Ezekiel 24 (BOKCV)
1 Katika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi, neno la BWANA likanijia kusema: 2 “Mwanadamu, weka kumbukumbu ya tarehe hii, tarehe hii hasa, kwa kuwa mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu kwa jeshi siku hii ya leo. 3 Iambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Teleka sufuria jikoni; itelekena umimine maji ndani yake, 4 Weka vipande vya nyama ndani yake,vipande vyote vizuri,vya paja na vya bega.Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri; 5 chagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;chochea mpaka ichemkena uitokose hiyo mifupa ndani yake. 6 “ ‘Kwa kuwa hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Ole wa mji umwagao damu,ole wa sufuria ambayo sasaina ukoko ndani yake,ambayo ukoko wake hautoki.Kipakue kipande baada ya kipande,bila kuvipigia kura. 7 “ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:huyo mwanamke aliimwagajuu ya mwamba ulio wazi;hakuimwaga kwenye ardhi,ambako vumbi lingeifunika. 8 Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,nimemwaga damu yakejuu ya mwamba ulio wazi,ili isifunikwe. 9 “ ‘Kwa hiyo, hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo:“ ‘Ole wa mji umwagao damu!Mimi nami nitalundikia kuni nyingi. 10 Kwa hiyo lundika kunina uwashe moto.Pika hiyo nyama vizuri,changanya viungo ndani yake,na uiache mifupa iungue kwenye moto. 11 Kisha teleka sufuria tupu kwenye makaampaka iwe na moto sana na shaba yake ingʼae,ili uchafu wake upate kuyeyukana ukoko wake upate kuungua na kuondoka. 12 Imezuia juhudi zote,ukoko wake mwingi haujaondoka,hata ikiwa ni kwa moto. 13 “ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutoka kwenye huo uchafu wako, hutatakasika tena mpaka ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua. 14 “ ‘Mimi BWANA nimesema, wakati umewadia wa mimi kutenda. Mimi sitazuia, mimi sitaona huruma wala sitapunguza hasira yangu, Utahukumiwa sawasawa na mwenendo na matendo yako, asema BWANA Mwenyezi.’ ” 15 Neno la BWANA likanijia kusema: 16 “Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote. 17 Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.” 18 Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa. 19 Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?” 20 Kwa hiyo nikawaambia, “Neno la BWANA lilinijia kusema: 21 ‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndilo BWANA Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga. 22 Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji. 23 Mtajifunga vilemba vichwani mwenu na kuvaa viatu vyenu miguuni mwenu. Hamtaomboleza au kulia, lakini mtadhoofika kwa sababu ya dhambi zenu na kulia kwa uchungu kila mtu na mwenzake. 24 Ezekieli atakuwa ishara kwenu, mtafanya kama yeye alivyofanya. Wakati jambo hili litakapotokea, mtajua kuwa Mimi ndimi BWANA Mwenyezi.’ 25 “Nawe, mwanadamu, siku ile nitakapoondoa ngome yao iliyo furaha yao na utukufu wao, kitu cha kupendeza macho yao, kile kilicho shauku ya mioyo yao, wana wao na binti zao vilevile, 26 siku hiyo atakayetoroka atakuja kuwapasha habari. 27 Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimi BWANA.”
In Other Versions
Ezekiel 24 in the ANGEFD
Ezekiel 24 in the ANTPNG2D
Ezekiel 24 in the AS21
Ezekiel 24 in the BAGH
Ezekiel 24 in the BBPNG
Ezekiel 24 in the BBT1E
Ezekiel 24 in the BDS
Ezekiel 24 in the BEV
Ezekiel 24 in the BHAD
Ezekiel 24 in the BIB
Ezekiel 24 in the BLPT
Ezekiel 24 in the BNT
Ezekiel 24 in the BNTABOOT
Ezekiel 24 in the BNTLV
