Genesis 36 (BOKCV)

1 Hivi ndivyo vizazi vya Esau (yaani Edomu). 2 Esau akaoa wake kutoka miongoni mwa wanawake wa Kanaani: Ada binti wa Eloni Mhiti, Oholibama binti wa Ana, mjukuu wa kike wa Sibeoni Mhivi, 3 pia akaoa Basemathi binti wa Ishmaeli, dada yake Nebayothi. 4 Ada akamzalia Esau Elifazi, Basemathi akamzaa Reueli, 5 Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wana wa Esau waliozaliwa kwake huko Kanaani. 6 Esau akawachukua wake zake, watoto wake wa kiume na wa kike na wote wa nyumbani mwake, mifugo yake pamoja na wanyama wake wengine wote na mali yake yote ambayo alikuwa ameipata akiwa Kanaani, akahamia katika nchi iliyo mbali na Yakobo ndugu yake. 7 Mali zao zilikuwa nyingi sana kiasi kwamba haikuwa rahisi wao kuishi pamoja, nchi waliyokuwa wakiishi isingewatosha wote kwa ajili ya mifugo yao. 8 Kwa hiyo Esau (ambaye ni Edomu) aliishi katika nchi ya kilima huko Seiri. 9 Hawa ndio wazao wa Esau, baba wa Waedomu, katika nchi ya kilima cha Seiri. 10 Haya ndiyo majina ya wana wa Esau:Elifazi, mwana wa Esau ambaye mkewe Ada alimzalia; na Reueli, mwana wa Esau ambaye mkewe Basemathi alimzalia. 11 Wana wa Elifazi ni:Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi. 12 Elifazi mwana wa Esau alikuwa pia na suria aliyeitwa Timna, ambaye alimzalia Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Ada mke wa Esau. 13 Wana wa Reueli ni:Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio waliokuwa wajukuu wa Basemathi mkewe Esau. 14 Wana wa Oholibama binti Ana, mkewe Esau, aliyekuwa mjukuu wa Sibeoni, aliomzalia Esau ni:Yeushi, Yalamu na Kora. 15 Hawa ndio waliokuwa wakuu miongoni mwa wazao wa Esau:Wakuu wa wana wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau ni:Temani, Omari, Sefo, Kenazi, 16 Kora, Gatamu na Amaleki. Hawa ndio waliokuwa wakuu waliotoka kwa Elifazi huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Ada. 17 Wakuu wa wana wa Reueli, mwana wa Esau ni:Nahathi, Zera, Shama na Miza. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa Reueli huko Edomu, waliokuwa wajukuu wa kiume wa Basemathi mkewe Esau. 18 Wakuu wa wana wa Esau ambao mkewe Oholibama alimzalia ni:Yeushi, Yalamu na Kora. Hawa ndio wakuu waliotoka kwa mke wa Esau, Oholibama binti Ana. 19 Hawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao. 20 Hawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile:Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 21 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori. 22 Wana wa Lotani walikuwa:Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani. 23 Wana wa Shobali walikuwa:Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. 24 Wana wa Sibeoni walikuwa:Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake. 25 Watoto wa Ana walikuwa:Dishoni na Oholibama binti wa Ana. 26 Wana wa Dishoni walikuwa:Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. 27 Wana wa Eseri walikuwa:Bilhani, Zaavani na Akani. 28 Wana wa Dishani walikuwa:Usi na Arani. 29 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori:Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, 30 Dishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri. 31 Wafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala: 32 Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba. 33 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. 34 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. 35 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. 36 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. 37 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake. 38 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. 39 Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. 40 Hawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:Timna, Alva, Yethethi, 41 Oholibama, Ela, Pinoni, 42 Kenazi, Temani, Mibsari, 43 Magdieli na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu, kufuatana na makazi yao katika nchi waliyoimiliki.Huyu ndiye alikuwa Esau, baba wa Waedomu.

