP
Ezekiel 13 in the ZBP