Genesis 39 (BOKCV)

1 Wakati huu Yosefu alikuwa amechukuliwa mpaka Misri. Mmisri aliyeitwa Potifa aliyekuwa mmojawapo wa maafisa wa Farao, mkuu wa ulinzi, akamnunua Yosefu kutoka kwa Waishmaeli waliomleta Misri. 2 BWANA alikuwa pamoja na Yosefu, naye akastawi, Yosefu akaishi nyumbani kwa bwana wake Mmisri. 3 Potifa alipoona kuwa BWANA alikuwa pamoja na Yosefu na kwamba BWANA alimfanikisha kwa kila kitu alichokifanya, 4 Yosefu alipata kibali machoni pa Potifa, akamfanya mhudumu wake. Potifa akamweka kuwa msimamizi wa nyumba yake, naye akamkabidhi kuwa mwangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho. 5 Kuanzia wakati huo Potifa alipomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nyumba na mali zake zote alizokuwa nazo, BWANA aliibariki nyumba ya Mmisri huyo kwa sababu ya Yosefu. Baraka ya BWANA ilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa, nyumbani na shambani. 6 Kwa hiyo Potifa akamwachia Yosefu uangalizi wa kila kitu alichokuwa nacho, Yosefu alipokuwa katika uongozi, Potifa hakuwa na sababu ya kujishughulisha na kitu chochote isipokuwa chakula alichokula.Yosefu alikuwa mwenye umbo zuri na sura ya kuvutia; 7 baada ya kitambo mke wa Potifa akamtamani Yosefu, akamwambia, “Njoo, ukutane nami kimwili!” 8 Lakini Yosefu akakataa. Akamwambia yule mwanamke, “Mimi nikiwa katika uongozi, bwana wangu hahusiki na kitu chochote katika nyumba hii, kila kitu alicho nacho amenikabidhi. 9 Hapa nyumbani hakuna aliye mkuu kuliko mimi. Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” 10 Ingawa yule mwanamke aliendelea kumshawishi Yosefu siku baada ya siku, Yosefu alikataa kukutana naye kimwili wala kukaa karibu naye. 11 Siku moja Yosefu akaingia ndani ya nyumba kufanya kazi zake, wala hapakuwepo na mfanyakazi yeyote ndani ya nyumba. 12 Mke wa Potifa akashika vazi Yosefu alilokuwa amevaa, akamwambia, “Njoo tukutane kimwili!” Lakini Yosefu akaacha vazi lake mkononi mwa huyo mwanamke, akatoka nje ya nyumba akikimbia. 13 Yule mwanamke alipoona kwamba Yosefu amemwachia vazi lake mkononi na kukimbilia nje ya nyumba, 14 akawaita watumishi wake wa nyumbani, akawaambia, “Tazameni! Huyu Mwebrania ameletwa hapa kutudhihaki! Aliingia hapa ndani ili akutane nami kimwili, lakini nikapiga kelele. 15 Aliposikia kelele za kuomba msaada, akaacha vazi lake kando yangu akakimbilia nje.” 16 Yule mwanamke akaliweka lile vazi karibu naye mpaka Potifa aliporudi nyumbani. 17 Ndipo akamweleza kisa hiki, akisema: “Yule mtumwa wa Kiebrania uliyetuletea alinijia ili kunidhihaki. 18 Lakini mara nilipopiga kelele kuomba msaada, akaliacha vazi lake kando yangu akakimbia nje ya nyumba.” 19 Potifa aliposikia kisa hiki mkewe alichomweleza, akisema, “Hivi ndivyo mtumwa wako alivyonitenda.” Hasira ya Potifa ikawaka. 20 Potifa akamchukua Yosefu na kumweka gerezani, mahali ambapo wahalifu wa mfalme walikuwa wamefungwa.Lakini wakati Yosefu alipokuwa huko gerezani, 21 BWANA alikuwa pamoja naye, akamhurumia na kumpa kibali mbele ya msimamizi wa gereza. 22 Kwa hiyo msimamizi wa gereza akamweka Yosefu awe mkuu wa wafungwa pamoja na kusimamia yote ambayo yalitendeka mle gerezani. 23 Msimamizi wa gereza hakujishughulisha tena na kitu chochote kilichokuwa chini ya uangalizi wa Yosefu, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja na Yosefu akimfanikisha kwa kila alichofanya.

