Genesis 45 (BOKCV)
1 Hapo Yosefu hakuweza kujizuia zaidi mbele ya wote waliokuwa wamesimama karibu naye, akapaza sauti, akasema, “Mwondoeni kila mtu mbele yangu!” Kwa hiyo hapakuwepo mtu yeyote pamoja na Yosefu alipojitambulisha kwa ndugu zake. 2 Naye akalia kwa sauti kubwa kiasi kwamba Wamisri walimsikia, hata watu wa nyumbani mwa Farao wakapata hizo habari. 3 Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yosefu! Je, baba yangu angali hai bado?” Lakini ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwa sababu walipatwa na hofu kuu mbele yake. 4 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Sogeeni karibu nami.” Waliposogea, akasema, “Mimi ni ndugu yenu Yosefu, yule ambaye mlimuuza Misri! 5 Sasa, msihuzunike wala msijichukie wenyewe kwa kuniuza huku, kwa sababu ilikuwa ni ili kuokoa maisha ya watu ndiyo sababu Mungu alinituma niwatangulie ninyi. 6 Kwa miaka miwili sasa imekuwepo njaa katika nchi, pia kwa miaka mitano ijayo hapatakuwepo kulima wala kuvuna. 7 Lakini Mungu alinitanguliza mbele yenu ili kuhifadhi mabaki kwa ajili yenu katika nchi, na kuokoa maisha yenu kwa wokovu mkuu. 8 “Kwa hiyo basi, si ninyi mlionileta huku, bali ni Mungu. Alinifanya kuwa baba kwa Farao, bwana wa watu wa nyumbani mwake wote, na mtawala wa Misri yote. 9 Sasa rudini haraka kwa baba yangu na mwambieni, ‘Hili ndilo mwanao Yosefu asemalo: Mungu amenifanya mimi kuwa bwana wa Misri yote. Shuka uje kwangu, wala usikawie. 10 Nawe utaishi katika nchi ya Gosheni na kuwa karibu nami, wewe, watoto wako na wajukuu wako, makundi yako ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, pamoja na vyote ulivyo navyo. 11 Nitawatunza huko, kwa sababu bado iko miaka mingine mitano inayokuja ya njaa. La sivyo, wewe na nyumba yako na wote ulio nao mtakuwa fukara.’ 12 “Mnaweza kujionea wenyewe, hata ndugu yangu Benyamini, kwamba hakika ni mimi ninayezungumza nanyi. 13 Mwambieni baba yangu juu ya heshima yote niliyopewa huku Misri, na kuhusu kila kitu mlichokiona. Mleteni baba yangu huku haraka.” 14 Ndipo akamkumbatia Benyamini ndugu yake na kulia, naye Benyamini akamkumbatia akilia. 15 Pia akawabusu ndugu zake wote, huku akilia. Baada ya hayo ndugu zake wakazungumza naye. 16 Habari zilipofika kwenye jumba la Farao kwamba ndugu zake Yosefu wamefika, Farao na maafisa wake wote wakafurahi. 17 Farao akamwambia Yosefu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Pakieni wanyama wenu mrudi mpaka nchi ya Kanaani, 18 mkamlete baba yenu na jamaa zenu kwangu. Nitawapa sehemu nzuri sana ya nchi ya Misri nanyi mtafurahia unono wa nchi.’ 19 “Mnaagizwa pia kuwaambia, ‘Fanyeni hivi: Chukueni magari ya kukokotwa kutoka Misri, kwa ajili ya watoto wenu na wake zenu, mkamchukue baba yenu mje. 20 Msijali kamwe kuhusu mali zenu, kwa sababu mema yote ya Misri yatakuwa yenu.’ ” 21 Hivyo wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yosefu akawapa magari ya kukokotwa, kama Farao alivyoagiza, pia akawapa mahitaji kwa ajili ya safari yao. 22 Kila mmoja mavazi mapya, lakini Benyamini akampa shekeli 300 za fedha, na jozi tano za nguo. 23 Hivi ndivyo vitu alivyotuma kwa baba yake: punda kumi waliochukua vitu vizuri vya Misri, punda wake kumi waliobeba nafaka, mikate na mahitaji mengine ya safari. 24 Akaagana na ndugu zake walipokuwa wakiondoka, akawaambia, “Msigombane njiani!” 25 Basi wakatoka Misri na kufika kwa baba yao Yakobo katika nchi ya Kanaani. 26 Wakamwambia baba yao, “Yosefu angali hai! Ukweli ni kwamba yeye ndiye mtawala wa Misri yote.” Yakobo akapigwa na bumbuazi; hakuwasadiki. 27 Lakini walipokwisha kumweleza kila kitu ambacho Yosefu alikuwa amewaambia, na alipoona magari ya kukokotwa Yosefu aliyokuwa amempelekea ya kumchukua aende Misri, roho ya baba yao Yakobo ikahuishwa. 28 Ndipo Israeli akasema, “Nimesadiki! Mwanangu Yosefu bado yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.”