In Other Versions

Genesis 36 in the ANGEFD

Genesis 36 in the ANTPNG2D

Genesis 36 in the AS21

Genesis 36 in the BAGH

Genesis 36 in the BBPNG

Genesis 36 in the BBT1E

Genesis 36 in the BDS

Genesis 36 in the BEV

Genesis 36 in the BHAD

Genesis 36 in the BIB

Genesis 36 in the BLPT

Genesis 36 in the BNT

Genesis 36 in the BNTABOOT

Genesis 36 in the BNTLV

Genesis 36 in the BOATCB

Genesis 36 in the BOATCB2

Genesis 36 in the BOBCV

Genesis 36 in the BOCNT

Genesis 36 in the BOECS

Genesis 36 in the BOGWICC

Genesis 36 in the BOHCB

Genesis 36 in the BOHCV

Genesis 36 in the BOHLNT

Genesis 36 in the BOHNTLTAL

Genesis 36 in the BOICB

Genesis 36 in the BOILNTAP

Genesis 36 in the BOITCV

Genesis 36 in the BOKCV2

Genesis 36 in the BOKHWOG

Genesis 36 in the BOKSSV

Genesis 36 in the BOLCB

Genesis 36 in the BOLCB2

Genesis 36 in the BOMCV

Genesis 36 in the BONAV

Genesis 36 in the BONCB

Genesis 36 in the BONLT

Genesis 36 in the BONUT2

Genesis 36 in the BOPLNT

Genesis 36 in the BOSCB

Genesis 36 in the BOSNC

Genesis 36 in the BOTLNT

Genesis 36 in the BOVCB

Genesis 36 in the BOYCB

Genesis 36 in the BPBB

Genesis 36 in the BPH

Genesis 36 in the BSB

Genesis 36 in the CCB

Genesis 36 in the CUV

Genesis 36 in the CUVS

Genesis 36 in the DBT

Genesis 36 in the DGDNT

Genesis 36 in the DHNT

Genesis 36 in the DNT

Genesis 36 in the ELBE

Genesis 36 in the EMTV

Genesis 36 in the ESV

Genesis 36 in the FBV

Genesis 36 in the FEB

Genesis 36 in the GGMNT

Genesis 36 in the GNT

Genesis 36 in the HARY

Genesis 36 in the HNT

Genesis 36 in the IRVA

Genesis 36 in the IRVB

Genesis 36 in the IRVG

Genesis 36 in the IRVH

Genesis 36 in the IRVK

Genesis 36 in the IRVM

Genesis 36 in the IRVM2

Genesis 36 in the IRVO

Genesis 36 in the IRVP

Genesis 36 in the IRVT

Genesis 36 in the IRVT2

Genesis 36 in the IRVU

Genesis 36 in the ISVN

Genesis 36 in the JSNT

Genesis 36 in the KAPI

Genesis 36 in the KBT1ETNIK

Genesis 36 in the KBV

Genesis 36 in the KJV

Genesis 36 in the KNFD

Genesis 36 in the LBA

Genesis 36 in the LBLA

Genesis 36 in the LNT

Genesis 36 in the LSV

Genesis 36 in the MAAL

Genesis 36 in the MBV

Genesis 36 in the MBV2

Genesis 36 in the MHNT

Genesis 36 in the MKNFD

Genesis 36 in the MNG

Genesis 36 in the MNT

Genesis 36 in the MNT2

Genesis 36 in the MRS1T

Genesis 36 in the NAA

Genesis 36 in the NASB

Genesis 36 in the NBLA

Genesis 36 in the NBS

Genesis 36 in the NBVTP

Genesis 36 in the NET2

Genesis 36 in the NIV11

Genesis 36 in the NNT

Genesis 36 in the NNT2

Genesis 36 in the NNT3

Genesis 36 in the PDDPT

Genesis 36 in the PFNT

Genesis 36 in the RMNT

Genesis 36 in the SBIAS

Genesis 36 in the SBIBS

Genesis 36 in the SBIBS2

Genesis 36 in the SBICS

Genesis 36 in the SBIDS

Genesis 36 in the SBIGS

Genesis 36 in the SBIHS

Genesis 36 in the SBIIS

Genesis 36 in the SBIIS2

Genesis 36 in the SBIIS3

Genesis 36 in the SBIKS

Genesis 36 in the SBIKS2

Genesis 36 in the SBIMS

Genesis 36 in the SBIOS

Genesis 36 in the SBIPS

Genesis 36 in the SBISS

Genesis 36 in the SBITS

Genesis 36 in the SBITS2

Genesis 36 in the SBITS3

Genesis 36 in the SBITS4

Genesis 36 in the SBIUS

Genesis 36 in the SBIVS

Genesis 36 in the SBT

Genesis 36 in the SBT1E

Genesis 36 in the SCHL

Genesis 36 in the SNT

Genesis 36 in the SUSU

Genesis 36 in the SUSU2

Genesis 36 in the SYNO

Genesis 36 in the TBIAOTANT

Genesis 36 in the TBT1E

Genesis 36 in the TBT1E2

Genesis 36 in the TFTIP

Genesis 36 in the TFTU

Genesis 36 in the TGNTATF3T

Genesis 36 in the THAI

Genesis 36 in the TNFD

Genesis 36 in the TNT

Genesis 36 in the TNTIK

Genesis 36 in the TNTIL

Genesis 36 in the TNTIN

Genesis 36 in the TNTIP

Genesis 36 in the TNTIZ

Genesis 36 in the TOMA

Genesis 36 in the TTENT

Genesis 36 in the UBG

Genesis 36 in the UGV

Genesis 36 in the UGV2

Genesis 36 in the UGV3

Genesis 36 in the VBL

Genesis 36 in the VDCC

Genesis 36 in the YALU

Genesis 36 in the YAPE

Genesis 36 in the YBVTP

Genesis 36 in the ZBP