In Other Versions

Genesis 39 in the ANGEFD

Genesis 39 in the ANTPNG2D

Genesis 39 in the AS21

Genesis 39 in the BAGH

Genesis 39 in the BBPNG

Genesis 39 in the BBT1E

Genesis 39 in the BDS

Genesis 39 in the BEV

Genesis 39 in the BHAD

Genesis 39 in the BIB

Genesis 39 in the BLPT

Genesis 39 in the BNT

Genesis 39 in the BNTABOOT

Genesis 39 in the BNTLV

Genesis 39 in the BOATCB

Genesis 39 in the BOATCB2

Genesis 39 in the BOBCV

Genesis 39 in the BOCNT

Genesis 39 in the BOECS

Genesis 39 in the BOGWICC

Genesis 39 in the BOHCB

Genesis 39 in the BOHCV

Genesis 39 in the BOHLNT

Genesis 39 in the BOHNTLTAL

Genesis 39 in the BOICB

Genesis 39 in the BOILNTAP

Genesis 39 in the BOITCV

Genesis 39 in the BOKCV2

Genesis 39 in the BOKHWOG

Genesis 39 in the BOKSSV

Genesis 39 in the BOLCB

Genesis 39 in the BOLCB2

Genesis 39 in the BOMCV

Genesis 39 in the BONAV

Genesis 39 in the BONCB

Genesis 39 in the BONLT

Genesis 39 in the BONUT2

Genesis 39 in the BOPLNT

Genesis 39 in the BOSCB

Genesis 39 in the BOSNC

Genesis 39 in the BOTLNT

Genesis 39 in the BOVCB

Genesis 39 in the BOYCB

Genesis 39 in the BPBB

Genesis 39 in the BPH

Genesis 39 in the BSB

Genesis 39 in the CCB

Genesis 39 in the CUV

Genesis 39 in the CUVS

Genesis 39 in the DBT

Genesis 39 in the DGDNT

Genesis 39 in the DHNT

Genesis 39 in the DNT

Genesis 39 in the ELBE

Genesis 39 in the EMTV

Genesis 39 in the ESV

Genesis 39 in the FBV

Genesis 39 in the FEB

Genesis 39 in the GGMNT

Genesis 39 in the GNT

Genesis 39 in the HARY

Genesis 39 in the HNT

Genesis 39 in the IRVA

Genesis 39 in the IRVB

Genesis 39 in the IRVG

Genesis 39 in the IRVH

Genesis 39 in the IRVK

Genesis 39 in the IRVM

Genesis 39 in the IRVM2

Genesis 39 in the IRVO

Genesis 39 in the IRVP

Genesis 39 in the IRVT

Genesis 39 in the IRVT2

Genesis 39 in the IRVU

Genesis 39 in the ISVN

Genesis 39 in the JSNT

Genesis 39 in the KAPI

Genesis 39 in the KBT1ETNIK

Genesis 39 in the KBV

Genesis 39 in the KJV

Genesis 39 in the KNFD

Genesis 39 in the LBA

Genesis 39 in the LBLA

Genesis 39 in the LNT

Genesis 39 in the LSV

Genesis 39 in the MAAL

Genesis 39 in the MBV

Genesis 39 in the MBV2

Genesis 39 in the MHNT

Genesis 39 in the MKNFD

Genesis 39 in the MNG

Genesis 39 in the MNT

Genesis 39 in the MNT2

Genesis 39 in the MRS1T

Genesis 39 in the NAA

Genesis 39 in the NASB

Genesis 39 in the NBLA

Genesis 39 in the NBS

Genesis 39 in the NBVTP

Genesis 39 in the NET2

Genesis 39 in the NIV11

Genesis 39 in the NNT

Genesis 39 in the NNT2

Genesis 39 in the NNT3

Genesis 39 in the PDDPT

Genesis 39 in the PFNT

Genesis 39 in the RMNT

Genesis 39 in the SBIAS

Genesis 39 in the SBIBS

Genesis 39 in the SBIBS2

Genesis 39 in the SBICS

Genesis 39 in the SBIDS

Genesis 39 in the SBIGS

Genesis 39 in the SBIHS

Genesis 39 in the SBIIS

Genesis 39 in the SBIIS2

Genesis 39 in the SBIIS3

Genesis 39 in the SBIKS

Genesis 39 in the SBIKS2

Genesis 39 in the SBIMS

Genesis 39 in the SBIOS

Genesis 39 in the SBIPS

Genesis 39 in the SBISS

Genesis 39 in the SBITS

Genesis 39 in the SBITS2

Genesis 39 in the SBITS3

Genesis 39 in the SBITS4

Genesis 39 in the SBIUS

Genesis 39 in the SBIVS

Genesis 39 in the SBT

Genesis 39 in the SBT1E

Genesis 39 in the SCHL

Genesis 39 in the SNT

Genesis 39 in the SUSU

Genesis 39 in the SUSU2

Genesis 39 in the SYNO

Genesis 39 in the TBIAOTANT

Genesis 39 in the TBT1E

Genesis 39 in the TBT1E2

Genesis 39 in the TFTIP

Genesis 39 in the TFTU

Genesis 39 in the TGNTATF3T

Genesis 39 in the THAI

Genesis 39 in the TNFD

Genesis 39 in the TNT

Genesis 39 in the TNTIK

Genesis 39 in the TNTIL

Genesis 39 in the TNTIN

Genesis 39 in the TNTIP

Genesis 39 in the TNTIZ

Genesis 39 in the TOMA

Genesis 39 in the TTENT

Genesis 39 in the UBG

Genesis 39 in the UGV

Genesis 39 in the UGV2

Genesis 39 in the UGV3

Genesis 39 in the VBL

Genesis 39 in the VDCC

Genesis 39 in the YALU

Genesis 39 in the YAPE

Genesis 39 in the YBVTP

Genesis 39 in the ZBP