In Other Versions
Genesis 45 in the ANGEFD
Genesis 45 in the ANTPNG2D
Genesis 45 in the AS21
Genesis 45 in the BAGH
Genesis 45 in the BBPNG
Genesis 45 in the BBT1E
Genesis 45 in the BDS
Genesis 45 in the BEV
Genesis 45 in the BHAD
Genesis 45 in the BIB
Genesis 45 in the BLPT
Genesis 45 in the BNT
Genesis 45 in the BNTABOOT
Genesis 45 in the BNTLV
Genesis 45 in the BOATCB
Genesis 45 in the BOATCB2
Genesis 45 in the BOBCV
Genesis 45 in the BOCNT
Genesis 45 in the BOECS
Genesis 45 in the BOGWICC
Genesis 45 in the BOHCB
Genesis 45 in the BOHCV
Genesis 45 in the BOHLNT
Genesis 45 in the BOHNTLTAL
Genesis 45 in the BOICB
Genesis 45 in the BOILNTAP
Genesis 45 in the BOITCV
Genesis 45 in the BOKCV2
Genesis 45 in the BOKHWOG
Genesis 45 in the BOKSSV
Genesis 45 in the BOLCB
Genesis 45 in the BOLCB2
Genesis 45 in the BOMCV
Genesis 45 in the BONAV
Genesis 45 in the BONCB
Genesis 45 in the BONLT
Genesis 45 in the BONUT2
Genesis 45 in the BOPLNT
Genesis 45 in the BOSCB
Genesis 45 in the BOSNC
Genesis 45 in the BOTLNT
Genesis 45 in the BOVCB
Genesis 45 in the BOYCB
Genesis 45 in the BPBB
Genesis 45 in the BPH
Genesis 45 in the BSB
Genesis 45 in the CCB
Genesis 45 in the CUV
Genesis 45 in the CUVS
Genesis 45 in the DBT
Genesis 45 in the DGDNT
Genesis 45 in the DHNT
Genesis 45 in the DNT
Genesis 45 in the ELBE
Genesis 45 in the EMTV
Genesis 45 in the ESV
Genesis 45 in the FBV
Genesis 45 in the FEB
Genesis 45 in the GGMNT
Genesis 45 in the GNT
Genesis 45 in the HARY
Genesis 45 in the HNT
Genesis 45 in the IRVA
Genesis 45 in the IRVB
Genesis 45 in the IRVG
Genesis 45 in the IRVH
Genesis 45 in the IRVK
Genesis 45 in the IRVM
Genesis 45 in the IRVM2
Genesis 45 in the IRVO
Genesis 45 in the IRVP
Genesis 45 in the IRVT
Genesis 45 in the IRVT2
Genesis 45 in the IRVU
Genesis 45 in the ISVN
Genesis 45 in the JSNT
Genesis 45 in the KAPI
Genesis 45 in the KBT1ETNIK
Genesis 45 in the KBV
Genesis 45 in the KJV
Genesis 45 in the KNFD
Genesis 45 in the LBA
Genesis 45 in the LBLA
Genesis 45 in the LNT
Genesis 45 in the LSV
Genesis 45 in the MAAL
Genesis 45 in the MBV
Genesis 45 in the MBV2
Genesis 45 in the MHNT
Genesis 45 in the MKNFD
Genesis 45 in the MNG
Genesis 45 in the MNT
Genesis 45 in the MNT2
Genesis 45 in the MRS1T
Genesis 45 in the NAA
Genesis 45 in the NASB
Genesis 45 in the NBLA
Genesis 45 in the NBS
Genesis 45 in the NBVTP
Genesis 45 in the NET2
Genesis 45 in the NIV11
Genesis 45 in the NNT
Genesis 45 in the NNT2
Genesis 45 in the NNT3
Genesis 45 in the PDDPT
Genesis 45 in the PFNT
Genesis 45 in the RMNT
Genesis 45 in the SBIAS
Genesis 45 in the SBIBS
Genesis 45 in the SBIBS2
Genesis 45 in the SBICS
Genesis 45 in the SBIDS
Genesis 45 in the SBIGS
Genesis 45 in the SBIHS
Genesis 45 in the SBIIS
Genesis 45 in the SBIIS2
Genesis 45 in the SBIIS3
Genesis 45 in the SBIKS
Genesis 45 in the SBIKS2
Genesis 45 in the SBIMS
Genesis 45 in the SBIOS
Genesis 45 in the SBIPS
Genesis 45 in the SBISS
Genesis 45 in the SBITS
Genesis 45 in the SBITS2
Genesis 45 in the SBITS3
Genesis 45 in the SBITS4
Genesis 45 in the SBIUS
Genesis 45 in the SBIVS
Genesis 45 in the SBT
Genesis 45 in the SBT1E
Genesis 45 in the SCHL
Genesis 45 in the SNT
Genesis 45 in the SUSU
Genesis 45 in the SUSU2
Genesis 45 in the SYNO
Genesis 45 in the TBIAOTANT
Genesis 45 in the TBT1E
Genesis 45 in the TBT1E2
Genesis 45 in the TFTIP
Genesis 45 in the TFTU
Genesis 45 in the TGNTATF3T
Genesis 45 in the THAI
Genesis 45 in the TNFD
Genesis 45 in the TNT
Genesis 45 in the TNTIK
Genesis 45 in the TNTIL
Genesis 45 in the TNTIN
Genesis 45 in the TNTIP
Genesis 45 in the TNTIZ
Genesis 45 in the TOMA
Genesis 45 in the TTENT
Genesis 45 in the UBG
Genesis 45 in the UGV
Genesis 45 in the UGV2
Genesis 45 in the UGV3
Genesis 45 in the VBL
Genesis 45 in the VDCC
Genesis 45 in the YALU
Genesis 45 in the YAPE
Genesis 45 in the YBVTP
Genesis 45 in the ZBP