Genesis 21 (BOKCV)
1 Wakati huu BWANA akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye BWANA akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi. 2 Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi. 3 Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia. 4 Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru. 5 Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa. 6 Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.” 7 Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.” 8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaki alipoachishwa kunyonya, Abrahamu alifanya sherehe kubwa. 9 Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki, 10 Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyo mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwanangu Isaki.” 11 Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe. 12 Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki. 13 Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.” 14 Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba. 15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka. 16 Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni. 17 Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale. 18 Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.” 19 Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe. 20 Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde. 21 Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri. 22 Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya. 23 Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.” 24 Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.” 25 Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya. 26 Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.” 27 Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano. 28 Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi, 29 Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?” 30 Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.” 31 Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo. 32 Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti. 33 Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la BWANA, Mungu wa milele. 34 Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.
In Other Versions
Genesis 21 in the ANGEFD
Genesis 21 in the ANTPNG2D
Genesis 21 in the AS21
Genesis 21 in the BAGH
Genesis 21 in the BBPNG
Genesis 21 in the BBT1E
Genesis 21 in the BDS
Genesis 21 in the BEV
Genesis 21 in the BHAD
Genesis 21 in the BIB
Genesis 21 in the BLPT
Genesis 21 in the BNT
Genesis 21 in the BNTABOOT
Genesis 21 in the BNTLV
Genesis 21 in the BOATCB
Genesis 21 in the BOATCB2
Genesis 21 in the BOBCV
Genesis 21 in the BOCNT
Genesis 21 in the BOECS
Genesis 21 in the BOGWICC
Genesis 21 in the BOHCB
Genesis 21 in the BOHCV
Genesis 21 in the BOHLNT
Genesis 21 in the BOHNTLTAL
Genesis 21 in the BOICB
Genesis 21 in the BOILNTAP
Genesis 21 in the BOITCV
Genesis 21 in the BOKCV2
Genesis 21 in the BOKHWOG
Genesis 21 in the BOKSSV
Genesis 21 in the BOLCB
Genesis 21 in the BOLCB2
Genesis 21 in the BOMCV
Genesis 21 in the BONAV
Genesis 21 in the BONCB
Genesis 21 in the BONLT
Genesis 21 in the BONUT2
Genesis 21 in the BOPLNT
Genesis 21 in the BOSCB
Genesis 21 in the BOSNC
Genesis 21 in the BOTLNT
Genesis 21 in the BOVCB
Genesis 21 in the BOYCB
Genesis 21 in the BPBB
Genesis 21 in the BPH
Genesis 21 in the BSB
Genesis 21 in the CCB
Genesis 21 in the CUV
Genesis 21 in the CUVS
Genesis 21 in the DBT
Genesis 21 in the DGDNT
Genesis 21 in the DHNT
Genesis 21 in the DNT
Genesis 21 in the ELBE
Genesis 21 in the EMTV
Genesis 21 in the ESV
Genesis 21 in the FBV
Genesis 21 in the FEB
Genesis 21 in the GGMNT
Genesis 21 in the GNT
Genesis 21 in the HARY
Genesis 21 in the HNT
Genesis 21 in the IRVA
Genesis 21 in the IRVB
Genesis 21 in the IRVG
Genesis 21 in the IRVH
Genesis 21 in the IRVK
Genesis 21 in the IRVM
Genesis 21 in the IRVM2
Genesis 21 in the IRVO
Genesis 21 in the IRVP
Genesis 21 in the IRVT
Genesis 21 in the IRVT2
Genesis 21 in the IRVU
Genesis 21 in the ISVN
Genesis 21 in the JSNT
Genesis 21 in the KAPI
Genesis 21 in the KBT1ETNIK
Genesis 21 in the KBV
Genesis 21 in the KJV
Genesis 21 in the KNFD
Genesis 21 in the LBA
Genesis 21 in the LBLA
Genesis 21 in the LNT
Genesis 21 in the LSV
Genesis 21 in the MAAL
Genesis 21 in the MBV
Genesis 21 in the MBV2
Genesis 21 in the MHNT
Genesis 21 in the MKNFD
Genesis 21 in the MNG
Genesis 21 in the MNT
Genesis 21 in the MNT2
Genesis 21 in the MRS1T
Genesis 21 in the NAA
Genesis 21 in the NASB
Genesis 21 in the NBLA
Genesis 21 in the NBS
Genesis 21 in the NBVTP
Genesis 21 in the NET2
Genesis 21 in the NIV11
Genesis 21 in the NNT
Genesis 21 in the NNT2
Genesis 21 in the NNT3
Genesis 21 in the PDDPT
Genesis 21 in the PFNT
Genesis 21 in the RMNT
Genesis 21 in the SBIAS
Genesis 21 in the SBIBS
Genesis 21 in the SBIBS2
Genesis 21 in the SBICS
Genesis 21 in the SBIDS
Genesis 21 in the SBIGS
Genesis 21 in the SBIHS
Genesis 21 in the SBIIS
Genesis 21 in the SBIIS2
Genesis 21 in the SBIIS3
Genesis 21 in the SBIKS
Genesis 21 in the SBIKS2
Genesis 21 in the SBIMS
Genesis 21 in the SBIOS
Genesis 21 in the SBIPS
Genesis 21 in the SBISS
Genesis 21 in the SBITS
Genesis 21 in the SBITS2
Genesis 21 in the SBITS3
Genesis 21 in the SBITS4
Genesis 21 in the SBIUS
Genesis 21 in the SBIVS
Genesis 21 in the SBT
Genesis 21 in the SBT1E
Genesis 21 in the SCHL
Genesis 21 in the SNT
Genesis 21 in the SUSU
Genesis 21 in the SUSU2
Genesis 21 in the SYNO
Genesis 21 in the TBIAOTANT
Genesis 21 in the TBT1E
Genesis 21 in the TBT1E2
Genesis 21 in the TFTIP
Genesis 21 in the TFTU
Genesis 21 in the TGNTATF3T
Genesis 21 in the THAI
Genesis 21 in the TNFD
Genesis 21 in the TNT
Genesis 21 in the TNTIK
Genesis 21 in the TNTIL
Genesis 21 in the TNTIN
Genesis 21 in the TNTIP
Genesis 21 in the TNTIZ
Genesis 21 in the TOMA
Genesis 21 in the TTENT
Genesis 21 in the UBG
Genesis 21 in the UGV
Genesis 21 in the UGV2
Genesis 21 in the UGV3
Genesis 21 in the VBL
Genesis 21 in the VDCC
Genesis 21 in the YALU
Genesis 21 in the YAPE
Genesis 21 in the YBVTP
Genesis 21 in the ZBP