Ezekiel 24 in the BOATCB
Ezekiel 24 in the BOATCB2
Ezekiel 24 in the BOBCV
Ezekiel 24 in the BOCNT
Ezekiel 24 in the BOECS
Ezekiel 24 in the BOGWICC
Ezekiel 24 in the BOHCB
Ezekiel 24 in the BOHCV
Ezekiel 24 in the BOHLNT
Ezekiel 24 in the BOHNTLTAL
Ezekiel 24 in the BOICB
Ezekiel 24 in the BOILNTAP
Ezekiel 24 in the BOITCV
Ezekiel 24 in the BOKCV2
Ezekiel 24 in the BOKHWOG
Ezekiel 24 in the BOKSSV
Ezekiel 24 in the BOLCB
Ezekiel 24 in the BOLCB2
Ezekiel 24 in the BOMCV
Ezekiel 24 in the BONAV
Ezekiel 24 in the BONCB
Ezekiel 24 in the BONLT
Ezekiel 24 in the BONUT2
Ezekiel 24 in the BOPLNT
Ezekiel 24 in the BOSCB
Ezekiel 24 in the BOSNC
Ezekiel 24 in the BOTLNT
Ezekiel 24 in the BOVCB
Ezekiel 24 in the BOYCB
Ezekiel 24 in the BPBB
Ezekiel 24 in the BPH
Ezekiel 24 in the BSB
Ezekiel 24 in the CCB
Ezekiel 24 in the CUV
Ezekiel 24 in the CUVS
Ezekiel 24 in the DBT
Ezekiel 24 in the DGDNT
Ezekiel 24 in the DHNT
Ezekiel 24 in the DNT
Ezekiel 24 in the ELBE
Ezekiel 24 in the EMTV
Ezekiel 24 in the ESV
Ezekiel 24 in the FBV
Ezekiel 24 in the FEB
Ezekiel 24 in the GGMNT
Ezekiel 24 in the GNT
Ezekiel 24 in the HARY
Ezekiel 24 in the HNT
Ezekiel 24 in the IRVA
Ezekiel 24 in the IRVB
Ezekiel 24 in the IRVG
Ezekiel 24 in the IRVH
Ezekiel 24 in the IRVK
Ezekiel 24 in the IRVM
Ezekiel 24 in the IRVM2
Ezekiel 24 in the IRVO
Ezekiel 24 in the IRVP
Ezekiel 24 in the IRVT
Ezekiel 24 in the IRVT2
Ezekiel 24 in the IRVU
Ezekiel 24 in the ISVN
Ezekiel 24 in the JSNT
Ezekiel 24 in the KAPI
Ezekiel 24 in the KBT1ETNIK
Ezekiel 24 in the KBV
Ezekiel 24 in the KJV
Ezekiel 24 in the KNFD
Ezekiel 24 in the LBA
Ezekiel 24 in the LBLA
Ezekiel 24 in the LNT
Ezekiel 24 in the LSV
Ezekiel 24 in the MAAL
Ezekiel 24 in the MBV
Ezekiel 24 in the MBV2
Ezekiel 24 in the MHNT
Ezekiel 24 in the MKNFD
Ezekiel 24 in the MNG
Ezekiel 24 in the MNT
Ezekiel 24 in the MNT2
Ezekiel 24 in the MRS1T
Ezekiel 24 in the NAA
Ezekiel 24 in the NASB
Ezekiel 24 in the NBLA
Ezekiel 24 in the NBS
Ezekiel 24 in the NBVTP
Ezekiel 24 in the NET2
Ezekiel 24 in the NIV11
Ezekiel 24 in the NNT
Ezekiel 24 in the NNT2
Ezekiel 24 in the NNT3
Ezekiel 24 in the PDDPT
Ezekiel 24 in the PFNT
Ezekiel 24 in the RMNT
Ezekiel 24 in the SBIAS
Ezekiel 24 in the SBIBS
Ezekiel 24 in the SBIBS2
Ezekiel 24 in the SBICS
Ezekiel 24 in the SBIDS
Ezekiel 24 in the SBIGS
Ezekiel 24 in the SBIHS
Ezekiel 24 in the SBIIS
Ezekiel 24 in the SBIIS2
Ezekiel 24 in the SBIIS3
Ezekiel 24 in the SBIKS
Ezekiel 24 in the SBIKS2
Ezekiel 24 in the SBIMS
Ezekiel 24 in the SBIOS
Ezekiel 24 in the SBIPS
Ezekiel 24 in the SBISS
Ezekiel 24 in the SBITS
Ezekiel 24 in the SBITS2
Ezekiel 24 in the SBITS3
Ezekiel 24 in the SBITS4
Ezekiel 24 in the SBIUS
Ezekiel 24 in the SBIVS
Ezekiel 24 in the SBT
Ezekiel 24 in the SBT1E
Ezekiel 24 in the SCHL
Ezekiel 24 in the SNT
Ezekiel 24 in the SUSU
Ezekiel 24 in the SUSU2
Ezekiel 24 in the SYNO
Ezekiel 24 in the TBIAOTANT
Ezekiel 24 in the TBT1E
Ezekiel 24 in the TBT1E2
Ezekiel 24 in the TFTIP
Ezekiel 24 in the TFTU
Ezekiel 24 in the TGNTATF3T
Ezekiel 24 in the THAI
Ezekiel 24 in the TNFD
Ezekiel 24 in the TNT
Ezekiel 24 in the TNTIK
Ezekiel 24 in the TNTIL
Ezekiel 24 in the TNTIN
Ezekiel 24 in the TNTIP
Ezekiel 24 in the TNTIZ
Ezekiel 24 in the TOMA
Ezekiel 24 in the TTENT
Ezekiel 24 in the UBG
Ezekiel 24 in the UGV
Ezekiel 24 in the UGV2
Ezekiel 24 in the UGV3
Ezekiel 24 in the VBL
Ezekiel 24 in the VDCC
Ezekiel 24 in the YALU
Ezekiel 24 in the YAPE
Ezekiel 24 in the YBVTP
Ezekiel 24 in the ZBP